Shalom Gospel Assembly

Shalom Gospel Assembly Barikiwa. Pia tunatoa huduma ya Ukombozi

Tunafanya huduma ya maombi na maombezi ili kuwafungua watu kutoka katika vifungo, nira, magonjwa mbalimbali, kufunguliwa kiuchumi (financial breakthrough)

Kufundisha wachungaji ili wakatumike maeneo mbalix2.

29/09/2025
Karibu
11/05/2023

Karibu

Shout out to my YouTube family! You continue to inspire and motivate me. 💞

https://www.youtube.com//community
13/03/2023

https://www.youtube.com//community

Welcome to our Brand Channel, please subscribe, share and comment. Don't forget view and comment on posts within COMMUNITY in our Brand ChannelEmail:lefthand...

0744 296 626JINSI YA KUFIKA KANISANIBETHEL CHURCH KIWALANIKupitia namba hii, unaweza kuwasiliana nasi na pia tunapokea s...
29/11/2022

0744 296 626
JINSI YA KUFIKA KANISANI
BETHEL CHURCH KIWALANI

Kupitia namba hii, unaweza kuwasiliana nasi na pia tunapokea sadaka yako kupitia hiyo namba
=====

Ukiwa Mnazi mmoja, panda mabasi yaliyoandikwa V/Viwandani - Mnazi Mmoja utashukia hapo hapo kanisani Betheli

Ukiwa Gongo la Mboto panda mabasi yanayoenda Tandika kwa kupitia Buza Ushukie Kwa GUDE unaweza kutembea hadi kanisani Betheli, ijapokuwa pia unaweza kuchukua bodaboda sh 1000.

Ukiwa Tandika panda basi la kwenda Mbezi au Gongo la Mboto na Ushukie Kwa GUDE

Ukiwa Kariakoo au Buguruni, panda basi linaloenda Yombo Relini au V/Viwandani Utashuka mlangoni kanisani Betheli

Ukiwa Mbezi karibu na kituo cha basi Magufuli Panda Mabasi yanayoenda Tandika kupitia Malamba Mawili au Buza Ushukie Kwa GUDE unaweza kutembea hadi kanisani Betheli Church Kiwalani au ukapanda bodaboda sh 1000

Karibu sana

Wiki hii yote kuanzia jana Jtatu hadi Jpili tarehe 4 Disemba 2022 tutakuwa kwenye kambi ya maombi ya Ukombozi kanisani B...
29/11/2022

Wiki hii yote kuanzia jana Jtatu hadi Jpili tarehe 4 Disemba 2022 tutakuwa kwenye kambi ya maombi ya Ukombozi kanisani Betheli Kiwalani Jijini Dar es Salaam. Ninakukaribisha katika maombi haya na Usipange kukosa

Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapata afya Marko 16:18

Karibu katika Ibada hii ya nguvu 31 July 2022
06/07/2022

Karibu katika Ibada hii ya nguvu 31 July 2022

15/04/2022
NDEGE YAANGUKA! MAOMBEZI BAADA YA SEMINA YAANGUSHA NDEGESemina iliyoanza Jumatano Kanisani Betheli, jana iliingia hatua ...
25/03/2022

NDEGE YAANGUKA!

MAOMBEZI BAADA YA SEMINA YAANGUSHA NDEGE

Semina iliyoanza Jumatano Kanisani Betheli, jana iliingia hatua ya pili kwa ndege huyo anayeonekana pichani kuanguka pale maombezi yalipokuwa yakiendelea.

Maombezi hayo ambayo walipokezana wawili, wa kwanza wao ni mwendesha semina, Mch POPAPO ISRAEL, mtoto wa nyumbani Betheli, mwenye ujumbe unaosema, "Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia adui yako shetani na kuupokea wokovu"

Na wa pili ni Askofu Elias Mwakalukwa, Mhitimu wa Degree ya Kwanza ya Uchungaji, Uongozi na Ustawi wa Jamii ambaye aliyaimarisha maombezi hayo na kuwaelekeza kanisa zima kuomba maombi ya toba ili watu wa Mungu waachiliwe huru.

Katikati ya maombezi hayo, baada ya maombi ya toba, ndege huyo alianguka ghafla akiwa amekaushwa huku akiwa amenyonyolewa mithili ya aliyekaangwa kwenye mafuta au kupigwa na shoti ya umeme bila kuungua!!!

Bishop Mwakalukwa akasema, YESU NI NURU GIZA KAMWE HALIWEZI KUSHINDA LAZIMA KAZI ZOTE ZA IBILISI ZIVUNJIKE HUO NI UCHAWI UMESHINDWA KWA JINA LA YESU

Mama Askofu, Bi Nesta Mwakalukwa akasema, "Hakika Mungu yuko kazini na fyekeo lake adui amedhoofishwa sifa na utukufu kwa Mungu"

Mwinjilist na mtumishi wa Mungu, John Charles Singano akatoa maoni yake na kusema, NIMEANGALIA KWA MAKINI NDEGE ALLIPOTOKEA SIJAPAONA ...NA KWANINI AANGUKE WAKATI WA MAOMBI...
HII INAAMMANISHA KUNA FALME ZIMEANGUSHWA CHINI NA KUNYAUSHWA NA JINALA YESU... BETHEL INAENDA VIWANGO VINGINE ..

Semina hiyo inanakshiwa na waimbaji wawili wa nyimbo za Injili, Nabwike Popapo na Daniel Safari. Kutokana na semina ilivyo, Daniel Safari aliimba wimbo wa "Mtoto kwa mzazi hakui"

Semina inaendelea tena leo jioni hapa kanisani Betheli Kiwalani kuanzia saa kumi... Karibu sana ushiriki maombi haya.

14/03/2022

* *

SEHEMU YA 3.

*MAMBO 🔟 UNAYOTAKIWA KUFAHAMU KUHUSU MSAMAHA.*

1. *KUMSAMEHE ALIYEKUKOSEA NI AGIZO.*

Msamaha ni AGIZO la Mungu kwa wale ambao wametukosea kwa mtu aliyeokoka na si HIARI.

Mathayo 6:14-15
*_"Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba yenu wa mbinguni ATAWASAMEHE ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu HATAWASAMEHE ninyi makosa yenu."_*

2. *HAKUNA KOSA LISILO SAMEHEWA.*

Mungu alipoagiza tusameheane hakuweka mpaka wa iana gani ya makosa tunayoweza kusamehe, kosa lolote ulilofanyiwa inatupasa kusamehe hata k**a limeleta uchungu kiasi gani katika maisha yetu.

3. *HAKUNA IDADI/KIWANGO CHA KUKOSEWA ILI USAMEHE.*

Tunapaswa kusamehe bila kuhesabu mara ngapi tumekosewa, ndio maana kwenye hatua za kusamehe tuliona kipengele cha kuondoa uchungu na kumbukumbu za mambo uliyokosewa.

K**a ukifanikiwa katika hatua hii kila kosa utakalotendewa litakuwa JIPYA maana hautakuwa na kumbukumbu ya makosa ya nyuma uliyotendewa.

*Mathayo 18: 21-22*

4. *HUWEZI KUKWEPA KUKOSEWA.*

Katika ulimwengu huu tulionao utakaa wapi ambapo utazungukwa na malaika ambao hawatakukwaza?

Ukikimbia makwazo kazini utayakuta nyumbani, ukiyakimbia nyumbani utayakuta kanisani. Hakuna sehemu ambayo hutakwazwa. ndio maana Yesu alisema _*"MAKWAZO HAYANA BUDI KUJA " .*_

Hivyo unachotakiwa kufanya ni kujizuia USIKWAZIKE UPESI maana kuna watu wapo k**a yai kitu kidogo tu kinaweza kuwakwaza na kuvunja mioyo yao, Jizoeshe kuwa na moyo mgumu unaoweza kuhimili makwazo ya kila iana .kinyume na hapo *UTAPATA TABU SANA."*

*Mathayo 18: 7*

5. *MSAMAHA NI KWA AJILI YAKO NA SI ALIYEKUKOSEA.*

Unaweza ukafikiri kutokumsamehe mtu ni kumkomoa kumbe unajikomoa wewe mwenyewe.

Kutokusamehe kunaleta uchungu moyoni na uchungu una madhara makubwa sana kiafya,kiroho,kisaikolojia na hata kijamii kwa yeye aliyebeba huo uchungu na si kwa aliyefanya kosa.

Mara nyingi wale ambao wamekwaza watu wengine huwa hawajui /hawajali maumivu waliyoyasababisha wao huwa huru na kuwa na amani wakiwaacha wenzao na uchungu mwingi miyoni mwao.

Hivyo samehe ili ujitoe kwenye hicho kifungo na USISUBIRI aliyekukosea akuombe msamaha.

6. *UPASWA KUSAMEHE HATA K**A ALIYEKUKOSEA HAJAOMBA MSAMAHA.*

Tumeona sababu ya 5 hapo juu kwamba msamaha unaleta faida kwako binafsi na si aliyekukosea .

Unaweza kusubiri uombwe msamaha wakat huyo aliyekukosea hajui k**a amekukosea au anaweza akawa anajua lakin asijali maumivu yako na hana mpango hata wa kuomba msamaha , JE utaendelea kumsubir mpaka lini? Au utamlazimisha aombe msamaha?

Kuna wengine ukiwalazimisha waone kosa lao Huwa wanakuja juu na wanaweza kukusabishia maumivu zaidi.

Unaweza ukatafuta watu wengine wawasuluhishe,k**a akikubali kosa lake sawa na k**a bado akikataa bado unapaswa kumsamehe ili wewe uwe na amani na usipoteze kibali chako kwa Mungu.

7. *UNAPASWA KUSAMEHE BILA KUJALI ALIYEKUKOSEA K**A AMEBADILIKA AU LA.*

Jambo unalopaswa kufahamu ni kuwa huna uwezo wa kumbadilisha mtu awe k**a vile utakavyo wewe( Hii inawahusu zaidi wana ndoa ).

Mnapokwazana na mwenzako huku ukilazimisha ili amani ipatikane basi ni lazima afanye/aishi vile utakavyo wewe basi huo mgogoro hautaisha.

Unawezaje kumrekebisha mtu mliyekutana ukubwani mliopitia malezi na mazingira tofauti ❓ UNAPASWA kukubaliana na mapungufu yake huku ukimuombea Mungu ambadilishe maana ni yeye pekee ndiye mwenye huo uwezo.

8. *KUSAMEHE NI UPENDO*

Kiwango chako cha upendo kitapimwa na uwezo wako wa kumsamehe aliyekukosea, Ukipenda SANA utasamehe sana na kinyume chake.

Maandiko yanasema upendo huvumilia yote,hauoni uchungu,hauhesabu mabaya na hustahimili yote. *1 Wakor 13: 4-7*

9. *MSAMAHA NI UFUNGUO WA UHUSIANO ULIOFUNGWA/UNAOLEKEA KUFA.*

Mnaweza mkawa mnakaa nyumba moja,mnalala pamoja ,mnakula pamoja lakini hamna mahusiano mazuri.

Unaweza ukajificha kwa nje isionekane k**a mpo tofaut lakini kuna mambo yataonesha TU UPANDE mmoja hauko sawa,na bila kukubali kusamehe basi uhusiano huo unaweza ukafa kabisa.

Kubali kuachilia ili mlinde uhusiano wenu maana hamna mahusiano yasiyo na changamoto( Kwa wanandoa) ,zilikuzidi sana basi mpelekee Mungu maana yeye hujishughulisha SANA na mambo yetu.

10. *KUSAMEHE SI UJINGA.*

Usiogope kusamehe kwa kujiona utakuwa mjinga , kusamehe ni jambo la kishujaa.

Kusamehe ni kujishusha na kujinyenyekesha ambayo ni SIFA walizonazo watu ambao wenye matarajio ya kuingia mbinguni.

_*"Akasema ,Amin nawaambia msipoongoka na kuwa k**a vitoto HAMTAINGIA KAMWE katika ufalme wa mbinguni. Basi yeyote AJINYENYEKESHAYE MWENYEWE k**a mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni."*_

*Mathayo 18 :3-4* .......................................

*Mwl John C Ntogwisangu*

*Watsap 0712 463 344*

Nizungumze nawe kiongozi wa eneo lako unalofanyia kazi. Popote pale unapodhamiria kufanya jambo jema lenye faida kwa jam...
11/03/2022

Nizungumze nawe kiongozi wa eneo lako unalofanyia kazi. Popote pale unapodhamiria kufanya jambo jema lenye faida kwa jamii nzima. Wapinzani hawakosekani

Na hii ndio maana kitabu hiki cha Nehemia, ni moja ya vitabu vyenye nguvu katika mafundisho ya uongozi

Nehemia 4:1
Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.

Nehemia 4:2
Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?

Nehemia 4:3
Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.

Nehemia 4:4
Sikia, Ee Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho;

Nehemia 4:5
wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.

Nehemia 4:6
Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaungamanishwa kiasi cha nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi.

Nehemia 4:7
Lakini ikawa, Sanbalati, na Tobia, na Waarabu, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;

Nehemia 4:8
wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo.

Nehemia 4:9
Bali sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku, kwa sababu yao, ili kuwapinga.

Kipo kitu ulicho jifunza. Washirikishe wengine

Mchungaji
Hilda Macha
Visiga Kibaha
0623 133717

TAFAKARI HAYA NA ULINGANISHE NA UONGOZI WAKO ULIVYOMungu akikuchagua na kukuweka mahali, endelea kutunza uaminifu mbele ...
11/03/2022

TAFAKARI HAYA NA ULINGANISHE NA UONGOZI WAKO ULIVYO

Mungu akikuchagua na kukuweka mahali, endelea kutunza uaminifu mbele za Mungu na kila uombalo, katika Bwana, utapewa.

Fuatilia mtiririko huu wa mawasiliano ya Sulemani na Mungu utaona tu mwenyewe uchague ni jinsi gani umtumikie Mungu

1 Wafalme 9:1
Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya,

1 Wafalme 9:2
basi, BWANA akamtokea Sulemani mara ya pili k**a alivyomtokea huko Gibeoni.

1 Wafalme 9:3
BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote;

1 Wafalme 9:4
na wewe, ukienda mbele zangu k**a alivyokwenda Daudi, baba yako, kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili, kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu,

1 Wafalme 9:5
ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; k**a nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli.

1 Wafalme 9:6
Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu,

1 Wafalme 9:7
basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.

Mch Hilda Macha
Visiga Kibaha
0623 133717

Address

Kiwalani
Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Wednesday 22:00 - 18:00
Friday 16:00 - 18:00
Sunday 08:00 - 10:00
10:00 - 13:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shalom Gospel Assembly posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share