22/08/2022
JINSI MKULIMA WA VIJIJINI NEW YORK NA MHUBIRI WA KAWAIDA WA BAPTIST ALIVYOINGIZA UZUSHI WA KUPOTEZA NDANI YA ‘DHEHEBU LA KIKRISTO’ NA YAKADUMU HATA LEO.(Part ONE)
Na Shemasi Jimmy 0659 611 252 Hallelujah watu wa Mungu, hakika tunakila sababu ya kumshukuru Mungu kwa wema na ukuu wake katika maisha yetu. Basi sifa na utukufu vina yeye hata milele. Leo tutaangalia jinsi mafundisho potofu yalivyoingia katika baadhi ya madhehebu ya kikristo kupitia mlango wa unabii wa Daniel.
Neno la Mungu linasema,’’ Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii’’ kumb 29:29. Ni wazi kua hakuna mwanadamu mwenye hekima ya kutoa tafasiri ya jambo ambalo halijafunuliwa na Mungu kupitia neno lake takatifu. Mambo yote ambayo Mungu imempendeza sisi tuyajue aliweza kuyatolea tafasiri ndani ya biblia. Ukisoma kwa utulivu kitabu cha nabii Danieli utagundua kua ni moja kati ya vitabu vigumu ambavyo si jambo rahisi kwa mwanadamu kupata tafasiri ya maono na doto kwa kutumia hekima zake. Iimpendeza Mungu kutufunulia badhi ya mambo ndani ya kitabu hicho, na baadhi ya mambo yamefanywa kua SIRI ya Mungu. Mfano wa baadhi ya mambo ambayo Mungu hakuyatolea ufafanuzi ni pamoja na:-
-majuma 70(Dan 9:24)
-majuma 62(Dan 9:25)
-siku 2300(Dan 8:14)
-siku 1290(Dan 12:11)
-siku 1335(dan 12:12)
BAADHI YA MAFUNDISHO YANAYOFUNGAMANISHWA NA UNABII WA DANIEL(AYA HIZO JUU) NI PAMOJA NA-
-Huduma ya patakatifu pa mbinguni
-wanafundisha pia kua Yesu aliingia patakarifu pa mbinguni tarehe 22.10.1844
Chimbuko la mapotovu hayo ni the Great disappointment(kukata tamaa kubwa) iliyoasisiwa na mkulima wa matunda na mwinjiristi wa kujitolea wa kanisa la babtisti aliyejulikana k**a Willium Miller.
Great disappointment katika harakati ya Millerite ilikuwa majibu ambayo yalifuata tangazo la mhubiri wa Baptist Miller kwamba Yesu Kristo atarudi Duniani kufikia 1844, kile alichokiita Advent. Uchunguzi wake wa unabii wa Danieli 8 wakati wa Ufufuo Mkuu wa Pili ulimpeleka kwenye hitimisho kwamba "utakaso wa patakatifu" wa Danieli ulikuwa utakaso wa ulimwengu kutoka kwa dhambi wakati Kristo angekuja, na yeye na wengine wengi walijiandaa, lakini Oktoba 22, 1844, walikuja na wakakatishwa tamaa.
Matukio haya yalifungua njia kwa Wasabato waliounda Kanisa la Waadventista Wasabato. Walisema kwamba kile kilichotokea Oktoba 22 haikuwa kurudi kwa Yesu, k**a vile Miller alifikiria, lakini kuanza kwa kazi ya mwisho ya Yesu ya upatanisho, utakaso katika patakatifu pa mbinguni, kuelekea kurudi mara ya pili.
MILLER ALIDAI UJIO WA PILI WA KRISTO ULIKUWA KARIBU
Kati ya 1831 na 1844, kwa msingi wa ujifunzaji wake wa Biblia, na haswa unabii wa Danieli 8: 14 - "Mpaka siku elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa" - William Miller, mkulima wa vijijini New York na Mhubiri wa kawaida wa Baptist, alitabiri na kuhubiri kurudi kwa Yesu Kristo duniani. Mafundisho ya Miller yanaunda msingi wa kitheolojia wa Seventh-day Adventism. Mada nne zilikuwa muhimu sana:
1. Matumizi ya Miller ya Biblia;
2. eskatolojia yake;
3. mtazamo wake juu ya ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili wa Ufunuo 14; na
4. Harakati ya miezi ya saba ambayo ilimalizika na "Kukata tamaa Kubwa".
ungana nami tena panapo majaliwa siku ya kesho kwa mwendelezo wa habari hii. Mungu akubariki kwa kutumia muda wako wa thamani kusoma chapisho hili.