16/04/2022
SOMO=MAHUSIANO YAKO NA MUNGU.
*Hapa kuna ujumbe wa muhimu sana sana kwetu leo ambao ni vema ukausoma ili ujue jambo likupasalo kulifanya.
.Mathayo 6:5.
5-Tena msalipo, msiwe k**a wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
*Hii inatufundisha kitu gani, Watu wengi wanawaza kua hapa tumezuiliwa kuomba kwa Sauti au kwa Nguvu ila tunatakiwa tuombe polepole tena tukiwa ndani alafu asikuone au kusikia mtu hapana, sio maana yake ngoja sasa tujifunze kwa kuona mfano mmoja mdogo hapa.
MFANO MR&MRS wakiwa wote mbele za watu wanaonekana wanapendana na kuheshimiana sana ila kwao wanalala vyumba tofauti.
*Sasa andiko hili linatuonyesha kwa kifupi kua Ukristo ni mahusiano yako na Mungu na sio vinginevyo, Maana unaweza kua kanisani unaomba sana na unaonekana upo shwari kabisa mbele ya macho ya watu ila nyumbani Yesu haupo naye.
*Unajua unapofanya jambo la ki Mungu ondoa kabisa zana ya watu au mtu kuona mfano unapoamua kutoa kitu kanisani kwa ajili ya Mungu huna haja ya mtu ajue kwani ukiruhusu mtu ajue nae akisema hongera ndio tayari ushapata thawabu yako hivyo Mungu hausiki tena hapo, jua kitu kimoja hakina thawabu mbili yaani ya watu na Mungu hapana.
*We hujawahi ona kuna watu hawawezi toa kitu kanisani mpka mchungaji aite watu mbele ili nini waonekane hao ndio waombao pembeni mwa njia na kupiga kelele ila kuna watu hata uiteje mbele hawaji ila utaona wametoa tena kingi hao ndio wanaojibiwa na Mungu mqana wameamua yeye aonaye sirini ndio pekee wakujua na kuwajibu.
*Ndugu usidanganywe na kujidanganya Mungu sio mwana siasa so ili upate chake lazima ufuate maelekezo yake na si vinginevyo jua UKRISTO NA KUTOA KUPO NDANI YA MAHUSIANO YAKO BINAFSI NA MUNGU NA SIO WATU.Barikiwa.
Kutoka 32:30.
30-Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu kwa BWANA, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.
Huko nyumbani kwako wewe na Yesu mnalala chumba kimoja au kanisani ndio tunawaona mpo sawa?