18/01/2025
SOMO: UUNGU WA YESU KRISTO
UTANGULIZI:
Shalom mtu wa Mungu, napenda kukukaribisha tujifunze kuhusu Uungu wa Yesu, maana ninajua mjadala uliopo juu ya Uungu wa Yesu na jinsi watu wengi hasa wale wasioamini katika Kristo. Kwasababu hiyo Leo nimeona niilete tafakari hii ili tujifunze zaidi. Somo hili tutajifunza katika vipengele k**a ifuatavyo.
1. SIFA ZA MUNGU
2. UFUNUO KUHUSU MUNGU
3. YESU NI NENO
4. YESU NI NURU
5. YESU NI HEKIMA
SIFA ZA MUNGU
1. Uzima wake ni wa Milele
Yn5:25-26, 5:21, 4:1-4, Yn10:27-28,
Rum6:23, 8:10.
2. Kutoa na kutwaa uzima au uhai
Yn5:21, Yn10:17-18.
3. Ana uweza wote
Mungu anaweza kufanya jambo lolote
Hakuna lililogumu kwake. Lk1:37,
Ayubu42:2. 38:1-12, Mat8:26-27.
4. Mungu anajua yote
1Yoh3:20, Isa40:28, Zab147:5,
Ayu37:16, Mat10:29, Zab139:23,
1kor3:20, Isa42:9,46:10,48:5-7.
5. Mungu yupo kila mahali
Yer23:23-24, Zab139:7-12,
Mdo17:24-28. Ukitaka kulithibitisha
siku za Leo, watu wanaomba sehemu
mbalimbali lakini pote anakuwepo na
anawatendea wanayoyahitaji.
6. Mungu ni Mfalme wa utukufu
Isa6:3, Eze1:1, kut20:18-21. Zab24:8-10
7. Mungu ni wa Milele
Mungu hafungwi na wakati majira wala
nafasi. Zab90:2.
8. Mungu ni mtakatifu
Yos24:19, Ufu4:8 1Pet1:15-16.
UFUNUO KUHUSU MUNGU
1. Mungu amejifunua katika utatu
mtakatifu
A. Mungu mmoja nafsi tatu
Vipengele 12 katika ungamo la
Mitume vimegawanyika katika
sehemu 3.
(1) inamuhusu Mungu Baba,
Muumba wetu.
(2) inamuhusu Mungu Mwana
(3) inamuhusu Mungu Roho
Mtakatifu atutakasaye.
AGANO LA KALE
Unapofatiria katika agano la kale
Ufunuo kuhusu Mungu haukuwa
Wazi sana kuhusiana na utatu
wake. Lakini katika agano jipya
huko wazi. Utagundua kuna
Mungu Mmoja lakini amejifunua
katika utatu. Mwa1:26, 3:22, 11:7.
Ukweli ni kwamba Mungu
alizungumza katika wingi,
tufanye, tushike n.k. Ni dalili ya
kwanza ya utatu. Katika
vipengele vingine Yesu
alifunuliwa k**a Mwana wa
Mungu. Pia ameitwa Bwana na
Mfalme. Mwa16:9. Kut3:27,
Amu6:12-16, Hag2:5-, Yoe2:28.
Mdo2:1-4.
AGANO JIPYA
katika agano jipya utatu wa
Mungu huko wazi zaidi, lakini ni
vyema tukafahamu kuwa Mungu
ni Mmoja nafsi tatu. 1Kor8:4.
Efe4:6. Mungu anatambuliwa au
kutambulika k**a Baba, Mwana
na Roho mtakatifu. Lk1:35,
Mat28:19,
Rum1:1-4,1kor12:3-6,2kor13:13-14.
Yuda1:20-21.
NAFSI ZOTE TATU NI MUNGU
1. Baba ni Mungu
2. Mwana ni Mungu
Majina yake yanathibitisha
- Immanuel - Mungu pamoja
nasi. Mat1:23.
- Alfa na Omega - Wakwanza na
wa mwisho. Ufu1:8, 22:12-13.
- Maandiko yanathibitisha wazi
kuwa Yesu ni Mungu.
1Yoh5:20, Rum9:5, Yn20:28,
Ebr1:7-9.
- Yesu mwenyewe amesema
Yn14:7-9.
- Aliye muona Yesu amemuona
Mungu. 1Yoh5:7-8. Yn14:7-9.
3. Roho Mtakatifu ni Mungu
Mdo5:3-7.
YESU NI NENO
1. Alikuwepo kabla ya uumbaji
2. Yupo Pamoja nasi hata sasa
3. Atakuwepo Milele yote
4. Neno ni Mungu
Yn1:1-3, Yn1:14, 1Yoh1:1-2, 1Tim6:15,
Isa9:6. Yer23:5-6, 33:16, Dan2:47,
Ufu19:13-16, 17:14.
YESU NI NURU
1. Nuru ya ulimwengu
2. Nuru ing'ayo gizani
3. Mungu ni Nuru.
Yn1:1-10, Yn8:12, 12:46, 12:35-36, 3:19.
Yn1:3, Kol1:16-17.
YESU NI HEKIMA
1. Hekima itokayo juu
2. Ilikuwepo kabla ya misingi ya
ulimwengu kuumbwa.
3. Yesu ni Mungu aliyefunuliwa k**a
hekima itokayo juu. 1Kor1:30, Flp2:6-8.
Mit8:22-36.
Ubarikiwe ninaamini k**a umekuwa katika hali ya kujifunza utakuwa umepata Kitu. Kwa mawasiliano zaidi tuwalisiane inbox.
Pastor. Isaya Kanyinda