God's Kingdom Church In the World

God's Kingdom Church In the World KANISA LA UFALME WA MUNGU DUNIANI

KTK HARAKATI ZA KUPINGA UKATILI KTK JAMII, VIONGOZI TAASISI YA KUPINGA UKATILI SMAUJATA JANA TUMEFIKA KTK OFSI YA DAS KI...
26/10/2023

KTK HARAKATI ZA KUPINGA UKATILI KTK JAMII, VIONGOZI TAASISI YA KUPINGA UKATILI SMAUJATA JANA TUMEFIKA KTK OFSI YA DAS KINONDONI,NA KUONGEA MAMBO KADHAA YAKUFANYA KTK HARAKATI ZA KUTOKOMEZA UKATILI KWA JAMII

20/04/2022

Yesu ndiye astahiliye kusifiwa na kuabudiwa peke anastahili

TUNATAKIWA KUTUBUShalom ndugu Watumishi wa Mungu, Wanadamu wote, Taifa la Tanzania na Mataifa yote:Mungu amesema nami us...
12/04/2020

TUNATAKIWA KUTUBU

Shalom ndugu Watumishi wa Mungu, Wanadamu wote, Taifa la Tanzania na Mataifa yote:

Mungu amesema nami usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 12/04/2020 kuwa ameruhusu Coronavirus kupiga sana mataifa makubwa kwa sababu Dunia imeelemewa na dhambi hivyo kwa ghadhabu yake amerehusu hili litokee.

Watu wamekuwa wanajitukuza ki uchumi, Mali walizonazo watoto, Ndoa; wanajitukuzia humo na kusahau kumuabudu na kumtegemea Mungu kwa maana ndiye muumba vyote hivyo.

Mungu amesema k**a wanadamu hawatabadilika na kuanza kumuabudu Mungu, baada ya Coronavirus inakuja ghadhabu kubwa zaidi ili kuwanyoosha zaidi.
😭😭😭😭

Soma Kolosai 3:5-8

Jamani waombolezaje tutubuuu na kuomboleza pengine Mungu anaweza akalegeza adhabu hiyo.

TUNATAKIWA KUFANYA MAOMBI YA REHEMA kwa sababu ya ghadhabu juu ya matukio yanayotukumba, ikiwa ni hili la Coronavirus na jingine ambalo alisema linakuja.

Mungu amesema dhambi imeelemea dunia. Mataifa makubwa yamekuwa yakijivuna kwa uchumi wao, mali zao na utajiri wao na kumuacha Mungu. Sasa Mungu amesema ameruhusu coronavirus k**a tu kuonyesha kuwa anayetakiwa kupewa Utukufu na kutukuzwa hapa Duniani ni mmoja tu ambaye ni Mungu Muumba wa Mbingu na nchi peke yake.

Tofauti na hapo watu wanapojisahau na maasi yanapoongozeka Mungu huachilia ghadhabu ili kuwanyoosha watu wamkumbuke kuwa yeye ndiye muumba wao. Kolosai 3:4-6

Na Mungu amesema baada ya hili anaachilia pigo lingine kubwa zaidi kupitia kushusha uchumi wa mataifa makubwa duniani ili watu wamrudie Yeye. (Mungu)

Sasa tunapoomba Maombi ya kuomboleza ya Rehema:

●Tamka dhambi tunazozijutia.

(Yeremia 8:6 - "Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, k**a farasi aendavyo kasi vitani")

Tunapotamka uovu tunaoutubia Mungu huruhusu damu ya Yesu iende mpaka katika uovu tuliotenda na kufuta na uovu unaondolewa kabisa.

Mfano:
Daudi aliomba rehema na kumwambia Mungu "je, sio mimi ndiye nilikosea na kufanya yaliyo maovu Sana?"
Ndipo Mungu alisikiliza Rehema hiyo na kuamuru malaika kurudisha upanga na kuiondoa tauni katika nchi ile.

Sasa; nafasi ya toba na kuomboleza na ya kila mmoja vile atakavyojisikia kutubu juu ya nchi na juu ya Dunia nzima.

Yoel 3:21 "Nami nitaitakasa damu ambayo sijaitakasa kwa maana Bwana ndiye akaaye sayuni"

Katika 2Nyakati 7:14 anasema tujinyenyekeze na kuomba na kumtafuta uso na kuziacha njia mbaya; atasikia toka Mbinguni na atatusamehe dhambi zetu na kuiponya nchi.

K**a wewe ni mwanaombi wa maombi ya kuomboleza wasiliana na mimi ili tupeane maelekezo zaidi. Tumia namba za simu 0754822287 au 0789960682.

Amen!

Kanisa,  Kanisa,  Kanisa!Kanisa jihadhari sana na watumishi ambao hawatendi sawasawa na  kweli ya Mungu. Ilikuwa alfajir...
11/04/2020

Kanisa, Kanisa, Kanisa!

Kanisa jihadhari sana na watumishi ambao hawatendi sawasawa na kweli ya Mungu.

Ilikuwa alfajiri, siku ya Jumatatu ya tarehe 06/03/2020 ambapo niliumia sana baada ya Mungu kunifunulia kuhusu watumishi wa Makanisa meeeengi makubwa na mengine madogo ndani na nje ya nchi kuwa Mungu yeye hawatambui katika Ufalme wake! Ni weeeengi mno jamani ila Mungu hajaniruhusu kuwataja kwa majina hadharani Ila ni watumishi wengi sana wamekengeuka.

Mungu amesema hawafuati maagizo yake bali wanafuata miungu ya dini zao wana viburi, hawana utii kabisa. Hivyo Mungu hawatambui katika ufalme wake!

Kwa Wachungaji, Mitume, Manabii, Maaskofu ,Wainjilisti, Waalimu
mnaojua mmepotea na kumuacha Mungu na mmefuata sauti zenu na si za Mungu; k**a mnataka kurejea katika Ufalme wake Mungu (ninawajua maana Mungu amenionesha Mara nyingi tu) mnaweza kunitafuta, niwape maelekezo ya kufanya ambayo Mungu anataka katika kuendelesha kazi yake ili msiendeshe kwa tamaa zenu kwa ajili ya kujitwalia Utukufu wenu.

Hamstahili kabisa kujitwalia utukufu wa Mungu. Mnamkasirisha Mungu na ghadhabu yake HAKUNA atakayeweza kustahimili. Na Mungu ameniambia Vita vinakuja juu ya wale wanaoenda kinyume naye.

Mti usiozaa matunda Mungu anakwenda kuukata sasa.
(Mathayo 3:10)

Somo: KUTAMBUA MAKOSA NA MAAMUZI YAKO BAADA YA KULITAMBUA .1:KUTAMBUA KOSA2.MAAMUZI YAKOBwana Yesu atukuzwe!Leo tujifunz...
10/03/2020

Somo: KUTAMBUA MAKOSA NA MAAMUZI YAKO BAADA YA KULITAMBUA .

1:KUTAMBUA KOSA
2.MAAMUZI YAKO

Bwana Yesu atukuzwe!

Leo tujifunze kuhusu mwanadamu unapotambua umekosea kwa Mungu, Unatakiwa ufanyeje?

Tutaangalia mifano ya watu waliokosea na kile walichoamua baada ya kugundua kuwa amekosea.

A.YUDA

Yuda msaliti alikuwa katika kundi la wanafunzi wa Yesu lakini kumbe alikuwa na roho ya usaliti ndani yake. Kusaliti ni kosa kubwa sana. Yuda alimsaliti Yesu kwa tamaa ya fedha tu. Akamsaliti Yesu ili ak**atwe na auwawe. (Yohana 13:2).

Yuda alipofanikisha usaliti wake, Yesu akak**atwa na kuteswa Kisha kuuwawa. Baada ya Yesu kufa ndipo Yuda akajuta sana akaamua kurudisha vile vipande 30 vya fedha akasema: "nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia". Mathayo 27:3

Kujutia kosa ni vizuri lakini baada ya kujua unatakiwa ufanyeje?

YUDA yeye aliamua kujinyonga na kufa badala ya kutubu na kuishi. Mathayo 27:3-5

Ukitenda kosa ukaona roho ya kifo, hapo ujue ni ushawishi wa shetani kutaka upotelee duniani. Ufe.!
Ila MUNGU anataka usife bali utubu na kugeuka na kuacha. Usijiue kwa kushindwa mtihani wa maisha au Jaribu gumu.Tambua kila jaribu lina njia ya kupokea na jaribu linampata mtu ili ajifunze; na kulishinda siyo kujiua!

Na shetani ndiye humtia mtu moyo wa usaliti. (Yohana 13:3)

Tuwe makini jamani; pia usimwamini mtu wakaribu yako aisee. Wanadamu hawaaminiki kwa asilimia mia .

Katika sehemu inayofuata tunaendelea kwa kumtazama Mtu wa pili ambaye ni MWANA MPOTEVU.

Asante sana na karibu GOD'S KINGDOM CHURCH BOKO -DAWASCO, Dar es Salaam.

SOMO: KUTAMBUA MBINU ZA SHETANIHalleluya!  Wana wa Mungu.Tunaendelea na somo letu la kuzitambua mbingu za shetani. Katik...
21/02/2020

SOMO: KUTAMBUA MBINU ZA SHETANI

Halleluya! Wana wa Mungu.

Tunaendelea na somo letu la kuzitambua mbingu za shetani. Katika sehemu hii tutaangalia Mbinu nyingine 2 ambazo shetani huzitumia.

Mbinu ya 4: Kuingia ndani ya Mtu Ili afanyike kuwa kwazo.

Tuangalie maandiko katika Mathayo 16:21-25 ambapo tunapata habari kuhusu Yesu Kristo alipoanza kuwaonya wanafunzi wake kuwa imempasa kwenda Yerusalemu na kupata Mateso mengi na kuuwawa; kwa wazee, wakuu, waandishi na makuhani ili kusudi litimie la kufa na siku ya tatu kufufuka.

Hapo tunaona Petro anaanza kuleta makwazo na kumwambia Yesu kuwa hayo, hasha, hayatatokea! Hapa tunaona vile Petro alitaka kuzuia kusudi la Mungu lisitimie kwa wanadamu.

Ndipo Yesu akamjibu Petro: "nenda nyuma yangu shetani, u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu Bali ya wanadamu"!

Hapo Yesu alimkemea shetani aliyekuwa amemuingia Petro. Lengo la Yesu lilikuwa kutii na kutimiza Mapenzi ya Mungu ya yeye kufa na kufufuka ili kutimiza maono ya Ufalme kuyaleta duniani K**a yalivyokusudiwa.

Usikubali shetani akutumie uwe kikwazo kwa mtu aliyebeba kusudi la Mungu!

Mbinu ya 5: Kuvuruga/kuwapepeta/kuwachanganya akili.

Katika kitabu cha Luka 22:24-34 tunapata habari za Yesu na wale mitume walipokuwa wameketi chakulani. Yesu akasema ole kwa atakayenisaliti. Baada ya kusema haya, mabishano yakaanza kuhusu "Ni Nani". Wakiuliza "Ni Nani" anayehesabiwa kuwa mkubwa.

Katika majibizano hayo Yesu akasema Simoni, Simoni tazama shetani amewataka ninyi awapepete, apate kuwapepeta K**a vile ngano. Lakini Yesu alimuombea imani yake isitindike (isiyumbe Iwe imara) ili naye atakapoongoka aimarishe ndugu zake!

Halafu tunaona Petro akijigamba kuwa: "niwapo nawe Yesu Ni tayari kwenda gerezani au hata kufa"!
Yesu, akitambua vurugu ya mawazoni mwake, akamwamwambia: "Petro; jogoo hatawika leo kabla wewe hujanikana Mara tatu ya kuwa hunijui"!

Hapo tuangalie kwanini shetani alimpepeta Petro? Jibu ni kwamba; ni kwakua alikuwa bado hajamwagiwa Roho Mtakatifu. Hivyo watu ambao hawana Roho Mtakatifu Ni rahisi kuchanganywa akili zao.

Tuepuke mbinu hizo za adui zisije kutusababisha tukawa Mbali na Mungu wetu!

Karibu sana kanisani; God's Kingdom Church, Boko, Dar es Salaam!

Tunakutakia siku njema na Mungu awe pamoja nawe!

SOMO: KUTAMBUA MBINU ZA SHETANI.Mpendwa msomaji, tunaendeleana somo la Kutambua mbinu  za shetani, Anazotumia kwa Wanada...
12/02/2020

SOMO: KUTAMBUA MBINU ZA SHETANI.

Mpendwa msomaji, tunaendeleana somo la Kutambua mbinu za shetani, Anazotumia kwa Wanadamu. Katika sehemu iliyopita tuliangalia mbinu ya KUJARIBU ambayo ndiyo aliitumia kwa Yesu Kristo.

Leo tunaangalia Mbinu ya 2. Mbinu hii ni:

HILA/KUUWA na kupoteza, kwa maana yeye ni sawa na Mwizi ambaye huja kuharibu!

- Kwa kutumia mbinu hii, yeye Shatani huja na mpango wa Kuiba ulichonacho, Kuua ama Kupoteza kabisa. Biblia inasema;
Mwivi haji ila Aibe,Achinje na Kuharibu. Yohana 10:10.

-Tuangalie shetani ndani ya Herode:

Baada ya kusikia Yesu amezaliwa, Herode alifadhaika sana na Yerusalem pia pamoja naye. Mathayo 2:3

Akaanza kutafuta habari mahali asipozaliwa Yesu, akaambiwa ni Betherehem ya Uyahudi maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii.

Herode alitaka kujua kwanini mahali Yesu alipozaliwa ili akaangamize kile kilicho ndani ya Yesu na aue kabisa. Hii ni hila ya Adui.

Herode alipoita Mamajusi kupata UHAKIKA pale Yesu alipoonekana na akawaagiza waulize kisha wamrudishie jibu; naye akajifanya eti anataka akamsujudie, huo ulikiwa ni uongo na ilikuwa ni Hila na mbinu ya shetani kutaka kumuua Yesu!

Mungu aliwaonya Mamajusi wasimrudie Herode, nao wakaenda zao kwa njia nyingine. Pamoja na mamajusi hao kuwa wachawi lakini Mungu aliweka utiisho na ulinzi juu ya mtoto Yesu. Mamajusi wakatii maongozi ya Mungu, wakayapuuza maneno ya Herode, mpaka Herode akafa ili tu mfalme Yesu atimize kusudi lililoko ndani yake.

MBINU YA 3

Mbinu ya tatu anayotumia ni KUMFUNGA MTU asifunguliwe.

Kufunga mtu asifunguliwe tunaweza kuona katika Mfano wa mwanamke mmoja ambapo Yesu alipokuwa akifundisha katika Sinagogi. Huyo mwanamke alikuwa na pepo wa udhaifu na alikuwa amepinda, hawezi kujinyoosha.

Yesu alipomwona akamwambia; "Umefungulia"! Yesu alipoweka mikono yake juu yake juu ya yule mwanamke, mwanamke akanyooka; akamtukuza Mungu.

Shetani, kupitia mkuu wa Sinagogi,
alikasirika kwa nini Yesu alimponya yule mwanamke siku ya Sabato.

Hapo tunaona vile adui shetani hataki mtu afunguliwe kutoka katika udhaifu wake kwa kutafutatafuta sababu k**a kisingizio tu; lakini Nia ya Shetani hakutaka yule mwanamke afungulie kutoka katika vifungo alivyokuwa navyo, maana shetani ndiye aliyemfunga.

Yesu hakutaka sheria zao za sabato zimfunge ndiyo maana alitii kile Mungu atakacho na alichoagizwa kutimiza katika ufalme wa Mungu duniani. Yesu Kristo alikuja ili aliharibu kazi zote za shetani.

Baada ya kumponya yule mwanamke, Yesu aliwaita wale watu kuwa ni wanafiki kwa maana walikuwa wanapindisha ukweli kwa kutaka kupindisha ukweli kuwa ni Heri kumfungua Mtu katika vifungo kuliko kumuacha akiteseka eti kwa Sababu ni siku ya sabato!

Hivyo tujifunze hapa kumtii Mungu na si yo shetani!

Somo: KUTAMBUA MBINU ZA SHETANIKatika somo hili tunakwenda Kujifunza na Kuzitambua mbinu za Ibilisi Shetani.Shetani ni n...
04/02/2020

Somo: KUTAMBUA MBINU ZA SHETANI

Katika somo hili tunakwenda Kujifunza na Kuzitambua mbinu za Ibilisi Shetani.

Shetani ni nani?

- Ni Roho chafu
- Ni Roho isiyo na mwili ambayo huwatumia wanadam katika kazi zake
- Ni Muasi aliasi Mbinguni.
(Ufunuo 12:7-9)
- Makao Yake Ni kuzimu
- Ni muongo (Ufunuo 12:9)

MBINU ZA SHETANI ANAZOTUMIA

1: KUSHAWISHI/KUJARIBU

Tutaangalia mfano wa jinsi alivyotaka kumjaribu Yesu akiwa nyikani. Habari hii iko katika kitabu cha Mathayo 4:1-11.

Katika habari hiyo tunaona Shetani akimwambia Yesu: "ikiwa ndiwe mwana wa Mungu amuru mawe haya yawe mkate".

Shetani alijua Yesu anao uwezo wa kuyageuza mawe yakawa mikate. Pamoja na kuwa na uwezo huo; lakini kwa nini Yesu amtii shetani?

Ndipo Yesu akamjibu: "imeandikwa Mtu hataishi kwa mkate tu Ila kwa kila neno litokalo kwa Mungu".

Shetani hakutaka kushindwa bali aliendelea tena kumshawishi Yesu. Akamchukua Yesu mpaka mji Mtakatifu akamuweka juu ya kinara Cha hekalu; akamwambia Yesu: "ukiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini kwa maana imeandikwa atakuagizia malaika zake na mikononi mwao watakuchukua usije ukajikwaa mguuni mwako katika jiwe".

Ni kweli imeandikwa hivyo katika Zaburi 91:10-12. Lakin Yesu hakutaka kumtii shetani. Ndipo akamjibu: "imeandikwa; usimjaribu Bwana Mungu wako".

Hapo si K**a Yesu hakujua kuwa akijitupa atadakwa na malaika Ila hakuona sababu ya yeye kumsikiliza na kumtii shetani; maana ukimsikiliza shetani na kumtii asemacho hapo unakuwa upo chini yake. Sasa Yesu alitambua wakumtii Ni Mungu tu.

Shetani akampa Yesu jaribu la tatu ambapo alimpeleka katika mlima mrefu, akamuonesha miliki zote za ulimwengu wa na fahari yake.

Akamwambia Yesu: "haya yote nitakupa ukianguka ukinisujudia"!
Yesu akamjibu akasema: "kwa maana imeandikwa, msujudie Bwana Mugu wako, umwabudu yeye peke yake"!

Hapo Yesu alikuwa anatambua kuwa fedha na dhahabu ni mali yake Mungu. Kwa hiyo anayestahili kusujudiwa Ni Mungu tu.

Hapo inabidi tujifunze katika vishawishi aletavyo shetani kwamba inabidi kujua namna ya kuvishinda; na tunavishinda kwa kutomtii na kwa pia neno la Mungu.

Anayetakiwa kumtii Ni Mungu tu. Hata katika ndoto, maono, sauti katika ulimwengu wa roho inabidi tutambue kuwa tunatakiwa kuwa macho na makini kumjibu shetani ajapo kwa ajili ya kukushawishi. Ukikubali katika ulimwengu wa roho, basi, katika ulimwengu wa mwili anakuwa amekuweza maana umemtii alipokutokea katika ndoto au katika maono na katika sauti. Ukikosea tu ukafuata anavyokushawishi, basi, unakuwa huna ujanja tena!
Ndio maana unatakaiwa kuwa makini Sana katika ndoto, maono na katika sauti za rohoni.

Amen!

Tutaendelea na kipengere cha Mbinu ya Pili ya Ibilisi anayoitumia katika kufanikisha kazi zake.

Kwa wakazi wa Dar es salam, tunakukaribisha katika Kanisa linalofahamika kwa jina GOD'S KINGDOM CHURCH, pale BOKO DAWASCO. Karibu uje usikilize Neno la Mungu la ukombozi.

Mwendelezo wa Somo linaloitwa:TAMBUA AINA YA  KIBALI CHAKO ILI UPATE USTAWI KATIKA MAMBO YOTE!Kuna aina kuu mbili za kib...
29/01/2020

Mwendelezo wa Somo linaloitwa:

TAMBUA AINA YA KIBALI CHAKO ILI UPATE USTAWI KATIKA MAMBO YOTE!

Kuna aina kuu mbili za kibali ambazo ni:

1.) Kibali cha Asili katika Ufalme wa Mungu na kibali Cha Asili katika Ufalme wa giza,
2.) Kibali cha Siri katika Ufalme wa Mungu na kibali Siri katika Ufalme wa giza.

Aina ya kwanza ya Kibali nilishaifafanua katika sehemu zilipopita, na sasa tunaingia katika aina ya pili:

KIBALI CHA SIRI CHA KIUNGU

Kibali hiki hutolewa kwa mtu mmoja tu kwenye familia ambaye Mungu humfanya k**a ndiye mkombozi wa Familia ambapo mtu huyo huwa ni mwenye kubeba jukumu zito katika familia yake ama katika ukoo. Yeye hujiona kwamba ndiye mwenye hilo jukumu kutokana na kugundua kuwa bila yeye kuyapigania mambo yanayohusu familia yake, basi, hakuna mwingine anayeweza kuona tatizo k**a aonavyo yeye.

Kibali hiki cha Siri cha Kiungu hutambuliwa katika wakati wa jambo ambalo Mungu anataka kulitenda. Mfano mzuri tunauona kwa Rahabu kahaba! Alikuwa na kibali hicho cha kiungu na alifanikiwa kuiokoa nyumba yake!

Yoshua 2:1-24, 12, ''BASI SASA NAWASIHI NIAPIENI KWA BWANA KWA KUWA NIMEWATENDEA HISANI, YA KWAMBA NINYI NANYI MTAITENDEA HISANI NYUMBA YA BABA YANGU; TENA NIPENI ALAMA YA UAMINIFU YA KWAMBA MTAWAPONYA HAI BABA YANGU NA MAMA YANGU, NA NDUGU ZANGU WANAUME NA WANAWAKE, NA VITU VYOTE WALIVYO NAVYO, NA KUTUOKOA ROHO ZETU NA KUFA.''

Kwa wakati huu tunaona Rahabu alionekana ana Kibali cha Siri cha Kiungu ambacho kilisababisha wokovu wa nyumba yote ya baba yake. Kabla haya yote hayajatokea habari za Rahabu hazikujulikana kwa maana hakuonekana k**a anaweza kustahili kuiletea wokovu nyumba yake kwa sababu alikuwa na sifa ya ukahaba.

Kibali hiki cha Siri kinamhusu mtu maalum sana katika ukoo ambaye ndiye pekee huandaliwa kuleta wokovu kwa familia yake. Ni mtu asiyejulikana na watu kwamba kupitia yeye kipo kibali cha Mungu juu ya nduguze. Na mtu huyo ni mtu anayepata nafasi ya mara moja; na huitumia vizuri kuleta wokovu kwa nduguze. Huwa hana ishara yeyote ya wazi bali hutambuliwa na Mungu kwamba alikusudiwa ndani ya wakati, kuhakikisha usalama unapatikana wenye wokovu katika jamii ya watu fulani.

Waamuz 1:24-25, ''HAO WAPELELEZI WALIMWONA MTU ATOKA KATIKA HUO MJI, WAKAMWAMBIA, TAFADHALI,UTUONYESHE MAINGILIO YA MJI HUU, NASI TUTAKUTENDEA MEMA''
"BASI AKAWAONYESHA MAINGILIO YA MJI, NAO WAKAUPIGA MJI HUO KWA MAKALI YA UPANGA; LAKINI HUYO MTU WALIMWACHA AENDE ZAKE, NA WATU WOTE WA JAMAA YAKE.''

Mtu huyu bila shaka hakudhaniwa, ndio mana hata jina lake halijapewa nafasi ya kujulikana. Hicho ni kibali cha Siri cha Mungu kwa ajili ya kusudi la kuokoa jamii ya watu fulani watakaosababisha kusudi la Kiungu kutimia kupitia wao. Watu hao hufanyika sehemu ya kukamilika kwa mpango huo!

Kibali hiki kipo kwenye nafasi kubwa ya kupokea wageni!! Mathayo 25:35, ''KWA MAANA NALIKUWA NA NJAA MKANIPA CHAKULA; NALIKUWA NA KIU MKANINYWESHA; NALIKUWA MGENI MKANIKARIBISHA"

SIFA ZA MTU MWENYE KIBALI CHA SIRI.

- Ana wepesi wa kuelewa siri za Mungu, na
- Hugundua kwa urahisi nia ya waovu. Hali hiyo inamsaidia kumlinda yeye mwenyewe miongoni mwa watu wabaya bila yeye mwenyewe kugundua!

Ni vigumu mno mwenye kibali hiki kujigundua kabla ya Wokovu wa Mungu kumfikia. Yaani ni Siri ya Mungu mwenyewe kumtengenezea mazingira ya kulitumikia kusudi lake; hata pasipo yeye mwenyewe kuelewa kwamba ni mwenye kibali cha Siri. Hii ni kwa kuwa utendaji wa Kibali hiki hujulikana katika tukio maalum ambalo mwenye Kibali cha Siri hujikuta akipigania kusudi la Mungu litimie na waovu wasifanikiwe katika hila zao.

Mwenye Kibali hiki cha Siri anaweza hata kufanana na waovu kitabia katika jamii yake. Hali hii humpa nafasi ya kuishi kwa uhuru bila kudhaniwa kwamba kuna wakati hatokuwa upande wao.
Mungu ndiye mwenye kuruhusu hali hiyo kwa lengo la kumlinda mtu huyo asitofautishwe na wabaya mpaka wakati wa kusudi utimie kikamilifu.

Wakati mwingine Mungu humfanya mtu mwenye kibali cha siri kuwa na ushujaa katikati ya jamii yake. Hali hiyo inafunua Kibali cha Siri kwa sehemu ndogo sana ili kuwatia wivu maadui za Mungu; lakini Mungu hamtambulishi kwamba ndiye atakayewaletea wokovu mkuu nduguze.

Jamii hii ya mashujaa wenye Kibali cha Siri, Mungu huwafanya mashujaa hao wasieleweke katikati ya ndugu zao na hata jamii yao na mfano mzuri tunauona kupitia Yeftha katika kitabu cha Waamuzi 11:1-11:

Historia ya Yeftha inatueleza kwamba alikuwa ni mtoto wa mwanamke kahaba; akaishi na nduguze wa baba mmoja lakini baadae wakamfukuza kuwa hataweza kurithi pamoja nao; kwa sababu yeye ni mtoto wa mwanamke mwingine na wao wamezaliwa kwa mama mmoja.

Ndipo Yeftha akawakimbia nduguze; akakaa katikati ya jamii ya watu mabaradhuli akaungana nao. Majira yalipofika ya Kibali cha Siri kufunuliwa; nduguze wakashindwa vita na wazee wa mji wakamfuata ili aje vitani apate kuwashindia kwa maana alikuwa ni shujaa; na mapatano yao walimpa nafasi ya kuwa mtawala wao:

Waamuzi 11:5-6:
''WAKAMWAMBIA YEFTHA, NJOO WEWE UWE KICHWA CHETU ILI TUPATE KUPIGANA NA WANA WA AMONI. YEFTHA AKAWAAMBIA WAZEE WA GILEADI, JE NINYI HAMKUNICHUKIA MIMI NA KUNIFUKUZA NITOKE KATIKA NYUMBA YA BABA YANGU?
''BASI KWANI KUNIJILIA HIVI SASA WAKATI MLIO KATIKA TAABU?"

Hivi ndivyo Mungu alikuwa ameificha Siri hiyo ya Kibali ndani ya Yeftha; kupigania utawala wa nduguze ili wakae katika usalama; baada ya watesi wao kuangamizwa na mwenye Kibali akatambuliwa katika nafasi ya ukuu; ambapo mwanzo haikuonekana nafasi hiyo.

K**a isingekuwa ni Kibali cha Siri bila shaka Yeftha angeuawa na nduguze na ukombozi wa Taifa lake usingepatikana.

KUTAMBULISHWA KWA MWENYE KIBALI CHA SIRI

Mungu huruhusu mabaya yaonekane katika jamii ya mtu mwenye kibali cha siri ili atakapomtambulisha awe na kitu cha kufanya ili kuufunua ukombozi uliokuwa ndani yake.

Amina!

Kwa mawasiliano zaidi ikiwa unahitaji ufafanuzi wa suala lolote hapa kwenye somo unaweza kupiga simu namba +255 694 269331 au kutuma ujumbe kwa njia ya Messenger.

Mungu wa Mbinguni azidi kukubariki unapoendelea kutembelea ukurasa huu.

SOMO: KIPAUMBELE CHENYE FAIDA- Kila mwanadamu anataka kile anachokifanya kwanza ndicho kimletee faida.- Kila mwanadamu a...
28/01/2020

SOMO: KIPAUMBELE CHENYE FAIDA

- Kila mwanadamu anataka kile anachokifanya kwanza ndicho kimletee faida.

- Kila mwanadamu anataka kuokoa muda.

- Kila mwanadamu anataka akianza kitu kisife. Yaani kiwe endelevu.

- Kila mwanadamu anataka asipoteze hela zake, nguvu zake na akili zake kwenye jambo ambalo hajui k**a litamfanikisha au la.

Shukrani na sifa ziende kwa Mungu, Baba Yetu wa Mbinguni kwa sababu:

1. Mungu mwenyewe hataki akuone unapoteza muda;
2. Hataki akuone unapoteza nguvu na kuwaza sana;
3. Hataki akuone unaanzisha kitu alafu kinakufa.

- Ndiyo maana Mungu akaamua suala la kutaka kujua nini uanze kukifanye duniani ili ufanikiwe, umuachie yeye ili akuambie kipi uanze kukifanya.

- Mungu ameamua suala la kipaumbele gani uwe nacho kwenye mipango yako binafsi, umuachie yeye akuambie, ili hicho kipaumbele anachokuambia kikifeli basi umlaumu yeye, maana yeye ndiye aliyekuleta duniani.

Kipaumbele ambacho Mungu anataka uwe nacho, ambacho ukikifanya kabla ya chochote kwenye maisha yako utafanikiwa ni hiki hapa katika:

Mathayo 6:33-34

■ 33: Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
■ 34: Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

K**a kipaumbele chako ilikua ni kununua gari kwanza; au kuwa na nyumba kwanza; au kusoma kwanza; au kuoa/kuolewa kwanza; au kununua kiwanja kwanza; Mungu anasema kipaumbele chake kwako ni wewe UTAFUTE KWANZA UFALME WAKE NA HAKI YAKE halafu hayo uliyokuwa umeyaweka k**a kipaumbele chako yatakujia yenyewe. Atakuzidishia!

Kwa kule kusema UTAFUTE maana yake ni nini?. Maana yake ni:

1. Hicho kinachotafutwa hakipo karibu na wewe, inabidi ukakitafute.
2. Kipo ila Kimefichwa
3. Jifunze ni kitu gani hicho inachobidi ukitafute, ili ukijue kwa uhakika
4. Fanya uchunguzi, ili kuwa na uhakika unachokitafuta ndiyo chenyewe.

Kwa sababu utakapopata huo Ufalme, utafanikiwa katika maisha ya kiroho na maisha ya kimwili pia. Pesa zitakuja kwako na kila ulichokuwa unakitamani kitakujia pia!

Wengi wetu tumetafuta Dini kwanza. Ndiyo maana wengine ni Wakristo hapa; wengine ni Waislam; wengine ni wafuasi wa dini ya kiBuddha; Wengine Wahindu n.k.

Bila kujua mtu unakuwa ukidhani kuwa ukiingia kwenye hiyo dini uliyopo ndiyo utapewa na Mungu mahitaji yako. Na hata sasa unaweza kuwa unashangaa ni miaka inapita lakini hizo pesa ulizokuwa unatarajia hujazishika!

Hii yote ni kwa sababu hujamuelewa Mungu alisema UTAFUTE NINI KWANZA, hakusema ukatafute Dini bali alisema UTAFUTE UFALME WAKE KWANZA.

Hizi dini haziwezi kutupatia mahitaji yetu. Bali tukiupata kwanza Ufalme hapo ndipo mengine yote tutazidishiwa. Kwa maneno mengine ni kusema Tutaongezewa!

Mimi naujua Ufalme wa Mungu. Nipo ndani yake. Nimeupata. Ila ilibidi niache vipaumbele vyangu vyote, ikiwemo dini yangu, elimu yangu, mahusiano na nikawekeza kwenye Ufalme na nikaupata. Sasa nazidishiwa yote niliyokua nayataka. Sina hofu na kesho yangu. Sina hofu na wachawi wala shetani kwa maana Ufalme nikiutumia sawa sawa unanihudumia kunikinga na hayo yote!

Ni maombi yangu kwamba Mungu wa Mbinguni atakusaidia ili uweze Kufanya kwanza kile ambacho ametuelekeza.

Amen!

Endelea kufuatilia masomo mahali hapa ambayo yatakusaidia kuujua huu Ufalme wa Mungu tunaozungumzia.

Kwa wale walioko Dar es Salaam unaweza kujumuika nasi pale Boko DAWASCO Kila siku za Alhamisi kuanzia saa Kumi jioni na Jumapili kuanzia saa Tatu asubuhi.

Kwa mawasiliano zaidi ikiwa unahitaji ufafanuzi wa suala lolote hapa kwenye somo unaweza kupiga simu namba +255 694 269331 au kutuma ujumbe kwa njia ya Messenger.

Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi Akubariki.

WATAMBUE 1: MKRISTO WA MWILINI 2: MKRISTO WA ROHONI3: MPAGANISEHEMU YA TATU (ya mwisho)MAPAGANI- Mpagani Ni mtu asiyeami...
26/01/2020

WATAMBUE 1: MKRISTO WA MWILINI 2: MKRISTO WA ROHONI
3: MPAGANI

SEHEMU YA TATU (ya mwisho)

MAPAGANI

- Mpagani Ni mtu asiyeamini kwa habari ya Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho mtakatifu.
Yawezekana anasikia Neno la Mungu Lakini Hana Imani nalo na Wala haamini kabisa.

- Mpagani anafananishwa na samaki aliye baharini lakini bado hajavunwa. Mtu wa namna hii ni sawa na kuwa bado yupo katika Giza.

- Mpagani hata hajui habari za kufunga na kuomba maana yupo katika Giza la dhambi na dhambi inakaa ndani yake mtu huyo anaitenda dhambi maana ndani yake halikai Neno jema.
Warumi 7:17-18

- Mpagani haamini Neno la Mungu wala kazi za Mungu na k**a tunavyojua asiye amini atahukumiwa. Na adhabu ya mpagani ni Hukumu. Marko 16:16 inasema aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa.
Unaweza kusoma pia Yohana 3:18.

- Mpagani ni Mtu anayempinga Mungu na kazi zake wala haamini K**a Mungu yupo ila mpagani anaamini miungu mingine ila sio Mungu wa Mbinguni.

K**a nilivyokwisha kueleza katika masomo yaliyotangulia kuwa watu wengi wanaitafsiri Neema vibaya: Wanatafsiri kuwa Neema Ni BAHATI ya Mtu Kuokoka. Hapana!
Neema siyo bahati k**a bahatinasibu. Ingekuwa hivyo basi kila Mtu angekuwa anastahili kuipata!

Lakini Neema ni kitendo cha Mtu kusikia Neno la Mungu na kuliamini Kisha kukubali kuokoka. Kwahiyo MPAGANI yeye hata Neno halijui wala hata akilisikia haliamini kabisa, kwa sababu hataki kuliamini kwa kuwa haamini Uwepo wa Mungu Baba muumba wa Mbingu na nchi.

Namna ya kuondoka kutoka Upagani ni mtu mwenyewe kuamua KUAMINI na ningependa wapagani wote, k**a kuna ye yote anasoma hapa, aamini leo kuwa Yupo
Mungu muumba wa Mbingu na nchi ambaye ndiye aliyewaumba hata wao na ndiye muumba wa vyote vilivyoko Duniani, katika nchi kavu na katika Bahari.

Mungu hapendizwi na watu wasiomuamini yeye. Kwa maana k**a hawamuamini wanachokingoja ni hukumu. Na hukumu yao ipo. Yohana 3:18

Bali wakimuamini na kumkubali atawapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu sawa sawa na Neno lake katika Yohana 1:12 lisemalo:

"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake"

Amina!

WATAMBUE 1: MKRISTO WA MWILINI 2: MKRISTO WA ROHONI3: MPAGANISEHEMU YA PILIMKRISTO WA ROHONISehemu hii ya somo inahusu M...
20/01/2020

WATAMBUE 1: MKRISTO WA MWILINI 2: MKRISTO WA ROHONI
3: MPAGANI

SEHEMU YA PILI

MKRISTO WA ROHONI

Sehemu hii ya somo inahusu Mkristo wa Rohoni, yaani ni yule Mkristo wa kweli.

SIFA ZA MKRISTO MKRISTO WA ROHONI

- Ana Roho Saba za Mungu ambazo ni:

i).Roho wa Maarifa
ii).Roho wa Uweza
iii).Roho wa Bwana
iv).Roho wa Hekima
v).Roho wa Ufahamu
vi).Roho wa Ushauri
vii).Roho wa Kumcha Bwana

Mkristo wa ROHONI, ambaye ndiye ana hizo Roho, tutaziona kwenye masomo yanayoendelea, hizi Roho humuwezesha kuwa Ni Mkristo Mteule ambaye maisha yake kwa wiki yanakuwa ni ya Kufunga + Kusoma Neno + na Kuomba.

Tukumbuke haki Yetu inatakiwa kuizidi haki ya Mfarisayo anayefunga Mara 2 kwa Juma. Mathayo 5:20.

- Mkristo wa Rohoni anausulubisha mwili; yaani anakuwa Mtu wa rohoni muda wote. Galatia 5:24

Mkristo wa ROHONI ni Yule anayejikana mwiili kwa kuusulubisha. Mfano hata siku ya kusimama madhabahuni kuhubiri Neno au kuongoza ibada ya sifa anatakiwa awe rohoni awe katika maombi ya mfungo, Yeremia 36:6, ili asiwalishe watu makapi ya mwilini maana afya ya mwili Ni chakula na afya ya Roho Ni Maombi ya kufunga na kusoma Neno la Mungu. Kwa hiyo ili Roho ashibe na awe na nguvu ni lazima umshibishe mara nyingi wa wiki.

Siku zote mwili hushindana na Roho sasa mwili ukiishinda Roho Basi umekufa kiroho. Chagua ufe kiroho au usulubishe mwili ili uwe hai kiroho.

Na siku zote mwili hata uulishe chakula vipi haunaga shukrani mpaka kuna vyakula vingine madakatari wanakataza usile baada ya kupata magonjwa. Sasa je, Raha ya chakula i wapi?

- Mkristo wa rohoni ameagizwa kumzidi farisayo katika haki. Luka 18:12

- Tunapousulubisha mwili kea kufunga tunashirikia mateso ya Kristo galatia 5:24

- Mkristo wa ROHONI anaongozwa na Roho na siyo mwili. Galatia 5:25.

Ukiona mwili unakuongaza na umeutii basi, jua hapo Roho hayupo inatakiwa usikilize Roho inakuongoza kufanya nini katika Mungu.

Kwahiyo kiwango cha kwanza unapoanza kutaka kufunga na kuomba unatakiwa uzidi zile siku za Farisayo alizofunga hiki. Ni kiwango Cha kwanza. Maana siku zote mwili Ni mwili wa dhambi hauna Nia nzuri na Roho. Warumi 7:23-25.

Na kiwango kikubwa cha Mtu kufunga na kuomba na kusoma Neno hapo hakuna ajuaye kipimo cha kiwango kikubwa Ila ukimwomba Roho Mtakatifu atatujulisha kiwango kikubwa cha kufunga na kuomba. Atakuongoza namna ya kufunga ili uwe kiwango cha juu chenye nguvu za Mungu na uwezo wa KiMungu.

Sehemu inayofuata tutamalizia na
Kuhusu MPAGANI ni mtu wa Namna gani.

Ikiwa una swali usisite kuuliza katika sehemu ya "comments"

Address

Boko
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when God's Kingdom Church In the World posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to God's Kingdom Church In the World:

Share