29/05/2023
πππππππ
*ππΏNENO LA MAARIFA NA UZIMA SIKU YA LEO JUMATATU TAREHE 29 MEI 2023*
πππππππ
*π―SOMO LA LEO - TUNAPOADHIMISHA PENTEKOSTEJIKUMBUSHE KWAMBA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU NI BURE - UKIONA KUNA KUUZIANA UPAKO WA MAJI/MAFUTA N.K UJUE UMEPIGWA NA KITU KIZITO- AMKA ILINDE IMANI YAKO NA KANISA AMBALO LIMENUNULIWA KWA DAMU YA THAMANIπ―*
*(Matendo ya Mitume 8:14-20)*
[14]Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
[15]ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
[16]kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.
[17]Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
[18]Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
[19]Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.
[20]Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.
*βTAFAKARI YA LEOβ*
_*Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. (Matendo ya Mitume 20:28)*_
*βANZA SIKU NA BWANAβ*
_Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. (Mathayo 10:8)_
πππππππ