Wanaume Waombaji & Wanawake Waombolezaji

Wanaume Waombaji & Wanawake Waombolezaji Kuutafuta uso wa Mungu kwa viwango vya kipekee na kusaidia wengine kumtafuta na kumjua Mungu.

MAOMBI DHIDI YA ROHO ZA MAUTI ZILIZOACHILIWA JUU YAKO AU WATU WAKO Kuna uhusiano gani kati ya mauti na visasi?Kazi ya vi...
31/05/2026

MAOMBI DHIDI YA ROHO ZA MAUTI ZILIZOACHILIWA JUU YAKO AU WATU WAKO

Kuna uhusiano gani kati ya mauti na visasi?

Kazi ya visasi ya kwanza ni kuharibu. Visasi vinabeba mashambulizi ambayo yanaachia mauti au roho zimgine haribifu kupata uhalali wa kushambulia. Ni mtangulizi war oho za uharibifu kwenye maisha ya mtu. Ndio maana mtu anapookoka na kuacha dhambi roho hizi humshambulia ili kumpunguza nguvu ya kujilinda na kuwa na kibali na ulinzi wa Mungu(Ufu 12:7-15).

Visasi huja k**a mishale. Ni mishale ya moto. Ukiwa haujavikwa silaha za Mungu vizuri ni rahisi sana kuuumiza yaaani kukuunguza k**a vile mtu aliyechomwa moto mwilini. Ndio maana ni muhimu sana k**a mwana wa Mungu na muombaji au muombolezaji kuzijua silaha za vita na kuweza kuzitumia, yaaani kuvaa mavazi ya kijeshi k**a katika ulimwengu wa mwili (Efe 6:10-18).

Watu wengi wanashindwa kuikwepa na/au kuizima mishale ya moto ya yule muovu sababu hawana silaha sahihi ambayo ni ngao ya imani(Ebr 6:16). Ngao ya imani humsaidia mtu kuweza kukwepa mishale ya moto inayorushwa pabnde zote na adui na majeshi yake yote na mawakala wake usiku na mchana wanapofanya vita na watakatifu. Unapokosa imani maana yake hakuna namna utaweza kuishinda hii mishale, na ikikupata itakuletea uharibifu mkubwa kwani utakuwa upo dhaifu sana rohoni kiasi kwamba mashambulizi mengine yanapita kwa wepesi.

Kwanini adui anatumia sana mauti?

Mauti inamuondoa mtu kwenye nafasi yake.

Watu wengi hawajui namna ya kupambana na mauti.
Ni kusudio la kukufisha ili ukatumikie ufalme wake muda uliobakia wa kuishi duniani. Maana yake, unachukuliwa kuitumikia kuzimu kwa muda uliobakia uliopaswa kuishi duniani. Watu wanaokuzunguka wanaona umekufa na unazikwa lakini hujafa kwa maana halisi, bali tu umeamishwa toka ufalme wa mwili Kwenda rohoni kwenye ufalme wa giza.

Unapokosa imani unakuwa k**a wimbi la Bahari linalopelekwa huku na huku na inapotokea hivyo Mungu hawezi kukusaidia kwasababu huamini anaweza kukusaidia(Yak1:6-8). Imani yako ndiyo inayokupa ulinzi na majibu ya maombi yako, na hiki ndicho Yesu alikuwa akisisitiza katika mafundisho yake. Adui akikuweza katika imani amekuweza kwenye vyote na wewew ni rahisi kutumiwa na ufalme wa giza kuliko unavyofikiri na hapa ndipo mauti hupata nguvu juu ya mtu.

Ukiona mauti imeachiliwa na ikapita kwa mtu anayeliitia jina la BWANA, jua mtu huyo imani yake ni baridi au vuguvugu na Mungu amemtapika. Mungu akikutapika maana yake unakosa ulinzi unaohitajika (Ufu 3:15-16). Mungu akikutapika ulinzi wake unakuondokea hata k**a bado unasali na mambo yako mengine yanaenda k**a ilivyokuwa kwa Sauli (1Sam 15:10-11,22-29).

Jambo linguine linaoumiza watu wengi ni kwenda wa BWANA pasipo kuwa wamejitakasa sana kwa ajili ya miunganiko waliyokuwa nayo na miungu mingine. Kufanyishwa sala ya toba ni jambo moja, lakini kuvikataa vitu ulivyoviabudu na kutaka Mungu kwa Kristo Yesu ndiye awe Mungu pekee ni jambo jingine. Unapokuwa na vinyago ufalme wa giza unakuwa na mamlaka juu yako na wanaweza kukushambulia wakati wowote. Wakumbuke wan awa Israeli walivyopigwa walipoenda kupigana na Ai kwasababu ya vinyago walivyokuwa wameshika na kuvilinganisha na Mungu aliye hai(Yos 7:1-26). Mungu ni Mungu mwenye wivu, hawezi kukupigania ukiwa umeshikilia miungu mingine(K*t 20:5; K*t 34:14; Kumb 4:24; Kumb 5:9; Kumb 6:15; Yos 24.19; Nah 1:2).

Hapa adui anapata haki ya kuwashtaki kwa Mungu kwa uhalali na chochote atakachoomba kipite, kitapita kwakuwa kuna uhalali kamilifu mkumbuke Ayubu alivyojaribiwa(Ayu 2).Mkumbuke pia Raheli aliyeiba na kuificha miungu ya baba yake. Hivyo, ili kuwa salama ni lazima kutubu kwa kina ili kujinasua kwenye vifungo hivi.
Kushindwa kusamehe na kuachilia ni jambo jingine linaloleta shida kwa watu wengi sana wanaoliitia jina la BWANA. Mungu katika Kristo Yesu yupo wazi kabisa juu ya kushindwa kusamehe. K**a huwezi kusamehe wengine hata ule msamaha aliokupa wewe unaondolewa, ukiondolewa maana yake nguvu za giza zinapata mamlaka ya kukutesa. Hili ni eneo la kuwa nalo makini sana na ni mlango mkubwa wa visasi na mauti(Mt 6:14-15; 2Sam13:1-32).

HASIRA. Mlango mwingine mbaya sana na mwepesi adui anautumia kwa watu wa Mungu. Kuipa hasira makazi kwenye moyo na fikra zako ni hatari sana kuliko unavyoweza kufikiri. Hasira hupofusha macho, hufanya moyo wako kutoweza kumkarbia BWANA, inakukea ukuta na mbaya zaidi inaondoa ulinzi wa Mungu unaokuzunguka, Ni hatari mno na watu wengi hawajui kwanini wanashambuliwa hasa na magonjwa yanayosumbua kuponyeka: Hasira. Ni lazima kuweza kudhibiti hasira zako ili kuwa salama (Mt 5:22; Gal 5:20; Efe 2:3; Efe 4:26-31; Kol 3:8; Yak1:20).

Ukiona umekosewa na moyo wako na fikra zako zinapanga kisasi, jua huna neema ya Mungu ndani mwako na unahatari kubwa ya kushambuliwa. Mwana wa Mungu unapaswa kuweza kusamehe wanaokuudhi na kuwaombea sio kuwalaani au kutaka kuwarudishia uovu kwa uovu bali unarudisha uovu kwa wema k**a Yesu ili kisasi kiwe juu ya BWANA na si juu yako (Rum12:14; Mt 5:43-48).

KURUDIA MAISHA YA DHAMBI BAADA YA WOKOVU BILA MAJUTO WALA KUJALI. Mlango mwingine mkubwa unaofanya watu wengi kufa mapema. Japokuwa hapa, mara nyingi Mungu huwachukua watu hawa kaba neema haijawaondoka kabisa(2Pet 2:20-22).

KUKOSA UTII KWA MUNGU. Kukosa utii ni dhambi kubwa sana mbele za Mungu, ndiyo iliyomkosesha Adamu na Hawa lakini pia ndio iliyomnyang’anya Sauli ufalme. Dhambi hii inafananishwa na dhambi ya uchawi na vinyago(1Sam 15: 22-23). K**a dhambi hii inafananishwa na uchawi maana yake unautumikia ufalme wa giza kiuhalali pasipo kujua na wanaweza wakakufanyia chochote kwa haki na mbingu zisifanye chochote. Isipokuwa Roho Mtakatifu hutoa maonyo kwa ndoto au neno au maarifa kabla uharibifu haujafanikiwa. Mauti inaweza kupita kwa kukosa utii.

MAAGANO AMBAYO MWANAFAMILIA AMEWAFUNGA WATU WAKE. Hapa ni pale mtu wa karibu kwenye familia anakuwa ametoa sadaka ya mauti juu ya watu wake kwasababu mbalimbali lakini hasa utajiri(Amu11:30-39). Maagano ya mababu na mabibi(maagano ya kiukoo) ambayo yameachwa kufanyika lakini hakuna mtu aliyetubia maagano haya na sadaka zilizokuwa zinatolewa na vitu vimeachwa tu kienyeji na hivyo kuwa na nguvu ya kudai watu wa ukoo husika(2 Fal 17:24-28; K*t 20:4-5).

KUONEA MJANE NA YATIMA ni laana ambayo inaweza kumtafuna mtu na uzao wake baada yake. Hata k**a wao wenyewe hawajui kilichotokea nyuma (K*t 22:22-24).

Visasi vipo unapokuwa mtu muombaji na unamtafuta BWANA kwa bidii na kutaka kubadilisha hali unazopitia au wanazopitia watu wako. Shida ni ulinzi kiasi gani ulionao ili hii mishale isikuguse, au hata ikikugusa iwe kidogo sana wala isikuletee shida.

Inawezekana milango iliyofunguliwa ikaleta shida? Ndio. Mlango wowote ukiwa wazi adui atautumia huo kukuwapiga na akiwa na uhalali atashinda. Ndio maana ni muhimu sana kuwa makini na njia zenu kuhakikisha humtendi BWANA dhambi au kuinua hati ya mashtaka juu yako. Inapotokea hati ya mashtaka imeinuka, kimbilia kiti cha rehema mara moja na kutubu.

Hivyo, ukiona roho za mauti zinaifuatilia sana familia yako au ukoo wenu chunguza kujua chanzo chake ili ujue namna ya kushugulika na kufunga mlango huo. Usiposhugulika na mzizi wa tatizo, tatizo haliwezi kuisha kwa wepesi. Hapa toba ya kina inaitajika ili BWANA arehemu na damu yake ikapate kutaka uovu wote na kumpa BWANA uhalali wa kuwatetea.

Heri ya Krismasi!Huduma ya Wanaumbe Wombaji na Wanawake Waombolezaji inakutakia heri katika siku hii kuu ya adhimisho la...
25/12/2025

Heri ya Krismasi!

Huduma ya Wanaumbe Wombaji na Wanawake Waombolezaji inakutakia heri katika siku hii kuu ya adhimisho la kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wa Ulimwengu.

"Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia" - LUKA 2:14.

Tuakupenda sana.

Address

Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wanaume Waombaji & Wanawake Waombolezaji posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share