26/10/2025
Nira ni kifaa kinachotumiwa kumshurutisha mnyama atii kwa lazima. Vifaa vingine vinavyotumika kutiisha kwa lazima ni pamoja na kulabu, na hatamu.
Kulabu na hatamu hufungwa kwanye pua na shingo.
Bwana Yesu alitumia mfano wa vifaa hivyo kuonyesha vile mtu anavyotakiwa kusaidiwa kutii. Pia, mitume wa Bwana Yesu waliichukulia ile torati ya Musa k**a nira. Kwa sababu inaulazima. Ni lazima mtu aitii torati. Asiyeitii torati huadhibiwa.
Lakini Bwana Yesu alileta nira nyingine tofauti na hatamu na kulabu na nira ya Musa. Aliielezea nira hiyo kuwa ni laini, inayomsaidia mtu kutii, badala ya kumlazimisha. Nira ya Bwana Yesu inamfanya mtu apende kutii, moja kwa moja toka moyoni mwake.
Tuendelee kujifunza...