Ubungo Christian Centre - TAG

Ubungo Christian Centre - TAG Karibu katika ukurasa wa chakula cha kiroho (Neno la Mungu) kutoka Ubungo TAG.

03/06/2026

Karibu Katika Ibada Zetu Kupitia Njia ya Mtandao Tutazame Live You Tube Channel Yetu (Ubungo Christian Centre)..

Huduma za Maombezi kwa Wenye Shida na Matatizo Mbalimbali ni Bure Kabisa

30/05/2026

πŸ”₯ MKUTANO MKUBWA WA INJILI πŸ”₯

Kanisa la TAG. Ubungo linakukaribisha katika siku nne za nguvu za maombi, ibada, neno la Mungu na uamsho wa kiroho.

πŸ“… Tarehe: 27 – 30 Mei 2026
πŸ“ Mahali: Ubungo Maziwa
🏫 Ukumbi: Shule ya Sekondari Excellence/Ubungo Modern
πŸ•˜ Muda: Saa 9:00 Alasiri hadi Saa 12:00 Jioni

Huduma zitatolewa na watumishi wa Mungu:
🎀 Mch. Godfrey Mulangwa
🎀 Ev. Sayuni Haule
🎀 Ev. Devotha Mbasa

β€œNjooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” β€” Mathayo 11:28

Usikose nafasi ya kukutana na Mungu, kupata faraja, uponyaji na kufanywa upya katika uwepo wake.

πŸ“ž Mawasiliano: +255 755 887 070 / +255 788 952 400

30/05/2026
Couples Refresher 2026 πŸ’œβœ¨Ni muda wa kufufua upendo na kuimarisha ndoa zetu! πŸ’‘πŸ”₯Jiunge nasi katika Wiki ya Idara ya CMF Ki...
03/05/2026

Couples Refresher 2026 πŸ’œβœ¨
Ni muda wa kufufua upendo na kuimarisha ndoa zetu! πŸ’‘πŸ”₯

Jiunge nasi katika Wiki ya Idara ya CMF Kitaifa, tukijifunza na kujengwa pamoja kupitia mafundisho yenye nguvu na ushuhuda halisi. πŸ™Œ

πŸ—“ Jumapili, 03 May 2026
⏰ Saa 9:00 Mchana – Saa 12 Jioni
πŸ“ TAG Ubungo

01/05/2026

ELIMU YA MADHABAHU
Tafsiri: Madhabahu ni daraja linalounganisha na kupitisha vitu kutoka ulimwengu wa roho kwenda ulimwengu wa mwili.
A. Aina za Madhabahu
β€’ Madhabahu ya Nuru: Ni ya Mungu; huleta mambo yote mema na baraka.
β€’ Madhabahu ya Giza: Ni ya shetani; huleta uharibifu na mambo yote mabaya.
β€’ Mifano ya Biblia: Nuhu alijenga madhabahu (Mwa 8:20) na Yoshua pia alijenga madhabahu (Josh 8:30).

NGUZO 5 ILI MADHABAHU IKAMILIKE
1. Mungu wa Madhabahu
β€’ Upande wa Nuru: Ni Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
β€’ Upande wa Giza: Ni mashetani na waganga.
2. Kuhani wa Madhabahu
β€’ Huyu ni msimamizi au mpatanishi anayehudumu kwenye hiyo madhabahu.
3. Washiriki wa Madhabahu
β€’ Upande wa Nuru: Maana yake ni jeshi la Malaika wanaofanya kazi pamoja na madhabahu hiyo.
β€’ Upande wa Giza: Ni mawakala na nguvu za giza zinazohusika.
4. Kafara au Sadaka ya Damu
β€’ Upande wa Nuru: Ni Damu ya Yesu iliyomwagika mara moja tu na ina nguvu ya milele.
β€’ Upande wa Giza: Zipo za aina tatu; damu ya ndege, damu ya wanyama, au damu ya wanadamu.
5. Nguvu ya Madhabahu
β€’ Upande wa Nuru: Nguvu hii inatoka kwenye madhabahu ya nuru (kwa Mungu).
β€’ Upande wa Giza: Nguvu hii inatokana na maunganisho ya madhabahu zote za upande wa giza.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ubungo Christian Centre - TAG posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ubungo Christian Centre - TAG:

Share