Mahubiri

Mahubiri Ukurasa huu wa Facebook ni kwa ajili ya neno la Mungu.

Inakusanya mahubiri ya kutoka kwa watumishi mbalimbali, kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu wa Mungu.

26/04/2026

Watoto wa kiume wametoka kwenye msitari. Hawapo tena k**a vichwa vya baadaye vya nyumba zao. Tunahitaji mabadiliko, ama sivyo, hatutakuwa tena na watu wa kuendesha taifa na kanisa.

๐™‰๐™„๐˜ฟ๐™ƒ๐˜ผ๐™ˆ๐™, ๐™๐™‹๐™€๐™‰๐˜ฟ๐™Š ๐™‰๐˜ผ ๐™ˆ๐˜ผ๐™๐™€๐™‰๐˜ฟ๐™Š  ๐™”๐˜ผ ๐™†๐™’๐˜ผ๐™‰๐™•๐˜ผ๐“œ๐“ฝ๐“พ๐“ถ๐“ฒ๐“ผ๐“ฑ๐“ฒ:๐“™๐“ฎ๐“ท๐“ผ๐“ฎ๐“ท ๐“ข๐“ฑ๐“พ๐“ถ๐“ชUfunuo 2:4-5Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upen...
14/04/2026

๐™‰๐™„๐˜ฟ๐™ƒ๐˜ผ๐™ˆ๐™, ๐™๐™‹๐™€๐™‰๐˜ฟ๐™Š ๐™‰๐˜ผ ๐™ˆ๐˜ผ๐™๐™€๐™‰๐˜ฟ๐™Š ๐™”๐˜ผ ๐™†๐™’๐˜ผ๐™‰๐™•๐˜ผ
๐“œ๐“ฝ๐“พ๐“ถ๐“ฒ๐“ผ๐“ฑ๐“ฒ:๐“™๐“ฎ๐“ท๐“ผ๐“ฎ๐“ท ๐“ข๐“ฑ๐“พ๐“ถ๐“ช

Ufunuo 2:4-5
Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

MAHUBIRI
Nidhamu ya kwanza ni ya kitu cha msingi ambacho kinatokana na mtu mwenyewe na hii ni nidhamu binafsi (self-discipline), ambayo ina uwezo wa kujitawala, kujizuia, na kufanya maamuzi sahihi hata wakati wa mgumu ili kufikia malengo ya muda mrefu. Inahusisha kusimamia hisia, muda, na tabia zako ili kuepuka visingizio na kuleta mafanikio.

Kukosa nidhamu binafsi ndiko chanzo kikubwa cha kushindwa maishani.

Nidhamu ya kwanza inatakiwa Kujidhibiti. Ni uwezo wa kufuata sheria au maagizo uliyojiwekea wewe mwenyewe ili kukuza tabia njema, au nidhamu ya kufanya kazi yako, au biashara yako ili ufikie malengo yako, uliyojiwekea mwenyewe. Hii inatakiwa ujidhibiti.

Nidhamu ya kwanza inahitaji Kuvumilia Magumu: Nidhamu inahitaji utayari wa kufanya kazi ngumu, ukijua kuwa mambo mengi huanza kwa ugumu kabla ya kuwa rahisi.

Nidhamu ya kwanza na tabia zinazotokana na hii k**a vile -nidhamu ya kihisia,
- nidhamu ya kifedha,
-Nidhamu ya kujiendeleza,
-Nidhamu ya mahusiano na watu.

Kimsingi, nidhamu ya kwanza ni uwezo wako wa kuamuru akili na mwili wako kufanya kile unachopaswa kufanywa, na si kile unachojisikia kufanya.

Usiache nidhamu ya kwanza, ndiyo itakungoza kwenye maendeleo yako.

Unamkuta mtu anaacha nidhamu ya kwanza. Watu watakuacha kwenye biashara, kanisani, kazi na hata mambo ya kijamii.

Nidhamu.ya kwanza
- itakufungulia milango
- inadumisha fursa
- inadumisha nafasi uliyokuwa nayo
- itakufanya uwe na uwezo wa kuendelea kwenye kazi

Nidhamu hii inatakiwa kwenye huduma, biashara, ndoa, masomo yako, kazi, jumuiya, mikataba, nk

Nitoe mfano mmoja. Sisi tuna vikoba, lakini kikoba chetu, hatujakiwekea sheria ili watu wawe na nidhamu ya kuleta marejesho kwa wakati.

Wanachama wameachwa ili watumie nidhamu waliyo nayo ya kwanza, ukitoka kwenye hiyo nidhamu kule mwishoni mwingine akichukua 1,000,000 wewe utaisha kuchuku 20,000.

Kwenye vile vya mtaani, watu wanalazimishwa kuwa na nidhamu. Usipoleta rejesho kwa muda, kuna adhabu, ukichelewa kwenye kikao adhabu, usipoudhuria kabisa kwa kutoa udhuru ulipia mawazo ya watu wengine, Hizi adhabu zinamfanya mtu kujidhibiti na kuieshimu nidhamu yake ndani ya vicoba.

Jiulize nidhamu.yako ya kwanza ipoje?
Kijana akiwa na wazazi wake, unafundishwa nidhamu mzuri, ya kwenda kanisani, kutoa sadaka, kufanya kazi, kufanya usafi wa mwili wake, kutoingia kwenye mambo ya kukuletea urahibu k**a kuvuta sigara, kunywa pombe, kuvuta bangi, kutafuta wanaume, kuvaa vizuri, nk. Ngoja akakae mwenyewe, anakuwa mchafu, hafanyi kazi, aendi kanisani, anaanza kunywa pombe, anavuta, nk. Anaacha nidhamu ya kwanza, anaingia kwenye mambo ya kumpotosha.

Ukikuta kwenye ndoa watu wakioana, ule upendo wa kwanza ni wa kimapenzi. Kila wakati ni lazima mume au mke ajue mwingine yupo wapi. Wakitoka wanatoka wote. Wakitembea wamekumbatiana. Wakati mwingine wanavaa nguo zinazofanana. Hii yote ni kwa sababu ya upendo wa kwanza au nidhamu ya kwanza. Ipite miaka mitano, unaweza kukuta kila mtu na lwake.

Ukiacha nidhamu ya kwanza, sahau kufanikiwa. Nidhamu ya kwanza ikipotea kuna tabia mbaya zinaonekana kwa watu. Akikuchelewesha, anaanza kukulaumu fanya haraka tunachelewa ataondoka mwenyewe kanisani, utasikia unanichelewesha.vMwingine wakati mwingine anakwenda kazini, anarudi asubuhi,wakati mwanzo alikuwa akirudi mapema.

Kwenye biashara na kazi ni hivyo hivyo. Ebu fikiria unapoanza biashara senti haipiti pembeni au unapoanza kazi nidhamu unayokuwa nayo, ngoja uzoee, hata boso aliyekupa kazi unaanza kumsema. Haa kazi gani hii.

Roho ya ushujaa inatakiwa ili urudi kwenye nidhamu ya kwanza. Roho ya ushujaa ni hatua ya mwisho ya udhihirisho wa Mungu. Joshua aliambiwa uwe hodari na moyo wa ushujaa,usiogope wala kuona hofu.

Yoshua 1:9

Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.

Hofu ni mlango wa kukuondoa kwenye nidhamu ya kwanza na kukurudisha nyuma. Hofu ni bidhaa inayoweza kuuziwa au kubebeshwa mtu. Kuijua siyo shida bali ulishabebeshwa na wewe ukaikubali.

Watu wanakuzulia hofu ili ushindwa au ukate tamaa. Kuna watu hawajaolewa au kuoa kwa sababu ya hofu. Hawaazishi biashara kwa sababu ya hofu. Hawaokoki kwa sababu ya hofu, na watu watanionaje.

Thamani ya fedha kwa mtu wa Mungu aiwezi kununua hofu.

"Kuna mtu nilisikia akisema hakuna kitu nafanya kinafanikiwa. Nikamuliza hili shati na suruale uliyovaa, umevaa wewe mwenyewe au ulivalishwa. Akasema nimevaa mwenyewe. K**a umevaa basi na vingine unaweza kuvivaa.

Kataa hofu. Huko nje hofu ni bidhaa waambie mimi sichukui. Ukiona mtu amefanikiwa usifikiri ana uwezo sana bali ameshinda hofu. Inua dhamani yako kwenye viwango ambavyo havitanunulia hofu.

Thamini yako ni nini, ni imani yako, uwezo wako kwa Mungu,nk.

Agano la Mungu ni bidhaa inayotufanya tusibebe hofu.

Kuna mtu alisema pembe tatu za tai. Mabawa, mdomo na kucha za tai na macho yake. Macho yake yanaweza kuona hadi ndani ya maji. Tunatakiwa tuwe na macho ya tai yaweze kuona mbali, maisha ya baadaye. Tai kipofu hafai.

Hatakiwi tuone hapa kwenye maisha bali uone mbali. Ukiona karibu wewe hufai.

Mwana wa Mungu hofu kwake ni bidhaa mbovu. Mwombe Mungu afungue mbawa zetu kwa Jina la Yesu. Lazima uwe hodari na kuwa shujaa. Kumbuka haijalishi utakwenda mbali kiasi gani hofu inakunyemelea. Upendo wa biashara unageuka. Hofu ni k**a pumzi unakuzunguka. Yesu alipotakiwa kuokoa ulimwengu alitiwa kwenye mikono ya wanyanganyi. Alisema kuwa kikombe hiki kiniepuke. Hofu ni asili ya maisha hata Yesu alikuwa nayo na uwe mwenye nguvu na hodari ndipo utakaposhinda.

Bibilia inasema umeacha upendo wako wa kwanza. Upendo ni vitendo siyo msisimko.

Usogope huko nje ukiona mambo ya kutisha. Ukiingia kwenye biashara wakikuunikia wanakuogopesha na wewe unaogopa. Wanakuambia nitakuharibia biashara yako. Wewe kimya kimya ingia kwenye maombi, Unasema Mungu niondolee hawa waua ndoto.

Hata k**a umefika mbali kiasi gani hofu itakurudisha chini. Kuna watu wamebeba kitu kikubwa kwa sababu ni waoga wameshindwa kuvionyesha wamekuwa mbilikimo. Hofu inaficha uwezo wako. Inaficha na kuuwa uwezo wa mtu.

Mtu anaweza kuwa na uwezo wa kushindana, watu utakisikia wakisema watanionaje. Wanadogosha uwezo aliyokupa Mungu, usipotumia hupati kitu.

Wewe inafikiri ni kitu gani kilimfanya Daudi amshinde Goliati, ni kwa sababu alishinda hofu ndani yake. Shinda hofu kwenye biashara yako, wewe Unazaje kushindana bila kushinda hofu.

Sema kwa jina la Bwana wa Majeshi nitaliweza hili.

Bwana atanipa kazi, atanipa kipato, Bwana atakuondolea hofu kwa Jina la Yesu.

Unasema sioni mlango, huko nje hakuna huruma, machozi hayasaidii chochote, ni lazima na uchague kwa ushujaa.

Usifikiri ukilia sana watakusaidia, vaa ujasiri wa kutoka hapa ulipo. K**a alivyoambiwa lbrahimu.

K**A UJAWEZA KUWA HODARI BADO UJAANZA KUISHA AHADI ZAKO ALIZOKUAHIDIA MUNGU.

Wale waliotumwa nchi ya ahadi waliona majitu wakaingiwa na hofu. Wawili tu walikuwa hodari. Bila ya kuwa hodari utaweza kuishi maisha yako. Huko nje jitengezee pumzi yako mwenyewe. Ukiona mtu aliyefanikiwa ni mtu aliyeshinda hofu.

Jinsi ya kushinda hofu ni kujiunganisha na Mungu ili uweze kupata njia za kupita katika maisha yako. Ukiwa naye hakuna hofu. Kila aliyejiunganisha na Mungu amejitengezea nguvu ya kushinda hofu na kuleta ushindi ndani yako.

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, hata katika maji hayatakugharikisha.

INATAKIWA KURUDI KWENYE YALE MATENDO, UPENDO NA NIDHAMU YAKO YA KWANZA. INATAKIWA UWE HODARO AU SHUJAA KUFIKIA UAMUZI HUO. K**A UJAWEZA KUWA HODARI BADO UJAANZA KUISHA AHADI ZAKO ALIZOKUAHIDIA MUNGU.

06/03/2026
06/03/2026

Fundisha watu kile kitu unachokiishi, ama sivyo utakuwa unawadanganya. Unafundisha wenzako kuwa uwe mvumilivu hata mme akioa mke wa pili. Hiyo siyo sawa. Ni lazima tuzipime hizo roho.

30/01/2026

๐™๐˜ผ๐˜ฝ๐™„๐˜ผ ๐™•๐™„๐™‰๐˜ผ๐™•๐™Š๐™•๐™๐™„๐˜ผ ๐™๐™Ž๐™๐˜ผ๐™’๐™„ ๐™’๐˜ผ๐™†๐™Š ๐™†๐™„๐™๐˜พ๐™ƒ๐™๐™ˆ๐™„ ๐™ˆ๐˜ผ๐™ˆ๐˜ฝ๐™Š ๐™ˆ๐™๐™ƒ๐™„๐™ˆ๐™ ๐™”๐˜ผ ๐™†๐™๐™๐˜ผ๐™‰๐™”๐™„๐˜ผ ๐™†๐˜ผ๐™•๐™„
Mtumishi: Jensen Shuma

๐™‰๐™€๐™‰๐™Š

๐™ˆ๐™ž๐™ฉ๐™๐™–๐™ก๐™ž 6:6-9
๐˜Œ๐˜ธ๐˜ฆ ๐˜ฎ๐˜ท๐˜ช๐˜ท๐˜ถ, ๐˜ฎ๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ฆ๐˜ฆ ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ถ๐˜ฏ๐˜จ๐˜ถ, ๐˜ก๐˜ช๐˜ต๐˜ข๐˜ง๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ณ๐˜ช ๐˜ฏ๐˜ซ๐˜ช๐˜ข ๐˜ป๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฆ ๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ฑ๐˜ข๐˜ต๐˜ฆ ๐˜ฉ๐˜ฆ๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฎ๐˜ข. ๐˜’๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜บ๐˜ฆ๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฅ๐˜ข, ๐˜ž๐˜ข๐˜ญ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ด๐˜ช๐˜ฎ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ช๐˜ป๐˜ช, ๐˜ธ๐˜ข๐˜ญ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ถ, ๐˜“๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฉ๐˜ถ๐˜ซ๐˜ช๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฌ๐˜ฆ๐˜ข ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฃ๐˜ข ๐˜บ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ญ๐˜ข ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ซ๐˜ถ๐˜ข; ๐˜๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ด๐˜ข๐˜ฏ๐˜บ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ญ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฆ ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ท๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ฐ. ๐˜Œ๐˜ธ๐˜ฆ ๐˜ฎ๐˜ท๐˜ช๐˜ท๐˜ถ, ๐˜ถ๐˜ต๐˜ข๐˜ญ๐˜ข๐˜ญ๐˜ข ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ต๐˜ข ๐˜ญ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช? ๐˜œ๐˜ต๐˜ข๐˜ฐ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ฐ๐˜ฌ๐˜ข ๐˜ญ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช๐˜ฌ๐˜ข ๐˜ถ๐˜ด๐˜ช๐˜ฏ๐˜จ๐˜ช๐˜ป๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฐ?

๐™ˆ๐˜ผ๐™ƒ๐™๐˜ฝ๐™„๐™๐™„

Leo tutakwenda na somo la uchumi k**a tulivyoona wiki iliyopita. Lakini kuna mambo ambayo ningependa uyajue tokea mwanzo wa mafunzo haya:

ยทAmini kuwa unaweza kutoka kwenye hali uliyonayo ya chini na kutengeze kipato cha kukutosha na ukamtolea Mungu wako kwa uhuru.

ยทSiyo mpango wa Mungu wewe uwe maskini. Watu wengi wamekuwa wakifikiri ya kuwa Mungu ndiye aliyewapangia kuwa maskini. Na hata wakristo wengine kudiriki hata kuuona umaskini k**a sehemu ya utakatifu na unyenyekevu.

Watu wengi wanapenda kuishi maisha matakatifu na wengi pia wanapenda kuokoka na kudumu ndani ya kristo, lakini swali linalowasumbua ni wafanyeje katika hali ngumu hii ya uchumi wapate chakula, malazi na mavazi kihalali bila kumkosea Mungu?

Ni lengo langu kukueleza katika ujumbe huu ya kwamba SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI.

Ni budi ufahamu ya kuwa maneno yako na matendo yako ni matokeo ya jinsi unavyowaza. Kwa maneno mengine naweza kusema ya kuwa maisha ya mtu yanategemea mtazamo wa mawazo yake. Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba jinsi ulivyo ni matokeo ya jinsi unavyowaza; kwa kuwa unayowaza ndiyo unayoyasema na kuyafanya.

๐™ˆ๐™ž๐™ฉ 23:7 (๐™–)
๐˜”๐˜ข๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ข๐˜ฐ๐˜ฏ๐˜ข๐˜ท๐˜บ๐˜ฐ ๐˜ฏ๐˜ข๐˜ง๐˜ด๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฎ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฆ, ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ช๐˜ท๐˜บ๐˜ฐ ๐˜ข๐˜ญ๐˜ช๐˜ท๐˜บ๐˜ฐ.

Wewe ni matokeo ya kile unachokifikiri na kwa sababu hiyo ni muhimu kufikiri pia kuhusu nini unakiwaza na k**a kina kibali mbele za Mungu. Ukiwaza mimi nitaweza NI KWELI UTAWEZA. Ukiwaza mimi ni maskini basi mdomo utakiri na utaendelea kuwa hivyo. Ukiwaza kwenye hali hii niniliyo nayo ya ufukara ni lazima nijitoe niwe na kipato cha kutosha. Hivyo hivyo utapata fursa na utapata kipato cha kutosha.

Neno la Mungu kwenye

๐™†๐™ช๐™ข๐™—๐™ช๐™ ๐™ช๐™ข๐™—๐™ช ๐™ก๐™– ๐™๐™ค๐™ง๐™–๐™ฉ๐™ž 8:18
"๐˜‰๐˜ข๐˜ญ๐˜ช ๐˜ถ๐˜ต๐˜ข๐˜ฎ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ข ๐˜‰๐˜ธ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข, ๐˜”๐˜ถ๐˜ฏ๐˜จ๐˜ถ ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฐ, ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ช๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฑ๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฏ๐˜จ๐˜ถ๐˜ท๐˜ถ ๐˜ป๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฑ๐˜ข๐˜ต๐˜ข ๐˜ถ๐˜ต๐˜ข๐˜ซ๐˜ช๐˜ณ๐˜ช, ๐˜ช๐˜ญ๐˜ช ๐˜ข๐˜ญ๐˜ช๐˜ง๐˜ถ๐˜ฏ๐˜จ๐˜ฆ ๐˜ข๐˜จ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ฐ ๐˜ญ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฆ ๐˜ข๐˜ญ๐˜ช๐˜ญ๐˜ฐ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฑ๐˜ข ๐˜ฃ๐˜ข๐˜ฃ๐˜ข ๐˜ป๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฐ, ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ข ๐˜ฉ๐˜ช๐˜ท๐˜ช ๐˜ญ๐˜ฆ๐˜ฐ.โ€

Nguvu za kupata utajiriโ€ zinamaanisha nini?

-Uwezo wa kiakili: kufikiri, kupanga na kuanzisha miradi yako kwa ajili ya maendeleo yako mwenyewe.
-Afya ya mwili: kuweza kufanya kazi na kutekeleza majukumu ya unayotaka kuyafikia.
-Maarifa na ujuzi: kupata elimu au mafunzo ya kazi mbalimbali.
-Fursa: Mungu kufungua milango ya nafasi za maendeleo.
-Hekima ya kifedha: matumizi mazuri ya mali na utunzaji wa raslimali.

Kwa hiyo, badala ya kumpa mtu pesa mkononi, Mungu humpa vitu hivyo ambavyo vikitumika kwa uaminifu, huzaa matokeo ya utajiri.

Mungu hategemei watu wakae tu wakisubiri muujiza wa kifedha. Badala yake, anabariki kazi za mikono yako.

Zaburi 90:17 โ€“ โ€œNa uzuri wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu; kazi ya mikono yetu uithibitishe.โ€
Methali 10:4 โ€“ โ€œMkono wa mtu mwenye bidii hutajirisha, bali wa mtu mzembe huletea
maskini.โ€

2 Wathesalonike 3:10 โ€“ โ€œK**a mtu hataki kufanya kazi, basi asile.โ€

Hii inaonyesha kuwa Mungu hutoa mafanikio kwa wale wanaojituma, si kwa wale wanaokaa tu wakisubiri utajiri ushuke kutoka mbinguni.

Tunafahamu ya kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya Mungu. Na naamini ya kuwa utakubaliana nami nikisema Mungu wetu si maskini kwa hiyo hatukuumbwa kwa mfano wa kimaskini wala sura ya kimaskini.

Kazi kazi kazi ndicho kitu ambacho Mungu anataka tufanye. Kwa maneno Mengine anasema tuache kuwa wavivu. Ukiwa mvivu utakuwa maskini

๐™ˆ๐™ž๐™ฉ๐™๐™–๐™ก๐™ž 6:6-9
๐˜ก๐˜ช๐˜ต๐˜ข๐˜ง๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ณ๐˜ช ๐˜ฏ๐˜ซ๐˜ช๐˜ข ๐˜ป๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฆ ๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ฑ๐˜ข๐˜ต๐˜ฆ ๐˜ฉ๐˜ฆ๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฎ๐˜ข. ๐˜’๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜บ๐˜ฆ๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฅ๐˜ข, ๐˜ž๐˜ข๐˜ญ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ด๐˜ช๐˜ฎ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ช๐˜ป๐˜ช, ๐˜ธ๐˜ข๐˜ญ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ถ, ๐˜“๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฉ๐˜ถ๐˜ซ๐˜ช๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฌ๐˜ฆ๐˜ข ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฃ๐˜ข ๐˜บ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ญ๐˜ข ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ซ๐˜ถ๐˜ข; ๐˜๐˜ถ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ด๐˜ข๐˜ฏ๐˜บ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ญ๐˜ข ๐˜ค๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฆ ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ท๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ฐ. ๐˜Œ๐˜ธ๐˜ฆ ๐˜ฎ๐˜ท๐˜ช๐˜ท๐˜ถ, ๐˜ถ๐˜ต๐˜ข๐˜ญ๐˜ข๐˜ญ๐˜ข ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ต๐˜ข ๐˜ญ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช? ๐˜œ๐˜ต๐˜ข๐˜ฐ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ฐ๐˜ฌ๐˜ข ๐˜ญ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฌ๐˜ข๐˜ต๐˜ช๐˜ฌ๐˜ข ๐˜ถ๐˜ด๐˜ช๐˜ฏ๐˜จ๐˜ช๐˜ป๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ฐ?

Tabia zilizopo kwenye familia yako ndiyo zinakufanya ufanikiwe au usifanikiwe katika maisha yako. Kuna tabia zikiwepo huwa zinawachelewesha kwenye maisha. Mtu akipata fedha anakuwa tofauti na wakati hana fedha. Issue hapa siyo mshahara mkubwa, kipato kikubwa cha biashara, siyo mali bali ni kwamba kuna tabia gani kunapokuwepo na hela. Hapo hakuna mapepo, laana wala mila ni kwamba unaposhika pesa ni shida, tabia inabadilika.

Every coin passed through your life siyo bahati mbaya. Kila pesa ina kusudi la Bwana. Kinacho-tuchelewesha ni kwamba hatuna nidhamu ya fedha.

i) ๐˜ผ๐™ฃ๐™–๐™จ๐™–

Anasa ni misuse of funds (ni kinyume na matumizi mazuri ya fedha). Anasa huwa inashindana na nidhamu ya fedha.

๐™ˆ๐™ž๐™ฉ๐™๐™–๐™ก๐™ž 21:17
๐˜”๐˜ต๐˜ถ ๐˜ข๐˜ฑ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข๐˜ด๐˜ข ๐˜ข๐˜ต๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ด๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช; ๐˜ˆ๐˜ฑ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜ฅ๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฎ๐˜ท๐˜ช๐˜ฏ๐˜บ๐˜ฐ ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ง๐˜ถ๐˜ต๐˜ข ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ต๐˜ข๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ต๐˜ข๐˜ซ๐˜ช๐˜ณ๐˜ช.

Kuna watu kula ni anasa, kusafiri ni anasa, kuvaa ni anasa, nk. Angalia hata Taifa linalopenda anasa ukikuta wanafanya kikao wanazungumza lakini hawatekelezi. Wanaweza kutumia milioni ishirini kwa mazungumzo tu bila matokeo yeyote.

Utasikia wakati mwingine kanisani watu wanadai ripoti za matumizi na mapato. Ebu tufikirie kuhusu wewe, tutafute ripoti yako ya matumizi na mapato, unatumia shilingi ngapi huko njiani. Je unajua kwa mwaka unaingiza shilingi ngapi? Unazo ngapi sasa? Inabidi kuwepo na mabadiliko kwenye maisha yako. Angali ni mangapi ya anasa uliyofanya yakiyokula pesa yako.

ii) ๐™†๐™ช๐™Ÿ๐™ž๐™›๐™–๐™ฃ๐™ฎ๐™– ๐™๐™–๐™Ÿ๐™ž๐™ง๐™ž ๐™ก๐™–๐™ ๐™ž๐™ฃ๐™ž ๐™ƒ๐™ช๐™ฃ๐™– ๐™†๐™ž๐™ฉ๐™ช

Kuna tabia watu waliyo nayo ya kujitutumua, kujimwambafyi au kujifutua kwenye matumizi yako. Unaona wenzako wananunua pochi nzuri na wewe unasema ni lazima ninunue.

๐™ˆ๐™ž๐™ฉ๐™๐™–๐™ก๐™ž 13:7
๐˜’๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ต๐˜ถ ๐˜ฎ๐˜ธ๐˜ฆ๐˜ฏ๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ซ๐˜ช๐˜ต๐˜ข๐˜ซ๐˜ช๐˜ณ๐˜ช๐˜ด๐˜ฉ๐˜ข, ๐˜ญ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ฉ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ช๐˜ต๐˜ถ; ๐˜’๐˜ถ๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ข๐˜ซ๐˜ช๐˜ง๐˜ข๐˜ฏ๐˜บ๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ด๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช, ๐˜ญ๐˜ข๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ข๐˜ฏ๐˜ข ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ญ๐˜ช ๐˜ฏ๐˜บ๐˜ช๐˜ฏ๐˜จ๐˜ช..

Sisi ebu tumwangalie huyu wa kwanza ambaye anajitajirisha lakini hana kitu. Unafanya manunuzi yako mahali palipo ghali, nk. Unafanya vitu ili watu wakuone na siyo kwamba yapo kwenye bajeti yako. Ukifanya hivyo kuna mahali utakula mtaji au fedha itakusumbua itakuwa haikutoshi kila siku.

iii) ๐™†๐™ช๐™›๐™ช๐™–๐™ฉ๐™– ๐™ˆ๐™–๐™ข๐™—๐™ค ๐™ฎ๐™– ๐™๐™ฅ๐™ช๐™ช๐™ฏ๐™ž

Hapa ni tabia ya kufanya mambo yasiyo na maana kwako.

๐™ˆ๐™ž๐™ฉ๐™๐™–๐™ก๐™ž 28:19๐™—... ๐˜‰๐˜ข๐˜ญ๐˜ช ๐˜ข๐˜ง๐˜ถ๐˜ข๐˜ต๐˜ข๐˜บ๐˜ฆ ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ฎ๐˜ฃ๐˜ฐ ๐˜บ๐˜ข ๐˜ถ๐˜ฑ๐˜ถ๐˜ป๐˜ช ๐˜ข๐˜ต๐˜ข๐˜ฑ๐˜ข๐˜ต๐˜ข ๐˜ถ๐˜ฎ๐˜ข๐˜ด๐˜ฌ๐˜ช๐˜ฏ๐˜ช ๐˜ธ๐˜ข ๐˜ฌ๐˜ถ๐˜ฎ๐˜ต๐˜ฐ๐˜ด๐˜ฉ๐˜ข.

Inawezekana mwaka 2025 umefanya mambo mengi ya kipuzi. Inatakiwa usiingie na hayo mambo kwenye mwaka huu wa 2026. Ebu fikiri ni watu wangapi wanafanya mambo ya kipuuzi kwenye social media, lakini wengine social media hiyo hiyo wanauza na kupata fedha.

Tuondoke kwenye mambo ya kupuzi yanapoteza muda wa kutengeneza fedha kwenye maisha yako.

iv) ๐™„๐™จ๐™๐™ž ๐™‡๐™š๐™ค ๐™†๐™ช๐™Ÿ๐™ž๐™ฌ๐™š๐™ ๐™š๐™– ๐™†๐™š๐™จ๐™๐™ค ๐™”๐™–๐™ ๐™ค

Mfumo wa maisha ya Chungu ni kwamba alichokipata leo alitengeneza future yake. Inatakiwa tuwe na ulazima wa kuwepo na usimamizi nzuri leo ili kutengeneza kesho yako. Kipindi hiki cha neema una mavuno, ulishafikiri utaishi vipi wakati wa jua au wakati wa baadaye kwenye maisha yako nje ya ajira, biashara, nk.

Hapa kuna watu wa aina mbili wakati wa neema.

๐™ˆ๐™ง๐™–๐™™๐™ž ๐™ˆ๐™ž๐™™๐™ค๐™œ๐™ค ๐™๐™ฃ๐™–๐™ฎ๐™ค๐™ฌ๐™š๐™ฏ๐™– ๐™ ๐™ช๐™–๐™ฃ๐™ฏ๐™– ๐™ฃ๐™–๐™ฎ๐™ค

Kufanya biashara yeyote au mradi wowote, hakutegemei MTAJI au ni fedha kiasi gani ulizo nazo. Inategemea WAZO ULILO NALO NAFSINI MWAKO. Aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Kwa hiyo usisingizie kuwa sina mtaji. Mawazo yako yametawaliwa na nini? Kinywaji, Kula mpaka iishe ndipo utafute fedha nyingine, mume ataleta hakuna kuangaika, baba na mama wapo ngoja nile starehe, fedha niliyopata haitoshi, ngoja niile.

Hiyo hiyo fedha kidogo unayoiona, Mtu mwingine ataiongeza mara mia. Leo tulisema ni siku ya kuvunja kibubu. Lakini kibubu kinachokuja ni kwa nguvu yako mwenyewe. Ukipanda haba utapata haba, ukipanda nyingi utapata nyingi.

Fedha hiyo hiyo utakayopata hapa siku ya leo, mwingine atatoka, mwingine atashindwa. Sababu ni nini. TABIA. KILICHOKO NDANI YAKO.

Hivi kweli tukipata kuna mtu atakumbuka hata kumtolea Mungu. Si unakwenda kuizungusha, ukipata faida, usiache kukumbuka Bwana Mungu wako.

Kumbukumbu ya Torati 28: 1-8 (Wasome wenyewe)

Kuna biashara nyingi unazoweza kuzianzisha kwa shilingi 20,000 na kuendelea.

ยท Biashara ya Mkate na Vitafunwa

ยท Biashara ya Uuzaji wa vitu vya nyumbani

ยท Biashara ya Maji ya Matunda (Juice)

ยท Uuzaji wa vitabu vya kichocheo

ยท Huduma za Usafishaji

ยท Huduma za kupiga picha

ยท Uuzaji wa Nguo Mitumba

ยท Huduma ya Kuosha Magari

ยท Kusuka Nywele, Kunyoa na Kupamba Watu

ยท Udalali ( udalali wa kila kitu)

ยท Biashara za ushonaji.

ยท biashara ya Popcorn (bisi)

ยท Dagaa waliokaangwa kufunga kwenye vifuko vya plastick

ยท Kuondoa michirizi kwenye ngozi za watu

ยท Kanga na vitenge

ยท Biashara za kucha

ยท Nguo za ndani

ยท ice cream za vifuko

ยท Biashara ya kutembeza uji wa kawaida na wa ulezi hasa maenea yenye asili ya baridi, jioni na asubuhi

ยท Kuuza maharage yaliyochemshwa watu wakaunge wenyewe

ยท Biashara ya rasta

ยท Jiko la Supu yenye Ladha nzuri

ยท Kusambaza bidhaa majumbani

ยท Kununua kuku wa nyama na kufuga kwa miezi miwili (nunua 6,500 hadi uza 20,000)
Kijiwe cha kuonyesha mpira

Vidokezo vya Mafanikio katika Biashara Ndogo

- Utafiti wa Soko: Kabla ya kuanza biashara, fanya utafiti wa soko ili kuelewa mahitaji ya wateja na ushindani.

-Ubunifu: Kuwa mbunifu na ubuni njia mpya za kuvutia wateja na kuongeza mauzo.
-Huduma kwa Wateja: Toa huduma bora kwa wateja wako ili kujenga uaminifu na wateja wa kudum
-Usimamizi wa Fedha: Simamia vizuri fedha zako kwa kuandaa bajeti na kufuatilia mapato na matumizi.
-Kuendelea Kujifunza: Jifunze kutoka kwa wajasiriamali wengine na endelea kuboresha ujuzi wako katika biashara.

MUNGU AWABARIKI TUWEZE KUWA MATAJIRI

Address

Kimara
Dar Es Salaam
25522

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mahubiri posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mahubiri:

Shortcuts

Share