kumtumikia_mungu

kumtumikia_mungu Hili grupu ni kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa njia ya kuhubiri kwa vitendo.

KUTIANA MOYO.6 Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu. (Isaya 41:6)7 Serem...
17/12/2023

KUTIANA MOYO.

6 Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu. (Isaya 41:6)

7 Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike. (Isaya 41:7).

πŸ‘‰πŸΎKwenye maisha tunatakiwa kutiana moyo na kushirikiana siyo kukatishana tamaa.

πŸ‘‰πŸΎKila mtu hapa Duniani anafaida ila asipotiwa moyo faida yake haionekani.

πŸ‘‰πŸΎMungu ametuumba na vipawa/Karama tofauti tofauti Ili katika uo utofauti tumtukuze yeye.

πŸ‘‰πŸΎKatika maisha Kuna nyakati tofauti tofauti ambazo katika hizo, Kuna wakati wa huzuni,kukata tamaa,kuchoka na katika nyakati hizo tunatakiwa kutiana moyo.

πŸ‘‰πŸΎTusiwe watu wa kukusoa tu, kulaumu tu Bali wambie wengine YESU ANAKUPENDA, UTAVUKA, BWANA HAJAKUACHA......

WhatsApp
https://chat.whatsapp.com/CYYsFKMWcgh0gOPEDgc8S3

Telegram.
https://t.me/spiritualbreakfast

Meja William
0757215614.

YESU NI MME WA WAJANE NA BABA WA YATIMA._22 Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.(Kutoka 22:22)...
18/11/2022

YESU NI MME WA WAJANE NA BABA WA YATIMA.

_22 Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.(Kutoka 22:22)._

23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao, (Kutoka 22:23)

24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima. (Kutoka 22:24)

Hili kundi ni la muhimu sana ukiwagusa umegusa moyo wa Mungu. Tuwapende,tuwajali,tuwasaidie,tuwaombee na kuwatetea.
Sisi tulio-mabarozi wa Yesu ni wajibu wetu kuwasaidia. Unapoweka malengo kwa ajili ya maisha yako kundi hili usilisahau.
Dini bora ni hipi?
πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»
_Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.(Yakobo 1:27)

Ni fursa unaweza fanya zaidi ya kutoa msaada na kutembelea kituo ukaamua, kuwasomesha,kuchukua na kuleawa
Kwa kufanya hivo unamkopesha Mungu,atakubariki wewe na uzao wako.

Meja William
0757215614.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when kumtumikia_mungu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to kumtumikia_mungu:

Share