22/06/2021
UMEUMBWA KWA
KUSUDI
Mhubiri 3:1 “Kila jambo na majira yake na wakati wake, kwa Kila kusudi chini ya mbingu”.
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu' karibu tujifunze neno la MUNGU.
Somo linasema umeumbwa kwa Kusudi, hii inamaana kuwa hakuna mtu aliyeumbwa kwa bahati mbaya na ndio maana ukisoma Mhubiri 3:1 ameongelea mambo matatu ya msingi: majira, wakati na Kusudi ambapo haya yakifanyika kwa usahihi jambo linakuwa na mafanikio sahihi. Binadamu yeyote ameumbwa na Mungu kwa majira sahihi, wakati sahihi na makusudi sahihi,
Yeremia 1:
4 Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” .
Hapo tunamwona Yeremia hakujua k**a aliumbwa kwa kusudi gani alipopewa kazi na Mungu yeye akajua Mungu amekosea kumbe Mungu alimuumba kwa Kusudi hilo. Ndugu yangu nikwambie ukweli kwamba hakuna bahati mbaya katka kuumbwa hivyo kataa kuishi kwa bahati mbaya. Kabla hujaja kwenye tumbo la Mama ulikuwa kwa Mungu k**a Roho isiyo na Mwili hivyo wazazi wako walitengeneza Mwili Mungu akakutuma Duniani kutimiza kusudi ukavaa mwili ndani ya tumbo la mama ukazaliwa kwa njia hiyo . Shetani ni mwongo anatazama kusudi lako tokea mbali anagundua utakuja kuwa nani baadae anaona umetumwa kuharibu kazi zake anaanza kukushambulia ili usitimize kusudi '.
Kutoka 1:
15 “Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua;
16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.”
Hapo farao ametambua kuna mtu atakuja kuwakomboa wana wa Israeli ametangaza watoto wasiachwe hai na kumbe ndani ya watoto hao ndio Musa anazaliwa, Unaona ni jinsi gani sababu kubwa ya mateso yako sio hivyo unavyooneka Sasa Bali vile kesho yako ilivyo kubwa
Na lengo ni kukuchelewesha au kukuzuia kabisa usifanye kusudi lililokuleta Duniani.
Mda mwingine Shetani anakuweka kwenye kazi flani ambayo anajua hutaweza kutimiza kusudi kwa wakati.. Mf “unakuta Mungu alipokuumba amekuwekea vipawa kwamba ukija Duniani uwe milionea ili uwasaidie Yatima Sasa shetani akiona hilo kusudi anaanza kukushambulia unaanza kuona Kila biashara unafanya hela hupati,..
Matendo ya Mitume 22:
8 “Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi.
9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.
10 Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye” .
Huyo aliitwa sauli kazi yake alikuwa askari aliyepewa kitengo cha kulitesa kanisa la MUNGU kumbe shetani alikuwa amejua alitumwa kuhubiri injili na kukuza kanisa kwa kiwango cha juu sana akamweka kuwa wa kulitesa kanisa. Hapo tunajifunza yupo mtu anafanya mambo mabaya k**a Wizi, Ulevi, Ukahaba, na mengine k**a hayo si kwa kupenda ni shetani ametazama hatma yake akajua madhara yake akaamua kumpeleka huko.. Yesu alipomtokea Sauli aliamua kumfanya upya na kumrudisha kwenye Kusudi na jina akam'badilisha akaitwa PAUL leo hii ukiongelea injili kwa mataifa unamwongelea Paul maana yeye ndio aliyeihubiri tujiulize ingekuaje k**a Paul angeendelea na lile kusudi la shetani ambalo ni kuharibu kanisa leo hii tungekuwa wap? Kuna mtu unakusudi kubwa tu lkn shetani anakuingiza kwenye dhambi ambayo inakutesa na kila ukijaribu kuiacha inakushinda lengo lake ni ww uishi nje ya kusudi la MUNGU.. Ndugu tafuta sana kuishi ndani ya kusudi la Mungu mafanikio sio kumiliki vitu vnavyoonekana kwa macho Bali nikuyajua mapenzi na makusudi ya Mungu na kuyatimiza kikamilifu hapo tunasema umefanikiwa,
Yohana 4:
34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. Jiulize je, hapo ulipo ni Mahali sahihi? Vp maisha unayoishi ndio kusudi la MUNGU kukuleta Duniani? Vp Yesu akirudi leo utavikwa taji kwa kazi aliyokutuma kufanya? Ndugu yangu hakuna jambo lisilo na Kusudi hata pesa uliyonayo k**a isipofanya kusudi la Mungu ni kazi Bure, hata kazi uliyo nayo k**a sio kusudi la Mungu hutapata matokeo.. Hivyo tafuta sana kuyatimiza kusudi la Mungu..
Maombi...
>Mwombe Mungu akujuze kusudi la yeye kukuumba.
>Kataa Kila kusudi la adui katka maisha yako.
>kataa Kila mpango wa Adui unaozuia usitimize kusudi
>Mwambie Mungu akupe wasaidizi watakaosaidiana na wewe kutimiza kusudi. Paul alikutanishwa na Anania akayajua mapenzi ya Mungu.
>Kataa Kila mahusiano ambayo adui ameyaleta kwako ili kuzuia Kusudi la MUNGU.
Ndugu hukuumbwa kwa bahati mbaya Mungu amekuleta Duniani ili umuwakilishe kwenye Kusudi flani hajakuleta ili uwe masikin k**a ilivyo Sasa wala mlevi, ila anataka kwa wewe watu waseme hakika Mungu yupo. Hivyo tafuta sana kuyatimiza yaliyokuleta ili siku zako zikiisha upokee malipo ya kazi yako..
Mungu akubariki sana ni mimi mwalimu
Sigfrid chuwa
Kwa maombi na ushauri unaweza kunipata kwa cm
0712220381 au
0748637804