19/08/2026
SOMO: UJUE ULIMWENGU WA ROHO. (Utendajikazi wake na matokeo yake kwenye maisha)....15.
NAMNA YA KUSHUGHULIKA NA ULIMWENGU WA ROHO KATIKA KULETA MATOKEO.
NAMNA YA KUSHUGHULIKA NA ULIMWENGU WA ROHO KATIKA KULETA MATOKEO.
Mungu akubariki kwa kuendelea kuwa mvumilivu kwa somo hili ambalo limekua lefu sana ila lengo ni kutaka upate maarifa ya kina kuhusu mambo ya rohoni.
Leo tutamalizia mfano wa mwisho katika somo letu.
Yesu Kristo alitabiriwa kuzaliwa, kufa na kufufuka tangu mwanzo wa mwanadamu kuasi.
Unakumbuka kwamba Mungu alisema kwa uzao wa mwanamke nyoka atapondwa kichwa na nyoka atauponda uzao wa mwanamke kisigino. Mwanzo 3:14,15.
Hapa ulimwengu wa roho tayari ulikua umeshatengeneza mpango wa Yesu kuzaliwa kuteswa, kufa na kufufuka, hii pia ilikua ni kanuni ya ulimwengu wa roho kumkomboa mwanadamu. Maana ulimwengu wa roho pia una kanuni, sheria na taratibu zake katika kukamilisha mpango wake (Hili ni somo lingine k**a Roho akinipa mafunuo tutajifunza).
Kwahiyo Yesu alipaswa kuwa uzao wa mwanamke, uzao wa mwanamke maana yake mtoto atakayezaliwa bila tendo la ndoa, maana unapaswa ujue uzao ni wa mwanaume mwanamke ana uzazi.
Pia kwenye Isaya inaonesha ni mwanamke gani atakayeleta huu uzao, maana hata aliyezaa k**a atazaa bila mwanaume pengine tungesema ndiye yule ulimwengu wa roho ulisema, lakini ulimwengu wa roho ukatoa ni mwanamke gani mwenye hiyo sifa ya kuzaa uzao wa kumponda kichwa nyoka (shetani), sifa hiyo ilikua ni BIKIRA (Isaya 7:14). Hapa tunapaona uthibitisho wa kile kitakachotokea, hapa tunapata kitu kingine kuhusu ulimwengu wa roho kwamba unasifa ya kuelekeza jambo gani litatokea, kwahiyo mambo ya ulimwengu wa roho yanatabia ya kuthibitisha ili kitakachotokea kiwe sahihi. Ulimwengu wa roho unazungumza, unahitaji masikio na macho ya rohoni ili shetani asikuchanganye. Lakini la nyongeza hapa ni kwamba Mika aliona mpaka sehemu atakayozaliwa Yesu (Bethlehem), manabii tofauti ila wanaona kitu kimoja. Hapa tunaona ulimwengu wa roho unaendelea kuthibitisha kile ambacho kilichokuwepo kwenye ulimwengu huo, kwahiyo kila kitu kilikua kilishafanyika, lakini ulimwengu wa roho unatabia ya kujifunua ili kwamba kikitokea tofauti na hapo hata k**a kinafanana fanana ila k**a kuna utofauti hata sehemu basi ujue kwamba hiko siyo shetani anataka kukupotosha.
Sasa somo lijalo tutaangalia Sababu na Matokeo, maana hapa tumeangalia chanzo.
Kumbuka kwamba hii mifano ni michache kati ya mingi inayoelezea kuzaliwa, kufa na kufufuka kwa Yesu, kumbuka pia Biblia nzima inamuelezea Yesu.
Tafadhali toa maoni yako umejifunza nini na umepata ufunuo gani katika somo hili, k**a ulipitwa na masomo ya nyuma tafadhili nitafute WhatsApp kwa namba hapo chini ili nikutumie masomo ya nyuma.
Shalom Shalom 🙏🏾
Ev. Elisha Samson
+255 716 472 317
+255 759 007 009