Ufufuo na Uzima PUGU

Ufufuo na Uzima PUGU UFUFUO NA UZIMA PUGU Ni Kanisa linaongozwa na Mchungaji Kiongozi Eldady Petro.Karibu Tuabudu Pamoja

UFUFUO NA UZIMA PUGU.BABA YETU: ASKOFU ELIDADI GWITEGOTAREHE: 25/6/2023SOMO: IBADA YA MIUNGU NA FAMILIA ILIYO MILIKIWA.-...
25/06/2023

UFUFUO NA UZIMA PUGU.

BABA YETU: ASKOFU ELIDADI GWITEGO

TAREHE: 25/6/2023

SOMO: IBADA YA MIUNGU NA FAMILIA ILIYO MILIKIWA.

-Familia tulizo tokea ni familia zilizo kuwa zikiabudu miungu. Na familia hizo zilikuwa zikimilikiwa na iyo miungu kwa kuwa kila kitu walicho kuwa wakikiomba na kukifanya lazima wafanye kupitia miungu wanayo iabudu. Na ndipo hapo izo familia zikamilikiwa na miungu mingine na kuwa mali za mashetani.

-Na sisi tumezaliwa katika familia ambazo zilimilikiwa.

Ufunuo wa Yohana 2:13

[13]Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

-Hapa tunaona katika maandiko kuwa tunatokea katika familia ambazo shetani alipata nafasi ya kuendesha maisha yao.

-Ila katika yote tunaweza kusambalatisha kwa kutumia upanga wa Rohoni kwa kufyeka na kuteketeza unaweza kuharibu madhabahu zote ambazo walikuwa wanatumia watu wa zamani katika miungu yao na kuweka Madhabahu ya Mungu wa kweli. Ambayo inaweza kuharibu na kusimamisha agano ambalo Mungu aliliweka kwa watu wake.

-Tunapaswa kushika sana jina la Mungu wetu na upanga wa rohoni kwakuwa upanga wake unamakali pande zote mbili hakuna adui ambae ataweza kusimama mbele yako.

-Tunapaswa kuwa waaminifu ndani ya bwana wetu na kubeba upanga wa rohoni ili kuweza kushindana na maadui katika ulimwengu wa rohoni.

-Wakolosai 1:13
[13]Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;

-Mwanzoni tulizaliwa katika familia zinazo abudu miungu, tulipo mwamini Yesu kuwa bwana na mwokozi wetu akatuamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake ambae katika yeye tuna msamaha wa dhambi. Lazima kujua kuwa kabla ya kuokoka ulikuwa katika familia ambayo inaongozwa na shetani kupitia miungu ya mababu zetu na baada ya kuokoka unaingia katika ukoo wa Yesu na umeokolewa katika dhambi.

- Katika hali ya kimwili bado ni mwana familia ila katika upande wa rohoni mtu unakuwa upo katika wokovu wa Yesu kristo ambako hakuna nguvu za giza kuna kukombolewa, kufutiwa dhambi na kuwa na uhakika wa maisha ya milele kwakuwa utakuwa unaishi maisha ya wokovu ambayo Mungu amewaandalia wale wote walio kubali kuwa wana wake. Kwa kutumia silaa za vita za rohoni ambazo huteketeza yale maagano yote ambayo mababu zetu walikuwa wakiyaishi kabla ya kumkubali na kumpokea bwana wetu Yesu kristo.

-Na katika kuamishwa katika ulimwengu wa giza na kwenda katika ulimwengu wa nuru lazima uwe na silaa za kuwashinda watu wa ulimwengu wa giza kwakuwa bado watakuwa wanakutafuta kwakuwa mwanzo walijimilikisha maisha yako. Hivyo unapaswa kuvaa silaa za rohoni jina la Yesu na damu ya Yesu juu ya upanga ukatao kuwili ili kuweza kuwashinda katika kweli.

-Ufunuo wa Yohana 5:9-10
[9]Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

[10]ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.

-Mungu amekufanya uwe kuhani na uwe mmiliki na katika maombi utakayo kuwa unaomba unaomba kanakamba wewe ni mmiliki wa pendo la Yesu kwaiyo chochote kilichopo duniani unapaswa kumili.

-Maandiko yote yaliyopo katika kitabu kitakatifu cha biblia hayafanyi kazi kwa sababu yameandikwa ila yanafanya kazi kwakuwa watu wameyajua na kuyaelewa sawa sawa na maandiko yanavyo sema kwa kuamini kwako.

-Anae sikia na kuyafanyia kazi atainuka na kumea sawa sawa na maandiko yanavyo sema. Na mtu atakae soma na kuacha k**a yalivyo hato badilika kamwe.

Waamuzi 6:12-13

[12]Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa.

[13]Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.

-Tunaona Gideon anafaham ya kuwa kuna vitu ukiwa na Mungu haviwezi kukupata.
Mungu yupo na sisi ila watu wake hawajui k**a Mungu yupo nao. Unapaswa ujue kuwa Mungu yupo na wewe ili kila unacho kiomba kipate kibali mbele zake ndipo anapo tenda kazi zake.

-Watu wengi walio okolewa na damu ya Yesu hukata manaa sana kwa sababu ya roho za mizimu zinazo endelea kutenda kazi ndani yake.

Waamuzi 6:12,25-26,28
[12]Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa.

[25]Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng’ombe wa baba yako, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;

[26]ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng’ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.

[28]Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa.

-Katika madhabau za kimiungu ikivunja lazimaa uyapenyaa zaidi.

-mizimu na majoka yakishapigwa haku kitu ambcho kitaweza kunyanyuka tena katika maisha yako.

- Na baada ya kutoka katika kuabudu ibada ya mizimu na kuwa katika nuru vifungo vyote vinakatika katika biashara, katika afya katika masomo katika uchumi na katika famili kwa ujumla. Kumiliki na kutawala kunakuwa ndani yenu na kuishi kusudi la Mungu duniani linapata kutimia.

MUNGU AMETENDA MAAJABU NAMI SIWEZI KUELEZA
24/05/2023

MUNGU AMETENDA MAAJABU NAMI SIWEZI KUELEZA

Karibu sana Ufufuo na Uzima Pugu
20/05/2023

Karibu sana Ufufuo na Uzima Pugu

KARIBU SANA
06/05/2023

KARIBU SANA

KARIBU SANA UFUFUO NA UZIMA PUGU MUDA NI KUANZIA SAA 2 ASUBUHI.
30/04/2023

KARIBU SANA UFUFUO NA UZIMA PUGU MUDA NI KUANZIA SAA 2 ASUBUHI.

Good Memories Jumapili ya tarehe 23.04.2023
23/04/2023

Good Memories Jumapili ya tarehe 23.04.2023

Karibu Sana Pugu
22/04/2023

Karibu Sana Pugu

Good Memories 16.04.2023..Follow us on Instagram as (bishopelidadi) and on YouTube as Ufufuo na Uzima Pugu
18/04/2023

Good Memories 16.04.2023..Follow us on Instagram as (bishopelidadi) and on YouTube as Ufufuo na Uzima Pugu

UFUFUO NA UZIMA PUGUS.N.P: ELDADI GWITEGOTAREHE: 16/04/2023SOMO: VITA YA KUYAMILIKI YALE ULIYO PEWA NA MUNGU.-Mungu akit...
18/04/2023

UFUFUO NA UZIMA PUGU

S.N.P: ELDADI GWITEGO

TAREHE: 16/04/2023

SOMO: VITA YA KUYAMILIKI YALE ULIYO PEWA NA MUNGU.

-Mungu akitaka kumsaidia mtu, hampi hela ila hulitumia neno lake. Kwakuwa anajua kupitia neno lake kila kitu kinapatika katika neno lake.

-Na neno la Mungu hutenda sawa sawa na mahitaji ya wanadamu. Na bwana hulituma neno lake sawa sawa na wakati wa uhitaji wa mtu kwa wakati husika.

-Zaburi 107:20
[20]Hulituma neno lake, huwaponya,
Huwatoa katika maangamizo yao.

-Hivyo unapo pata neno unapaswa kujua Mungu anataka kukuvusha katika jambo lako.

-Kuna kupewa na kumiliki. Unaweza ukawa umepewa lakini haumiliki. Vita hii ni kwa ajili ya kumiliki kile ulicho pewa katika ulimwengu wa roho ili kije kutimia kwako katika ulimwengu wa mwili.

Yoshua 1:6
[6]Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.

-Tunapata kuona Mungu katika neno lake huwa anamuandaa mtu ili afanye kupitia yeye kile ambacho amekiandaa kwa ajili ya watu wake.

-Yoshua 1:7-8
[7]Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.

[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

-Kila mwenye kumiliki yupo wa kummilikisha.

Yoshua 18:3
[3]Yoshua akawauliza wana wa Israeli, akasema, Je! Hata lini mtakuwa walegevu katika kuingia kwenu na kuimiliki hiyo nchi, ambayo yeye BWANA, Mungu wa baba zenu, amewapa?

-Tunapata kuona kuwa watu wengi wa ulimwenguni ni walegevu kufikia kumiliki kile ambacho Mungu amewaandalia watoto wake.

-Tunapaswa kusali sana bila kuchoka ili kupata kile ambacho tumepewa ahadi na bwana kuwa tutamiliki na kutawala kila ambapo tutakanyaga.

-Yoshua 14:12
[12]Basi sasa unipe mlima huu, ambao BWANA alinena habari zake siku hiyo; kwani wewe ulisikia siku hiyo jinsi Waanaki walivyokuwa huko, na miji ilivyokuwa mikubwa yenye boma; yumkini yeye BWANA atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza watoke nje, k**a BWANA alivyonena.

-Unaweza ukawa umepewa ila ujapewa umiriki wa mahali husika. Kutokana na walinzi wa nguvu za giza wanao zuia mambo ya Mungu kutendeka.

-Mungu anaweza akawa amekuweka ili upate elimu, maisha mazuri ya kumpendeza Mungu, kuwa na afya nzuri ila majoka na mizimu huzuia kufika katika kile ambacho umepangiwa kufika katika hatima ya umiliki wako.

Waamuzi 18:9-11
[9]Wakasema, Haya, inukeni, twende tukapigane nao; kwa maana tumeiona hiyo nchi nayo ni nchi nzuri sana; nanyi, je! Mwanyamaa tu? Msiwe wavivu kwenda, na kuingia, ili mpate kuimiliki nchi hiyo.

[10]Hapo mtakapokwenda mtawafikilia watu wakaao salama salimini, na hiyo nchi nayo ni kubwa; kwa kuwa Mungu ameitia mikononi mwenu; ni mahali ambapo hapana kupungukiwa na kitu cho chote kilicho duniani.

[11]Basi wakatoka hapo watu mia sita waliovaa silaha za vita, wa jamaa ya Wadani, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli.

Waefeso 1:3
[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;

-Swali la kujiuliza Mungu ametubaliki kwa baraka ya vyote je wewe unavyo vyote?

-Jibu ni kwamba tunapaswa kupigana vita ya rohoni kwa kuwa wapo walio shikiria baraka zetu katika ulimwengu wa roho wasio taka tumiliki vile tulivyo pewa na Mungu. Tunapigana vita nao ili tuweze kurudisha vitu vyetu vyote na kuwa wamiliki halali wa hati zetu.

-Na mwenye kumiliki ni yule alie kuwa hodari katika kazi ya bwana.

-Katika kuomba ili kupata kile cha rohoni ambacho Mungu ameweka kwa ajili ya wana wake. Tunapaswa kuombea nafsi ambayo imenenewa mabaya na kuwekewa vizuizi katika kupata kile ambacho kimeandaliwa katika ulimwengu wa mwili na haya yote tutayapata kutoka rohoni pale Mungu atakavyo ijaza roho nguvu kwa ajili ya kutenda na kutimiza lile kusudi la Mungu la kuachilia baraka kwa wana wake na waweze kuzimili katika haki.

MFUMO WA KUOMBA KUWEZA KUPATA KILE AMBACHO MUNGU AMETUBARIKI KUTOKA ROHONI.

ROHO ➡️ NAFSI ➡️ MWILI.

-Roho hatakiwi kufanya vita katika mwili kwakuwa silaa yake si katika mwili.

-Nafsi inapaswa kutenda kazi na mwili ili waweze kufikisha kusudi la Roho linalo takiwa kutendeka katika mwili.

-Mwili hutenda na kukamilisha yale yote ambayo yamesha achiliwa Rohoni ili yaweze kutimia katika ulimwengu wa mwili. Na haya yote hupitia kutoka Rohoni na kupitia katika nafsi ya binadamu ni pale tunapo pata mawazo na kufanya jambo juu ya kitu fulani na ndipo mwili utekeleza sawa sawa na nafsi inavyo mtuma kufanya. Ndipo apo kile ambacho kimepangwa na Mungu kinatimia katika ulimwengu wa mwili.

Ufunuo wa Yohana 5:9
[9]Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

-Tunapata kuona kuwa Yesu alikuja na kufa kwa ajili ya watu wote wa ulimwengu kwa ajili ya kuwanunua na kuwa wana wa Mungu. Ili waje waketi katika kiti cha enzi cha baba na kuwa ufalme na makuhani wa Mungu. Na kuruhusu kupata vitu vyote vya duniani kutawala na kumiliki k**a wana wa ufalme wa mbinguni.

TUTAKUWA NA MAOMBI YA SIKU SABA KWA AJILI YA KUWASHINDA WANAOZUIA TUSIMILIKI,

Ni Maombi ya Kuwaondoa Wanaozuia Tusimiliki,
Jumatatu hadi Jumpili,

Siku saba za kuomba maombi ya kuwaondoa waliotuzuia Tusiyamiliki Tuliyo pewa.

09/04/2023

SIRI USIOIJUA| ZAMANI WATU WENYE PEPO WALIPIGWA KWA MAWE|

Desturi ya zamani ilikuwa watu wenye pepo walikuwa wakipigwa kwa mawe mpaka kufa, Lakini baada ya kuja Yesu Kristo akabadili utaratibu huo
Luka 10:2,16-17
[2]Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.
[16]Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
[17]Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
Luka 10:18
[18]Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni k**a umeme.
Luka 10:19
[19]Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

Kuanzia hapo Sio Tena kuokota mawe kupiga watu wenye mapepo Bali kutoa mapepo kwa Jina Lake (Yesu Kristo)..
K**a Unampenda Yesu .Like pia share Siri hii usisahau Kufollow ukurasa wetu.

09/04/2023

Luka 10:2,16-17
[2]Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.
[16]Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
[17]Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.

Address

Pugu/Kisumu
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufufuo na Uzima PUGU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ufufuo na Uzima PUGU:

Share

Category