Grace and Truth Int Church

Grace and Truth Int Church We preach Christ and him crucified

30/05/2026

KUIELEWA INJILI WITH PASTOR ROBERT

16/05/2026

KUIELEWA INJILI WITH PASTOR ROBERT MWAISAKA

09/05/2026

KRISTO NA KANISA(HUDUMA) - Pastor Shadrack Lugala

UPANDE WA KIHISTORIA WA BIBLIA.Mojawapo ya makosa unayoweza kuyafanya ni kudhani kwamba Biblia uliandikiwa wewe.BIblia i...
08/03/2026

UPANDE WA KIHISTORIA WA BIBLIA.

Mojawapo ya makosa unayoweza kuyafanya ni kudhani kwamba Biblia uliandikiwa wewe.

BIblia iliandikwa Kwa ajili Yako, lakini haikuandikwa Kwako(The Bible was written for you, not to you).

Katika Fahamu za waandishi wa Biblia, hukuwepo wewe, Bali kulikuwa na hadhira maalumu kabisa ya wakati wao waliyoikusudia.

Kutokana na hili, Mazingira Yao yaliamua matumizi ya misamiati mbalimbali katika uandishi wa Biblia, ambayo siyo lazima iwe misamiati tunayoitumia sisi katika Jamii yetu.

Kwa sababu Biblia ni kazi ya Fasihi, ambayo inahusisha matumizi ya Lugha. Hakuna Namna inaweza kutenganishwa na ushawishi wa Utamaduni wa Jamii husika katika matumizi ya lugha.

K**a utamaduni wao sio utamaduni wetu, basi lazima tutambue kwamba misamiati iliyotumika kuandika Biblia inaweza isiwe Kwa Hakika ile ambayo tunaitumia katika Jamii zetu. Maneno yanaweza kufanana Kwa sababu watafsiri wa Biblia waliyaweka katika namna yanayoweza kusomeka katika lugha zetu. Kufanana Kwa maneno hakuamui kufanana Kwa maana.

Kwa sababu hii, inamlazimu mwalimu na mwanafunzi wa Biblia kuwa makini katika usomaji wa Biblia Kwa kutumia lugha zetu, lakini akiwa anafanya hivyo anapaswa awe na heshima kubwa Kwa lugha ya asili ya uandishi wa Biblia ambayo iliathiriwa na utamaduni wao.

Misamiati ya Biblia Ina msingi wa kihistoria. Hii historia inapaswa iheshimiwe tunaposoma maandishi husika Ili tusipoteze maana iliyokusudiwa na waandishi.

Kwa mfano;

Wakati Musa anaandika kitabu Cha Mwanzo, aliandika Kwa upekee kabisa kwa ajili ya Jamii ya Wana wa Israeli waliotoka Misri kuelekea Kanani, akiwafunulia Mpango wa Mungu wa wokovu uliokuwepo Toka Mwanzo Ili waweze Kuamini Kwa ajili ya Wokovu. Matukio ya kwenye kitabu Cha Mwanzo yalichukuliwa kutoka katika Jamii ya Mashariki. Kwa hiyo utamaduni wa mashariki umeathiri Kwa kiasi kikubwa matumizi ya misamiati na uundaji wa matukio ya kwenye kitabu Cha Mwanzo.

Utakuwa huitendei Haki Biblia, Wala hujitendei Haki wewe mwenyewe k**a msomi wa Biblia ukilipuuza hili.

Unaposoma misamiati k**a "Agano", "Haki ya mzaliwa wa kwanza", "madhabahu" n.k , hupaswi kuisoma katika muktadha wa Jamii ya wamburu au wamasai.

Unaposoma matukio k**a ya "kukata Agano", "Ibrahimu kumpa Melkizedek sehemu ya 10 ya nyara za vita", "Esau kupoteza Haki ya mzaliwa wa kwanza" n.k

Utamaduni wa Jamii ya Mashariki unapaswa ukujie kichwani mwako Katika uundaji wa matukio husika. Kwa hiyo unapoyapa tafsiri matukio hayo ni lazima utamaduni wao ukusaidie kuweza kupata tafsiri sahihi, nje ya hapo utapoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi hatimaye utapotoka na kuwaingiza wengine katika upotovu.

Kujifunza lugha ya asili ya maandishi ya Biblia itasaidia kuweza kuelewa muktadha wa matumizi ya misamiati husika, Kwa sababu utamaduni una athari kwenye matumizi ya Lugha.

Huu ni wito Kwa ajili ya Juhudi na umakini katika usomaji wa Biblia nje ya hapo utamtukana. Kila mtu anayefundisha kinyume na Elimu yako inayopuuza haya niliyoyaandika Hapa.

Kufanikisha hili "unamhitaji mwalimu"

Rudia Tena Kusoma sentensi Ya Mwisho.

Robert Mwaisaka,
Grace and Truth Int. Church,
Bunju B, Dar es salaam.
0657922658

07/03/2026

07/03/2026

Uchaguzi wa Mungu upo katika Kristo

Address

Mbweni, Masaiti
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Grace and Truth Int Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Grace and Truth Int Church:

Share