22/11/2022
ILINITISHA.! HILI NI JAMBO LA KWELI LILILOTIKISA MAISHA YANGU.
MTOTO WAKO HAITAJI TU ELIMU IMSAIDIE KUKUA KITAALUMA. HAITAJI TU ELA ILI KUMSAIDIA KIUCHUMI.
ANAHITAJI NGUVU KUBWA YA IMANI KUMUOKOA NA NGUVU ZA KIPEPO. HATA WEWE MWENYEWE
K**A HUJAWAHI ONA HUWEZI AMNI. NAKWAMBIA HIKI KISA KILICHOHARIBU MAISHA YANGU NA KUBADILI MWELEKEO. KISA CHA KWELI KILICHONIPATA NIKIWA SHULE.
Asubuhi na mapema kipindi cha Math(Hisabati) kikaanza huku mwalimu akionekana mwenye furaha tofauti na siku zote. Ilinishangaza lakini sikuitilia maanani kwani furaha au huzuni ya mwalimu ni maisha yake mwenyewe. Nilisogeza kiti changu kwa mbele taratibu, nikakaa vizuri kwenye meza yangu ambayo siku zote ilikuwa ikikaa mbele upande wa ukutani. Haikuwa ngumu Sana hivyo nilielewa yaliyokuwa yakifundishwa. Nikiwa nimetulia tuli nazidi kusikiliza, nikasikia sauti kali na nzito kutokea nyuma ikiniita.! La haula.! Ilinishtua sio kwamba lilikuwa jambo geni kuitwa, bali ile sauti ilitisha kwani haikuwa ya mmoja wa wanafunzi darasani wala mwalimu ubaoni. Nilishtuka sana nikaogopa lakini nikajikaza kiume nikageuka nyuma taratibu nikaona watu wote wametulia wanamsikiliza mwalimu. Kwaiyo hawakuiskia sauti? Kwaiyo hawakuuona uso wangu ulivyo jaa tafurani? Nilijua tayari mambo yashaharibika kwani hiyo sauti haikuwa ngeni masikioni kwangu kwani kila nikiisikia huwa mambo yanaharibika. Nilirudisha macho ubaoni nikakuta ubao umeshajaa maandishi Mwanzo hadi mwisho. Kwamba mwalimu ashafundisha somo refu kiasi icho? Sikuelewa.!! nilivyokaza macho ubaoni Ili nijitahidi kunakili haraka haraka mifano iyo, niligundua kitu cha tofauti kwenye maandishi. Hayakuwa maandishi ya kawaida. Ilikuwa michoro ya kutisha makaburi, masanamu ya kutisha, na alama za XX huku jina langu likiwa limechorwa kwa herufi kubwa hapo ubaoni. Nilianza kutetemeka mwili, huku jasho likitiririka k**a maji, mak**asi yalianza kunidondoka. Mara sauti ile ikasikika tena, muda huu iliita kwa nguvu, kwa kitisho tena ilikuwa karibu nyuma yangu....inaendelea