Tumekaribia Nyumbani

Tumekaribia Nyumbani Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tumekaribia Nyumbani, Religious organisation, Tabata kimanga, Dar es Salaam.

Kuufikia ulimwengu kwa ujumbe wa malaika watatu k**a ulivyooneshwa katika Ufunuo 14:6-12, kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo ulio karibu sana

PAMBANO KUUKwa namna fulani hatujui ni kwa nini hasa dhambi ilizuka katika viumbe vikamilifu vya Mungu, na kwamba dhambi...
10/11/2021

PAMBANO KUU
Kwa namna fulani hatujui ni kwa nini hasa dhambi ilizuka katika viumbe vikamilifu vya Mungu, na kwamba dhambi hiyo ikawa ni mwanzo wa kile tunachokielewa k**a "Pambano kuu". Hata hivyo tunajua jambo moja, na tunalijua vizuri sana pia kwamba : k**a wanadamu tumenasa katikati ya pambano hili kuu. Ni pambano ambalo kati yetu hakuna awezaye kulikwepa.

Ufunuo 12 : 7-9, Biblia inasema kulikuwa na vita mbinguni. Hatujui vita mbinguni inamaanisha nini; yaani, hatujui ni aina gani ya mapambano halisi yaliyopiganwa zaidi ya kutupwa shetani na malaika zake. Ukweli ni kwamba Biblia haisemi chochote kuhusu matokeo ya kimwili ya mgogoro huu uliotokea mbinguni badala yake inashughulika na matokeo yake ya kiroho hapa duniani

Katika kiini cha vita siku zote huwa kuna swala linalogombaniwa, linaweza kuwa masuala ya mipaka, maslahi ya kiuchumi, kitamaduni au itikadi kali. Vita ya mbinguni k**a inavyoelezwa na unabii wa ufunuo licha ya kutopiganwa kwa zana za kidunia, haijapungua katika ukali. Ni vita ya kiroho, ikiwa na taswira za kimaadili na kisheria. Suala linaloshindaniwa ni sheria ya Mungu.

Shetani si msh*taki wa ndugu tu pia ni msh*taki wa Mungu. Amekuwa akidai kuwa sheria za Mungu si za haki na ni za kidhalimu. Jambo hili sasa ni lazima liamuliwe katika uwanja wa vita wa ulimwengu ambao ni utii wa mwanadamu. Wakati ibilisi anatumia udanganyifu, kupotosha ukweli, kupiga vijembe, kulazimisha uharibifu na silaha zingine za aina hiyo, silaha aliyoichagua Kristo ni upendo

Pambano kuu lilikuja duniani wakati Shetani alipowadanganya Adam na Hawa kwa ulaghai na udanganyifu, akageuza utii wao kutoka kwa Mungu kwenda kwake mwenyewe. K**a wangeendelea kuwa waaminifu kwa kile ambacho Mungu alikuwa amewaambia, k**a wangetii maagizo yake rahisi, dunia hii tunayoijua pamoja na maumivu yake, majaribu na mateso visingekuwepo kamwe.

Katika kushughulikia hili janga, Mungu ambaye alikuwa ameliona hili likitokea "kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu (Efe 1: 4), aliandaa mpango wake wa wokovu. Ni ule ambao tunaujua k**a mpango wa ukombozi na si mwingine zaidi ya kumtoa mwanaye pekee kuja kurejesha imaya iliyokuwa imeporwa kutoka kwa Adam na Hawa. Yesu alifaulu mahali ambapo Adam alishindwa.

Yesu alipata ushindi dhahiri pale msalabani, sikuzote changamoto imekuwa ni mahali tunapoweka utii wetu, upande ulioshinda au upande ulioshindwa. Pambano bado linapamba moto na udanganyifu upo siku zote, vita juu ya mioyo na akili zetu inaendelea kwa hiyo tumaini na ombi letu ni kwamba kwa neema ya mungu tuujue udaganyifu wa shetani na hivyo itusaidie siyo tu kumchagua Kristo, gali pia kuendelea kuwa naye kwani, k**a alivyoahidi "atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka" (Mt 24 : 13).

MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI UJUMBE HUU

Ni miaka imepita sasa tangu unabii wa Daniel kutolewa, falme zimepita tena k**a zilivyotabiliwa kwenye njozi ya mfalme N...
20/05/2021

Ni miaka imepita sasa tangu unabii wa Daniel kutolewa, falme zimepita tena k**a zilivyotabiliwa kwenye njozi ya mfalme Nebukadneza Danieli 2 : 31-45

Watawala wenye nguvu na mashuhuri wameinuka ulimwenguni na hatimaye wakaanguka, Dunia imeshuhudia nyakati tofauti tofauti za usitawi pamoja na huzuni, maisha ya mwanadamu yamekuwa machungu na tena ya kukatisha tamaa,,

Lakini katikati ya dhoruba liko tumaini, hakika dunia inaweza isiwe mahali salama, jambo jema ni kwamba tuna mji umeandaliwa baada ya haya yote kupita hatimaye tutaiacha dunia yenye huzuni, vita, njaa, mateso, magonjwa, misiba,

Mwokozi wetu YESU alitoa ahadi ambayo itatimia wakati mfupi ujao "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi, Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi ; K**a sivyo ningaliwaambia maana unaenda kuwaandalia mahali, Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali nitakuja tena niwakaribishe kwangu ili nilipo mimi nanyi mwepo. Yohana 14:1-3

Jipe moyo mpokee YESU awe Bwana na mwokozi wa maisha yako hakika hatuko mbali " Tumekaribia nyumbani"

Ubarikiwe mpendwa

"TUMEKARIBIA NYUMBANI"Ni karne ya 21 sasa na dunia inaenda kasi sana, mwanadamu amepiga hatua kubwa katika maendeleo ya ...
15/02/2020

"TUMEKARIBIA NYUMBANI"

Ni karne ya 21 sasa na dunia inaenda kasi sana, mwanadamu amepiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na pia ki-teknolojia.

Ndani ya karne hii dunia imeshuhudia visa vingi vya ukosefu wa amani , Vita kila mahali, vitendo vya ukatili, mauaji ya kutisha, unyanyasaji wa kingono, matetemeko ya ardhi, bahari kuvuka kingo zake na kufunika watu na majumba , majanga ya moto, vimbunga, joto kuongezeka, ukosefu wa maadili, uharibifu mkubwa wa mazingira na kubwa zaidi magonjwa hatari na yenye kutisha ambavyo vyote kwa pamoja vimegharimu maisha ya maelfu ya wanadamu.

Ni dhahiri kwamba dunia haiko katika wakati wa furaha kwani kila kukicha taarifa za habari na vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kutangaza matukio ya hatari na ya kutisha na hofu imetanda karibuni kotekote.

Ushahidi wa kijiografia na tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kwamba kwa karibu miaka michache ijayo dunia inaweza kuwa sio mahali salama pa kuishi. Achilia mbali hizo tafiti zote na uweke uelewa wako wa kawaida, utakubaliana na mimi kwamba kutokana na mikasa yote inayomkumba mwanadamu katika zama hizi basi dunia haiko katika hali nzuri kila mtu ana hofu, maisha yamekuwa machungu ni kana kwamba kuna jambo la kutisha li karibu kuikumba dunia.

Mtu aweza kujiuliza je kuna maisha baada ya maisha ya hapa duniani,,?? Jibu ni NDIO Kuna maisha na tumaini liko, takribani miaka elfu mbili iliyopita alizaliwa mkombozi YESU KRISTO ambaye alitoka mbinguni kuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini na kabla ya kurudi mbinguni kwa baba yake alitabiri kuhusu dalili za kurudi kwake kuwachukua watakatifu wake na kuwapeleka katika makao ya amani mbinguni juu, kinachotokea duniani wakati huu ni utimizwaji wa unabii huo na hapana shaka "TUMEKARIBIA NYUMBANI"

YESU alisema "Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu" YOHANA 16:33

MUNGU akubariki sana

Address

Tabata Kimanga
Dar Es Salaam

Telephone

+255757636765

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tumekaribia Nyumbani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share