Neno La Leo

Neno La Leo Neno La Leo is here to provide all people with daily word of God from the Holy Bible.

31/05/2026

2Timotheo1:5-6
"nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki,ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi,na katika mama yako Eunike,nami nasadiki wewe nawe unayo. Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu,iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu."

Imani thabiti inaweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine k**a Timotheo alivyoirithi.
HEBU LEO TUMSHUKURU MUNGU KWA KUWA AMESIKIA MAOMBI NA TOBA YETU NA MALENGO YETU MAPYA KATIKA KUIKABILI NUSU NYINGINE YA 2026, Huku tukiamini tumeacha alama kwa vizazi vijavyo!
AMEN

30/05/2026

MWANZO 21:1-2
“Bwana akamwangalia Sara k**a alivyo kuwa amesema, naye akamtendea k**a alivyokuwa amenena.
Sara akachukua mimba, akamzalia Ibrahimu mwana katika uzee wake, kwa wakati ule Mungu aliokuwa amemwahidia.”

Tunapouhitimisha mwezi wa tano, tunaamini Mungu aliyemtembelea Sara na kutimiza ahadi yake ndiye Mungu wetu leo.
K**a Sara alivyopokea muujiza wake baada ya kusubiri, nasi tupokee majibu yetu na tuzae matunda kwa utukufu wa jina lake.

Bwana atukumbuke, atutembelee, na atujibu maombi yetu kwa wakati wake mkamilifu.

29/05/2026

ISAYA 42:16
"Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha"

Kwa mwezi mzima tuliazimia kugeuza mienendo yetu na kumrudia Mungu kwa Imani thabiti isiyotetereka ,basi tunaamini Mungu atatuongoza kwa namna ambayo haielezeki. Atatuvusha na kutuokoa kwa namna ya ajabu kwa ajili ya utukufu wake!
TUMTUMAINIE MUNGU MAANA AMETENDA!

28/05/2026

HESABU 6:24-26
"BWANA akubarikie, na kukulinda;BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;
BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani"

K**a tulivyoamua toka mwanzo wa Mwezi wa tano kuwa tujitafakari na kuomba Toba ya kweli ili tunapoingia nusu ya pili ya mwaka 2026 tuwe tayari kuzipokea Ahadi na Baraka zote Mungu alizotuandalia,
Amani yake itatufuata kila siku maishani.
TUNAAMINI AHADI HIZI ZINAENDA KUTIMIA KWETU K**A MUNGU ALIVYOAHIDI.
AMEN.

26/05/2026

1 NYKT 4:10
"Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba"

Bado tunayo nafasi yakumrudia Mungu kwa Imani thabiti,Toba ya kweli,na maamuzi toka moyoni ya kubadili mienendo yetu isiyofaa ,NAYE ATATUPA KILA AINA YA USAIDIZI,ULINZI NA FURAHA YA MILELE.

25/05/2026

ZABURI 103:3-4
"Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema"

Ni majira na nafasi maalumu kwa Mwezi huu wa tano kujitafakari kwa kina ,kubadili njia zetu zusizompendeza Mungu na Yeye ameahidi kutuosha uovu wetu na kutuponya roho na miili yetu dhidi ya maradhi,umasikini,na mauti.
Pia atatutenga na wasioamini na kutupa rehema zake.
Hatujachelewa,ni majira yetu sasa,kwa Imani tumrudie yeye kwa Toba yenye ISIYO NA SHAKA MAANA AMEAHIDI,NA ATATENDA MENGI KULIKO TUNAVYODHANI.

24/05/2026

YAKOBO 5:17-18
"Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake"

Mungu ametupa Uwezo wa kufunga na kufungua jambo; ila lazima kwa Imani k**a Eliya, tuliishi Neno lake kwa kumaanisha toka nafsini kwetu,na hakika yeye atatupa kila aina ya usaidizi!
Tuamue sasa, kumcha Mungu k**a Eliya,na Mungu atatukuzwa kupitia matendo yetu!
HAKIKA KUFUNGA NA KUFUNGUA KU NDANI YA UWEZO WETU!

23/05/2026

ZABURI 1:3
"Naye atakuwa k**a mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa"

Siku y leo na siku zote zizilizoko mbele yetu Mungu akatupande k**a mbegu izaayo sana katikati ya mito na vijito, tukazae matunda kwa majira, lolote letu lisinyauke na kila tufanyalo kikachanue na kuzaa matunda mema sana,ili Mungu wetu akapate Utukufu.
KATIKA JINA LA YESU KRISTO.AMEN

22/05/2026

AYUBU 1:1
"Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu"

Ukamilifu na uelekevu, kuamcha Mungu na kuepukana na uovu zikawe sifa zetu kuanzia sasa mpaka mwisho wa maisha yetu hapa ulimwenguni!
HII IKAWE SALA NA MAOMBI YETU KWA MUNGU TOKA SASA,NAYE ATATUKUMBUKA K**A AYUBU.
AMEN

21/05/2026

ZAB 109:3-4
"Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka,
Wamepigana nami bure,
Badala ya upendo wangu wao hunish*taki,
Ijapokuwa naliwaombea"

Mungu utukinge na kutusaidia pale ambapo watesi wetu na wale wote, tunaowapenda na kuwaombea ila wao hukaa mafichoni na kutuumiza kwa maneno ya chuki ,laana na kutuonbea mabaya!
*lMUNGU UWE NGAO YETU DHIDI YA MANENO YA CHUKI NA MASHAMBULIO MABAYA YANAYOTOLEWA NA WATESI WETU.

AMEN

Address

70377
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 06:30 - 22:45
Tuesday 06:30 - 22:00
Wednesday 06:30 - 22:30
Thursday 06:30 - 22:30
Friday 06:30 - 22:45
Saturday 06:00 - 22:45
Sunday 08:30 - 20:00

Telephone

+255620180668

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Neno La Leo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share