19/05/2022
Kupima.
Sio kila huduma ( ministry ) inayoinuka / kanisa linalochipuka ni feki.
Kuna kitu kipya ambacho hakipo mahali unaposali Unaweza kujifunza.
Vile vile sio kila huduma inayoinuka au kanisa linalochipuka ni la kuaminika.
Wengine feki wanataka kutumia ujinga k**a kigezo cha kuwatumikisha watu.
Jifunze kupima.
Ndio alisema tutawambua kwa matunda yao.
Lakini embu jiulize , vipi k**a wewe ndio hilo shamba?
Upo tayari kusubiri matokeo?
Upo tayari kusubiri uone ni zao gani litamea ndio ufanye maamuzi ?
Vipi k**a yatakuwa matokeo hasi.
Wengi wameona isiwe kesi , wameamua kujiaminisha kuwa hakuna jipya Kwenye hizi huduma na haya makanisa.
Je ni kweli?
Jibu ni hapana.
Yapo mengi ya kujifunza ambayo pengine Mfumo / msingi wa kanisa / kusanyiko / dhehebu ulilopo huwezi kujifunza au hairuhusiwi kufundisha kutokana na sababu za kimapokeo ( Dogmas )
Kwa hiyo Ukiona kuna huduma imeinuka nje ya kusanyiko ulilopo pengine pioneer wake alikuwa mtu wa kwenu ila ameamua kuanzisha hiyo huduma pembeni kidogo ,embu punguza spidi kidogo , weka hisia pembeni , tafakari katika misingi ya neno , kabla hujaanza kuzungumza kinyume na huyo mtumishi , kabla hujaanza kumwita majina ya ajabu ajabu , feki , msaliti , mlafi wa madaraka ,mpenda fedha n.k
Vile vile tafakari kwa kina kabla hujaanza kutoa support yako ya kifedha n.k
Kwa sababu kwa kusaidia huduma feki itajiungamanisha na madhara pasipo kujua , vile vile kwa kusaidia huduma ya kweli utajipatia thawabu mbele za Mungu.
Kwa sababu billia inasema:
Mathayo 10:40-42
[40]Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.
Vile vile kanisa la thiaira lilionywa kuhusu manabii wa uongo:
Ufunuo wa Yohana 2:20-23
*Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. ]Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; nami nitawaua watoto wake kwa mauti.
Kwa hiyo ni vyema ukajua kupima kila huduma katika misingi ya neno ili uweze kunufaika na huduma ambazo Mungu anaziinua.Kwa mtu aliyeoka , na Roho mtakatifu yupo active ndani atajua tuu hapa kuna kitu hakipo sawa.Roho mtakatifu ni mwaminifu ataku alert tuu.
Tatizo ni kwamba k**a haupo vizuri Kwenye neno na umdhaifu rohoni Hisia zinaweza kukuzidi kete ukajikuta unampotezea Roho mtakatifu.Na hawajamaa feki wanajua sana kucheza na hisia za watu hawajagi kichwa kichwa , they are professional killers in the spirit
Ulimwengu wa sasa unapiga hatua sana katika eneo la maarifa.
Sio elimu - Dunia tuu , maarifa ya kiroho yanaongezeka kwa kasi sana.
Madamu ule Mwisho haujafika , Bado kuna vitu vingi sana hatujavijua , Bado kuna kweli nyingi sana zitazidi kufunuliwa.
Madamu hutajifikia katika ule ukamilifu , hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo basi kuna mengi sana ya kujifunza.
Kwa nini ipo hivi ?
Kwanza ni hatari sana kupokea huduma inayoinuka katika ya kusanyiko bila kuwa na uhakika wa hiyo huduma.
Pili , madhehebu / makanisa / huduma zilizopo ni kazi ya Mungu ambayo kwa sehemu fulani inajumuisha utashi wa kibinadamu yaani pioneers.Kwa hiyo inaweza kuhitaji mabadiliko makubwa sana ya kimfumo ili kuondoa hicho kiasi cha utashi kilichotumika kitu ambacho wengi hawawezi kuvumilia kwa sababu zisizo na mashiko kiroho ( sababu binafsi ).Na kwa sababu hawapotayari kubadili hiyo misingi ni ngumu sana hizi huduma mpya kufanikiwa katikati ya hilo kusanyiko kwahiyo wengi
Je , kiwango cha utashi wa kibinadamu kilichotumika kinafanana dhehebu moja na jingine?
Jibu ni hapana
Kiwango cha utashi kilichotumika kinatokana na kiwango cha ufahamu alichokuwa nacho huyo pioneer kipindi anaanza hiyo huduma.kwa hiyo haiwezekana ukakuta kuna dhehebu lipo perfect 100 % ingawa yametofautiana level of perfection kutokana na bidii yayoweka katika kulisoma na kulifafanua neno , kumtafuta Mungu Na hatua ya ukuaji kiroho ( growth stage which has nothing to do with the age ).
Kitu pekee ambacho Unaweza kufanya ili kuhakikisha hubaki nyuma kiufahamu , ni kijikita katika kusoma na kulifafanua neno katika nuru ya Yesu Kristo yaani kazi ya msalaba.
Update your mind day after day
Hapa lazima utahitaji waalimu waliojikita kutoa mafundisho ya kitume ili wakutengenezee msingi imara , kwa kufanya hayo utajijengea uwezo mzuri wa kuchambua huduma inayoinuka kila siku.
Kwa nini mafundisho ya kitume?
Waefeso 2:20 biblia yasema:
[20]Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
Mitume katika kutufundisha , manibii katika kututhibitisha.
Yaani Mitume kwanza , manabii baadae.
Shalom.