12/01/2026
MAMBO YANAYOTOKEA PAPO HAPO MTU WA MUNGU ANAPOTENDA DHAMBI
đź“–Mwanzo 3:1-24
📍Kutengwa na Mungu (Kifo cha kiroho)
Mtu wa Mungu anapotenda dhambi tu, hutengwa na Mungu
Kitendo cha kutengwa na Mungu ndio kifo cha kiroho ndani ya mtu.
Ikumbukwe kwamba:
"Kifo cha kiroho hutangulia kifo cha kimwili, na kifo cha kimwili anachokutana nacho mwanadamu sasa ni Matokeo ya kifo cha kiroho alichokutana nacho Adamu pake Edeni".
đź“–Mwanzo 2:17
[17] walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, "kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika."
Adamu alipotenda dhambi pale pale alitengwa na Mungu(kufa kiroho).
Nuru na giza havikai pamoja, Dhambi ni giza na utakatifu ni nuru, shetani alipopewa nafasi kwa ruhusa ya Adam ndipo Mungu alijitenga naye automatic
Mwanadamu akapoteza ushirika wake na Mahusiano yake ya karibu na Mungu
📍Kupoteza sura ya Mungu ndani yako.
Mwanadamu aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu kwa namna alivyo kuwa kabla ya dhambi.
đź“–Mwanzo 1:26, 1Petro 2:17
Ukamilifu wa Kiungu ulikuwa ndani yake, aliwa,a katika ukamilifu wa Kiungu, alienenda katika ukamilifu wa Kiungu, aliamua katika ukamilifu wa Kiungu.
Kabla ya dhambi, Adamu anafanya kazi ukamilifu ya kutoa majina kwa viumbe vyote na anagindua hakuna wa kufanana naye
Baadaye Mungu alimtia katika Usingizi mzito asijitambue, akamuondolea sehemu ya ubavu na kumuumba Eva kutoka katika mifupa na nyama zake , akamweka karibu yake akaondoka
Adamu alipokuja kuamka katika Usingizi wake alipimuona tu Eva, akatambua huyu ni nyama katika zangu na mifupa katika yangu,
Anasema ataitwa mwanamke kwa sababu alitoka kwa mwanaume, Tena akampa na jina ataitwa Hawa (Eva) mama wa wote walio hai
Sasa ukiangalia hapa, unagundua Adamu alikuwa moamilifu katika njia zake kwa sababu akili, ufahamu na mawazo yake yalikuwa makamilifu hivyo alikuwa anaona mambo k**a Mungu alivyoyafanya ingawa wakati Mungu anafanya yeye hakuwepo.
Dhambi ilipokuja ilimfarakanisha mtu na sura ya Mungu ndani yake, ndipo kukatokea gap kubwa sana kati ya Sura na Mungu na mwanadamu.
Hata imekuwa mawazo ya Mungu na mwanadamu vimeachana patefu sana, njia za mwandamu na ufahamu wake vimeachana mbali na sana na alivyo Mungu kwa sababu sura ya Mungu haipo Tena ndani ya mwanadamu.
Hivi ndivyo inavyotokea kwa mtu wa Mungu anapotenda dhambi, Kuna kuwa na muachano mkubwa sana kati yake na Mungu katika mtazamo, mawazo na njia. [Isaya 55:8-9]
📍Kupoteza Haki na Mamlaka.
Mungu ni mtawala wa mbingu na nchi, alipomfanya mwanadamu kwa sura na kwa mfano wake alimweka awe mtawala wa nchi.
Hivyo mwanadamu alikuwa na Haki pamoja na mamlaka ya kutawala nchi kwa sababu ya sura na mfano wa Mungu aliokuwa amepewa.
Lakini, baada ya anguko Adamu alipoteza Haki na Mamlaka ya kutawala nchi kwa sababu alikuwa mateka wa shetani kuqnzia hapo akawa mtumwa wake
Kila mtenda dhambi ni mtumwa wa dhambi
Ikumbukwe kwamba:
Dhambi unaweza kushinda kabla hujatenda kwani wewe unakuwa na nguvu na dhambi inakuwa DHAIFU kwako, lakini dhambi ukiisha kutenda tayari imekushinda na wewe ni mateka na mtumwa wake kwani I akuwa na nguvu dhidi yako nawe unakuwa DHAIFU dhidi yake.
Badala ya kutawala mwanadamu anakuwa mtumwa wa dhambi chini ya shetani
Ndiomaana mtu akitenda dhambi mara moja ni rahisi zaidi kutenda Tena na tena, na zaidi sana ni rahisi KUONGEZA na dhambi nyingine nyingi juu yake.
Daudi alitenda dhambi ya kuzini na mke wa Uria, ikazaliwa dhambi ya uongozi haraka, mara ikazaliwa dhambi ya kuua hapo hapo, akamuua Uria
Hii ndio kuwa mtumwa wa dhambi chini ya shetani, unaweza kutumiwa kufanya dhambi yoyote k**a shetani apendavyo.
📍Hukumu ya Mungu huanzia papo hapo.
Adamu alihukumiwa pale pale katika bustani ya Eden, Mungu alitamka hukumu zake kwa Adamu, Eva na kwa nyoka
Wakati mtu anasubiri kifo cha kimwili, akishatenda dhambi papo hapo anahukumiwa na matokeo ya hukumu huanza kufanya kazi kuanzia hapo
Adamu alifukuzwa kwenye bustani ya Eden,
Ardhi ililaa iwa kwa ajili yake
Akazidishiwa taabu, mzigo na ugumu wa maisha
Kwamba itamgharimu jamsho na MAUMIVU ili aweze kula na kunywa
📍Kuondokewa na utukufu wa Mungu.
Utukufu ni vazi la Kiungu ambalo huwavika na kuwafunika watu wa Mungu
Utukufu wa Mungu ni uwepo wa Mungu, nuru ya Mungu na kibali cha kiungu juu ya mtu.
Utukufu wa Mungu k**a vazi, hufunika aibu na madhaifu au mapungufu ya mwanadamu.
Utukufu wa Mungu, hufunika maisha ya mtu wa Mungu na kila kitu chake na afanyacho hufunikwa nao, hivyo huonekana kiutofauti hata k**a ni cha kawaida sana
Adamu na Eva walikuwa uchi wote wawili, lakini kwa kuwa walifunikwa na utukufu wa Mungu hawakuoneana haya
Lakini walipotenda dhambi, ndipo utukufu wa Mungu ukajitenga nao Ikawa ni k**a mtu aliyevuliwa nguo mbele ya watu.
Wote wawili wakajikuta wako uchi, wakaoneana haya wakakimbia na kushona majani ili kuficha aibu yao.
Mtu akitenda dhambi, uwepo na utukufu wa Mungu hujitenga na kuondoka na hapo ndipo aibu ya mtu huwa peupe na kufuatana naye huonekana wazi kwa kila mtu.
📍Kuondokewa ulinzi wa Mungu.
Mungu huwalida watu wake kwa ulinzi wake ili wasivamiwe na nguvu za falme na mamlaka nyingine.
Lakini dhambi hutendeka kwa hiari ya mtu mwenyewe kwa Ushawishi wake, dhambi ikishatendeka hufukuza ulinzi wa kiungu na kufungua milango ya uvamizi wa nguvu za giza.
Utukufu wa Mungu na uwepo wa Mungu huondoka pale dhambi inapoingia na kuchukua nafasi kwenye maisha ya mtu
Uwepo wa Mungu na utukufu wa Mungu ni kinga, ni boma, na ulinzi wa Kiungu juu ya mtu wa Mungu wakati wote awapo Mtakatifu.
Dhambi inapochukua nafasi kwenye maisha ya mtu ndipo uwepo na utukufu wa Mungu hutoweka na kujitenga mbali, mtu huwa k**a mji ulioachwa wazi wezi na wavamizi huingia k**a wapendavyo.
Uvamizi wa nguvu za giza k**a vile mapepo huwa rahisi sana kwa mtu ambaye ameondokewa uwepo na utukufu wa Mungu kwa sababu ulinzi wake umeondolewa.
Dhambi humwondolea mtu utiisho na nguvu za Mungu, na kumfanya kuwa mtu wa kawaida sana asiye na madhara kwenye ulimwengu wa roho wa giza.
Hivyo basi;
Ni muhimu mnoo kutunza utakatifu ulio nao kwa sababu ndio uzima wako, sura ya Mungu kwako, ndio nguvu yako, ndio HAKI na mamlaka yako, ndio ulinzi na usalama wako.
Mungu akubariki sana, karibu icc
Pst. Simon Mwamakimbula
Tag - icc king'azi - Mungu Kwanza
Sunday, 11 January 2026
Simu: +255755153801