Efatha Church-Kigamboni TV

Efatha Church-Kigamboni TV Healing & Deliverance by the Blood of JESUS CHRIST.

Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye as...
30/08/2026

Nehemia 8:10 “Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.”

Furaha ya Bwana inapokuja ndani yako inakupa nguvu, inakupa kuwa hodari na shujaa kwa nini? Kwa sababu kile ulichokula ndicho kinachokupa furaha, kipi hicho? Neno la Mungu linakupa furaha, na ni nguvu yako. Unapopata hiyo furaha inakupa nguvu na wepesi.

Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.”

Nini maana ya furaha ya wokovu? Unapokula Neno la Mungu ambalo ni mkate wa uzima linakupa furaha. Roho ya wepesi ni nini? Ni kujua namna ya kufanya mambo kwa haraka na kwa wakati pasipo kupoteza majira yaliyowekwa. Kwa maana kuna muda wako wa kuanzisha biashara, kujenga au kuanziasha jambo fulani sasa kwa wewe kulijua Neno litakupa furaha na hiyo furaha itakusaidia kufanya mambo kwa wepesi na kwa wakati sahihi.

Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.”
Kwa kulifahamu Neno unakuwa unatenda katika haki na ukamilifu, kwa nini Neno lina nguvu namna hii? Neno lina nguvu ili kukufanya wewe uwe mshindi katika kila eneo la maisha yako.

Neno la Mungu lina maeneo saba ya muhimu sana:-

1. Ukilielewa Neno kamwe hauwezi kuwa masikini,
2. Neno ni mkate wa uzima: linatupa nguvu,
3. Neno ni mwanga wa miguu yetu;
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”

Soma Neno, tafakari neno, kula neno, tamka Neno, kwa namna unavyofanya hivyo ndivyo unaruhusu neno likae ndani yako, namna unavyotenda na kukiri neno ndivyo linakaa ndani yako na kuanzia hapo kila utakachokitenda kitakaa kwa nini? Kwa sababu neno linakuwa ndani yako.

©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira

Unawezaje kupata uhai? Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Neno ndiy...
30/08/2026

Unawezaje kupata uhai?
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Neno ndiyo mkate, ukilisikia Neno la Mungu na ukalipokea ndipo imani inaumbika ndani yako kwa maana hiyo uhai unaumbika ndani yako na Neno linasema “Yote yawezekana kwake aaminiye.”

Sasa je! Kwa nini wewe unakwama k**a unayo imani? Ukiona unakwama maana yake ni kuwa huenda ulionja mkate (Neno la Mungu) haujalila na ndiyo maana kwako hakuna uhai kwa maana k**a ulikula huo mkate (Neno la Mungu) wewe utakuwa hai na kila ulichonacho kitakuwa hai.

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

Watu gani wanaruhusa ya kuomba? Yohana 10:9 “Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.”

Yule ambaye anaruhusa ya kuomba ni yule ambaye amekubali kukaa ndani yake mzima mzima, je unaingiaje ndani yake mzima mzima? Kwa namna unavyolifahamu Neno, namna unavyolifahamu neno ndivyo unavyoingia kwake.

1 Yohana 1:1-4 “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu)… ”

Ukifikia mahali pa kulijua Neno la Mungu ndipo imani inaumbika ndani yako na uzima unaumbika kwako pia; hapo ndipo furaha inaanza. Tunapozungumzia furaha ya Bwana tunazungumzia uhakika wa kujua kile kilichopo mbele.

©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira

NENO LA UZIMAWaefeso 6:10 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.” Huu mstari unaongele...
30/08/2026

NENO LA UZIMA

Waefeso 6:10 “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.”

Huu mstari unaongelea mambo mawili (2) ya kwake:
1. Uwe hodari
2. Uwe katika nguvu na uweza wake,

Haya ndiyo maeneo mawili (2) ambayo unapaswa kuyafahamu ili uweze kuwa mshindi, ua uweze kuwa na nguvu katika Yeye.

Nini maana ya kuwa hodari? Ni kuwa mshindi, yeyote ambaye ana nguvu huwa mshindi daima, mara zote aliye hodari katika mashindano ndiye anayechukua medali ya ushindi, hata darasani yule ambaye anawaongoza wengine anayeelewa masomo kuliko wengine ndiye aliye hodari; kwa nini ni hodari? Ni kwa sababu alielewa; kwa maana hiyo tunakuwa hodari kwa kuelewa.

Nini kinachotupa kuwa hodari?
Marko 9:23 “Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.” Yesu hapa alikuwa anamaanisha nini? Alimaanisha kuwa yeyote aaminiye ni hodari na anakuwa mshindi, kwa nini? Kwa sababu ana imani. Imani inakupa wewe ushindi katika kila jambo.

Luka 1:37 “kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.” Kwa Mungu kila jambo linawezekana hakuna lisilowezekana kwake, hii inamaana kuwa, mimi, wewe au yeyote akiwa na Mungu hakuna lisilowezekana.

Wafilipi 4:13 “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Kwa maana hiyo unahitaji nguvu ili uweze kufanya mambo yote na upate kushinda katika hayo yote.

Uweza au nguvu hiyo tunaipataje?
Yohana 6:51 “Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”

Uweza au nguvu hiyo tunaipata kwa kupitia Neno la Mungu ambalo litatupa sisi uzima. Mkate (Neno la Mungu) linatoa uzima, uhai unatoa uhai na mauti inatoa umauti, sasa! je! Wewe umebeba nini?

©Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira

2 Corinthians 9:7 “Each of you should give what you have decided in your heart to give, not reluctantly or under compuls...
30/08/2026

2 Corinthians 9:7 “Each of you should give what you have decided in your heart to give, not reluctantly or under compulsion, for God loves a cheerful giver.''

2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende k**a alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu hum...
30/08/2026

2 Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende k**a alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”

© Mtume Eliakunda Mwingira

TESTIMONY
30/08/2026

TESTIMONY

USHUHUDA
30/08/2026

USHUHUDA

Zaburi 145:1-5 ‘’Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.Kila siku nitakuhimidi, N...
30/08/2026

Zaburi 145:1-5 ‘’Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani.Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.’’

Address

Ungindoni
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church-Kigamboni TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church-Kigamboni TV:

Shortcuts

Share