Ushindi ministry

Ushindi ministry Isaya 41:10 Usiogope maana mi ni pamoja nawe ,usifadhaike maana Mimi ni Mungu wako nitakutia nguvu ,

08/08/2026

✓MAMBO MATANO YANAYOUA HATIMA NA KESHO ZA WATU

1. MAISHA YA ZINAA NA DHAMBI
Huu ni adui namba Moja kwa sababu kwenye zinaa kuna maeneo matatu kwa wakati moja ,kuna Nafsi, Utashi, na roho

✓Nafsi Inapenda raha ya sasa. Bila kuikandamiza inakugeuza mtumwa.
Na hata ukisoma Wagalatia 5:16 “Enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza matamanio ya mwili.”
✓kwenye Utashi ni Uwezo wa Kuamua ,Maana Mungu amekupa uwezo wa kuchagua. Utashi dhaifu ndio unaosema “mara moja tu”.
Yakobo 1:14-15 “Bali kila mtu hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe... kisha tamaa ikichukua mimba, huzaa dhambi.”
✓ kwenye eneo la Nyota ya Mtu / Vizingiti vya Kiroho,Zinaa inachanganya roho mbili kuwa moja. Unabeba mzigo wa mtu mwingine.
UKISOMA 1 Wakorintho 6:18 Maandiko yanasema “Kimbieni uasherati. Kila dhambi mtu afanyayo iko nje ya mwili; bali anayefanya uasherati anadhuru mwili wake mwenyewe.”
✓1 Wakorintho 6:16 “Hujui ya kuwa yeye aliyeungani
shwa na kahaba amekuwa mwili mmoja naye?”
✓Matokeo Yake ni kazi inakufa, fedha inatoroka, ndoto zinakatika, una mzigo usio wako. Mtu asiye huru kiakili hawezi kufuata hatima.

2. KUAHIRISHA MAMBO / UVIVU
Huu ni kaburi la ndoto. Unaua kesho yako kwa kusema “kesho”.
Methali 6:9-11 “Ee mvivu, utalala hadi lini? Utapata umaskini k**a mnyang’anyi, na upungufu k**a mtu aliye na silaha.”
✓Mhubiri 9:10“Cho chote mkono wako upatacho kukifanya, kifanye kwa nguvu zako zote.”

✓3. HOFU NA MAWAZO YA "SIWEZI"
Hofu inakufunga kabla hujajaribu. Inakukosesha kuingia kwenye ahadi ya Mungu.
✓2 Timotheo 1:7 “Kwa maana Mungu hakutupa roho ya uoga, bali ya nguvu, na ya upendo, na ya kiasi.”
Ukisoma Yoshua 1:9 “Sikuamuru mimi? Uwe na nguvu, uwe na moyo wa ushujaa. Usiogope wala usifadhaike...”

✓4. KULINGANISHA MAISHA YAKO NA YA WENGINE
Ulinganisho unaua shukrani na unafunga macho yako kuona fadhili za Mungu kwako.
2 Wakorintho 10:12 “...wakijipima wenyewe kwa wenyewe, na kujilinganisha wenyewe na wenyewe, hawana ufahamu.”
Zaburi 139:14“Nakushukuru kwa

07/08/2026
ufanikiwe katika mambo yote,Afya,elimu ,rohoni,n.k
27/07/2026

ufanikiwe katika mambo yote,Afya,elimu ,rohoni,n.k

Address

Temeke
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ushindi ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Ushindi ministry:

Shortcuts

Share