Eden holiness ministry

Eden holiness ministry Holiness for the glory of God and inheritance of enternal Life

27/12/2025

Mungu aliye hai afanikishe mipango Yako kirahisi sana 2026

21/12/2025

shalom shalom mtu wa Mungu.
nakuombea wewe pamoja na familia Yako mvuke salama mwaka 2025 na kuingia 2026

SOMO: “SADAKA INAPOTUMIKA KUTENGENEZA MAISHA YA FAMILIA YALIYOFUNGWA NA SADAKA” (Sehemu ya pili)MWL. CHRISTOPHER MWAKASE...
02/08/2022

SOMO: “SADAKA INAPOTUMIKA KUTENGENEZA MAISHA YA FAMILIA YALIYOFUNGWA NA SADAKA” (Sehemu ya pili)

MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.
SIKU YA PILI 22 JULAI 2022, TABORA

LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE
👉🏼https://youtu.be/Km-flK5j_CU

NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA
👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda

UTANGULIZI
LENGO LA SOMO
Kutumia mbinu za ki Biblia ili kujinasua toka kwenye vifungo vibaya vya maisha vinavyotokana na sadaka.

1Wafalme 12:26-27
“Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. K**a watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda.”

Alikuwa akijua siri iliyoko kwenye sadaka jinsi ambavyo inaweza kuk**ata moyo wa mtu na kuushikilia na kuusukuma kufanya vitu ambavyo yule mwenye huo moyo hakuwa hata amekiwazia. Lakini kuna nguvu zilizowekwa ndani ya sadaka ambavyo si watu wengi sana wanajua.

Leo nataka tuangalie kipengele hiki UHUSIANO WA SADAKA NA MWILI KIMAISHA

soma 1Wafalme 18:30,36-39
Kwa kujifunza jambo hili la Uhusiano wa sadaka na mwili kimaisha tuangalie mambo kadhaa ili uweze kuelewa kirahisi:-

JAMBO LA KWANZA
SADAKA INAWEZA KUTAWALA NA KUFUNGA MAENEO KADHAA YA MTU NA FAMILIA YAKE

1Wafalme 18:38
“Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji.”

Hii inaelezea jinsi ambavyo Eliya alitengeneza ile madhabahu na vitu alivyokuwa ameweka. Ukisoma vizuri utaona jinsi ambavyo alichukua mawe 12 yakiwakilisha watoto 12 wa Mzee Yakobo au kuwakilisha kabila 12 za Taifa la Israeli, pamoja na kwamba waliokuwa chini ya Rehoboamu walikuwa 10 lakini alikuwa anataka kutuonyesha ya kwamba kitu kilichofanyika pale kilikuwa kikigusa na wale wengine ambao hawakuwepo katika ile idadi. Kwa hiyo alikuwa akitafuta namna ya kuwakilisha kitu kizima mbele za Bwana.

SOMO:-"Sadaka Inapotumika Kutengeneza Maisha ya Familia Yaliyofungwa na Sadaka"Unaweza kutumia njia zifuatazo kutuma sadaka yako kwetu:- M-PESA ...

SOMO: “SADAKA INAPOTUMIKA KUTENGENEZA MAISHA YA FAMILIA YALIYOFUNGWA NA SADAKA” (Sehemu ya kwanza)~ MWL. CHRISTOPHER MWA...
02/08/2022

SOMO: “SADAKA INAPOTUMIKA KUTENGENEZA MAISHA YA FAMILIA YALIYOFUNGWA NA SADAKA” (Sehemu ya kwanza)

~ MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE.
SIKU YA KWANZA 21 JULAI 2022, TABORA.

LINK YA SOMO LA HILI YOUTUBE 👉🏼https://youtu.be/PaKxcRjxYKs

NAMBA ZA KUTUMA SADAKA, MAOMBI NA SHUHUDA
👉🏼https://bit.ly/Sadaka-Maombi-Shuhuda

LENGO LA SOMO
Kuweza kujifunza kutumia mbinu za Kibiblia ili kujinasua kutoka kwenye vifungo vibaya vya maisha vinavyotokana na Sadaka.

Mungu anaachilia upako wa matengenezo katika msimu huu. Mungu anatafuta mtu mmoja atakayekuwa tayari kufanya matengenezo kwa ajili ya Familia, Nchi na Dunia kwa ujumla.

Tunapoweka utangulizi wa Somo kuna Mambo tutayaangalia ambayo yatakuwa msingi wa somo kadri tunavyoendelea kujifunza.

JAMBO LA KWANZA
SADAKA INAWEZA KUTUMIKA KUFUNGA MIOYO YA WATU KIMAISHA

Soma 1 Wafalme 12:26 - 33 Katika habari hii unaona kuwa Sadaka inaweza kufunga mioyo ya watu na chochote unachotoa k**a sadaka maana yake umekielekeza kwa Mungu au miungu kwa sababu ndiyo inayoweza kupewa sadaka na kuielewa.

Maandiko yanatueleza habari za Yeroboamu kuhusu nafasi ya mfalme Sulemani. Yeroboamu alikuwa anaongoza kabila 10 na Mwana wa mfalme Sulemani yaani Rehoboamu kubaki na kabila 2. Hili jambo usilitazame kutoka kwenye ngazi ya kitaifa bali kwa ngazi ya kifamilia.

Hizi kabila 12 ni watoto 12 wa mzee Yakobo (yaani watoto wa familia 1) kwa hiyo kabla taifa halijawa taifa, kuna watu wanatakiwa kujengwa na wao watakuwa wa kujenga familia. Sawa na maandiko kusema Mungu alijenga taifa kutoka kwa mtu mmoja yaani Adamu.

MSINGI WA TAIFA, HAUKO KWENYE TAIFA BALI UPO KWA MTU MMOJA MMOJA NDANI YA TAIFA HALAFU WAO HUUNDA FAMILIA IKIFUATIA NA TAIFA KUUNDWA.

Mtu mmoja akiharibika, taifa zima linaharibika: familia zikiharibika, taifa linaharibika kwa sababu ndio misingi iliko. Mambo yakitengamaa huko ni rahisi sana taifa kuwa imara.

1 Wafalme 12:26 - 27**
“Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. K**a watu hawa wakipanda

SOMO:-"Sadaka Inapotumika Kutengeneza Maisha ya Familia Yaliyofungwa na Sadaka"Unaweza kutumia njia zifuatazo kutuma sadaka yako kwetu:- M-PESA ...

28/06/2022

The rupture is really,the second come of Jesus is soonest,plz wash well your garment to enter his kingdom
Decide to leave all others behind for Jesus

Address

Kihonda
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 06:00 - 00:00
Tuesday 06:00 - 00:00
Wednesday 06:00 - 00:00
Thursday 06:00 - 00:00
Friday 06:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 06:00 - 22:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Eden holiness ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Eden holiness ministry:

Share