ReGen Online Fellowship

ReGen Online Fellowship ReGen Online Fellowship 🌐🔥
📍 Your Online Home for Faith & Fellowship
🙌 Youth • Purpose • Power
✨ Faith. Fellowship. Fire.

10/10/2025

Ujumbe wa Leo:
Acha maneno ya watu yakae nyuma yako, lakini rehema ya Mungu ibaki mbele yako.
By Elisha Elijah.

15/09/2025
14/09/2025

🌙 Night Reflection & Prayer

📖 “Nitapumzika kwa amani na kulala usingizi, kwa kuwa Wewe, BWANA, peke Yako unaniweka salama.” (Zaburi 4:8)

✨ Tafakari ya Usiku:
Kabla ya kulala, kumbuka: usalama wako si kwa uwezo wako, bali kwa ulinzi wa Mungu. Achia hofu zote na mwamini Yeye akulinde.

🙏 Maombi:
“Bwana, nakushukuru kwa siku uliyoniwezesha. Ninakabidhi mawazo, hofu na mipango yangu mikononi mwako. Nipe pumziko lenye amani na unilinde usiku huu. Amina.”

Footer: Faith | Fellowship | Fire
100M Followers

14/09/2025

☀️ Midday Reflection & Wisdom

📖 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
— Yeremia 29:11

💡 Fikiria Hili Leo:
Kati ya changamoto zako zote, Mungu bado ana mpango uliojaa tumaini kwa ajili yako. Hata pale unapohisi umekwama, Yeye ana njia mpya ya ushindi.

✨ Jitamkie Leo:
“Najua maisha yangu yako mikononi mwa Mungu, na hatima yangu imejaa tumaini na baraka.”



Followers

Usiku – Evening Devotion + Prayer (Tafakari na Maombi)Aya ya Biblia:“Kwa amani nitajilaza, na kulala usingizi; Kwa maana...
13/09/2025

Usiku – Evening Devotion + Prayer (Tafakari na Maombi)

Aya ya Biblia:
“Kwa amani nitajilaza, na kulala usingizi; Kwa maana Wewe, Ee Bwana, peke Yako, ndiwe unifanyaye kukaa salama.” (Zaburi 4:8)

💡Tafakari:
Haijalishi changamoto za siku, Mungu anakupa nafasi ya kupumzika na kulala kwa amani. Usiache kuishukuru leo yako na kuiombea kesho yako kabla ya kulala.

🙏Maombi ya Ushirika:
“Bwana, tunakushukuru kwa siku hii. Tunakuomba uilinde familia yetu ya ReGen, utupe usingizi wa amani, na utuongoze ili kesho yetu ikawe ya baraka.
Andika AMEN hapa chini ikiwa unashirikiana nasi!”

👉Tamka maneno haya kabla hujalala:
“Nitalala kwa amani, kwa maana Bwana ndiye ulinzi wangu. Kesho yangu iko mikononi mwa Mungu.”

🌍 Karibu ReGen Online Fellowship! Hii ni jukwaa la vijana na wote wanaotamani kumjua Mungu zaidi, kukua kiroho, na kuish...
12/09/2025

🌍 Karibu ReGen Online Fellowship!

Hii ni jukwaa la vijana na wote wanaotamani kumjua Mungu zaidi, kukua kiroho, na kuishi maisha yenye kusudi. 🙏🔥

➡️ Tunakuletea mafundisho ya Biblia, maombi ya pamoja, ushauri wa maisha, na ushirika wa kiroho – yote kupitia mtandao.
➡️ Lengo letu ni kurejesha kizazi hiki kwa Kristo, tukijenga imani, tumaini na upendo. 💡❤️

Kila wiki utapata:
✅ Mafundisho mafupi na yenye kugusa maisha
✅ Maombi ya kiroho na faraja
✅ Ushauri na motisha
✅ Ushirika wa mtandaoni na familia ya imani
✅️Uchambuzi wa neno la Mungu kwa kina
✅️Maswali na majibu .

🤝 Tunakukaribisha ujiunge nasi kwenye safari hii – Kizazi Kilicho Hai kwa Kristo – Tunaishi kwa Kusudi, Tunatenda kwa Nguvu!
Faith,fellowship,Fire🔥

11/09/2025

Shalom, Leo tunafungua ukurasa wetu rasmi wa ReGen Online Fellowship – Restoring Generation, mahali ambapo vijana wanapata mwanga, motisha, na mafunzo ya kiroho ili kuishi kwa kusudi na kutenda kwa nguvu! 💪✨

Tunakuletea:
🔥 Mafundisho ya kila siku yenye nguvu ya kiroho
🔥 Nukuu na ujumbe wa msukumo kwa vijana
🔥 Ratiba za maombi na tafakari
🔥 Uchambuzi wa kina wa neno la Mungu
🔥Maswali na majibu
🔥Shuhuda

Tunakusudia kukuunganisha na kizazi kilicho hai, chenye shauku ya kumjua Mungu zaidi na kuishi maisha yenye maana.

👉 Jiunge nasi kwenye safari hii ya kiroho na usisahau kushiriki, kupenda, na ku-comment ili kuhamasisha wengine.

Kauli mbiu yetu:
Faith Fellowship Fire🔥

Address

Kahama Shinyanga
Dar Es Salaam

Telephone

+255756453850

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ReGen Online Fellowship posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to ReGen Online Fellowship:

Share