Genuine Global Christian Kingdom Youth Network

Genuine Global  Christian Kingdom Youth Network STIRING HOLLYNESS ,REVIVAL & CHURCH RE-FORMATION AMONG YOUTH ALL OVER THE WORLD

SEMINA SEMINA SEMINASIKU YA PILISOMO.NAFASI YA ROHO MTAKATIFU MAISHA MWAKOTutakuwa LIVE kwenye account hii kuanzia saa k...
19/06/2024

SEMINA SEMINA SEMINA

SIKU YA PILI
SOMO.NAFASI YA ROHO MTAKATIFU MAISHA MWAKO

Tutakuwa LIVE kwenye account hii kuanzia saa kumi na nusu leo hadi saa kumi na mbili,karibu ujifunze ukue kiroho.

Wako Mtumishi Cosmas Karoly
Nikifundisha toka AKUZAMU INTERNATIONAL CHURCH,KONDOA MJINI

NAFASI YA ROHO MTAKATIFU MAISHANI MWAKOSEHEMU YA KWANZA(PART 01)FUATILIA KWA UMAKINI,UTAPATA CHA KUKUSAIDIASOMO: FAIDA Z...
17/06/2024

NAFASI YA ROHO MTAKATIFU MAISHANI MWAKO

SEHEMU YA KWANZA(PART 01)

FUATILIA KWA UMAKINI,UTAPATA CHA KUKUSAIDIA

SOMO: FAIDA ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NA KUMTII MAISHANI MWAKO

Utangulizi
Roho mtakatifu ni nafsi ya Mungu kati ya nafsi tatu za Mungu hivyo Roho Mtakatifu ni Mungu.

-Roho Mtakatifu siyo nguvu,siyo maji,siyo moto wala siyo upepo bali hizo ni ishara anazoweza kujitambulisha kuwa yupo mahali hapo anapokuwepo saa hiyo

-Alikuwako toka wakati wa uumbaji ingawa kuja kukaa na kumuongoza mwanadamu akiwa ndani ya mwanadamu alikuja siku ya 50 baada ya kupaa kwa Yesu kwenda mbinguni
-Yeye ndiye msaidizi,mwalimu na kiongozi wetu k**a kanisa la Mungu(wana wa Mungu) mpaka Kristo atakaporudi kulinyakua kanisa(watakatifu walioshinda)
-Bila kujazwa Roho Mtakatifu,mwanadamu hawezi kuishi maisha ya ushindi.

Maandiko ya utangulizi

*Mwanzo 1:2 (Roho mtakatifu anatajwa kwa mara ya kwanza,hapa anashiriki katika uumbani,anatajwa k**a Roho ya Mungu)
*Yoeli 2:28,29(Roho atabiriwa kuwa atakuja kukaa na kuwaongoza wanadamu)
*Yohana 14:15 Yesu Kristo awausia wanafunzi wake kuwa akienda kwa Baba atamwomba ili amlete msaidizi mwingine,hapa anatajwa k**a Roho wa kweli.
*Matendo 1:8 Yesu awaambia wanafunzi wake jinsi watakavyotambua kuwa Wamejiliwa na Roho Mtakatifu
*Matendo 2:1-4 Roho Mtakatifu aja na kuwajaza wanafunzi wote wa Yesu waliokuwa wamekusanyika ghorofani wakimngoja kwa shauku kubwa.

Ili uone faida za Kujazwa Roho Mtakatifu ni lazima ukubali kumtii kwa namna anavyokuongoza na utende sawa na anavyokuelekeza ndani ya moyo wako.

Utatambuaje kuwa umejazwa Roho Mtakatifu?

Jibu:Utatambua pale utakaponena kwa lugha nyingine kadiri Roho Mtakatifu atakavyokujalia kutamka na siyo kwa kuiga wengine wanavyonena ila ndani yako utapata msukumo wa kunena ambao ukikubali kufungua mdomo na kunena ndivyo utakavyonena na ukinyamaza hutanena maana umenyamaza

LENGO LA SOMO:
Kukujengea shauku ambayo ndiyo ufunguo mmojawapo utakaokusaidia ujazwe na uendelee kujazwa Roho Mtakatifu.



FAIDA KUMI ZA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NA KUMTII MAISHANI MWAKO

1.*ANATUPATIA MAJIBU SAHIHI HATA KWA VITU TUSIVYOVIJUA/TUSIVYOVITAMBUA*
Marko 13:11
-Haijalishi ni jambo gumu au ni jambo usilotambua jibu lake,useme nini,ufanye nini..Basi ukitulia na kumwambia Roho Mtakatifu na ukatulia kusikiliza toka ndani yako,utatoka na suluhisho ambalo ni bora
-Shida ya watu waliowengi ni kuogopa na kusahau kuwa yupo anayejua yote naye ni Roho Mtakatifu.

2.ANATUPATIA UJASIRI AMBAO BILA YEYE HATUWEZI KUWA NAO

Hapa tunaweza kujifunza kwa Petro.
Kabla Petro Hajazwa Roho Mtakatifu
Marko 14:66-72
-Tunaona hapa Petro ni muoga kwelikweli anahofu ya wayahudi wanaotaka kumuua Yesu,Petro alimkana Yesu kuwa hamjui mara tatu.

Petro baada ya kujazwa Roho Mtakatifu
Matendo 2:1-4(anajazwa Roho)
Matendo 2:14-29 (Petro awahubiria kwa *ujasiri* ,ameupata wapi ujasiri,umeletwa ndani yake na Roho aliyemjaza.
-Hivyo tunapojazwa Roho Mtakatifu tunakuwa hatuna hofu.

3.*ANATUPATIA UFANISI ILI KUPATA MATOKEO AU FAIDA KUBWA*

-Ukitaka kuwa mfanisi na mwenye kupata matokeo na faida kubwa au kufanya vitu vya viwango vya juu,wewe hakikisha unabakia umejaa Roho kisha mtii katika yale anayokuongoza..

Tunajifunza kwa Petro baada ya Kujazwa Roho anahubiria watu kwa mara moja wakaokoka watu *wapata 3000*.
Je 3000 siyo matokeo makubwa?
-Ukiona umechoka maisha duni,tafuta kujawa na Roho kisha mtii mara zote,hutabaki k**a ulivyo
Soma Matendo 2:38,41.

4.ANATUPA KUSHINDA MAJARIBU

Ili uwe na uhakika wa kushinda majaribu mbalimbali ni lazima ujazwe Roho Mtakatifu na uendelee kuongeza viwango vya ujazo mara kwa mara ukichochea kupitia maombi na kunena kwa lugha mara kwa mara ikiwezekana kila siku ya maisha yako.

Tunajifunza kwa Yesu pale alipojawa na Roho Mtakatifu ndipo akaenda kujaribiwa na Ibilisi jangwani na akashinda majaribu yote
Soma
Luka 4:1 ( Kwanza Yesu alijawa Roho Mtakatifu ndipo akaenda nyikani kujaribiwa)
Luka 4:13(shetani ak**aliza majaribu yote huku amefeli kumshinda Yesu)
-Ukitaka ushindi dhidi ya majaribu ya kila namna hakikisha umejaa Roho wakati wote.

HIVYO KUJAWA NA ROHO MTAKATIFU NA KUMTII NI MUHIMU SANA SANA KWA USTAWI WA MAISHA YAKO.

Wako mtendakazi shambani mwa Bwana,Cosmas Mbairah Karoly
Contact me at [email protected]
Mobile 0788 183 346/ 0678 416 676

USIDANGANYWE NA WANAOSEMA TATIZO LA AFRIKA NI IBADA NYINGI AU MAOMBI MENGI1. Wao wanaabudu sanamu zisizoongea wala kujit...
07/03/2024

USIDANGANYWE NA WANAOSEMA TATIZO LA AFRIKA NI IBADA NYINGI AU MAOMBI MENGI

1. Wao wanaabudu sanamu zisizoongea wala kujitikisa

2. Wao wanaabudu wanyama ambao wewe huku AFRIKA unawala k**a chakula

3. Wao wana vikundi vya siri vya waabudu Shetani

4. Wao wameamua kumuabudu Shetani kwa mlango wa nyuma kupitia ushoga, usagaji, picha za uchi, kujichua, ngono ya watoto wachanga, utoaji mimba na kila takataka kinyume na maadili

5. Wao wanatambikia waliokufa au kuheshimu waliokufa, hii ni ibada, sio heshima

6. Wao wanafanya ngono k**a sadaka, k**a maelekezo ya kuwasaidia kuwa na nguvu rohoni

7. Wao wameamua kuua taasisi ya ndoa kwa makusudi na kupromoti zinaa, uasherati na ngono holela, hii ni ibada! Sexual rituals

8. Wengine wana vyumba ndani kwao wanaabudu nyie mkilala, leo wanakushambulia uache kuomba mno au kuwa na ibada nyingi, JIDANGANYEEEE!

Rafiki yangu,
K**a ni kuomba hatujaomba bado,
K**a ni mifungo ndio kwanza tunataka 7 kavu iwe k**a ilivyo masaa 12 kutwa,
K**a ni mikesha ya maombi tunataka kila siku ya Mungu kuwe na watu wanakesha makanisani,
SHETANI AMECHELEWA KUPIGA KELELE UPANDE HUU, WALA HATUKOSI KUZIJUA HILA ZAKE...
Askofu Dickson Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI
07.03.2024

USIOGOPEMpendwa wangu nakusalimu kupitia jina lipitalo majina yoteNajisikia moyoni mwangu kukusemesha jambo moja tu kuwa...
15/02/2024

USIOGOPE

Mpendwa wangu nakusalimu kupitia jina lipitalo majina yote

Najisikia moyoni mwangu kukusemesha jambo moja tu kuwa USIOGOPE
..Unataka kufanya uamuzi wa jambo bora katika mapenzi ya Mungu litakalobadilisha hatima ya maisha yako na kuwa baraka kwa wengi..USIOGOPE,fanya tu maana hakuna atakayekufanyia ili ubadili hatima yako
...Unataka kufanya uamuzi mgumu ambao wengine wanaokuzunguka hawajawahi kuufanya na wamekuambia ni jambo lisilowezekana kabisa labda wanakuangalia kwa jinsi ya nje na huku ndani yako unapata uhakika kuwa fanya...USIOGOPE,fanya sawa na maelekezo ndani yako
...Haohao wanaosema utashindwa na ni jambo lisilowezekana,mara tu utakapofanya na matokeo chanya kuonekana watakuja kukuambia tulijua tu wewe unaweza..watakuambia maneno kibao kuonesha wapo upande wako...USIOGOPE.

Ukitaka kuwa na kufikia ndoto zako lazima ufanye bila kuogopa...USIOGOPE.

2 Timotheo 1:7
[7]Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Ni mimi ndugu yako
Cosmas Mbairah Karoly
Nimekuandikia uwe na moyo uliochangamka unapofanya jambo lako bila KUOGOPA..

Ukitaka kuwasiliana nami kwa jambo lolote
la utukufu kwa Mungu
0788183346/0678416676
[email protected]
Care Mission International
Dar Es Salaam
Tanzania

TUNAPOMALIZA MWAKA 2023.NIANDIKE MACHACHE KWAKO WEWE RAFIKI YANGU KUPITIA UKURASA HUU..Najua kuwa mwaka 2023 haujawa rah...
31/12/2023

TUNAPOMALIZA MWAKA 2023.

NIANDIKE MACHACHE KWAKO WEWE RAFIKI YANGU KUPITIA UKURASA HUU.
.Najua kuwa mwaka 2023 haujawa rahisi sana kwako kwasababu ya changamoto za hapa na pale kwasababu upo unaishi hapa duniani kwasababu hazitaisha maadamu upo hapa duniani na hili Yesu Kristo mwenyewe alishasema na hasa kwa wale wanaotamani kutenda mapenzi ya Mungu kwenye kila eneo.
Yohana 16:33
[33]Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
...Pamoja na changamoto ulizopitia naamini kuna maeneo mengi sana ya maisha yako Mungu amekupigania na ukapata ushindi..Hata k**a ulishindwa bado Mungu hajashindwa,ni suala la muda tu,,rudia tena kwa msaada wa Mungu utashinda,,usikate tamaa 2024 ni mwaka wako...Kuna maeneo au mambo au kona mbalimbali ukitizama na kutafakari,,unasema k**a si Mungu nisingevuka
...Kwa mitego niliyokuwa nimewekewa looo k**a si Mungu leo nisingevuka salama
....Jinsi maadui zangu walivyokuwa wamenipania..loo nisingetoboa mwaka.
.....Kuna wakati bajeti ziligoma ukaona huwezi kufanikisha mipango na hata mwezi utaishaje ila ghafla ukavuka na sasa upo ukingoni mwa mwaka 2023,,hakika ni Bwana.
.....Kuna mwingine uliumwa au uliuguza na ukakata tamaa ila kiajabu uponyaji ukaingia au unafuu ukaja hata sasa ni ebeneza.

***Zaburi 116:12 {SWALI}
[12]Nimrudishie BWANA nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
What shall I render unto the LORD for all his benefits toward me?

***{JIBU} Zaburi 50:23
[23]Atoaye dhabihu za kushukuru,
Ndiye anayenitukuza.
Naye autengenezaye mwenendo wake,
Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
Whoso offereth praise glorifieth me: and to him that ordereth his conversation aright will I shew the salvation of God.

***Usisahau kumtolea Mungu sadaka ya kumshukuru Mungu pale kwenye madhabahu unapolelewa kiroho..Biblia inasema Mungu anapendezwa kwa hiyo.Jambo lingine hata k**a hutapata nafasi ya kwenda kanisani leo kabla mwaka haujageuka pata muda umwambie Mungu shukurani za moyo wako na umweleze kile umeadhimia(mipango yako ya mwaka 2024)

Maana Mungu hakuwekei mipango ila wewe ndiwe mwenye kuiweka ila yeye anakuwezesha unapoingia kwenye utekelezaji.
Mithali 16:1
[1]Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.
The preparations of the heart in man, and the answer of the tongue, is from the LORD.

Nakutakia baraka tele na ushindi maradufu kwa mipango uliyoiweka/utakayoiweka ya mwaka 2024.See you next year by the grace of God,i love you my esteemed friend.

Ni mimi ndugu yako,mtenda kazi shambani mwa Bwana
Ev.Cosmas Mbairah Karoly
@+255 678 416 676 & 788 183 346.

AMKA UWAAMSHE WENGINE(KWA WALIOMPATA KRISTO KWA JINSI YA WOKOVU)...SOMA MPAKA MWISHO UTAPATA CHA KUKUSAIDIANakusalimu ra...
28/12/2023

AMKA UWAAMSHE WENGINE
(KWA WALIOMPATA KRISTO KWA JINSI YA WOKOVU)...SOMA MPAKA MWISHO UTAPATA CHA KUKUSAIDIA

Nakusalimu rafiki yangu katika Bwana.

Kwa mapenzi yake Mungu nimependa kukuandikia awe rafiki na msomaji wangu.

Leo tujiulize na kujijibu swali lifuatalo

SWALI..JE UNAMUWAKILISHA YESU KRISTO(MUNGU) SAWASAWA MAHALA ALIPOKUWEKA?/ALIPOKUPANDA?/ALIPOKUFANYIA NAFASI?.........Katika kujibu swali hili,muktadha wa mahala alipokuweka ni pana..Yaweza kuwa ni ni
1.Mahala unapofanya kazi zako za kukupa kipato..Wanasema wewe ni nani?,,wewe ni mtu wa kawaida kawaida au wanasema wewe ni nani?..wanakuita mama mchungaji?au mama askofu? au mama mlokole?au mama misimamo? au mama mtumishi?(kwa wanawake)..K**a huitwi kwa majina haya kaa chini jitafakari na uchukue hatua (ya kufanya toba)maana kuna kitu hakiko sawa ndani yako yaani umewafanania mataifa tayari...either kwa matendo,mavazi(muonekano),kwa maneno..Unanena nini?
..K**a mwanaume wanakuitaje?
je ni baba mchungaji?,au baba mwinjilist? au baba askofu?,au baba mtumishi? au baba misimamo?..Maana huli rushwa au ganji nawo(hazikuhusu)..Haushiriki unafiki,uzushi,uzinzi,wizi,ulevi na usengenyaji nawo(huvikuhusu hivi)....K**a hawakuiti hayo majina na yanayofanana na hayo kaa chini,lia kisha amua kufanya toba ya kweli maana tayari dunia imekumeza na hakuna wa kukutoa isipokuwa Kristo peke yake.

2.Yaweza kuwa ni shuleni/chuoni
Wanafunzi wenzako wanakutambua k**a nani?...Wanakutambua kwa urahisi k**a mtu unayemfuata Kristo au msanii ndani ya Kristo?,,unajua wasanii wamejaa maigizo na mizaha...
....Ishi maadili ya Kikristo,mfuate Kristo sawa na neno lake nawe automatically utafanana naye mpaka kusema kwako,kutembea kwako ,kucheka kwako n.k

Jizoeze kufanya yafuatayo kila siku nawe utafanana na Kristo na ndivyo wengine watakavyokutambua.

1.Soma na tafakari neno la Mungu kila siku walau hata nusu saa tu k**a unasema uko bize sana na dunia
2.Jizoeze kuomba kila siku walau hata saa 1
3.Fanya matendo ya ukarimu kwa wengine kwa kadiri upatapo fursa kufanya hivyo.
4.Jitahidi mshuhudie walau mtu mmoja asiyemjua Yesu kwa siku
5.Mche Mungu,jiepushe na uovu.......

Mathayo 26:73
[73]Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha. .....
Hata usemi wako wakutambulisha..

Wako mpendwa
Mwinjilisti,Cosmas M Karoly.
Dar Es Salaam,Tanzania.
@0678416676/0788183346.
[email protected]

06/11/2023

“Watu wengi sana wanakufa wakiwa na miaka 25 na wanazikwa wakiwa na miaka 75” - Benjamin Franklin aliwahi kusema.

____Alisema hili baada ya kuchunguza na kugundua kuwa kuna mamilioni ya watu ambao wanapoteza matumaini ya ndoto yao wakiwa Vijana na...
..baada ya hapo wanaamua kuendesha maisha yao kwa mazoea bila kujaribu kufanya mambo Makubwa kwenye Maisha hadi wanazeeka na kuondoka duniani.

Leo unapoanza siku yako Kumbuka kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na kusukuma siku (Living Vs Surviving).

Kusukuma siku ni kuamua kuendelea na mfumo wa kawaida wa maisha k**a unavyokutaka bila kuwa na malengo Makubwa ya maisha yako.

Hii inatokea pale unapojikuta unaamka unaenda ulikozoea kisha unarudi kulala...
..ila ukijiuliza - “Hivi kuna Kitu gani kikubwa nataka kukifanikisha kwenye maisha?”

Unajikuta bado hauna jibu.

Mfumo huu ni hatari sana kwa sababu Inawezekana kila mtu anakutamani unavyoishi, kwa nje watu wanakuona umefanikiwa kwa sababu ya mali unazomiliki.

Cheo ulichonacho...

Umaarufu wako..

Kazi nzuri...

Elimu yako kubwa...

Ama gari unaloendesha...
..lakini ndani yako unajua kabisa kuwa haupigi hatua na hauridhiki na maisha yako.

Namna pekee ya kutoka katika hali hii ni kufanya maamuzi thabiti kuhusu maisha yako (Critical Decision).

Fanya maamuzi muhimu kuhusu mwelekeo wa Maisha.

Fanya maamuzi kuhusiana na mahusiano yako, kuhusiana na kazi yako, kuhusiana na Kitu unachokifanya sasa.

Amua kupata Muda wa kutafakari na dhamiria kuwa kila utakachokifanya kuanzia leo kitachangia katika MAONO yako...
..na sio kujaza ratiba yako ya siku tu.

Naomba nisaidie kushare makala hii na mtu mwingine ambaye unatamani naye ajifunze k**a mimi na wewe.

Unahangaika kutimiza malengo yako kwa kipindi kirefu bila mafanikio?

See You At The Top

Joel Arthur Nanauka

TANGAZO LA SEMINA YA SIKU 7  KUPITIA WHATSAPP KUANZIA TAREHE 17/07/2023 HADI 23/07/2023SOMO:*KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU NA...
12/07/2023

TANGAZO LA SEMINA YA SIKU 7 KUPITIA WHATSAPP KUANZIA TAREHE 17/07/2023 HADI 23/07/2023
SOMO:*KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE KATIKA MAISHA YETU NA KANISA KIUJUMLA*

WALENGWA
1.Watu wote wenye kiu ya kujua maana ya kila karama na namna ya kutambua inapokuwa katika utendaji kazi wake
2.Wote wenye Shauku ya kuona karama mojawapo au hata kadhaa zikitenda kazi ndani yako katika kusudi lake husika sawa na agenda apendavyo Roho Mtakatifu.
3.Watumishi wa Mungu katika huduma zao mbalimbali ambao wanatamani kudhihirika katika utumishi wao kwa karama hizi ambazo kwangu huziita *nyenzo* na *vitendea kazi muhimu* ndani ya shamba la Bwana.
4.Watumishi wanaotamani kuona na kutembea katika wimbi la uamsho ndani ya siku hizi za Mwisho.

*ZINGATIA*:
1.Kwa mtu ambaye hajaokoka na anatamani kujiunga na semina hii,nitafute kwenye whatapp namba yangu ya 0788 183 346 kabla ya tarehe ya kuanza semina ili nikupe maelekezo ya awali kwasababu ukiingia moja kwa moja hutaweza kuelewa ntakayokuwa nafundisha au semina hutanufaika nayo.
2.Kwa wenye vigezo tayari utaingia direct kwenye group kupitia linki iliyoambata na tangazo hili.

MAELEKEZO MENGINE
1.Kwa siku tano za mwanzo ntafundisha kupitia voice note na utafuatilia.
2.*Muda wa semina kuanza*
Nitafundisha asubuhi ila wewe una uhuru wa kufuatilia muda wowote kwa kadiri ya nafasi na muda wako.
3.Ukiwa na swali,maoni au nyongeza kwa jambo husika linaloweza kuboresha andika kisha nami nitafuatilia na kukujibu
4.Kwa jumamosi na jumapili nitafundisha nikiwa live kwenye page yangu na nitafanya maombi ya ujazo wa Roho Mtakatifu na kudhihirika kwa Karama zake kwako,usikose.
5.Share tangazo hili kwenye page yako na wahusika watafuatilia sawa na maelekezo.

Baraka za Mungu zikufuate na kukupata unapoendelea kumtukuza Mungu aliyehai.

*Ingia whatsapp kupitia link ifuatayo*
https://chat.whatsapp.com/ICsLtkLHLPN1JWrts6YByo

Wako Cosmas Karoly
Mtenda kazi shambani mwa Bwana.

Get phones, tablets, Mobile Broadband and SIM Only deals on the UK’s Fastest 5G Network.

Jumapili ya tarehe 10 mwezi huu wa Saba nitakuwa Kondoa mjini kwa ajili ya huduma kwenye kanisa la FPCT KONDOA MJINI.Nak...
07/07/2022

Jumapili ya tarehe 10 mwezi huu wa Saba nitakuwa Kondoa mjini kwa ajili ya huduma kwenye kanisa la FPCT KONDOA MJINI.

Nakukaribisha Sana sana.

CHANZO CHA HOFU NA KUTOKUFANIKIWA KATIKA MAISHA NI KUTOTAMBUA WEWE NI NANI NA NINI THAMANI YAKO.

Mwanzo 1:26
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
And God said, Let us make man in our image, after our likeness: and let them have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over the cattle, and over all the earth, and over every creeping thing that creepeth upon the earth.

*Usijidharau,thamani yako ni kubwa Sana.
*Thamani yako unaitafuta/unaijua unapoanza kuchunguza na kujua kuhusu asili yako.
*Jinsi roho yako alivyoiumba Kuna vitu ambavyo aliviweka vya asili yake ambavyo
1.Sura yake
2.Mfano wake
3.Nguvu ya kutawala/kumiliki.

Kwa picha hiyo unaweza kuelewa kwanini Mungu anamwita mwanadamu "mungu" na yeye mwenyewe ni Mungu wa "miungu"
Zaburi 82:6
[6]Mimi nimesema, Ndinyi miungu,
NA
Yohana 10:34-35
[34]Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?
[35]Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
NB:Kila mwanadamu liyekombolewa toka utumwa wa dhambi/aliyeokoka sawa na Yohana 10:35 anarudishiwa asili ya uungu iliyopotea pale Edeni.

English Translation.

*Don't undermine yourself/despise/put down yourself,you are highly precious.
*You get your value when you start evaluating your genesis/origin
*The way He created your spirit,He put things which carry His origin which are
1:His image
2.His likeness
3.Power of Dominion

With this view,you can now know why God calls human "god" and Himself is a God of "gods"
Psalm 82:6
[6]I have said, Ye are gods; and all of you are children of the most High.
&
John 10:34-35
[34]Jesus answered them, Is it not written in your law, I said, Ye are gods?
[35]If he called them gods, unto whom the word of God came, and the scripture cannot be broken;

These and much more,on Sunday morning of 10th July 2022 at FPCT CHURCH,KONDOA TOWN,DODOMA TANZANIA,will be spoken in detail.If you are in town do'nt miss.
For those away i promise you not much longer you will be able to access the teachings from our YouTube Channel which will be created,pray for that.

You are unique despite what they told you,relie on God's information about you and not people

Wewe ni wa pekee,tegemea vile Mungu anavyosema kuhusu wewe na si wanadamu.

I love you/Nawapenda

God bless you/Mungu awabariki.

Your brother,
Cosmas Karoly
Dar Es Salaam
Tanzania.
[email protected]
WhatsApp # (+255) 621 846 755.

Jumapili ya tarehe 10 mwezi huu wa Saba nitakuwa Kondoa mjini kwa ajili ya huduma kwenye kanisa la FPCT KONDOA MJINI.Nak...
06/07/2022

Jumapili ya tarehe 10 mwezi huu wa Saba nitakuwa Kondoa mjini kwa ajili ya huduma kwenye kanisa la FPCT KONDOA MJINI.

Nakukaribisha Sana sana.

02/07/2022

YESU ALIKUJA KUOKOA KILICHOPOTEA/JESUS CAME TO SAVE THE LOST

Kilichopotea ni nini?

Kilichopotea ni mwanadamu ambaye yupo chini ya kifungo Cha dhambi,hajampa Yesu maisha yake,hajaokoka.

Luka 19:10/Luke 19:10
[10]Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.
For the Son of man is come to seek and to save that which was lost.

Yohana 3:18/John 3:18
[18]Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
He that believeth on him is not condemned: but he that believeth not is condemned already, because he hath not believed in the name of the only begotten Son of God.

Ufunuo wa Yohana 16:15(Rev 16:15)
[15](Tazama, naja k**a mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Behold, I come as a thief. Blessed is he that watcheth, and keepeth his garments, lest he walk naked, and they see his shame.

1 Wathesalonike 4:16-17(1Thes 4:16)
[16]Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
For the Lord himself shall descend from heaven with a shout, with the voice of the archangel, and with the trump of God: and the dead in Christ shall rise first:

[17]Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Then we which are alive and remain shall be caught up together with them in the clouds, to meet the Lord in the air: and so shall we ever be with the Lord.

K**a ni kwennye mpira wa miguu,basi tupo dakika ya tisini kipenga kitapulizwa muda wowote.
If we consider soccer behold we're in the 90th min.

Dalili zote zinatimia,Yesu yu karibu kurudi.
All signs are getting full filled,the second coming of Jesus is near.

HUJAOKOKA,OKOKA SASA MAANA WOKOVU NDIYO TIKETI YA KUINGIA KWENYE JIJI ZURI LA MBINGUNI.

ULIYEOKOKA ENDELEA KUJITAKASA,TUNZA VAZI LAKO LA HARUSI,PUNDE SI PUNDE BWANA HARUSI(YESU) ANAINGIA.

DHAMBI YOYOTE HAITAKURUHUSU KUINGIA MBINGUNI.

KWA MLIOKOKA ZIFANYENI AKAUNTI ZENU ZA MITANDAO YA KIJAMII MADHABAHU YA KUWAHUBIRIA WENGINE HABARI ZA WOKOVU,YESU ATAKUPENDA NA KUKUVIKA TAJI SIKU ILE NAWE UTAN'GARA K**A NYOTA.

Mungu wa mbingu na nchi akubariki.Nakupenda.

God of heaven and Earth bless you richly,i love you.

Ev. Cosmas Karoly
Dar es salaam
Tanzania
[email protected]
WhatsApp #(+255) 621 846 755.

PENTECOST IS POWER ENCOUNTERTHERE IS NO LIMIT TO FULFILLING GOD'S VISION IN YOU WHEN YOU HAVE ENCOUNTER WITH PENTECOSTAL...
06/06/2022

PENTECOST IS POWER ENCOUNTER

THERE IS NO LIMIT TO FULFILLING GOD'S VISION IN YOU WHEN YOU HAVE ENCOUNTER WITH PENTECOSTAL EXPERIENCE

Acts 2:41
Then they that gladly received his word were baptized: and the same day there were added unto them about three thousand souls.

Do you see,three thousand souls harvested same day.

So we see when we have Holy spirit,His power is the power that brings about multiplication as we engage in the work with Him.

The revelation here is if we obey what the Holy spirit is instructing us to do,the outcome is
*Expansion in whatever you do for His glory
*Elevation
*Increase in all aspects of life

And vice versa is true when you are not filled with the Holy Spirit.

I wish you blessed day my friend.

#

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

PENTEKOSTE NI NGUVU

HAKUNA MPAKA KATIKA KUTIMIZA MAONO MUNGU ALIYOWEKA NDANI YAKO UNAPOKUTANA NA NGUVU YA PENTEKOSTE(UNAPOJAZWA ROHO MTAKATIFU/UNAPOKUWA UMEBATIZWA KATIKA ROHO MTAKATIFU)

Matendo ya Mitume 2:41
[41]Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

Je unaona hapo, watu elfu tatu wameokoka ndani ya siku moja

Hivyo tunaona Happ kuwa tunapoingia kazini tukiwa tumejazwa Roho Mtakatifu lazima kuwe na maongezeko.

Sasa ufunuo ama uelewa tunaoupata tunaposoma mstari huo Ni kuwa tukitii yale Roho Mtakatifu anatuagiza tuyafanye hali tumejazwa naye na ishara yake kuu ikiwa ni kunena kwa lugha mpya Ni
*Kupanuka katika chochote tukifanyacho kwa ajili ya utukufu wake.
*Kuinuliwa katika nyanja mbalimbali za maisha
*Kuongezeka katika nyanja mbalimbali za maisha.

Na usipojazwa Roho Mtakatifu matokeo yake ni kinyume na yaliyosemwa Happ juu.

Nakutakia siku njema rafiki yangu.

Wako/yours
Cosmas Mbairah Karoly
Dar es salaam
Tanzania
Email: [email protected]
(+255) 678 416 676/788 183 346 na kwa/ and for WhatsApp 621 846 755
#

Address

Yombo Kilakala
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Genuine Global Christian Kingdom Youth Network posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share