28/04/2022
ππͺππ‘ππ‘π π‘ππ£ππ¦πͺπ ππ¨π¨π‘πππ π?
π Naungama kwa sababu naogopa siku nikifa nitaenda motoni.
π Naungama kwa sababu kesho nataka kupokea Komunyo takatifu.
π Naungama kwa sababu najiandaa kusali vema novena ya Mtakatifu fulani niliyoichagua.
π Naungama kwa sababu nataka kubariki ndoa yangu, ili niepukane na uchumba sugu.
π Naungama kwa sababu nataka kufunga milango yote ya laana, ili mapepo yasinishambulie.
π Naungama kwa sababu Padre anione ili anipe pongezi na kunitolea mfano mzuri mbele ya Waamini.
π Naungama kwa sababu ni mazoea yangu niliyojiwekea tangu zamani ya kuungama angalau mara kwa wiki.
π Naungama kwa sababu wengine pia wanaungama, bila wao ukweli nisingeungama.
π Naungama kwa sababu nataka kujionyesha mbele za watu kuwa mimi ni Mtakatifu sana kuliko wao.
π Naungama kwa sababu mimi ni Mtumishi wa Altare na jumapili ni zamu yangu kutumikia.
π Naungama kwa sababu mimi ni Msimamizi wa Kipaimara nimeagizwa na Askofu niungame kila ninapopata nafasi.
π Naungama kwa sababu mimi ni Padre na nimeamuriwa kufanya hivyo ili niadhimishe Misa takatifu kikamilifu.
π Naungama kwa sababu mimi ni Mtawa pale Parokiani nisipoungama Waamini wengine watanifikiriaje.
π Naungama kwa sababu tu ya kutimiza sheria za Kanisa ambazo nilifundishwa tangu utotoni k**a Mkristo Mkatoliki.
π Mpendwa! K**a wewe ni miongoni mwa wale wanaoungama kwa sababu mbalimbali nilizozitaja hapo juu, basi tambu kitubio chako sio sahihi mbele za Mungu. Daima unapaswa kuungama kwa sababu tu umemkosea Mungu, na upo tayari kujenga upya urafiki wako na Mungu ulioharibiwa na dhambi zako za kila mara.
π Hivyo usiungame k**a hujadhamiria kuacha maovu yako, hata k**a kuungama ni haki yako. Kwani kuungama kwa mazoea ili kujionyesha kwa watu, haikusaidii kitu. Maana Kitubio cha kweli kinaanzia ndani ya moyo wako kwa njia ya toba na majuto ya dhati, halafu kinatimizwa kwa nje unapokwenda kwa Padre.
π§π¨π π¦πππ¨ π¬ππ¦π¨ ππ₯ππ¦π§π’...