KKKT Azania Front Cathedral

KKKT Azania Front Cathedral KKKT ( D.M.P) USHARIKA WA AZANIA FRONT

01/09/2026

TUMPENDE NA KUMJALI JIRANI YETU.

1 Yohana

1 Samweli 23: 16 - 22

26/08/2026

WEMA NA FADHILI ZA MUNGU JUU YA MAISHA YAKO.

πŸ“– 2 Samweli 9:

3. Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.

4. Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari.

5. Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari.

πŸ“Œ Tufuatilie kupitia J3 - Ijumaa
- Ibada za Asubuhi na Mchana

YouTube / AzaniaFrontCathedral /

Tunamshukuru Mungu kwa Ibada ya Jumapili hapo jana, πŸ“– SOMO:Tutumie Ndimi Zetu kwa Utukufu wa Mungu πŸ“– AYA YA SIKU:"Mwanzi...
24/08/2026

Tunamshukuru Mungu kwa Ibada ya Jumapili hapo jana,

πŸ“– SOMO:
Tutumie Ndimi Zetu kwa Utukufu wa Mungu

πŸ“– AYA YA SIKU:
"Mwanzi uliopondeka hutauvunja, Wala utambi utokao moshi hutauzima"

Ibada yetu iliongozwa na Dean Chediel Lwiza, akiwa pamoja na Askofu Katherine, Mch. Victor Makundi pamoja na Mch. Rusungu.

πŸŽ™οΈ Muhubiri katika Ibada ya pili na ya tatu Bishop Dkt Katherine Finegan; Alitoa historia fupi juu ya mji wa kale wa Kaisaria Filipi uliopo kusini mwa Mlima Hermoni. Alitueleza ya kuwa hapo ni mahali ambapo Yesu aliwauliza wanafunzi wake yeye ni nani?
Mathayo 16: 13-16.
.
🎢 Kwaya kuu, Agape, upendo, vijana zilihudumu kwa njia ya uimbaji
Tunawatakia wiki ya baraka na Mungu akasimame nanyi nyote katika majuku yenu ya kazi na familia.

πŸ˜‡ Pia Ibada yetu ya tatu iliambatana na Ibada ya ubatizo wa watoto wadogo. Watoto watatu walibatizwa.

πŸ“Œ Tukumbuke, tunahimizwa kutumia vyema ndimi zetu kwa utukufu wa Mungu.

- Maneno mazuri yanaleta amani, upendo na mshik**ano bali maneno mabaya na machafu yanaleta mifarakano.

πŸ“‹Yakobo 3:14.
Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.


Karibu kwenye Ibada , siku ya Bwana ya 12 baada ya utatu.Leo tunaongozwa na somo lenye Kichwa" TUTUMIE NDIMI ZETU KWA UT...
23/08/2026

Karibu kwenye Ibada , siku ya Bwana ya 12 baada ya utatu.

Leo tunaongozwa na somo lenye Kichwa

" TUTUMIE NDIMI ZETU KWA UTUKUFU WA MUNGU "

~ Yakobo 3: 5-12

5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6. Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
7. Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8. Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9. Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
11. Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12. Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu.


Tunamshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi zima la upimaji kuanza na kuosha salama siku ya leo.Mungu awabariki waliotoa hu...
22/08/2026

Tunamshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi zima la upimaji kuanza na kuosha salama siku ya leo.

Mungu awabariki waliotoa huduma za kuwapima wahitaji na kutoa ushauri kwa watu wote walioweza kufika siku ya leo.

Asante kwa ofisi ya Mchungaji pamoja na k**ati ya Afya na ustawi ya kanisa Kuu kwa maandalizi mazuri. Mpaka wakati mwingine. πŸ™

3 Yohana 1:

2. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.

---------------

Katika picha ni baadhi ya matukio ya kwenye baadhi ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyoandaliwa hapa Kanisani..Hu...
22/08/2026

Katika picha ni baadhi ya matukio ya kwenye baadhi ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyoandaliwa hapa Kanisani..

Huduma zinaendelea kutolewa kwa watu wote waliojitokeza hapa Kanisa kuu Azania Front, karibu sana.




Kabla ya huduma zote , tulianza kwa Ibada fupi iliyongozwa na Mch. Joseph Mlaki na Mch.Kulwa.      Mchungaji Kulwa akise...
22/08/2026

Kabla ya huduma zote , tulianza kwa Ibada fupi iliyongozwa na Mch. Joseph Mlaki na Mch.Kulwa.






Mchungaji Kulwa akisema neno na Watu waliojitokeza kupata huduma za Afya hapa kanisani.

Dkt. Swai akisema neno kwa watu waliojitokeza kupata buduma ya Afya siku ya Leo.

3 Yohana 1:
(3 John)

2. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.
---------------
Beloved, I pray that you may prosper in all things and be in health, just as your soul prospers.

Watoto wakiendelea kupata huduma, kutoka kwa watoa huduma waliopo hapa Kanisani.

Watoto wakiendelea kupata huduma, kutoka kwa watoa huduma waliopo hapa Kanisani.

Katika picha , ni baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kupata huduma za Afya zinazoendelea kutolewa hapa Kanisani.

Katika picha , ni baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kupata huduma za Afya zinazoendelea kutolewa hapa Kanisani.

Katika picha , ni baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kupata huduma za Afya zinazoendelea kutolewa hapa Kanisani.

Katika picha , ni baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kupata huduma za Afya zinazoendelea kutolewa hapa Kanisani.

Tabasamu baada ya kupata huduma nzuri ya kinywa na meno kutoka kwa Madaktari waliopo hapa Kanisani.

3 Yohana 1:
(3 John)

2. Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.
---------------
Beloved, I pray that you may prosper in all things and be in health, just as your soul prospers.

21/08/2026

Shalom πŸ‘‹ !

- Katika video ni Maendeleo ya Ujenzi wa nyumba katika kituo chetu cha Kiroho Kiharaka.

- Nyumba mbalimbali zinaendelea kujengwa na tunamshukuru Mungu kwa sadaka zinazoendelea kutolewa kusaidia kukamilisha ujenzi huu na wale wote ambao wanaendelea kuchukua nyumba moja na kujenga. Mungu awabariki.

- Karibu tuendelee kumtolea Mungu sadaka zetu ili kusaidia maendeleo ya Kiharaka Spiritual Center na kazi ya ujenzi unaoendelea kwa njia zifuatazo.

πŸ› CRDB BANK -

A/c no: 01J1022962300
Jina: Azania Front Spiritual Center

πŸ› MAENDELEO BANK-

A/C No: 013824676021
Jina: Azania Front Cathedral

πŸ› M-PESA LIPA NAMBA

NO: 579 579 4
Jina: Azania Front Cathedral

πŸ“Œ Kwa Maelekezo zaidi; Karibu katika ofisi ya Mchungaji hapa Kanisa kuu Azania Front.

πŸ”ˆ KARIBU TUIJENGE KIHARAKA β›ͺ️β›ͺ️β›ͺ️ !!!!

TANGAZO LA SIKU YA AFYA CHECK  KWA WASHARIKAWapendwa Washarika katika Kristo,Bwana Yesu Asifiwe!Uongozi wa Kanisa unapen...
20/08/2026

TANGAZO LA SIKU YA AFYA CHECK KWA WASHARIKA

Wapendwa Washarika katika Kristo,

Bwana Yesu Asifiwe!

Uongozi wa Kanisa unapenda kuwakaribisha washarika wote, pamoja na familia zenu, marafiki na majirani, kushiriki katika Siku ya Uchuguzi wa Afya zetu.Litakalofanyika terehe 22 Agosti 2026 kuanzia saa 2 hadi saa 9.30 mchana. Lengo la siku hii ni kuhamasisha kinga ya magonjwa, kutambua matatizo ya afya mapema, na kutoa elimu pamoja na ushauri wa kitaalamu kupitia wataalamu wa afya kutoka fani mbalimbali.

πŸ”ˆ HUDUMA ZOTE NI BURE !!!

JUMAMOSI HII ya Tarehe 22. 08. 2026

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na:

1.Afya ya Wanawake:
a.Elimu kuhusu ukomo wa hedhi (Menopause)
b.Elimu na uchunguzi wa awali wa saratani ya shingo ya kizazi
c.Elimu ya kujichunguza matiti
d.Ushauri kuhusu masuala mbalimbali ya afya ya wanawake

2.Afya ya Wanaume:
a.Elimu kuhusu afya ya tezi dume
b.Ushauri kuhusu kuongezeka kwa tezi dume na magonjwa mengine ya tezi dume
c.Ushauri wa jumla kuhusu afya ya wanaume

3.Afya ya Watoto:
a.Ufuatiliaji wa ukuaji wa mtoto
b.Tathmini ya lishe na ushauri wa lishe bora
c.Tathmini ya maendeleo ya ukuaji wa mtoto (Early Childhood Development)
d.Tathmini
Ushauri wa lishe bora kwa watoto.
4.Chakula na Lishew kwa watu wazima:
Elimu kuhusu ulaji unaofaa kwa afya njema.

5.Magonjwa Yasiyoambukiza:
a.Upimaji wa shinikizo la damu na ushauri
b.Upimaji wa kisukari na ushauri
c.Ushauri wa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
d.Elimu ya kujikinga na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza

6.Afya ya Kinywa na Meno:
a.Uchunguzi wa afya ya meno na kinywa
b.Ushauri kuhusu namna bora ya kutunza afya ya meno

7.Afya ya Macho:
a.Uchunguzi wa macho
b.Ushauri na matibabu ya awali kulingana na mahitaji

8.Afya ya Akili:
a.Ushauri nasaha kuhusu afya ya akili
b.Elimu ya kuimarisha ustawi wa afya ya akili

9.Huduma za Mifupa, Tiba ya Viungo na Urekebishaji:
a.Ushauri na uchunguzi wa magonjwa ya mifupa na viungo
b.Ushauri kuhusu matatizo ya nyonga
c.Uchunguzi na ushauri wa maumivu ya mgongo, shingo na maungio
d.Ushauri wa tiba ya viungo (Physiotherapy)

10.Magonjwa ya Kuambukiza:
a.Upimaji na elimu kuhusu Kifua Kikuu (TB)
b.Upimaji wa Virusi vya UKIMWI (HIV) pamoja na ushauri nasaha

17/08/2026

Address

Kivukoni Road/Sokoine Drive
Dar Es Salaam
11101

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KKKT Azania Front Cathedral posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to KKKT Azania Front Cathedral:

Shortcuts

Share