10/02/2026
Bwana Apewe sifa....
UMUHIMU WA KUDUMU KATIKA NENO LA MUNGU.
Watu wote wanatamani sana kuishi maisha ya raha yaani ( mbinguni) hamna hata mmoja anahitaji kuingia moto wa milele.
Kituko kilichopo duniani watu ,rafiki,jamaa anapokufa wengi uandika jumbe ...Mungu aiweke au ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi ...hamna anayetamani hata mpendwa wake aende motoni.
👉Niseme hayo yote baada mtu kufa hakuna njia ya kuamua kuhusu hukumu yake tena hata tufanye ibada nyingi haiwezekani tena kuikoa nafsi yake ikiwa amekufa katika dhambi...hii ni njiaa tu tunaitumia walimwengu KUFARIJI WAFIWA NDUGU ZAKE.
SABABU ZA KUDUMU KATIKA NENO LA MUNGU.
Kinachofanya Mungu atuweke katika mbingu yake ni kule kuishi kwa kuongoza na neno la Mungu.
1.Neno la Mungu ni taa.(ZABURI 119:105)hii ni kusema neno ni mwangaza kwetu wanadamu tunapokubali kuongozwa na neno giza alitakuwa juu yetu.
Kuhusu kuingia mbinguni njia ya ile ya uzima wa milele ni nyembamba na imesonga sana ili kuipita tunahitaji nuru ya Kristo,lakini kuhusu njia ile ya dhambi ni pana kweli wala haibani mtu lakini mwisho ni upotevu milele(MATHAYO 7:13).
Njia ya wenye dhambi ni giza tupu,tumezungukwa na giza hakuna nuru hata kidogo(AYUBU 10:22) Pasipo kuongozwa na taa haiwezekani kuiona mbingu.
Hata Israel ili waione njia waendeayo usiku Mungu aliwaongoza kwa nguzo ya moto NENO LA MUNGU NI NGUZO YENYE NURU HATA LEO .(KUTOKA 13:21).
2.Neno la Mungu ni Dira au Ramani sahihi,sisi ni wapitaji tu na safari yetu ni sikuzote tukiwa hapa duniani hatuna makao ya kudumu tunahitaji ramani sahihi ili tufike salama tunakopaswa kuelekea(ZABURI 39:12, WAEBRANIA 11:13,1PETRO 2:11)
👉Msafiri asiyejua aendako ili aweze kufika ni muhimu kuwa na ramani vinginevyo atapotea maana ajue aendako .
Dira kazi ya ni kumpa mwelekeo msafiri ili afike aendako,hata nahodha bahari anapoongoza meli anahitaji uelekeo na si vinginevyo lazima awe na chombo kiitwacho dira na kwetu waamini ili kufika salama safari yetu ni kudumu katika neno ambalo ni dira yetu.
3.Neno la Mungu ni njia,Yesu Kristo anaitwa neno la Mungu(YOHANA 1:1) na yeye ndio njia kwetu watoto wa Mungu.
👉Hakuna hata mmoja wetu anayeweza kukutana na Mungu pasipo njia yake ambayo ni neno la Mungu (YOHANA 14:6).
4.Neno ni alama ya njia yetu,k**a unavyoona alama za barabarani ndivyo lilivyo neno la Kristo kwetu watoto wa Mungu...ndilo linaweza kutupa tahadhari,maonyo,kutuongezea umakini na kutuonyesha mwendo tunapaswa kwenda nayo maana neno la Mungu ndiyo Hekima ya Mungu mwenyewe.
👉Tukiwa sisi ni wasafiri basi imetupasa kufata alama zote tukitii kwa ukamilifu neno la Mungu (1KORINTHO 10:5-11)
K**a uonavyo wamiliki wa vyombo vya moto na wasafiri wanapokubali kufuata maonyo yote hueluka ajali na mauti,hivyo nasi kwa alama za neno tunaweza kuepuka mauti ya milele na anguko la dhambi ...uzinzi,ulevi,uasherati,kuabudu sanamu,kutegemea wanadamu k**a kinga na ulinzi...nk safarini.
5.Neno la Mungu ni mkono wa Bwana wa kutuongoza,kipofu awezi kwenda peka yake atatumbukia mashimo,ataumia,bali anahitaji aliye mzima wa macho...anayeona vizuri hivyo neno ni Mungu na ndio mkono uwezao kutuongoza vema ili tusipotelee njiani(MATHAYO 15:14)
👉Neno la Mungu linationgoza ili kutimiza mapenzi ya Mungu.
Chochote unacho tamani kupokea kutoka kwa Mungu kipo ndani ya neno la Mungu.Neno la Mungu linabadilisha lolote hata linaweza kuumba upya tabia.(Ufunuo 12:11)
Kwa neno tunamshinda shetani na ubaya wake.
Ubarikiwe sana..