07/09/2026
RHAPSODI YA UHAKIKA
Jumatatu , Septemba 7, 2026
Mchungaji Chris
SEMA KILE ALICHOSEMA
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? (Waebrania 13:5-6).
Mungu hakutupatia Maandiko kwa ajili tu ya taarifa, hamasa, au maagizo ya kimaadili. Ijapokuwa kwa hakika Maandiko hutujenga na kutuelimisha. Waebrania 13:5-6 hutupa hekima [na maono] ya ajabu sana ya kusudi kuu la sababu ya Mungu kuzungumza na sisi. Neno Lake huzaa ndani yetu na kwa ajili yetu kile likizungumziacho. Na nitaelezea jinsi ambavyo hili linatenda kazi.
Baada ya kuwa amesema katika mstari wa tano, “…kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa,” mstari wa 6 unasema, “Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye...” Ona matokeo: Alisema ili ukapate kusema. Hii ni mojawapo ya kanuni za muhimu zaidi katika maisha ya Ukristo. Mungu anakupa Neno Lake ili uweze kulipokea kwenye roho yako na kusema sawasawa na Neno lilo hilo kwa kukubaliana Naye.
Hivyo, katika Ukristo, tunazungumza lugha ya Mungu, tunatangaza Neno Lake kwa ujasiri na tuna kile tunachotamka. Tayari Mungu anaishi ndani yako kwa Roho Wake. K**a shauku Yake ingekuwa ni kukuendesha tu basi, Asingehitaji kuzungumza na wewe kupitia Maandiko. Lakini Anataka uwe mshiriki mwenye kuhusika vyema katika uzoefu wa kiungu, katika utendaji kazi wa Neno Lake, kwa kuzungumza katika makubaliano na Yeye.
Hivyo ndivyo namna imani itendavyo kazi. Walipokea Neno la Mungu kwenye roho yako na kulitamka. Watamka kweli Yake kuhusiana na afya yako, baadaye yako, fedha zako, familia yako, na kila eneo la maisha yako. Neno la Mungu kinywani mwako ni Mungu anazungumza; nguvu Zake huenda na kutenda kwa niaba yako, ikipangilia mazingira [na hali] mbalimbali kwenda kwa faida yako.
Wengi wanatamani Neno la Mungu litimizwe kwenye maisha yao ila hawalineni. Lakini, Neno huwa fanisi tu maishani mwako na kwenye mazingira yako pale unapolitamka kwa ujasiri (uthubutu). Kwahiyo, siku zote tamka uzima, ushindi, haki, afya, usitawi, na mamlaka. Hii ndio siri ya maisha ya Kikristo ya shangilizo [na ushindi].
SALA
Baba Mpendwa, ninashukuru kwa Neno lako ulilonipa niishi kwalo na kulitamka kwa ujasiri. Ninanena katika makubaliano na kweli yako kuhusiana na maisha yangu, na Neno lako hushinda ndani yangu kwa nguvu. Maisha yangu yanaendeshwa kwa Neno lako, na ninatembea kiuendelevu katika ushindi, imani, mamlaka, na utukufu, katika Jina la Yesu. Amina.
MASOMO ZAIDI:
Marko 11:23; Warumi 10:8-10; 2 Wakorintho 4:13
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
2 Wakorintho 6:3-7:1 & Mithali 20-21
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
2 Wathesalonike 1:1-12 & Yeremia 25
**********************************************
Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”
Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional
Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye https://www.rhapsodyofrealities.org