21/05/2019
MAMBO MATATU YALIYO AJABU KWANGU, NAAM MANNE JUU YA UHUSIANO WA MTU NA MUNGU.
Na Daima Kashililika
Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne yanayostaabusha juu ya uhusiano wa mtu na Mungu.
1. MAZINGIRA
Uhusiano wako na Mungu hutegemea sana mazingira uliyopo, hali ya kiroho ya eneo ulipo, upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya Mazingira(Ardhi) na Imani ya mtu au Jamii,
Mazingira ni moja kati ya mambo ya ajabu kutufanya sisi kusitawi katika kumjua Mungu au kudumaa***(kati ya Ajali mbaya duniani).
Inategemea sana mbegu imepandwa katika udongo wa aina gani ili kukua na kuzaa matunda, Udongo naouzungumzia hapa ni Mazingira,
2. WATU
Umezungukwa na watu wa aina gani, Umezungukwa na watu wenye mitazamo gani, Wenye misimamo ipi katika Imani, Wana nguvu gani katika Kumtafuta Mungu, Ni watu(Marafiki, Familia, Ndugu na Jamaa).
Huwa haitegemei sana Viwango vyao vya kiroho na Mahusiano yao na Mungu kukufanya wewe ukue, Ila ni kichocheo kikubwa cha kukua kwako,
Akili zetu wanadamu zimeundwa katika namna ya kuchangamana na watu na mazingira ndipo kutuumba kuwa katika namna Jamii Inayotuzunguka na Mungu hutuona, Hakikisha upo katika jamii ya watu sahihi ili ndani yako pia uumbike sawa na Mungu anavokutazama.
3. HALI
Ni Hali ya Uchumi, Afya, hali ya inayoruhusu hali isiyoruhusu, Vyote huwa ni mambo ya msingi kuzingatia juu ya mahusiano yako na Mungu,
Kuna wengine pamoja na mali nyingi walizonazo lakini mahusiano yao na Mungu si tajiri, wengine ni masikini wa mali hata rohoni, wengine wakati wote tunawaza hatuwezi, wakati mwingine magonjwa tuliyonayo, Hali ya afya, husababisha watu kukata tamaa na maisha, na kuona kuwa Mungu labda hawezi tena,
Kumbuka hali uliyonayo iwe nzuri au isiwe nzuri hata siku moja isiwe ni sababu ya kutoka katika Imani (Kuharibu mahusiano yako na Mungu)
4. MAJIRA NA NYAKATI
Hapa nazungumzia Muda, Kati ya vitu Mungu amempa mwanadamu ni muda*** Na ukifika wakati hukutumia muda sawasawa na Mungu anavyosema uwe na uhakika, utaishi maisha yako yote na udhihirisho wa Mungu katika ujumla wakati hutouona lakini Mbinguni utakwenda, Hutoyafaidi Maisha Ambayo Mungu aweyaweka kwa ajili yako hapa duniani. Tumia muda Vizuri.
K**a mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; Isaya 1:19
Yaani k**a mkikubali na kutii haya hakika yake ni kula mema (Yameandaliwa yatari na kuwekwa kwa ajili ya mimi na wewe) juu ya uso wa Ulimwengu huu.
Yesu anakupenda.
Utukufu Heshima Enzi na Adhama zina Mungu aliyeziumba Mbingu na Nchi.
.
Daima Kashililika
0757357871
Habari Njema Ministry 2019