08/09/2021
KUTOKA KWENYE KIWANGO CHA KUOMBA KWENDA KWENYE KIWANGO CHA KUAGIZA
Kila mtu huomba, huomba sana tena huomba, huomba Kila Siku, Kila Siku ni maombi. Huomba kwa uchungu pale mtu anapokuwa na matatizo au tatizo zito. Huomba kwa kuugua. Pia kuna maombi mepesi ambayo siyo ya kuumia wala kuugua, mtu anaomba kwa kulilux. Neno linasema ombeni bila kukoma, bila kukoma ni mpaka pale mtu atakapopata kile kitu anachokitaka. Lakini mtu anatakiwa apige hatua kutoka kwenye Kiwango cha kuomba kwenda kwenye Kiwango cha kuagiza. Kuomba ni kubembeleza, kurudia-rudia maneno, yaani asubuhi umeomba hilo, mchana, usiku, kesho hilohilo, keshokutwa hilohilo yaani unarudia-rudia kutokana na uhitaji wako. Kuomba mtu anaomba hadi analia machozi, anaumia, anaugua maumivu makali. Nk. Kuna wakati mtu anatakiwa avuke kiwango hicho cha kuomba na kwenda kwenye kiwango cha kuagiza. Kumb 12:20 "Ukisema nataka kula nyama, waweza Kula nyama kwa kufuata yote inayotamani roho yako". Mtu anayeagiza anasema nataka, Nipe au Niletee kitu fulani. Kuna kipindi mtu anamwambia MUNGU, BWANA nataka unifanyie hiki kitu, BWANA nipe kitu fulani. Na MUNGU anafanya bila AJIZI. Ukifikia hiyo hatua ni raha sana.