Efatha Church Mongolandege

Efatha Church Mongolandege EFATHA MAANA YAKE FUNGUKA. WE BRING THE WORLD TO JESUS

MTUMISHI:PRECIOUS IBRAHIMUSOMO:UKIRIUkiri ni nini? Ni kules kusema jambo,ambalo umeambiwa uliseme ukiwa na uhakika nalo....
29/06/2025

MTUMISHI:PRECIOUS IBRAHIMU
SOMO:UKIRI

Ukiri ni nini? Ni kules kusema jambo,ambalo umeambiwa uliseme ukiwa na uhakika nalo.

Mfano; neno moja katika kanisa la wana Efatha tunalitumia lakini lina maana kubwa. Sana na unapolitamka linafanya mambo makubwa sana ni neno Efatha maana yake FUNGUKA linapatikana kwenye kitabu cha Marko 7:30.

Neno hili unapolisema wakati unaombea wagonjwa au waliofungwa na vifungo mbalimbali k**a mapepo na magonjwa alafu ukisema neno Efatha yaani FUNGUKA katika jina la Yesu na ukiamini wanafunguliwa na kuponywa .unachotakiwa kuamini na kukiri wakati huo huo unapokea. Nguvu ya Mungu inayozidi ili kumfungua au kumponya.

Unapotumia neno la ukiri litakupa ushindi inategemea na wewe umeamini nini.

Mathayo 15:21-28. "Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako k**a utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile"

Tunaona imani ya huhu mwanamke mkananayo,akingangana mpaka akapata alicbokiwa anakipigania na hiyo yote au kilichomuwezesha kupata akitakacho ni imani yake kwa Bwana Yesu.

MTUMISHI:FAITH RICHARDSOMO:KUWASILIANA NA MUNGU KWA NJIA YA KUSIFU .Kusifu ni nini? Ni njia moja wapo ya kuwasiliana  na...
29/06/2025

MTUMISHI:FAITH RICHARD
SOMO:KUWASILIANA NA MUNGU KWA NJIA YA KUSIFU .

Kusifu ni nini? Ni njia moja wapo ya kuwasiliana na Mungu

Zaburi 117:1. "Haleluya.
Enyi mataifa yote, msifuni BWANA,
Enyi watu wote, mhimidini"

Kumsifu Mungu ni kueleza uzuri aliokua nao na matendo makuu aliyotufanyia.Kwa maana si bila yeye hatuwezi kitu chochote kwakiwa tu ata kiwa apa mda huu ni kwa neema yake.

Kumsifu Bwana ni kumwinua kumtukuza kumwangaza na kukukili matendo yake anayokwenda kutufanyia katika maisha yetu yajayo.Mungu wetu amesema yeye anatuwazia mema kila iitwapo leo.

Kwa ujumla kumsifu Mungu kunaitaji utulivu, unyenyekevu, utii na utulivu.ni lazima twende mbele za Mungu tukiwa safi kimwili na ata kiroho pia ili kumpendeza Mungu wetu wakati wa sifa na hata wakati usiyo wa sifa.

Tunatakiwa tujitengeee na dhambii kwa kiwa dhambi ndio inatufanya sisi kukaa mbali na Mungu wetu wa mbinguni.Ni lazima tujitengeee na dhambi ili tuweze kiwa safi kiroho na ata kimwlli pia mda wote wakati wowote na mahali popote ili Mungu wetu afurahi.

Sifa inqnvuvu sana inapokuwepo katikati yenu.Mungu anashuka katikati ya sifa, na anaposhuka magonjwa,vifungo, maumivu ,mateso ya kila haina , uchawi n.k yoteee yataondoka kwako maana yeye ameshuka kuja kuwaoa hitaji la mioyo yenu.

"Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina ...
29/06/2025

"Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu."

SHEREHE YA WATOTO  YA TAREHE 28/6/2025 KANISA LA EFATHA MONGOLA NDEGE,UKONGA MOMBASA DAR ES SALAAM TANZANIA.MTUMISHI.GLO...
29/06/2025

SHEREHE YA WATOTO YA TAREHE 28/6/2025 KANISA LA EFATHA MONGOLA NDEGE,UKONGA MOMBASA DAR ES SALAAM TANZANIA.

MTUMISHI.GLORY FANUEL

Zaburi 150:1-2. "Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake"

©️MTUMISHI GLORY FANUEL, -EFATHA CHURCH MONGOLANDEGE

MATUKIO KATIKA PICHAWATUMISHI WALIHITIMU WAKIPOKEA VYETI VYA ROHO MTAKATIFU
06/04/2025

MATUKIO KATIKA PICHA

WATUMISHI WALIHITIMU WAKIPOKEA VYETI VYA ROHO MTAKATIFU

MTUMISHI: PAULO MPEGESASOMO:MZALIWA WA KWANZAMzaliwa wa kwanza ni lango la baraka au laana katika familia, Mzaliwa wa kw...
06/04/2025

MTUMISHI: PAULO MPEGESA
SOMO:MZALIWA WA KWANZA

Mzaliwa wa kwanza ni lango la baraka au laana katika familia, Mzaliwa wa kwanza hukombolewa kwa sadaka.Mzaliwa wa kwanza akishakombolewa baraka huja kupitia yeye.Mzaliwa wa kwanza ni msingi unaobeba uchumi,ndoa,elimu n.k hvivyo shetani hupambana nae huyo mzaliwa wa kwanza ili hayo yote yasipite kwenye hiyo familia

Hesabu 18:15
Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea Bwana cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa.

Mzaliwa wa kwanza wa mnyama wafaa kutolewa kwa Bwana lakini mzaliwa wa kwanza wa mwanandamu lazima akombolewe kwa sadaka ambayo hiyo sadaka hubaki madhabahuni na kupitia hiyo sadaka Mungu huambatana na huyo mzaliwa wa kwanza kwa kila anachokifanya maana sadaka inanena mema.kupitia sadaka ya mzaliwa wa kwanza humtoa kunako matambiko ya mizimu ya familia yao, yaliyo fanyika pale ulipozaliwa.Mzaliwa wa kwanza akikombolewa familia nzima inakombolewa na baraka zinaanza kuingia katika familia

Kutoka 34:20
Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena kwamba hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu.

MATOLEO:MTUMISHI: ERICA SAROZaburi 23:1-6.         "Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.Katika malisho ya...
06/04/2025

MATOLEO:

MTUMISHI: ERICA SARO

Zaburi 23:1-6. "Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele."

Tunapomtolea bwana matoleo yeye hutu chunga na huisha nafsi zetu na kutuongoza katika njia za haki kwa hajiri ya jina lake, unapopitia katika changamoto yoyote yeye anakufanyia usaidizi na anakufadhiri kwa kila unalo pitia

"Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidini. Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminif...
06/04/2025

"Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidini. Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa Bwana ni wa milele."

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 6/4/2025 KANISA LA EFATHA MONGOLA NDEGE,UKONGA MOMBASA DAR ES SALAAM TANZANIA.ASKOFU: GLORY MNY...
06/04/2025

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 6/4/2025 KANISA LA EFATHA MONGOLA NDEGE,UKONGA MOMBASA DAR ES SALAAM TANZANIA.

ASKOFU: GLORY MNYAMBO

Yohana 18:1. "Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake."

©️ASKOFU GLORY MNYAMBO, -EFATHA CHURCH MONGOLANDEGE

Nadhiri ya Hana ilisababisha kumpata Samweli,Hivyo nadhiri yako itasababisha upate vingi nyumbani mwako.Sadaka ya mzaliw...
30/03/2025

Nadhiri ya Hana ilisababisha kumpata Samweli,Hivyo nadhiri yako itasababisha upate vingi nyumbani mwako.Sadaka ya mzaliwa wa kwanza inasababisha milango yake ya baraka ifunguliwe ata k**a imefungwa.

Sadaka ya mzaliwa wa kwanza(limbuko) humkumbusha Mungu kwa habari ya hicho ulichokitolea sadaka pia ni ulinzi maana Mungu huangalia kwa ukaribu.

Mwanzo 13:13. "Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.

Mzaliwa wa kwanza wa mnyama unaweza kumtolea sadaka au ukamtoa yeye mwenyewe ili mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu uafaa kumbokoa kwa sadaka

©️MTUMISHI PAULO MPEGESA EFATHA CHURCH MONGOLANDEGE.

Samweli alifanyika limbuko mbele za Bwana, na Hana aliendelea kuwa anapokea baraka ya uzao wake .Samweli alitolewa limbu...
30/03/2025

Samweli alifanyika limbuko mbele za Bwana, na Hana aliendelea kuwa anapokea baraka ya uzao wake .Samweli alitolewa limbuko mbele ya Bwana pamoja na sadaka.

Fungu la kumi kazi yake ni kusababisha au kuzalisha baraka.Limbuko kazi yake ni kukalisha baraka.Kitu kinachofanya baraka zikae ndani ya familia ni limbuko sadaka ya mzaliwa wa kwanza wa kitu chochote iwe wa
binadamu, wanyama(Mifugo), Mazao, Biashara.Chochote cha kwanza unachozalisha cha kwanza ni cha Bwana.Hivyo tafuta kitu cha kusababisha ili kukalisha hizo baraka ndani yako.

Ili uweze kumiliki kiwe chakwako ni lazima ukikomboe kwa sadaka.Mungu humwangalia mzaliwa wa kwanza na shetani pia anamwamgalia mzaliwa wa kwanza maana mzaliwa wa kwanza ni lango la kupitisha baraka kwa mwanadamu .

Hivyo ili biashara yako au kazi yako iweze kusonga mbele au kukua kutoka kiwango cha chini kwenda kiwango cha juu ni lazima utoe sadaka ya limbuko(sadaka ya mzaliwa wa kwanza).

©️MTUMISHI PAULO MPEGESA EFATHA CHURCH MONGOLANDEGE

Address

Ukonga
Dar Es Salaam

Telephone

+255699496740

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Mongolandege posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church Mongolandege:

Share