The Promises Of GOD Ministry-PGM

The Promises Of GOD Ministry-PGM KWAKUWA AHADI ZOTE ZA MUNGU NDANI YA YEYE NI NDIYO, TENA AMIN.��

Online SeminarWith: Minister PANDISHA"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES And AMEN." { 2 CORINTHIANS 1:2...
20/06/2022

Online Seminar
With: Minister PANDISHA

"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES And AMEN." { 2 CORINTHIANS 1:20 }

Somo: Uponyaji Wa Mungu Kwa Kuwekewa Mikono.

NUKUU
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; Kwa Jina Langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakita wadhuru kabisa; WATAWEKA MIKONO YAO JUU YA WAGONJWA, NAO WATAPATA AFYA." { Marko 16:17-18 }

"Wala hakuweza kufanya muujiza wowote huko, isipokuwa ALIWEKA MIKONO YAKE JUU YA WAGONJWA WACHACHE, AKAWAPONYA." { Marko 6:5 }

"Mungu akafanya KWA MIKONO YA PAULO miujiza ya kupita kawaida." { Matendo 19:11 }

Katika mikono ya mwanadamu kuna nguvu na siri nyingi sana katika mambo ya kiroho. Huduma ya kuwekea mikono ina mapana sana. Ila katika somo hili, tutaangazia nguvu ya UPONYAJI WA MAGONJWA NA MADHAIFU kwa kuwekea mikono.

✓Katika maisha yako Muamini ni lazima kujua ni kwa jinsi gani TUNAMUAMINI MUNGU. Kwa JINSI GANI TUNATAKIWA KUMUAMINI YESU KRISTO. Jibu ni kwamba TUNAMUAMINI MUNGU KWA KULIAMINI NENO LAKE. KILE ALICHOKISEMA, KILE ALICHOKIAHIDI KATIKA NENO LAKE.
"Naye Yesu akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hatoishi kwa mkate ( chakula ) tuu, bali ( Ataishi ) KWA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWA MUNGU" { Mathayo 4:4,Luka 4:4 }
Kumbe Imani halisi ni KUMUAMINI MUNGU KUPITIA KULIAMINI NENO LAKE. Kumbe, jinsi ulivyolisoma Neno La Mungu katika Biblia yako, ndivyo hivyohivyo litakavyofanya k**a utaliamini na kulikubali. Neno La Mungu limekuja kwetu ili LITIMIZE MAPENZI YA MUNGU KWETU.
"Maana ahadi zote za Mungu zilizopo ndani ya Yesu Kristo ni NDIYO Tena AMEN" { 2 Korintho 1:20 } [ Amen maana yake ni HAKIKA au Kweli hasa nisemavyo ]
Unatakiwa kuwa na Uhakika na Neno Lake. Mungu hawezi kusema Uongo wala hana sababu ya kusema Uongo.
"Mungu si mwanadamu hata aseme uongo....iwapo amelisema hatalitenda.? Iwapo amenena hatalitimiliza.? { Hesabu 23:19 }
✓Unachopaswa kufanya ni jambo hili
"Amini kuamini kwako na Tilia mashaka Mashaka yako" Ukiona unakuwa na mashaka na Neno la MUNGU kwamba
"Hii haipo hivi"
"Hii si ya nyakati hizi"
Au
"Hili linawezekana kwa watu maalumu au watumishi wa MUNGU peke yao"; Ukiwaza kwa mashaka hayo ujue wewe siyo MUAMINI na hakuna kitakachofanyika hata k**a Neno limesema hivyo. Ukiliamini Neno la MUNGU kwamba hivi lilivyo ndivyo; Utakuwa muamini kwelikweli na utaanza kumpendeza MUNGU.
"Pasipo imani haiwezekani kumpendeza (MUNGU)".{Waebrania 11:6}

✓Sasa Neno la MUNGU linatuagiza KUWAWEKEA WAGONJWA MIKONO YETU ili wawe wazima. Na nilazima ujue kwamba halisemi wachungaji au walimu wawekee wagonjwa mikono, hapana, linasema WAAMINI. Hii inamaana kwamba hata k**a UMEOKOKA dakika iliyopita, ukiweka mikono yako juu ya mgonjwa atakuwa mzima. Na ukumbuke Neno la MUNGU halisemi weka mikono juu ya mgonjwa wa malaria na kichomi tu, hapana , ni kwa mgonjwa wa ugonjwa wowote ule, ulio na jina na hata usio na jina.
Shida ya hili Neno kutokukubalika kirahisi mioyoni mwa waamini ni mbili:-

1. Waamini hatufundishwi juu ya maisha ya imani ya kumuamini MUNGU na NENO lake na hivyo tunaendelea kuishi na wagonjwa majumbani na hospitali tukiona ni sawasawa wao kuumwa.

2. Shetani amepofusha fikra/akili zetu ili tusimuamini MUNGU na NENO lake.
"Ndipo (YESU) akawafunulia akili zao, wapate kuyaelewa na maandiko".{Luka 24:45}.

"mungu wa dunia hii amepofusha fikra(akili) zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU" { 2 Korintho 4:4 }.

✓ Huduma ya KUWAWEKEA MIKONO WAGONJWA ili wawe wazima ni AHADI YA YESU KRISTO MWENYEWE k**a tulivyoona katika Neno lake {Marko 16:17-18} na hii imedhihirika kwanza katika huduma yake Yesu Mwenyewe na hata kwa waliotii neno hili. Hapa nakuonesha kwa uchache tu walioweza kuwasaidia wagonjwa kwa kuwawekea mikono na wakawa wazima.

"Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona akaanguka miguuni pake, akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, UWEKE MKONO WAKO JUU YAKE, apate kupona na kuishi". { Marko 5:22-23 }

"Wakafika Bethsaida, wakamleta kipofu, WAKAMSIHI AMGUSE. Ndipo AKAWEKA TENA MIKONO YAKE JUU YA MACHO YAKE, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi". { Marko 8:22,25 }
"Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi (kiguvumizi) wakamsihi AMWEKEE MIKONO"{Marko 7:32}
" WATAWEKA MIKONO YAO juu ya wagonjwa nao watapata afya. { Marko 16:18 }
" Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo la udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyooka kabisa. YESU alipomwona alimuita, akamwambia mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. AKAWEKA MIKONO YAKE juu yake (yule mama), naye akanyooka mara hiyo, akamtukuza MUNGU" { LUKA 13:11-13 }
"Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, AKAWEKA MIKONO YAKE JUU YA KILA MMOJA AKAWAPONYA". { Luka 4:40 }
"Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, AKAWEKA MIKONO YAKE JUU YAKE na kumpoza". { Matendo 28:8 }
"(YESU) ALIWEKA MIKONO YAKE juu ya wagonjwa wachache, AKAWAPONYA".{ Marko 6:5 }
"YESU akajibu akasema, muwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya".{ Luka 22:50-51 }

UKIAMINI, HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA MUNGU. MUAMINI MUNGU KWA NENO LAKE NA UWEKE MIKONO YAKO JUU YA WAGONJWA; OMBA KWA IMANI; WATAPATA AFYA. AMINI NAKUAMBIA. MIMI NILIAMINI HIVYO IKAWA HIVYO.

STAY IN CHRIST JESUS IN THE NAME OF JESUS, Amen.

Online SeminarWith: Minister PANDISHA"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES; And AMEN" { 2 CORINTHIANS 1:2...
14/06/2022

Online Seminar
With: Minister PANDISHA

"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES; And AMEN" { 2 CORINTHIANS 1:20 }

Somo: USIZITII TAMAA ZA MWILI WAKO.
Mwili Hauna Mpango Wa Kuokoka Wala Kwenda Mbinguni.

NUKUU
".......... Sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatayo roho huyafikiri mambo ya roho. Kwakuwa, nia ya mwili ni MAUTI; bali nia ya roho ni UZIMA NA AMANI. Kwakuwa ile nia ya mwili ni UADUI JUU YA MUNGU, kwamaana haitii sheria ya Mungu wala haiwezi kutii; WALE WAUFUATAO MWILI HAWAWEZI KUMPENDEZA MUNGU" { Rumi 8:4-8 }

"Kesheni muombe, msije mkaingia majaribuni. ROHO I RADHI LAKINI MWILI NI DHAIFU" { Mathayo 26:41, Marko 14:38 }

"Msiipende dunia wala mambo yaliyomo kwenye dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani TAMAA YA MWILI, NA TAMAA YA MACHO, NA KIBURI CHA UZIMA, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. NA DUNIA INAPITA, PAMOJA NA TAMAA ZAKE, BALI YEYE AFANYAE MAPENZI YA MUNGU, ADUMU HATA MILELE" { 1 Yohana 2:15-17 }

Roho ya mtu [Ambayo ndiyo mwanadamu mwenyewe] asili yake ni Mbinguni. Wewe si wa duniani hapa. Na ingepaswa kuwa kwamba Mtu Anapookoka tu, Anapomkiri Yesu Kristo na Kumkubali kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake, Mwana wa Mungu Aliye Hai, Aliyetumwa na Mungu Toka Mbinguni Kuja duniani kuwaokoa wanadamu toka kwenye umiliki wa shetani na dhambi zao, kwa Kumkiriri hivyo na kumkubali, Mwanadamu Alipaswa Kunyakuliwa Aende Zake Mbinguni kwenye Asili yake. Lakini kutokana na hitaji kubwa la kuusimamisha na kuutangaza Ufalme wa Mungu hapa duniani, wanadamu tumelazimika kuendelea kubakia hapa duniani hata baada ya kuokoka kwetu. Haya utayaelewa vizuri k**a utayatafakari maombi ya Bwana wetu YESU KRISTO katikasura ya 17 ya Injili ya Yohana hasa hasa mstari wa 14-16. Lakini, mwili asili yake ni hapa hapa duniani, siyo mbinguni k**a ilivyo roho. Na mwili hauwezi kwenda Mbinguni. Utabaki hapahapa duniani kwenye asili yake.
"Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele. Nayo mavumbi kuirudia nchi k**a yalivyokuwa, Na roho kumrudia Mungu aliyeitoa." { Mhubiri 12:5,7 }
"........….hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ULITWALIWA; KWAMAANA U MAVUMBI WEWE; NAWE MAVUMBINI UTARUDI" { Mwanzo 3:19 }
Kwahiyo, ukiupenda mwili wako na kuutimizia tamaa zake, SI MWILI WAKO WALA ROHO YAKO ITAKAYOKWENDA MBINGUNI.
Kumbuka tumesema hapo juu kwamba Mungu hawezi kufanya jambo duniani bila ya msaada wa mwili wako. Hata NENO WAKE [Mwana wake/ YESU] alilazimika kuuvaa mwili wa kidunia ili aweze kuyafanya mapenzi yake hapa duniani. "Naye NENO alifanyika mwili, akakaa kwetu......." { Yohana 1:14 }
"Maana si tu ni wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, NI JENGO LA MUNGU" { 1 Korintho 3:9 }
✓Lakini pia shetani hawezi kuufanya uharibifu wake na ubaya wake bila ya kupitia mwili wa mtu.
Kwahiyo, UNA UCHAGUZI WA YUPI APITIE MWILI WAKO KUJIDHIHIRISHA KWA MATENDO YAKE KUPITIA WEWE. AMA NI ROHO WA MUNGU KWA UFALME WA MUNGU HAPA DUNIANI AMA NI shetani KWA UHARIBIFU NA UBAYA.
"Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii (Kumruhusu Akutumie) MMEKUWA WATUMWA WAKE yule mnayemtii; kwamba ni UTUMISHI WA DHAMBI ULETAO MAUTI AU UTUMISHI WA UTII ULETAO HAKI" { Rumi 6:16 }
"Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo.? Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu Aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu.? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE; MAANA MLINUNULIWA KWA THAMANI. Sasa basi, MTUKUZENI MUNGU KATIKA MIILI YENU" { 1 Korintho 6:15, 19-20 }
✓Lakini Neno linasema, "Kila atendae dhambi (Atimizae tamaa za mwili) afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi" { 1 Yohana 3:4 } Na ukiwa muasi unafananishwa na MCHAWI. Waweza kuona sasa ile dhambi ambayo shetani anakudanganya uione ni ndogo mno inavyokuweka kundi moja na WACHAWI WAKUBWA siku ya hukumu. "KWANI KUASI NI K**A DHAMBI YA UCHAWI" { 1 Samweli 15:23 }
✓Siku zote, mwili hupenda kurudia kukifanya kile mwili ulichozoezwa kukifanya. Ukiwa na tabia fulani au mtindo fulani wa maisha, mara kwa mara mwili wako utakupigia kelele kuyalilia utende yale mambo uliyouzoeza mwili wako kuyatenda. Ukiwa ni mlevi wa pombe au sigara au dawa za kulevya au k**ari, lazima baada ya muda tuu, mwili wako utakupigia kelele kuvihitaji vitu hivyo. Usitarajie shetani kuja kukujaribu na kukushawishi kwa dhambi ambayo hujawahi kuifanya. Anajua uwezekano wa yeye kukuk**ata katika hiyo ni mdogo. Kwa mfano, k**a hujawahi kutumia dawa za kulevya, shetani hawezi kuuambia mwili wako ukupigie kelele kutumia dawa za kulevya. Atahakikisha anakupitisha kwenye kona ile ambayo wewe ni dhaifu na umeshauzoeza mwili wako kufanya hayo. "Basi na sisi pia, kwakuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, NA DHAMBI ILE ITUZINGAYO KWA UPESI, na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu" { Ebrania 12:1-2 }
✓Kuiacha tabia uliyoizowea si kitu rahisi. Lakini ngoja nikuulize swali, KWANI UKIACHA UZINZI UTAKUFA.?, UKIACHA POMBE UTAKUFA.? UKIACHA WIZI UTAKUFA.?
✓Mungu asingekuambia USIZINI k**a ingekuwa huwezi kuishi bila kuzini. Asingekwambia usiseme UONGO k**a ingekuwa huwezi kuishi bila kusema UONGO. TATIZO NI WEWE KUJIENDEKEZA NA HUJAAMUA KUSHINDANA NA DHAMBI.
"Hamjafanya VITA hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi." { Ebrania 12:4 }
Pambana. Pigana na dhambi. Jichunguze ujue ni maeneo gani unanaswa na dhambi kirahisi. Angalia vitu unavyopenda kuvitazama. Picha, Video. Nyimbo unazopenda kusikiliza. Mazungumzo yako. Aina ya marafiki na tabia zao. Unachokula, Unachosikia, Unachotazama kina ushawishi mkubwa sana wa kuiendea dhambi yako. Matumizi mabaya ya Mitandao ya kijamii, baadhi ya vipindi katika Televisheni, baadhi ya movies na nyimbo za kidunia unazozipa nafasi moyoni mwako, vina mchango mkubwa wa kukunasa katika dhambi yako HASA YA TAMAA YA MWILI NA TAMAA YA MACHO. "Msidanganyike; Mazungumzo mabaya, huharibu tabia njema. Tumieni Akili k**a ipasavyo wala msitende dhambi" { 1 Korintho 15:33-34 }
"Wala msimpe ibilisi nafasi" { Efeso 4:27-32 }
✓K**a ukiamua kwa dhati utaishinda dhambi yoyote hata k**a mwili ukikupigia kelele. Maanisha kumuishia Yesu. Mkabidhi maisha yako na njia zako zote. Mtumaini Bwana, naye atatenda. "Kaeni ndani yangu (Yesu), nami ndani yenu. K**a vile tawi lisivyoweza kuzaa likiwa peke yake, lisipokaa ndani ya mdhabibu; kadhalika nanyi msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; nanyi ni matawi; akaae ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana. MAANA PASIPO MIMI, NINYI HAMUWEZI KUFANYA NENO LOLOTE." { Yohana 15:4-5 }
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu Naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili." { Yakobo 4:7-8 }
"Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, SI KUMUAMINI TU, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE" { Filipi 1:29 }
"Wapenzi, nawasihi k**a wapitaji na wasafiri, ZIHEPUKENI TAMAA ZA MWILI ZIPIGANAZO NA ROHO" { 1 Petro 2:11 }
"Tangu sasa, msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, BALI KATIKA MAPENZI YA MUNGU, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kuyafanya mapenzi ya Mataifa; kuenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu, isiyo halali." { 1 Petro 4:2-3 }
"WENYE MACHO YAJAAYO UZINZI, watu wasiokoma kutenda dhambi, WENYE KUHADAA ROHO ZISIZO IMARA, WENYE MIOYO ILIYOZOEZWA KUTAMANI, WANA WA LAANA" { 2 Petro 2:14 }
"Basi wapenzi wangu, kwakuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha MUNGU" { 2 Korintho 7:1 }
"Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtozitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwasababu mwili hutamani ukishindana na roho, na roho kushindana na mwili, kwamaana hizi zimepingana hata hamuwezi kufanya mnayoyataka" { Galatia 5:16-17 }
"Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu.." { Yohana 6:63 }
"Kwamaana, wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, K**A WAKINASWA TENA NA KUSHINDWA, HALI YAO YA MWISHO HUWA MBAYA KULIKO ILE YA MWANZO. Maana ingekuwa heri kwao k**a wasingeliijua njia ya haki, kuliko kuijua kisha kuiacha ile amri Takatifu waliyopewa" { 2 Petro 2:20-22 }
"Wale washukao shimoni HAWAWEZI KUITARAJIA KWELI YAKO" { Isaya 38:18 }
"Kwamaana, hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha Mbinguni na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja Neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, WAKAANGUKA BAADA YA HAYO, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WATUBU, kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao na kumfedhehesha kwa dhahiri" { Ebrania 6:4-6 }
"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imekwishafunuliwa, nayo yatufundisha KUKATAA UBAYA NA TAMAA ZA DUNIA, tupate kuishi kwa kiasi na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa...........ambaye (Yesu Kristo) alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake Mwenyewe, WALE WALIO NA JUHUDI KATIKA KUTENDA MEMA. { Tito 2:11-12,14 }
"Lakini, UASHERATI USITAJWE KWENU KAMWE, wala uchafu wowote, wala kutamani, K**A IWASTAHILIVYO WATAKATIFU." { Efeso 5:3 }
"Enyi wazimzi, hamjui kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu.? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu." { Yakobo 4:4-5 }
"LAKINI ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI" { 2 Timotheo 2:22 }
"Kila mmoja wenu ajue KUUWEZA MWILI WAKE Katika utakatifu na heshima" { 1 Thesalonike 4:4 }

UNAZO NGUVU ZA KUUSHINDA MWILI. AND SO GOD HELP YOU. Amen.

Online SeminarWith: Minister PANDISHA"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES And AMEN" { 2 CORINTHIANS 1:20...
07/06/2022

Online Seminar
With: Minister PANDISHA

"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES And AMEN" { 2 CORINTHIANS 1:20 }

Somo: UPONYAJI KATIKA JINA LA YESU.

Yesu Kristo ni Utimilifu wa mambo yote. Yeye ni mambo yote katika yote. ( Kolosai 3:11 ). JINA LA YESU linaweza kufanya jambo lolote lile hata k**a linahusu Uumbaji. Jina hili hapo mwanzo lilikuwa Jina la Mungu Baba Mwenyewe, akamrithisha Yesu Kristo (Mzaliwa wake wa kwanza) [ Yohana 17:11-12 ] [ Ebrania 1:4 ]. Jina la Yesu lina Mamlaka, Amri na Uwezo juu ya mambo yote na hali zote. Juu ya falme na mamlaka, juu ya pepo, juu ya magonjwa, juu ya nguvu za giza, juu ya adhabu, juu ya kesi, juu ya utasa, juu ya uvimbe, juu ya fedheha au aibu yoyote ile, juu ya kazi yoyote ya shetani, juu ya baraka na ushindi, juu ya kila jambo.

NUKUU.

"AMIN, AMIN, Nawaambia, Mkimuomba Baba neno lolote (kitu chochote) atawapa KWA JINA LANGU (YESU) { Yohana 16:23 }

"Nanyi mkiomba lolote KWA JINA LANGU, hilo litalifanya; ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno (jambo) lolote KWA JINA LANGU, hilo nitalifanya. { Yohana 14:13-14 }

"Mungu alimuadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa Jina La Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA Kwa Utukufu wa Mungu Baba." { Filipi 2:9-11 }

"Amefanyika bora kuliko malaika, kwa kadiri Jina alilolirithi lilivyotukufu kuliko lao" {Ebrania 1:4}

Katika maisha ya mitume wa Yesu, tunakutana na ndugu ambaye alikuwa mlemavu wa miguu. Hakuwahi kutembea hapo kabla tangu utoto wake kwa kuwa alikuwa mlemavu wa miguu tangu alipokuwa akiishi tumboni mwa mama yake.
"Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake, alichukuliwa na watu, ambao walimuweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao hekaluni. Mtu huyu alipowaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro akamkazia macho pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Akawaangalia akitarajia kupata kitu toka kwao. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha wala dhahabu, lakini nilichonacho ndicho nikupacho. KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI, simama uende. Akamshika mkono wa kuume akamuinua, mara nyonga zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda akirukaruka na kumsifu Mungu. Watu wote wakamuona akienda, akimsifu Mungu. Wakamtambua ya kuwa yeye ndiyo yule aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka kwenye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa na mshangao, wakastaajabia mambo yale yaliyompata." { Matendo 3:1-10 }

"Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, K**A KWAMBA TUMEMFANYA MTU HUYU AENDE KWA NGUVU ZETU SISI, au kwa utauwa wetu sisi.? Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake YESU, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe. Bali ninyi mlimkana Yule Mtakatifu, Yule Mwenye Haki, mkataka mpewe muuaji; mkamuua Yule Mkuu wa Uzima, ambaye MUNGU amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake. Na KWA IMANI KATIKA JINA LAKE, JINA LAKE LIMEMTIA NGUVU MTU HUYU mnayemuona na kumjua; NA IMANI ILE ILIYO KWAKE YEYE ( YESU ) IMEMPATIA MTU HUYU UZIMA HUU MKAMILIFU mbele yenu ninyi nyote." { Matendo 3:12-16 }
Hakika Jina La Yesu kwa ndugu huyu lilifanya kitu kigumu mno kuwa chepesi sana na rahisi mno.
Hata wewe hapo Kwa kuliamini Jina La Yesu waweza kuuamuru ugonjwa umtoke mtu naye akawa mzima.

Petro na Yohana waliendelea kuwahubiri watu pale hekaluni juu ya Kumuamini Yesu na Jina Lake na Toba, lakini Makuhani, akida wa hekalu na Masadukayo hawakupenda mahubiri yale, Wakawak**ata. Wakawafunga gerezani mpaka kesho yake.
"Hata asubuhi, wakubwa na wazee wa hekalu na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, na Anasi Kuhani mkuu na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake kuhani mkuu. Walipowaweka katikati wakawauliza, Ni kwa nguvu gani na kwa jina la nani, ninyi mmefanya haya" { Matendo 4:5-7 } Petro, hali akiwa amejawa nguvu za Roho Mtakatifu, akawajibu, "Jueni nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI, ambaye ninyi mlimsulubisha na Mungu akamfufua katika wafu, KWA JINA HILO, mtu huyu anasimama akiwa mzima kabisa mbele yenu." { Matendo 4;10 } "WALA HAKUNA WOKOVU KATIKA (kiumbe au mtu) MWINGINE AWAYE YOTE, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo [isipokuwa JINA LA YESU] { Matendo 4:12 }
✓Katika Agizo Kuu la Yesu Kristo kwetu sisi wanafunzi wake, lililopo katika Marko 16, tunaoneshwa pia jinsi JINA LA YESU lilivyopewa umuhimu mkubwa kwetu ili kutusaidia kuifanikisha huduma yetu na agizo tuliloagizwa. "Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.......Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, KWA JINA LANGU, watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka, hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa, wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya" { Marko 16:15,17-18 } Waweza kuona, ISHARA zote hizi zenye thamani kubwa zimeanzia pale Bwana aliposema KWA JINA LANGU (YESU)
✓Hawa Mitume wa Yesu walilielewa na kulifaulu vyema somo hili la NGUVU ILIYOPO KATIKA JINA LA YESU. Na JINA HILI liliwanufaisha sana katika huduma zao. Katika Matendo 9, "Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote , akawatelemkia na watakatifu walioko Lida. Akamuona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, MTU HUYU AMELALA KITANDANI MIAKA MINANE, MAANA ALIKUWA AMEPOOZA. Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka ujitandikie. Mara akaondoka. Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamuona (Ainea akiwa mzima kabisa), wakamgeukia Bwana." { Matendo 9:32-35 }
✓Paulo nae aliifahamu siri hii ya Nguvu ya Uponyaji Iliyopo katika JINA LA YESU k**a ilivyoagizwa katika Agizo Kuu, ya kwamba, KWA JINA LA YESU,atatoa pepo. Naye alitoa pepo wengi kwa JINA LA YESU. "Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo la uaguzi, akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu Aliye Juu, wenye kuwahubiri njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, NAKUAMURU KWA JINA LA YESU KRISTO, MTOKE MTU HUYU. Akamtoka saa ileile" { Matendo 16:16-18 }. Pepo yule alitii na kumtoka ndugu yule sawasawa na Neno La Mungu katika Marko 16;17.
✓"Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, HATA PEPO WANATUTII KWA JINA LAKO." { Luka 10:17 }
KWA JINA LA YESU hakuna nguvu wala wakala wa shetani anayeweza kukaa. Atakimbia tuu.
✓"Yohana akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TULIMUONA MTU ANATOA PEPO KWA JINA LAKO.." { Luka 9: 49 }

ANGALIZO: Usithubutu kulitumia JINA LA YESU ikiwa wewe mwenyewe siyo wa YESU ama waendelea kuishi katika dhambi. { Matendo 19:13-16 }
Namuomba Bwana YESU akupe kufahamu Nguvu iliyopo katika JINA LAKE ili uitumie kwenye huduma yako, likae moyoni mwako na milele kwenye paji la uso wako.
"Kisha nikaona, na tazama HUYO MWANA-KONDOO, Amesimama juu ya mlima Sayuni na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja nae WENYE JINA LAKE NA JINA LA BABA YAKE LIMEANDIKWA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO ZAO" { Ufunuo 14:1 }

"Nao watamuona uso wake, NA JINA LAKE LITAKUWA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO ZAO." { Ufunuo 22:4 }

01/06/2022

Online Seminar
With: Minister PANDISHA

"For All The Promises Of God In Jesus Christ Are YES And AMEN" { 2 CORINTHIANS 1:20 }

Somo: UPONYAJI WA KIMUNGU.

Kiukweli kuhusu Uponyaji wa Magonjwa Yetu wanadamu, Mungu ALISHATUPONYA. Shida ipo kwetu hatulikubali hilo. Hatuyaamini MAANDIKO.

Nukuu

"Mwenyewe aliutwaa UDHAIFU WETU Na kuyachukua MAGONJWA YETU" { Mathayo 8 : 17 }

"Hakika, ameyachukua masikitiko { MAGONJWA } yetu, amejitwika huzuni { MAUMIVU } yetu" { Isaya 53 : 4 }

"Yeye Mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, ili tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki, na kwa kupigwa kwake MLIPONYWA" { 1 Petro 2:24 }

Siri ya ushindi wa kila eneo, kila tatizo, huzuni, baraka, mafanikio, kimwili na kiroho ipo katika IMANI YAKO KATIKA NENO LA MUNGU. Neno La Mungu, ni Mungu Mwenyewe Anasema. K**a kuna NENO/ANDIKO lolote ulilisoma au kulisikia, ukaliamini na likakupa matokeo ya kuliamini kwako, BASI UNATAKIWA UYAAMINI NA MAANDIKO MENGINE YOTE yaliyopo kwenye Biblia ili nayo yakupe matokeo. " Maana AHADI ZOTE ZA MUNGU ZILIZOPO NDANI YA YESU KRISTO ni NDIYO Tena AMEN" { 2 Korintho 1:20 }. Usitilie shaka Imani yako katika NENO LA MUNGU. Amini Kuamini Kwako, Na Tilia Shaka Mashaka Yako. Najua Akili yako inaweza kuk**atwa na adui ikakuzuia kuliamini Neno La Mungu. ".......mungu wa dunia hii amepofusha akili (fikra) zao wasioamini, isiwazukie (isiwafikie) Nuru ya Injili ya Utukufu wake Kristo Yesu aliye Sura Ya Mungu." { 2 Korintho 4:4 }.
"Ndipo ( Yesu Kristo ) akawafunulia akili zao, wapate kuelewa na Maandiko." { Luka 24:45 }
Neno la Mungu ni Amin na Kweli. Linavyosema ndivyo linavyotenda.
"Huku akijua hakika ya kwamba Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi" { Warumi 4:21 }
Hivi UNAVYOAMBIWA KUHUSU IMANI UNAJUA TUNAAMINI NINI.? UNAJUA KUMUAMINI MUNGU TUNAMAANISHA KITU GANI.? Tunamuamini Mungu kwa kupitia Neno Lake. ANASEMA, ANATENDA, TUNATAZAMA KISHA TUNAMUAMINI. Tunamuamini MUNGU kupitia ahadi zake alizotuahidi katika Neno Lake. Kumbe k**a hivi ndivyo ilivyo UNATAKIWA KUMUAMINI MUNGU NA NENO LAKE.
✓Kwamfano hapa amesema "AMEUCHUKUA UDHAIFU WETU NA KUYACHUKUA MAGONJWA YETU" [ Mathayo 8:17 ], na k**a unakubali kwamba Neno Lake ni NDIYO na AMIN, sasa kwanini uendelee kuukumbatia huo ugonjwa hapo kitandani..?
✓"Kwa KUPIGWA KWAKE MLIPONYWA" [ 1 Petro 2:24 ], k**a unamuamini Mungu, sasa kwanini usiliamini Neno Lake na kuchukua hatua za KUUKIRI UZIMA NA KUUKATAA UGONJWA..?
✓".......Na kwasababu Mimi (Yesu) ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai" [ Yohana 14:14 ]
Mungu huchukia magonjwa, huchukia kutokuongezeka, huchukia huzuni, huchukia mahangaiko kwa watoto wake. Mungu hapendi tuwe wagonjwa wala magonjwa hayaletwi na Mungu. Magonjwa yanatokana na shetani. "Kwakuwa Bwana hatamtupa mtu hata milele. Kwamaana Moyo Wake haupendi kuwatesa wanadamu wala kuwahuzunisha" [ Maombolezo 3:31,33 ]
"Maneno hayo niliyowaambia ni ROHO tena ni UZIMA" [ Yohana 6:63 ]. Mungu ni Mungu wa Afya Njema Na Uzima. K**a Mungu angekuwa anayafurahia magonjwa kwa wanadamu asingelituma Neno Lake KUTUPONYA. [ Zaburi 107:20 ]
Madaktari duniani kote wanaamini kwamba kazi wanayoifanya ya kuokoa maisha ya watu na kuponya afya zao ni Kipaji na Utaalamu waliyopewa na Mungu kuwasaidia binadamu wenzao hapa duniani. Nao wanaamini kwamba WANAFANYA KITU CHA KIMUNGU. Kumbe UZIMA, AFYA NJEMA, UHAKIKA, FURAHA, AMANI NA MAFANIKIO NI MAPENZI YA MUNGU KWA WANADAMU. Na magonjwa, maradhi na udhaifu ni kazi za shetani kwa kuwataabisha wanadamu.
Hiyo ndiyo sababu iliyompelekea Mungu Kumtuma mwana wake hapa duniani ili kuziharibu kazi za shetani. Na moja wapo ya kazi za shetani ni magonjwa. Naye YESU katika huduma yake alikuwa akiponya magonjwa na madhaifu ya kila namna kwa watu. "Jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa ROHO MTAKATIFU na kwa nguvu; naye (YESU) akazunguka huko na huko akitenda KAZI NJEMA NA KUPONYA WOTE WALIOONEWA NA IBILISI" [ Matendo 10:38 ]
✓Dr. A.B Simpson, muanzilishi wa Umoja wa Kimisionari wa Kikristo, alisema "Kuna Wakristo wengi wazuri na watakatifu ambao kwa uhalisia wanambeba shetani na kuzunguka nae ndani ya miili yao katika sura ya magonjwa na maradhi na wanamkumbatia badala ya kumkemea"
Neno la Mungu linasema "MPINGENI SHETANI NAYE ATAWAKIMBIA" [ Yakobo 4:17 ]. Ikiwa shetani hajakimbia, basi uwe na uhakika kwamba hujampinga. Ikiwa kazi zake za magonjwa na maradhi zimo ndani yako, hazijakuacha; basi ujue hujampinga na umemkaribisha. Hii pia inawezekana imesababishwa na kutokuyajua Maandiko au kiburi chako cha kutokukubali na KULIAMINI NENO LA MUNGU.
"Kwakuwa Mimi ni BWANA NIKUPONYAE" [ Kutoka 15:26 ]
✓Kwakuwa tunaamini kwamba MUNGU anachukia sisi kuwa wagonjwa, kinachotakiwa kwako ni KUKIRI UZIMA NA KULIAMINI NENO LA MUNGU kwamba UMEPONYWA NA KUUKATAA UGONJWA.
✓Hapa nitakupitisha katika Maandiko machache uone jinsi ulivyo mkubwa mpango wa MUNGU wewe kuwa na Afya Njema.
"Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami (Bwana) NITAKUONDOLEA UGONJWA KATI YAKO. HAPATAKUWA NA MWENYE KUHARIBU MIMBA, WALA ALIYE TASA, katika nchi yako, na hesabu ya siku zako nitazitimiza" [Kutoka 23:25-26 ]
"Mabaya hayatokupata wewe, wala tauni (Magonjwa) hayatoikaribia hema (nyumba) yako" [Zaburi 91:10]
"Ee nafsi yangu mhimidi Bwana, wala usizisahau fadhi zake zote; Akusamehe maovu yako yote; AKUPONYE MAGONJWA YAKO YOTE" [Zaburi 103:2-3 ]
"Na uweza wa BWANA ulikuwepo (ndani ya Yesu) ili apate KUPONYA" [ Luka 5;17 ]
"(Yesu) akawatuma (wale Thenashara) wautangaze Ufalme wa Mungu na KUPONYA WAGONJWA" [ Luka 9:2 ]
"Naye (Yesu) alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao na kuihubiri habari njema ya Ufalme NA KUPONYA MAGONJWA NA MADHAIFU YA KILA AINA" [ Mathayo 9:35 ]
"Wakamuendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; AKAWAPONYA. Hata ule mkutano wakastaajabu walipowaona mabubu wanasema, , vilema wanakuwa wazima, viwete wanatembea na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli" [Mathayo 15:30-31 ]
"Akawaambia, Enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.....Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa Jina Langu watatoa pepo...... Wataweka mikono yao juu ya WAGONJWA, nao watapata AFYA" [ Marko 16:15,17-18 ]
"Na tena akaja mtu mwenye UKOMA akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. Yesu akanyoosha mkono akamgusa, akisema NATAKA; TAKASIKA. Na mara UKOMA wake ukatakasika" [ Mathayo 8:2-3 ]
Umeona hapo..? Kumbe YESU ANATAKA WATU KUTAKASWA UKOMA WALIONAO, KUPONYWA MAGONJWA WALIYONAYO. Na anachokitaka YESU ndicho anachokitaka BABA. Yesu Mwenyewe alisema, "Kwakuwa Mimi sikushuka toka Mbinguni ili nije niyafanye mapenzi yangu, BALI MAPENZI YAKE ( BABA ) ALIYENIPELEKA." [Yohana 6:38 ] Kila kitu alichokifanya YESU akiwa hapa duniani, yalikuwa ni mapenzi ya BABA. Kumbe ni mapenzi ya BABA MUNGU sisi sote kuwa wazima na kuponywa magonjwa na madhaifu yote.
"Mimi (YESU) siwezi kufanya neno mwenyewe..... kwasababu siyatafuti mapenzi yangu mimi mwenyewe, bali mapenzi yake BABA aliyenipeleka" [Yohana 5:30 ]
"Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; MIMI (YESU) NALIKUJA ILI (WANADAMU) WAWE NA UZIMA, KISHA WAWE NAO TELE" [ Yohana 10:10 ]

Chukua hatua za IMANI na uamini kwamba U MZIMA maana ulishaondolewa huo ugonjwa wako tangu zamani. Stay BLESSED.

Online SeminarWith: Minister PANDISHA"For All The Promises Of God In Jesus Christ, Are YES And AMEN." { 2 CORINTHIANS 1:...
28/05/2022

Online Seminar
With: Minister PANDISHA

"For All The Promises Of God In Jesus Christ, Are YES And AMEN." { 2 CORINTHIANS 1:20 }

Somo: Ukiri Ni Msingi Wa Maisha Ya Imani.

Nukuu:
"Lakini pasipo IMANI haiwezekani kumpendeza [MUNGU]" { Ebrania 11:6 }

"Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa IMANI." { Warumi 1:17,. Ebrania 10:38 Habakuki 2:4, Galatia 3:11 }

"Mwanadamu haishi kwa mkate tuu, bali huishi kwa kila Neno Litokalo Kinywani Mwa Mungu" { Kumbukumbu La Torati 8:3, Mathayo 4:4, Luka 4:4 }

Somo la MAISHA YA IMANI limeweza kufundishwa vizuri sana na Watumishi mbalimbali wa Yesu Kristo; Walimu, Wachungaji n.k. Hatahivyo bado kuna kitu kikubwa ambacho Wakristo/Waamini wengi wanakikosa kuhusu IMANI na hivyo kushindwa KUMPENDEZA MUNGU.
✓Kinachokosekana hapa ni KWA JINSI GANI TUNAKUWA WATU WA IMANI. KWA NAMNA GANI TUNAMUAMINI MUNGU.
"IMANI chanzo chake ni kusikia NENO LA KRISTO" { Warumi 10:17 } Kumbe TUNAMUAMINI MUNGU KWA KULISIKIA, KULISOMA, KULITAFAKARI NA KULIAMINI NENO LA MUNGU.
✓ Vile unavyoliona Neno La Mungu linasema ndivyo hivyohivyo Mungu alivyomaanisha. Mungu hana sababu ya kukuambia uongo wala kukufariji kwa maneno matupu. Hawezi kupingana na Neno Lake wala kusema kisha asifanye. Si mwanadamu hata akuambie uongo. [Hesabu 23:19. Isaya 55:11] Ikiwa mwanadamu ambaye aweza kukuambia uongo huwa unamuamini kwa maneno yake matupu, KWANINI MUNGU AMBAYE HAWEZI KUSEMA UONGO USIMUAMINI KWA NENO LAKE LILILO HAI.? "Maana AHADI ZOTE ZA MUNGU ZILIZOPO NDANI YA YESU KRISTO NI NDIYO TENA NI AMINA." { 2 Korintho 1:20 }
Tunamuamini Mungu. Tunaamini kile anachoahidi katika Neno Lake. Amini tu. Jizoeze kuamini kila anachokisema Mungu katika Neno Lake.
✓Sasa ngoja turudi katika somo letu.
UKIRI
Kulikiri NENO LA MUNGU.
Kukuri au Ukiri ninaouzungumzia hapa siyo KUTUBU. Siyo kukiri dhambi. Siyo kuungama dhambi. { 1 Yohana 1:9 } Hata hivyo usisahau kwamba hilo la kutubu/kuungama dhambi, lafaa sana katika maisha ya Ukristo.
Lakini kuna Kukiri kwa namna/jinsi nyingine ambako ndiko hasa natamani unielewe. Tena uwe makini na mwenye shauku kufuatilia hili kwasababu ndiyo Maarifa na Akili yaliyoongelewa katika Hosea 4:6 na Luka 24:45.
Kanuni ya Kiroho ambayo ni wachache sana wanaijua na kuiishi ni hii: KUKIRI KWETU NDIYO HUAMUA USHINDI WETU WA MAISHA YA KIROHO (IMANI) au kushindwa na kuishi pasipo kuitegemea imani.
Kukiri ni nini.? Kukiri ni KUKUBALI. Kukubali ni KUAMINI MOYONI NA KUWA NA UHAKIKA kwamba hivyo ilivyo ndiyo ilivyo. Na usisahau tumesema kwamba Tunachokiamini Wakristo ni KILA ANACHOKISEMA MUNGU KATIKA NENO LAKE.
Kumbe Kukiri ni Kukubali kwamba hivyo Neno La Mungu linavyosema ndiyo lilivyo. Ukifika katika nukta hiyo ya KULIAMINI NENO LA MUNGU BILA YA SHAKA MOYONI ndipo Hosea 4:6 itageuka na kuwa MTU WANGU ANAFANIKIWA KWAKUWA AMEYAPATA MAARIFA (Kanuni) na Luka 24:45 itakuwa ZIMEFUNULIWA AKILI ZAKE AMEPATA KUYAJUA MAANDIKO.
✓Sasa tuangalie Neno hili "Kwamaana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki; na kwa kinywa HUKIRI Hata kupata wokovu {Warumi 10:10 }
✓Kukiri kwako (maneno yako) ndiyo yenye hatma ya Uponyaji na Mafanikio yako. Kinywa chako ndiyo maisha yako. { Mithali 6:2,. Mithali 18:20,. }
Kwa kadri utavyozidi kudumu katika kuliamini Neno La Mungu ndipo ufahamu na akili yako itakavyoimarika na kupata MPENYO katika mambo ya kiroho na kimwili.
Hili jambo(Hii Kanuni) siyo nyepesi kuiishi na kuizowea kwa haraka maana najua hukuwahi kufundishwa kuhusu KULITEGEMEA NENO LA MUNGU.
"Neno Lako ni taa ya miguu yangu; Na mwanga wa njia zangu" { Zaburi 119:105 }
Maisha ya IMANI (Ya kuongozwa na Neno La Mungu) ndiyo maisha ambayo Yesu anataka akirudi akukute unayo. "........walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je, ataiona IMANI duniani.?" { Luka 18:8 } Huko KUMUAMINI MUNGU NA NENO LAKE, je, atakapokuja Mwana wa Adam, atakiona hicho moyoni mwako.?
✓Liamini Neno Lake. Wala usiwe na shaka. Alivyosema ndivyo alivyomaanisha. AMINI KUAMINI KWAKO NA TILIA SHAKA MASHAKA YAKO. "Huku akijua HAKIKA kwamba MUNGU aweza kufanya yale aliyoahidi" {Warumi 4:21 }
"Mungu si mtu aseme uongo.....Iwapo amesema, HATALITENDA.? Iwapo amenena HATALITIMIZA.?" { Hesabu 23;19 }
"Maana Neno La Mungu li hai, tena lina Nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili...." { Ebrania 4:12 }
Katika Mathayo 8:10 Yesu anasema hajaioma imani kubwa namna ile katika Israeli yote. Imani ile ameiona kwa nani..? Aliiona kwa yule Akida aliyemwambia Yesu kwamba sema NENO kisha mtumishi wangu atapona. Kwa maana nyingine ni kwamba Yesu alikuwa analitazama NA KULIKIRI NENO na watu waliielewa nguvu ya NENO katika uponyanyi na mambo mengine yahusuyo masuala ya kiimani na kiroho. Au kwa maneno mengine yule Akida alikuwa anamwambia Yesu LITUMIE NENO LA MUNGU K**A UNAVYOLITUMIAGA KUWAPONYA WENGINE. { Mathayo 8:5-13 }
✓Ngoja tu nikufikirishe katika jambo hili kidogo...'Hivi kulikuwa na haja gani au ulazima upi wa Mungu kutuambia MPINGENI shetani naye atawakimbia..? { Yakobo 4:7 } au 'Tazama nimewapa Amri/Nguvu/Mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui....' { Luka 10:19 } ilhali Yeye Mwenyewe Mungu awe anajua kwamba hilo alilolisema kwetu haliwezekani..? NAKUAMBIA KWELI, K**A MUNGU AMESEMA MPINGE SHETANI ATAKUKIMBIA HIVYO NDIVYO ILIVYO na ukiona hajakukimbia basi ujue bado hujampinga sawasawa. Na tatizo litakuwa kwako siyo kwenye Neno La Mungu.
Amini tu. Hii ndiyo siri ya maisha ya imani. Ukipinga hiunipingi mimi unapingana na Neno Lake. "......Nalo Neno mnalolisikia siyo langu, ila ni lake Baba (Mwenyewe) aliyenipeleka." { Yohana 14:24 }
✓Kumbuka, hujazoezwa kuishi kwa kulitegemea Neno La Mungu. Hivyo ukianza kulifanyia kazi hili utaonekana k**a mtoto mdogo au aliyerukwa na akili na ujiandae na vikwazo hivi.
A). Shetani.
Atakuzuia na kusema katika akili yako kwamba Hapana; hilo Neno halina maana hiyo. Siyo hivyo. Na kuamini hivyo ni kujipotezea muda tu. Mwishowe utachekwa tu. Hapana, hilo Neno si kwa ajili yako ni kwa ajili ya watu fulani wenye kibali maalumu kwa Mungu. Wewe huyajui vizuri mambo haya n.k.'
Mfano "Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, na kuyachukua magonjwa yetu" { Mathayo 8:17 } Andiko/Neno hili linamaanisha kwamba hutakiwi kuendelea kulala hapo kitandani na kuendelea kuukiri ugonjwa. Unatakiwa kusimama na kukiri kuwa wewe ni mzima Kwakuwa kwa kupigwa kwake pale msalabani Yesu Kristo aliyachukua magonjwa na madhaifu yangu nami nilipokea UPONYAJI zamani sana zaidi ya miaka 2000 iliyopita. { 1 Petro 2:24 } lakini shetani atakuletea uongo wake na kusema utajiumiza bure, usiinuke hapo kitandani, madaktari walisema wewe bado, utulie, Hilo Neno halipo hivyo.' USILIKUBALI HILO SHAURI LA shetani. Wewe amini Mungu amekuponya chukua hatua za imani, inuka uendelee na mambo mengine ya ujenzi wa Taifa na ujenzi wa Ufalme wa Mungu hapa duniani. [ Marko 2:1-5,11-12; Matendo 9:32-35 ]
Yesu anapokuambia 'Jitwike godoro lako uende', usitilie shaka Neno Lake. Jitwike uende. Na utakapoanza kuondoka ndipo IMANI yako itakapochukua nafasi ndani yako na utakuwa mzima [ Yakobo 2:17 ]
✓Hata mashetani Wanaliamini Neno La Mungu na kutetemeka. Kwa hiyo kuamini peke yake hakutoshi. Chukua hatua ya kutenda sawa na unavyoamini ili kuithibitisha imani yako. [ Yakobo 2:19,20,24 ]

B). Akili na Mawazo yako.
Kabla Ukristo haujatufikia, Afrika tulizoezwa kuwategemea waonaji ( watu wanaosimama katikati ya miungu na wanadamu ) ili kusikiliza mahitaji ya watu na kuwaombea na kuwasikiliza mizimu na miungu. Hilo bado lipo hata sasa. La kuwategemea watumishi pekee. Waafrika wamezoezwa kwenda kwa watumishi na kudhani kwamba hao ndiyo pekee wenye kibali cha kusikilizwa na Mungu ili kusikiliza na kutatua haja zao za kimwili na kiroho. HAWAJAZOEZWA WAO BINAFSI KUMTEGEMEA MUNGU NA KULITEGEMEA NENO LAKE MUNGU. Waafrika wanawategemea watumishi na vitu vyao ( mafuta, maji, vitambaa, unga, p**i, chumvi, keki n.k ). Kwahiyo ukianza kuwekeza kwenye kulitegemea Neno La Mungu na AHADI ZAKE; na kwakuwa majibu yanaweza yasije kwa wakati unaoutaka wewe, akili na mawazo yako vitakwambia 'wewe huna imani, utachelewa sana, nenda kwa mtumishi fulani, wenzio wamefunguliwa jana, shauri yako n.k.' Ukifanya hivyo hutoizowesha akili na moyo wako KULITEGEMEA NENO LA MUNGU bali mtumishi na vitu vyake.
Sasa naomba nieleweke hapa; Sipingi watu kwenda kuombewa au kuwashirikisha Mama na Baba zao wa kiroho mambo yao ya kiroho ila ninachojaribu kukuonesha hapa ni kwamba TUNAMTEGEMEA MUNGU NA NENO LAKE KWANZA kisha tunawaendea hao waliopo KWA KUSUDI LA KUTUKAMILISHA SISI WATAKATIFU [ Efeso 4:12 ]
✓Ifahamike hapa kwamba kila Muamini anayo Mamlaka na Nguvu (KWA KUMUAMINI MUNGU NA KULIKIRI NENO LA MUNGU) dhidi ya nguvu zote za yule adui; dhidi ya magonjwa, dhidi ya umasikini, dhidi ya kifo n.k.
Ukiweka IMANI YAKO juu ya mtumishi fulani, hauwezi kumpendeza MUNGU maana MUNGU anapendezwa na IMANI YA KUMUAMINI YEYE NA AHADI ZAKE ZOTE ZILIZOPO KATIKA NENO LAKE.
•Ukiwa safari ama sehemu ambayo huwezi kuwa na mawasiliano na huyo mtumishi wako utafanyaje.? Ulishawahi kuwaza k**a siku za kuishi mtumishi wako hapa duniani zikiisha naye akienda kuishi na Yesu utaishije.?
✓Ndugu, unao uwezo wa kufanya mengi na makubwa kuliko mtumishi wako k**a ukijifunza na kujizoeza kuishi kwa KUMTEGEMEA MUNGU NA KULIKIRI NENO LAKE KINYWANI MWAKO MUDA WOTE. { Marko 16:17-18 }
Sasa anza kutafuta Maandiko na uyakiri kila wakati kinywani mwako. Uyaamini na kijiona hivyo k**a Neno linavyosema.
Kwa kukuwekea msingi, ngoja nikupe mtaji huu mdogo uuhifadhi moyoni mwako na uamini kwamba hivi NENO linavyosema ndivyo lilivyo kwangu.

1). "Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya." { Kutoka 14:14 }

2). "Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani." { 1 Petro 1:5 }

3). "Amin, Amin, Nawaambia, Yeye aniaminie Mimi, kazi hizi nizifanyazo mimi, yeye nae atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atazifanya..." { Yohana 14:12 }

4). "Mabaya hayatokupata wewe; Wala tauni haitoikaribia nyumba yako. Kwakuwa atakuagizia malaika zake; Wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu katika jiwe. Utawakanyaga simba na nyoka; Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwakuwa umekaza kunipenda; Nitamuokoa na kumuweka palipo juu. Kwakuwa amelijua Jina Langu. Ataniita nami nitamuitikia; nitakuwa pamoja nae taabuni. Nitamuokoa na kumtukuza. Kwa siku nyingi nitamshibisha; Nami nitamuonesha wokovu wangu" { Zaburi 91:10-16 }

5). "Nayaweza mambo yote katika Yeye Anitiae Nguvu." { Filipi 4:13 }

6). "Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya, sasa litachipuka, je, hamtalijua sasa.? NITAFANYA NJIA HATA JANGWANI, na mito ya maji nyikani." { Isaya 43:18-19 }

7). "Basi atukuzwe yeye awezae kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayokazi ndani yetu." { Efeso 3:20 }

8). "Kwa maana Yeye ( MUNGU ) hujishughulisha sana na mambo yenu." { 1 Petro 5:7 }

9). "Ninyi mwatokana na Mungu; nanyi mmewashinda, kwasababu Yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko aliye katika dunia." { 1 Yohana 4:4 }

10). "Kwasababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako." { Isaya 43:4 }

11). "Usiogope; kwamaana walio upande wetu ni wengi kuliko wale walio upande wao." { 2 Wafalme 6:16 }

12). "Mkiniomba jambo lolote kwa Jina Langu, hilo NITALIFANYA" { Yohana 14:14 }

Neema Ya Mungu Baba, Na Upendo wa Bwana wetu YESU KRISTO na Ushirika wa ROHO MTAKATIFU vikae na roho yako Kwa Jina La Yesu Kristo, Amina.

Address

Kinondoni
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Promises Of GOD Ministry-PGM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share