26/11/2018
Shalom. Namtukuza Mungu sana kwa ajili yenu rafiki zangu. Leo tuangalie kidogo kuhusu NGUVU YA KIAPO. watu wengi mnaelewa kuhusu neno kiapo, ni neno la kawaida katika ulimwengu wa ceiling. Watu wanaapa wakiwa mahak**ani, kwenye chaguzi mbalimbali nk. Lakini kwenye ulimwengu wa roho kiapo ni hatari kinaambatana na kutoa uhai. Waebrania 6:16-17 imeandikwa mwanadamu huapa kwa aliye mkuu kuliko wao,na ukomo wa mashindano yote ni kiapo. Kumbe mtu anaapa kwa aliye mkuu ni ama Mungu aliye hai, mzimu, Bibi, babu nk. Huwezi kuapa kwa mdogo. Yoshua 6:26 baada ya kutumia nguvu nyingi kuiangusha Yeriko Yoshua aliwaapisha wana wa Israel kuwa mtu yeyote atakayeinuka kuujenga Yeriko akianza Kuchimba msingi tu atafiwa na mtoto wake wa kwanza, akianza kuinua kuta atafiwa na mwanae mdogo wa kiume. Baada ya miaka mingi sana kupita na Yoshua hayupo tena akainuka mfalme Hiel akataka kuujenga Yeriko kuanza tu Mtoto wake wa kwanza akafa, bado akokomaa alivyoinua kuta mwanae mdogo wa kiume akafa sawa na neno (kiapo) alilonena Yoshua mtumishi wa Mungu. 1wafalme 16:34.Ndugu zangu kuna mtu anaweza kuapa na kutoa kafara kwa waganga wa kienyeji wachawi kuwa hautoolewa, hautozaa, hautofanikiwa, utafilisika, utakufa ,utafukuzwa Kazinja, lazima uachike lakini yuko Mungu aliye hai na mimi k**a kuani wa Mungu natamka yeyote aliye apa kichawi juu yako basi uovu ule umpate yeye ktk jina la Yesu.