Mchungaji Karubanda

Mchungaji Karubanda Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mchungaji Karubanda, Religious Center, Bunda.

06/05/2024

Yohana 15:13
Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

28/09/2022

Mithali 28 :14,16 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.


¹⁶ Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.

27/07/2022

Ecclesiastes 8:15 So I commend the enjoyment of life, because there is nothing better for a person under the sun than to eat and drink and be glad. Then joy will accompany them in their toil all the days of the life God has given them under the sun.

24/06/2022

Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache.
(Mithali 24:10)

Sunday School Kids Today
03/04/2022

Sunday School Kids Today

19/03/2022

TAG JOGOO
Baraka Center
Semina Ya Maombi
(Day 3)
Ijumaa 18-03-2022
Dar Es Salaam

Somo: Kufunga na Kuomba
Na: Mchungaji Kefa

Mathayo 17:21
Esther 4:16

- Kufunga na kuacha kula na wakati mwingine pia kunywa kwa sababu ya shughuli za kiroho.
- Unapofunga lazima uombe. Usikae njaa tu.
- Na maombi ni popote. Iwe ofisini, kwenye gari, barabarani e.t.c.

Faida za kufunga na kuomba
- Isaya 58

Maangalizo Katika Kufunga na Kuomba

1. Usifunge kwa kushindana na mtu.
- Mungu hayupo kwenye mashindano.
- Ona hitaji binafsi, ama la kanisa, ama la kijamii, kwa mapenzi ya Mungu.

2. Jiepushe na kila mawazo ama sauti mbovu zitakazokujia wakati wa maombi.
- Unapokuwa unafunga, ulimwengu wa roho huwa wazi. Na unaweza kusikia sauti zote. Ya Mungu na ya Shetani. Lazima ujifunze na uweze kupambanua kati ya sauti hizi mbili.
- Na ukiwa kwenye maombi na ukasikia sauti yenye utata ama ujumbe wenye utata, nenda kwa mchungaji mara moja.

3. Funga ndefu, lazima uanze na maandalizi.
Mf. Katika funga ya siku saba, acha kula nyama siku 4 kabla na kula sana mboga mboga za majani. Kula vyakula vyenye uhai. (Matunda matunda, karanga ama maziwa.)
- Katika maombi haya ya kufunga, lazima uijali afya yako pia.

4. Unapofungua, fungua polepole.
- Unapokuwa umefunga, utumbo wako huwa umenywea. Usifungue kwa vyakula vigumu k**a ugali etc. Especially unapokuwa umefunga fungo ndefu. Hata k**a unakuwa na hamu ya vyakula vigumu. Anza na vitu k**a uji, juice isiyo kali, supu isiyo na nyama n.k.

6. Utakapokuwa umejizoeza kufunga, Mungu ataanza kuachilia karama. Utaanza kuona vitu ambavyo watu hawavijui na vya ndani sana na vya sirini. Kuwa makini sana ukifikia hatua hii. Zidi kushuka! Usiwe na kiburi! Zidi kushuka na kunyenuekea. Usimdharau Mchungaji wako wala viongizi wako. Usijiinue na kujiona una upako kushinda wengine. Kuwa makini sana. Jishushe!
(Hiyo ndiyo siri pekee)
Usijiine bora kuliko wengine. Bali waone wengine bora kukuliko. Waone wengine wana upako kuliko wewe. Itakusaidia na itakulinda na utadumu sana katika huduma.

Faida za Kufunga

Isaya 58:8-14
- Hapa kuna faida k**a 19. Chambua Polepole.

(Usiache kusoma mistari hii. Itakuongezea mwanga na nuru na ufahamu na hamu ya kufunga na kuomba.)

***
Ujumbe huu umeletwa kwako na
Force Focus Ministries
00:00 HRS
All The Time Is The Time Of Worship.
Dar Es Salaam
Tanzania.
Stay Connected.
***

17/03/2022

TAG JOGOO
Baraka Center
Semina Ya Maombi
(Day 2)
Alhamisi 17-03-2022
Dar Es Salaam

Somo: Kufunga na Kuomba
Na: Mchungaji Kefa

Mathayo 17:21
Esther 4:16

- Kufunga, ni kuacha kula, na wakati mwingine kuacha kunywa kwa kusudi ama shughuli za kiroho.

- Watu wanaofunga na kuomba, siku zote huwa ni washindi, kwa sababu, vita yao hawapigani mwilini, bali rohoni.
- Nguvu ya Rohoni inapatikana kupitia maombi ya kufunga
- Shetani hakai ndani ya mtu bila faida. Na faida ya shetani ni uharibifu. Na utamng'oa tu kwa kupitia maombi.

Note This:
- Unapokuwa katika utumishi wa kimungu, yaani unashughulika na kundi ama watu wa Mungu, mf. Mchungaji, Mwinjilisti etc, Usisahau kuombea familia yako pia na kushughulika nao katika upande wa kiroho chao. Watumishi wengi huhudumia kundi na kusahau familia zao. Hilo linaweza kufungua mlango wa uharibifu katika familia yako, na hata katika utumishi wako

- Wakati wewe umekaa na kurekax, kuna watu wengine wanatumia nyota yako kwa ajili ya kujifaidisha wao na kukuzorotesha wewe. Huwezi kuyajua haya na kujifungua kutoka katika vifungo hivi k**a hufungi na kuomba.
- Jiwekee ratiba ya kufunga na kuomba. Usiyapuuzie maombi haya.
- Kuna vifungo vya kutokuzaa, kutokuolewa ama kuoa, magonjwa, umaskini n.k. na hapa hutoboi bila Maombi ya Kufunga.

- Katika kitabu cha Esther, tunaona maisha yao yaliokolewa kwa kupitia mfungo wa siku 3.

- Maombi ya mfungo yatabadilisha mfumo wako wa maisha. Na utainuka na watu watashangaa, kwani utainuka utukufu hadi utukufu.

= Aina za Mifungo
1. Funga kavu
- Funga hii ni ya siku 3.
- Huli wala hunywi. Inapozidi siku 3 ni funga ya kimungu. Mungu ndio anakupa maelekezo.
- Mwanadamu anakaa siku 5 mpaka 6 bila chakula, na hapo afikapo anapoteza maisha. Usifunge mfungo mrefu, zaidi ya siku 3 kavu, bila maelekezo ya Mungu. Tumia chakula laini ama kunya maji ama vinywaji laini.
- Musa alifunga siku 40 kwa muongozo wa Mwenyezi Mungu mwenyewe.
- Yesu nae alifunga 40.

2. Funga Nusu
i. Funga ya Daniel
- Danieli 10
- Danieli aliacha vitu vitamu na vitu kadhaa.

ii. Funga ya milo miwili.
- Unaruka baadhi ya milo. Unaruka milo miwili.
Eidha unaacha kunywa chai na cha mchana unakula usiku etc.

iii. Funga ya mlo mmoja
- Unaruka mlo mmoja kwa siku.

iv. Unaacha kula milo migumu.
- Unaweza ukawa unakunywa vitu vya majimaji tu. K**a juice, maziwa etc

v. Funga ya Yohana mbatizaji.
- Yohana alikula nzige na asali pekee.
- Hapa unaweza ukachagua vitu vya kuacha.

*Unaponuia katika maombi ya kufunga, hakikisha unafanya k**a ulivonuia. Usibadilishe mfungo juu kwa juu, ama kukomea njiani. Utapoteza baraka zako.

3. Funga ya maji tu
- Hii unaweza kufunga mpaka siku 7.
- K**a itakuwa ni zaidi, lazima umuone Mchungaji wako kwa ajili ya Muongozo.
- Na unatakiwa uwe na sababu maalum ya kufunga maombi marefu.
- Unaweza ukafunga maombi haya hata siku 40, lakini lazima Mchungaji awe na taarifa, na lazima iwepo sababu maalum ya kufanya maombi ya namna hii. Vinginevyo utajiua bure...

- UKWELI MAOMBI YA KUFUNGA YANA FAIDA, LAKINI USIFUNGE KWA KUHATARISHA MAISHA YAKO. TUMIA HEKIMA KATIKA KUFUNGA.

4. Funga ya Kulazimishwa
- mf. Ukiwa unaumwa. Unakosa hamu ya chakula, ama ukila unatapika ama vyovyote, lakini huwezi kula. Chakula hakipiti. Hata k**a ni chakula unachokipenda ama hata k**a ni chakula kizuri.
- Pia wakati wa msukosuko. Mf. K**a maeneo yenye vita. Utakuta watu wanaweza kuwa na pesa, lakini hawana chakula.

5. Funga ya wazi. Funga ya Hadhara.
- Huu ni mfungo ambao watu tunatangaziana kufunga.
- Kutoa funga hii, funga zingine zote zinatakiwa kuwa siri. Iwe yako binafsi ama kikundi.
- Maombi haya huwa ni ya mapatano. Mf. Maombi ya kanisa zima, maombi ya kitaifa e.t.c.

- Unapokuwa kwenye maombi haya ya mapatano, usisahau pia kujiombea mahitaji yako.
- Maombi haya huwa na nguvu sana.

REMEMBER:
-Popote walipofunga na kuomba, mabadiliko yalitokea. Mungu yupo, na Anatenda.

***
Ujumbe huu umeletwa kwako na
Force Focus Ministries
00:00 HRS
All The Time Is The Time Of Worship.
Dar Es Salaam
Tanzania.
Stay Connected.
***

16/03/2022

TAG JOGOO
Baraka Center
Jumatano 16-03-2022
Semina Ya Maombi
Somo: Maombi Ya Kufunga
Na: Mchungaji Kefa
Mathayo 17:21
Esther 4:16

- Ipo siri kubwa sana na matokeo makubwa sana katika maombi ya kufunga.
- Unapojua siri hii basi utapenya na hutoathirika kisaikolojia.
- Wengi leo hawafungi, wakijihurumia na wakoogopa njaa, lakini wanasahau kuwa, unapoacha kufunga na kuomba, unapoteza Baraka zako nyingi.
- Wengine husema, hata nikiomba, kwani Mungu hasikii? Lakini elewa kuwa, kuna tofauti kati ya maombi ya kufunga na kutokufunga. Na hata majibu huja tofauti.
- Kuna nguvu ya ajabu na matokeo ya ajabu katika maombi ya kufunga na kuomba.

= Maana ya Maombi ya Kufunga
- Kufunga ni kuacha kula na wakati mwingine kuacha kunywa kwa kusudi ama shughuli malum ya kiroho
- Usiahirishe tu kula, ama unafunga kwa sababu hauna pesa wala chakula. Lakini maombi haya, chakula kipo, lakini unaacha kula na kuutafuta uso wa Mungu.
- Maombi haya ya kufunga, lazima UNUIE.
- Ni kukana na kuyakataa mambo mengi ya kimwili ama ya kidunia, ili kuyafuata mambo ya kiroho.
- Wakati mwingine ukifunga, tulia mahala na kumtafuta Mungu. Usianze kutembea tembea huko na huko, ama ndo unapanga safari ya kumtembelea mtu. Utajiletea majaribu ya kukataa chakula pale utakapokaribishwa.

- Ukishaanza kufunga na ukajizoeza, mifungo mingine utaanza kuelekezwa na kuongozwa na Mungu mwenyewe.
- Kuna vita kadha wa kadha ambazo zinatuandama. Uchawi upo na mashambulizi yapo. Lakini katika maombi ya kufunga na kuomba tu, tunaweza kushinda.
- Usiyapuuze maombi ya kufunga, maana ipo siri kubwa katika maombi haya.
- Jiwekee ratiba za kufunga na kuomba
- Watu wanajihusisha na maombi ya kufunga huwa wajasiri. Hawaogopi hata mapepo. Na huwa wapo tayari muda wote kwa ajili ya vita.
- Roho Mtakatifu huwa anajua wakati wa mbele kuna nini, ama tunapitia mambo magumu kwenye maisha, na Roho Mtakatifu atakuongoza kufunga na kuomba, na inabidi utii anapokuongoza. Utapokaidi hutopata mpenyo.
- Hakuna jambo gumu limshindalo Mungu. Lakini Mungu hatendi tu pasina ya sisi kuchukua hatua.
- Ukianza kuona matokeo ya kufunga na kuomba, hutoacha kufanya hivyo. Na itakuwa ni tendo lako la mara kwa mara

=Mambo ya Kuzingatia wakati wa Maombi Ya Kufunga

1. Epuka shughuli nyingi na za kuchosha zisizomtukuza Mungu. Mf. mazoezi
- Pata muda wa kuomba. Usikae tu njaa bila kuomba. Kwa sababu lengo la kufunga ni kuomba
Isaya 30:15
- Tulia, pumzika na mtafute Mungu.
- Sio kwamba usiende kazini, lakini punguza shughuli na pata muda wa kuomba.

2. Funga kusema-sema ovyo. Acha mizaha-mizaha
Mathayo 12:37
Mithali 17:38
- Ukiweza kupata eneo la utulivu, ni vizuri zaidi.

3. Punguza kuhangaikia mwili wako sana kupita kiasi
Mf. Mama anakaa jikoni muda mrefu akihangaikia chakula na hapati muda wa kuomba.

4. Panga utaratibu
- Lazima uwe na ratiba. Saa ngapi utasoma neno, na wakati gani utautumia kuomba.
- Pia, unaweza ukawa umekaa mahala patulivu, lakini ukalala tu na usiombe wala usisome neno. Lakini panga utaratibu kwamba, muda huu nitasoma Neno na muda huu nitaomba. Na fanya bila kukiuka ratiba. Usilale tu.
- Pia unapokuwa katika maombi, kumbuka kujiombea na kuombea mambo yako ya Nyumbani.

***
Ujumbe huu umeletwa kwako na
Force Focus Ministries
00:00 HRS
All The Time Is The Time Of Worship.
Dar Es Salaam
Tanzania.
Stay Connected.
***

Sunday ServiceSunday School
27/02/2022

Sunday Service
Sunday School

27/02/2022

SOMO: UTOAJI WENYE BARAKA
Na: Mch. Winfrod
TAG Mbezi Beach.
Sunday Service

=> Kila mtu anatamani, pale anapotoa, aone matokeo yake katika wema.

=> UTOAJI wa Cain na Abel

- Utoaji wako unaweza ukafanya ubarikiwe ama la.

- Katika agano la kale, palikuwa na sadaka ya mnyama. Anachukuliwa na anatolewa kwa kuhani. Yule mtu anaweka mikono yake juu ya mnyama na anakiri dhambi zake. Kisha yule mnyama anachinjwa k**a sadaka. Lakini hii haikuondoa dhambi, bali dhambi ilifunikwa.

- Lakini, kwa Sadaka ya Damu ya Yesu pale Calvary, Dhambi ziliondolewa.

1. SADAKA YA KAWAIDA

- Haina kiwango.
2 Cor 9: 6-12

- WAKRISTO NI MATAJIRI

- Ni kwa kadri mtu unavyopenda. Haulazimishwi.

Remember:
- Give, and it shall come back to you, Good measures, shaken, pressed down, and Running over.
- Toa, na kwa kipimo kile mpiacho ndicho mtakachorudishiwa, kikiwa kimejazwa, kimesukwa sukwa, kikimwagikia.

2. Sadaka ya Shukurani.
- Hii hutolewa kwa kumrudishia Mungu utukufu pale mtu anapokuwa amevushwa na Mungu.
- Hii unamaanisha, MUNGU NDIYE MWENYE KUKUONGOZA.

- Tunawezeshwa, na Mwenyezi Mungu.

3. Sadaka ya MALIMBUKO
Mithali 3:9-10

- Hii ni kuwa, unamtambua Mungu kuwa yeye ndiye wa kwanza. Lazima Mungu kwanza, kabla ya sehemu nyingine yeyote.

Malaki 3:8-10

- Lengo kuu la kusudi, ni , Kuwepo chakula cha kutosha nyumbani mwa Bwana.

4. Fungu la Kumi.

- Fungu la kumi ni kipimo cha uaminifu kwa Bwana.

- Tithe (1/10)

5. Sadaka ya Nabii
Mwanzo 20:
Mwanzo 31:13

6. Nadhiri

Unamwambia Mungu, ' K**a Mungu ukinifanikisha hili, basi mimi nitakufanyia hili na hili' Lakini tukishavuka, tunasahau. Hii Mungu analifuatilia sama.

Mhuburi

7. Machangizo Mbali mbali

Kutoka 35:4-5,. 36:2-7

- Hii ni kwa ajili ya Kuifanikisha kazi ya Mungu ili isonge mbele.

- Siku zote kumbuka, Unapotoa, haumpi mtu , bali Mwenyezi Mungu.
- Na hii ni kwa wale wanaotambua, wapi wametoka.

- Kuwajali Yatima na Wajane.

- Na unapotoa, lazima ujihesabu kuwa hujatoa.

Mathayo 25:

Matendo 9:
- Sadaka ya Dorcas ilimrudushia uhai.

Prophetic word:
'Kwa sadaka yako, UHUISHWE TENA.,'

Elisha na mwanamke Mshunami

- Sadaka ya mwanamke Mshunami ilinena mpaka Elisha akauliza, Mwanamke huyu afanyiwe NINI?

PROPHETIC WORD:
SADAKA YAKO IKANENE SASA KATIKA MAISHA YAKO. KILE KITU ULICHOPUNGUKIWA, BASI MWENYEZI MUNGU AKUJAZE.

*** # # #***

23/01/2022

NIV, Proverbs 23:9
Do not speak to fools, for they will scorn your prudent words.

15/01/2022

THEME: Is God Asleep?
BY: Mch. Karubanda.
TEXT: Psalms 44:23

Awake, why sleepest thou, O Lord? arise, cast us not off for ever. (Psalms 44:23|KJV/Ps/44_23/KJV)

- You can ask yourself this question any time when you sit down and evaluate and see the reality of today's daily life. One, Most of us live a careless life. We do issues without consideration. And two, We may be passing through a situation or a circumstance, that you wonder if God is there or not, and if He is there, Doesn't He see!

- When we take the view of the evils been done by one person to another, when we see the devorce, mudders, brutality, hate, skimming, plotting evil, and whatsoever more you can think of.

- Or, you are in a situation like David in Psalms 44, When he sees around him and realizes, His life is not what he knows it should be. He looks evil doers prosper and his enemies gain through his wealth and strength, and he remains frustrated and forsaken, so he asks God, Are you asleep? Awake Then and see!

- Is it at your work place, or at home. Is it happening to your neighbor,or to your relative. Is it in your family, is it your spouse or siblings,... Whatsoever it Is,...

YET GOD DOES NOT SLUMBER!!!

He will not suffer thy foot to be moved: he that keepeth thee will not slumber. Behold, he that keepeth Israel shall neither slumber nor sleep. (Psalms 121:3-4|KJV/Ps/121_3-4/KJV)

- In Jeremiah God tells us to call Him.

Call unto me, and I will answer thee, and shew thee great and mighty things, which thou knowest not. (Jeremiah 33:3|KJV/Jer/33_3/KJV)

* David wondered, He has God, The King, The Maker, The Author and The Finisher of our faith, The Lord of Lords, The Provider, and whatsoever you can praise Him, and yet David was passing through a hard time.

David said NO! ENOUGH IS ENOUGH! And he called God!

- In any thing you undergo, CALL GOD. HE ISN'T ASLEEP.

Stay Blessed

***

Mchungaji Karubanda.
Force Focus Ministries
+ 255 758 342501
Dar-Es-Salaam - Tanzania.

Address

Bunda
255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mchungaji Karubanda posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Mchungaji Karubanda:

Share