Bunda mjini sda church

Bunda mjini sda church Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Bunda mjini sda church, Religious organisation, Bunda.

09/05/2025

KUTOKA KUKATALIWA MARA 30 HADI KUWA BILLIONAIRE: SAFARI YA AJABU YA JACK MA!

Alizaliwa mwaka 1964 katika familia maskini katika mji mdogo wa Hangzhou, China. Wakati watoto wengi walikuwa wakicheza hovyo mitaani, Jack Ma alikuwa akihangaika kujifunza Kiingereza kwa kuzungumza na watalii waliokuja kwenye mji wake.

Alitembea kilomita nyingi kila asubuhi kwa miaka 9 kwenda kwenye hoteli moja maarufu ili aweze kufanya mazoezi ya Kiingereza bure.

Hakuwa mwerevu darasani. Alifeli mtihani wa kuingia shule ya sekondari mara mbili. Alipojaribu kujiunga na Chuo Kikuu cha Kiserikali, alikataliwa mara tatu.

Hatimaye alifanikiwa kujiunga na chuo baada ya juhudi zisizoisha. Lakini hata baada ya kuhitimu, changamoto hazikuisha. Alituma maombi ya kazi 30 – zote alikataliwa. KFC walipoajiri wafanyakazi 24, yeye ndiye pekee aliyekataliwa. Polisi walikataa kumpa kazi. Hata alipojaribu kuomba kazi k**a waiter, bado alikataliwa.

Lakini ndani ya moyo wake, Jack alijua: "Siku moja nitafanya kitu kikubwa."

Aliendelea kuthubutu. Mwaka 1995, alipokuwa Marekani kwa mara ya kwanza, alikutana na kitu kipya – “Internet”. Aligundua kuwa China haikuwa na uwepo wowote wa mtandaoni. Hapo ndipo wazo la kuanzisha kampuni ya mtandaoni likazaliwa.

Aliporudi nyumbani, alianza kampuni ya kwanza – ilifeli. Akaanzisha ya pili – ikafeli tena. Familia na marafiki wake walimwambia: "Achana na hii ndoto yako ya kipuuzi."

Lakini hakuacha. Mwaka 1999, akiwa na marafiki 17 ndani ya sebule ya nyumbani kwake, alianza kampuni mpya: “Alibaba”. Wakati huo, hakuna aliyeamini kuwa biashara ya kuuza bidhaa mtandaoni kutoka China ingeweza kufanikiwa.

Alikuwa hana pesa. Hakukuwa na benki iliyotaka kumkopesha. Lakini alijua moja – “Vision bila pesa ni ya thamani kuliko pesa bila vision”.

Leo hii, Alibaba ni moja ya makampuni makubwa zaidi duniani. Jack Ma, mtu ambaye alikataliwa kila kona, amekuwa mmoja wa matajiri wakubwa duniani. Hakuiacha ndoto yake, hata dunia ilipomwambia haiwezekani.

Kwa mujibu wa Bloomberg, hadi Machi 7, 2025, Jack Ma alikuwa na utajiri wa dola bilioni 40.3, akishika nafasi ya 39 duniani kwa utajiri. Katika orodha ya matajiri wa China, Jack Ma alishika nafasi ya 7 kwa utajiri wa dola bilioni 28.57. [Bloomberg]

—-----------------------------------------------------------------------------

Kukataliwa si mwisho wa ndoto. Kushindwa si laana. Mapito ni sehemu ya safari ya mafanikio. Ukiwa na ndoto, uthubutu na moyo usiokata tamaa – dunia haina budi kukusikiliza.

Vipi upande wako?

K**a umeguswa na hadithi ya Jack Ma, tuambie kwenye comment: Ni jambo gani ambalo hujawahi kukata tamaa nalo licha ya kukataliwa mara nyingi? 👇

✍️ Liganga

©️ 2025 Tarris Media Tz

Haki Zote Zimehifadhiwa

!

11/04/2025

Karibu Kwa ibada ya kesho ndani ya jengo la kanisa jipya hapa ni baada ya upauaji HAKUNA KUPOA

10/04/2025
10/04/2025

Ni Kwa uweza wa Mungu tunasonga mbele

09/05/2024

Tunamshukuru Mungu kwamba anatuwezesha tunasonga mbele kufanikisha tunamjengea nyumba mzuri ya kupendeza sana kwa utukufu wa jina lake

10/11/2022
01/08/2022

Karibuni kwenye sikukuu ya Vibanda

26/11/2021

NAKUKUMBUSHA KUHUSU NGURUWE

1: Ni mnyama MCHAFU SANA na ndio maana Mungu alikata kula NYAMA YAKE wala kuigusa MIZOGA YAKE

2: Anakula kitu chochote hata k**a ni KICHAFU KIASI gani, yeye anakula tu. Hata MAVI ANAKULA. Yan nguruwe ni "CHOO KINACHOTEMBEA"

3: Madaktari bingwa duniani na wanasayansi wote wanakubali kuwa NYAMA YA NGURUWE NI CHAFU SANA. Wewe ni nani mpaka upinge ?

4: nguruwe hana NGOZI NGUMU k**a aliyonayo NG'OMBE na MBUZI, wanamkwangua tu manyoya kisha anakua tayari kuliwa. Kwahyo nguruwe anaingiliwa na WADUDU kwa urahisi sana.

5: Nyama na Nguruwe ina MINYOO ambayo inaonekana baada ya kuiweka nyama hyo juani kwa dk 30 au zaidi.

6: Nyama ya nguruwe ina MAFUTA MENGI SANA ambayo yanaharibu mwili wa binadamu.

7: Analala sehemu CHAFU SANA, kwahyo nyama yake haiwez kuwa SAFI KABISA.

Hebu ifike wakati TUACHE KULA NYAMA YA NGURUWE kwasababu ni DHAMBI na pia INA MADHARA MAKUBWA SANA KIAFYA

06/11/2021

Karibu katika sabato ya Kumtukuza Bwana kwa njia ya nyimbo hapa kanisani Bunda mjini SDA ambapo Kuna kwaya mbalimbali zilizoaliokwa

12/08/2021

Bilionea MNigeria Femi Otedola alipoulizwa kwenye interview, ya Simu na Mtangazaji wa Radio, "Sir ni kitu gani unachokumbuka kilichokufanya uwe na furaha maishani?"

Femi alijibu:
"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha yangu na mwishowe nilielewa maana ya furaha ya kweli."

Hatua ya Kwanza ilikuwa ni kutafuta Mali na kulimbikiza. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyoihitaji.

Nikaingia hatua ya pili ya kujinunulia vitu vya thamani. Lakini niligundua kuwa vitu vyote hivi vinakupa furaha ya muda tu ambayo haidumu.

Nikaingia hatua ya tatu ya kufanya miradi mikubwa. Ni katika hatua hii nilikuwa ninasambaza 95% ya Diesel Nigeria yote na Africa Kwa ujumla. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa Vessel Africa na Asia. Lakini pia hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeifikiria.

Hatua ya nne ilikuwa ni kipindi ambacho Rafiki aliniomba kununua Wheelchairs Kwa ajili ya watoto walemavu. Walikuwa k**a watoto 200 hivi.

Baada ya kuombwa na rafiki yangu nilinunua Wheelchairs 200 mara moja.

Lakini pia aliniomba niambatane naye ili nikawakabidhi watoto zile wheelchairs. Nilijiandaa nikaambatana naye.

Nikawagawia zile wheel chairs Kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona furaha ikitawala kwenye nyuso za hawa watoto. Nikawaona wamekaa kwenye wheelchairs, wakizunguka na kufurahia.

Ilikuwa ni k**a wako Picnic wakisherehekea ushindi wa bahati nasibu.

NiIihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipotaka kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu yangu. Nilijaribu kujinasua taratibu lakini alinikazia macho akinitazama usoni.

Niliinama chini nikamuuliza, kuna kitu kingine unahitaji?

Jibu alilolitoa mtoto huyu sio tu kwamba lilinipa furaha bali pia lilinifanya nibadili kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Mtoto huyu alisema:
*"Ninakuangalia ili niikumbuke Sura yako, siku nikikukuta mbinguni niweze kukutambua na kukushukuru tena."*

Je Wewe mwenzangu, utakumbukwa Kwa lipi utakapoondoka kwenye hiyo Kampuni, Ofisi, Biashara, Kazini au mahali unapoishi?
Je kuna Mtu atatamani kuuona uso wako tena siku za usoni?.

Address

Bunda

Opening Hours

08:00 - 18:00

Telephone

+255767400328

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bunda mjini sda church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Bunda mjini sda church:

Share