Biblia nuru ya maisha

Biblia nuru ya maisha Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Biblia nuru ya maisha, Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, Bensonbarnaba125@gmail. com/0752699647 WhatsApp, Bunda.

22/08/2023

DAWA YA MCHAWI YOYOTE ANAYEKUSHAMBULIA NI HII HAPA?
HESABU 23:23
Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
DAWA NAMBA NO: I-USIWAOGIOPE WACHAWI
ISAYA 41:10-13
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa k**a kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia. Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.
MAELEZO
WACHAWI BAADHI WANA TABIA YA KUTOA VITISHO, MFANO TUONE K**A UTATAFANIKIWA, HAUTAZAA, HAUTAPONA, HAUTAOLEWA NA MENGINE
ZABURI 35:1-9
Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie. Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia, Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya. Wawe k**a makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini. Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa Bwana akiwafuatia. Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu. Uharibifu na umpate kwa ghafula, Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe; Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
MAMBO YA KUZINGATIA IKIWA NI KWELI UMESHASHAMBULIWA
SOMA HAYO MAFUNGU YA BIBLIA OMBA KWA IMANI UTAPATA USHINDI KWA KWA JINA LA YESU, USHINDI NI WAHAKIKA:
KUANZIA LEO TUTAKUWA NA MAOMBI YA KUVUNJA NGUVU ZA GIZA NA MASHAMBULISHI YAKE NA MAAGANO ULIYOFANYIWA YA KICHAWI NA UGANGA IKIWA UNAMGONJWA AMESHAMBULIWA NA

22/08/2023

WA :

Jina la BWANA lipewe sifa!!!!

Kujazwa Roho Mtakatifu, ni kitendo cha kumpa nafasi Roho Mtakatifu, ili atawale Maisha yako wakati wote, ina maana chochote unachofanya utaongozwa na Roho Mtakatifu.Na Roho Mtakatifu anapofanya makazi ndani ya mtu anafanya makao ya kudumu, labda mtu mwenyewe aanze kukengeuka kwa kukaidi sauti ya Roho Mtakatifu. 1 5:19 Msimzimishe Roho;

Roho Mtakatifu sio upepo wa Baiskeli, kusema kwamba kuna muda unajaa, na kuna muda unatoweka na inabidi ujaze tena, Roho Mtakatifu tangu alipodhihirishwa siku ya Pentekoste, yeye yupo kwa kila mtu na wakati wote kwa anayemuamini Yesu na kubatizwa, ina maana ukiwa na Roho Mtakatifu mahali popote yupo pamoja nawe, iwe ni shambani, Kanisani, shuleni, Safarini nk.maana uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu ndio uwepo wa Mungu na Yesu Kristo ndani ya mtu, 8:9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

Sasa inashangaza kumsikia Mkristo anasema anaongozwa na Roho Mtakatifu, ila maneno yanayotolewa kinywani mwake hayasadifu uwepo wa Roho Mtakatifu, na hata Matendo anayoyatenda hayasadifu uwepo wa Roho Mtakatifu, lakini kila siku anapoenda kanisani, kuna kuwa na kipindi cha kujazwa na Roho Mtakatifu au kumuita Roho Mtakatifu. Sasa ikiwa mtu ukienda kanisani ndipo unajazwa na Roho Mtakatifu, kwa hiyo ina maana kwamba Roho Mtakatifu anapatikana Kanisani tu, na anakuja kwa msimu, kwa hali hii inaonesha kwamba kuna wakati baadhi ya watu wanajiongoza wenyewe bila Roho Mtakatifu, wakati Yesu aliahidi kwamba Roho Mtakatifu atakuwa ndani yetu milele: 14:16-17Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

Upo wakati inabidi tuwe makini sana na aina ya roho na k

18/06/2023

✍️Fundisho la utatu linakana kuwa Yesu si mwana wa Mungu halisi. Fundisho hilo linadai Yesu ni mwana wa Mungu kwa kujifanya.
✍️Fundisho hilo linakana Yesu hakuzaliwa na Mungu bali Biblia inatufunulia wazi kuwa yesu alizaliwa na Mungu. ( Mithali 8:22-24)
✍️Fundisho hilo linamkana Roho wa Mungu na badala yake wameleta mungu roho ambaye hapatikani ndani ya biblia.(1 cor 2:11)
✍️Fundisho hilo linamweka Baba, Mungu kukaa na umri moja na mwanaye lakini imani ya Biblia haizungumzi ivo.
✍️Fundisho hilo linatufanya kukosa kujua mpango wa wokovu wetu kutoka kwa Mungu wetu kwa sababu hatuwezi kujua aliyekuja kutukomboa. (John 3:16)
✍️Fundisho hilo linatunyanganya uzima wa milele. ( Uzima wa milele ni kumjua Mungu Baba na Yesu (John 17:3)
✍️Fundisho hilo ni la wakatholiki.
✍️Ni fundisho la uongo.
✍️Wanalolitetea kua la ukweli Biblia inawaita kuwa makafiri/waasi. Lakini kwa huu ulimwengu wa sasa wanalolikakataa ndo wanaitwa waasi /makafiri na madhehebu ya sasa.
✍️Wanalolitetea fundisho la utatu Biblia inawaita wapinga Kristo.
✍️Lilingizwa katika SDA mwaka wa 1981.

18/06/2023

YESU NI MWANA WA MUNGU? NI MWANA WA MUNGU TANGU LINI? NA KWA NAMNA GANI NI MWANA WA MUNGU ❓

Tunaenda kuangazia nadharia ya tano, ili twende sawia pitia sehemu zilizo tangulia karibu mtoto wa Mungu.

5️⃣Yesu hakuwa Mwana halisi wa Mungu mpaka alipofufuliwa katika wafu. Na kwamba aliitwa Mwana wa Mungu akiwa Mbinguni kwa unabii kuwa atafufuliwa katika wafu.

📚Msingi wa nadharia hii upo katika Matendo13:33-34. Ambayo husema kwamba:
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽

📚
[33]ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; k**a ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili,
Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.

[34]Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi,
Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.

📚Wakati ambapo nakiri kuwa Unabii huu wa zaburi ulitimia wakati ambapo Yesu alifufuliwa toka kwa wafu, ni ukweli pia kwamba Yesu kuwa Mwana wa Mungu hakukuanza wakati alipofufuliwa. Hiki huwa ni kichaka cha wanatheolojia wanaokitumia, kuzima habari nzima ya Uwana wa Yesu kabla ya vitu vyote.

📚Kitabu cha Waebrania kimeeleza vizuri sana hilo fungu, na kuweka bayana kuwa huo sii Unabii unaotimia tu wakati wa ufufuo wa Yesu, ama kuzaliwa kwake na maryamu, bali ulitimia pia alipozaliwa na Baba kabla ya kuwepo kwa vitu vyote.

🍓Hebu turejee kidogo ktk kitabu cha Waebrania.

📚Biblia yasema hivi:"👇🏽

📖Waebrania 1:5-6
[5]Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa?
Na tena
Mimi nitakuwa kwake baba,
Na yeye atakuwa kwangu mwana?

[6]Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,
Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.

👆👆👆Ukisoma mafungu hayo kwa umakini utagundua kuwa fungu la sita ni mwendelezo wa fungu la tano.

📚Katika Fungu la tano Mungu anamtambulisha Yesu miongoni mwa malaika kuwa Yeye ndiye Mwanaye mzaliwa wa pekee,(Mwanaye wa kuzaa) na fungu la sita tunaona Huyo Mzaliwa wa Mungu anatumwa duniani, na malaika wanaagizwa kumwabudu.

📚Kama Fungu la tano lina

Address

Bensonbarnaba125@gmail. Com/0752699647 WhatsApp
Bunda

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Biblia nuru ya maisha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share