15/12/2018
Bwana Yesu asifiwe.ufufuo na uzima kagera ni kanisa la kiroho lenye makao makuu manispaa ya bukoba mjini, kata ya Nshambya chini ya Kiongozi Askofu Leonardo Mtashubirwa,akiwa chini ya kiongozi mkuu wa Ufufuo na Uzima Tanzania na dunia nzima Bishop Dr.Josephat Gwajima.Ufufuo na uzima Kagera ina makanisa yanayotoa huduma za kiroho yanayopatikana mkoa mzima wa kagera,wilaya kwa wilaya, Tarafa kwa Tarafa,kata kwa kata na Kijiji kwa Kijiji.Ndugu zangu watu wa Mungu,Bwana Yesu anaokoa,anaponya,anafufua watu na maisha yao,analinda na kuokoa na nguvu za Giza (wachawi,majini,mizimu,majoka,na mapepo ya kila namna) kimbilia kwa Yesu waganga wa kienyeji hawana kitu Tena ,nenda kwa Yesu ndio msaada pekee.soma Yeremia 17:5na 7(amelaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa Kinga yake na moyoni mwake amemwacha Bwana.Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana,ambaye Bwana ni tumaini lake.
Ufufuo na uzima kagera inapenda kumshukuru Bwana Yesu kwa kufikisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake hapa Kagera.
Kwa hiyo Ufufuo na uzima kagera inapenda kuwakaribisha wanakagera wote bila kubagua dini ya mtu na watanzania wote kwa ujumla na nchi jirani katika sherehe (jubilehi) ya kutimiza miaka kumi itakayofanyika kanisani Ufufuo na uzima KAFUNJO KAMACHUMU.,ITAKAYOFANYIKA TAREHE 22-12-2018 JUMAMOSI.karibu upokee neno la uzima,uponyaji,maombezi na majibu ya muujiza wako.Bwana Yesu akubariki.amina