28/07/2022
TABIA NA JAMII
Umewahi kuskia mtu amekosea, halafu akaambiwa "hapa umekosea, tena umemkosea MUNGU", lakini majibu yake yakawa ni haya, "vyema, mahusiano yangu na MUNGU, ni suala binafsi! Sitaki ulizungumzie". Umewahi kuona mtu anafanya kitu katika namna isiyo sahihi lakini akakataa kurekebishwa?! Nina imani umewahi.
Nataka kusema nini?! Nataka kusema hivi, kwamba; Ni kweli yawezekana unaweza kufanya mambo peke yako! Ni kweli mahusiano yako na MUNGU, ni suala binafsi! Lakini, nataka nikwambie hivi, pamoja na hayo yote, "Jamii (yoyote ile), ina mchango mkubwa katika kufanya kwako mambo! Jamii, ina nafasi katika kuyajenga mahusiano yako na MUNGU! Jamii, ina nafasi katika kurejesha sura (tabia) ya MUNGU ndani yako". Yaani, kwa Lugha nyingine ni kwamba, "ukamilifu unafikiwa kwa kukusanyika, sio kwa kujitenga na watu''.
KWA NINI NI HIVYO?!
- Paulo anatuweka wazi kabisa katika somo la leo kwamba, MUNGU ameweka katika jamii zawadi mbalimbali, karama mbalimbali, na maarifa mbalimbali ya kutufanya tufikie ukamilifu. Yaani, ili tufikie ukamilifu katika mambo yote, ili tufikie ukamilifu wa kikristo, ili kazi ya huduma ikamilike, ili mwili wa Kristo ujengwe, ili sura nzuri ya MUNGU irejee ndani yetu, MUNGU ametoa vipawa mbalimbali katika jamii (Waefeso 4:11), vipawa ambavyo tukiviunganisha, tukasikilizana na kwenda kwa pamoja , tunafikia ukamilifu! Si wa kikristo pekee (Waefeso 4:12), bali ukamilifu katika mambo yote pia.
Je, haiwezekani kwa mtu kuufikia ukamilifu wa Kikristo peke yake pasipo jamii?!
- Kwa hakika inawezekana kuwa Mkristo peke yako kabisa! Inawezekana kuufikia ukamilifu peke yako kabisa. Wanaume na wanawake hawafungwi chini ya shinikizo linalowazunguka! Kwamba, "ni lazima kutegemeana" ili kushinda, hapana. Wanaume na wanawake wanaweza kusimama peke yao k**a wakristo! Wanaume na wanawake wanaweza kusimama peke yao na kuufikia ukamilifu pasipo msaada wa jamii!!! Tumelishuhudia hili mara nyingi, karne nyingi wakristo wengi wamekuwa wakisimama peke yao na kushinda pasipo jamii.
Anachojaribu kutwambia Paulo katika somo la leo ni kwamba, "Ukamilifu unaweza kufikiwa zaidi kwa haraka na kwa uzuri, pasipo mateso wala maumivu, k**a tutafanya kazi kwa pamoja katika ushirika na kila mmoja" (Waefeso 4:12). "Kazi ya injili inaweza kufika kwa watu wengi zaidi ikiwa tutakaa katika jamii (Waefeso 4:12), Lakini pia, falme na mamlaka za uovu zitaangushwa, ikiwa tutashirikiana k**a jamii ya Kikristo na kila mmoja akifanya sehemu yake! Tazama waefeso 3:10.
Ni kweli injili itaenea hata kwa kusimama peke yako, lakini kwa vikwazo vingi, na si kwa wengi k**a ambavyo tungesimama k**a jamii. Ni kweli kusimama peke yako, kutatikisa na kuangusha falme na mamlaka za uovu, lakini si k**a ambavyo ingekuwa k**a tungesimama pamoja. Ni kweli ukisimama peke yako utafika katika safari yako ya ukamilifu, lakini kwa mateso mengi, k**a ambavyo tumeshuhudia wenzetu waliokuwepo kabla, kina Danieli, Ayubu, Yusufu, Ibrahimu, Mitume, walivyoteseka mpaka kuufikia ukamilifu. Lakini sasa, tutafanyaje ikiwa jamii yenyewe inaenda mbali zaidi na BWANA?! Tutafanyaje ikiwa jamii yenyewe inamkataa BWANA?! Hapa ndipo linapokuja swala la kusimama peke yako na kuvumilia mateso mpaka kuufikia ukamilifu.
Nipende tu kusema hivi, shetani anajua nguvu iliyopo katika ushirika, anatambua kwamba, k**a tutashirikiana kwa pamoja na kila mmoja akafanya sehemu yake, mara moja, injili itaenea, ufalme wake utaangushwa na tutaweza kuufikia ukamilifu wa Kikristo mara moja- Hii ndio sababu anafanya kila liwezekanalo kuvuruga ushirika! Kuvuruga jamii.
K**a jumuiya ya Kanisa, k**a jamii ya Kikristo, nashauri, tungekaa na kuliangalia swala hili na kutafuta ni kwa namna gani tunaweza kudumu katika ushirika. Kwa nini?! Kwa sababu muda umeenda sana, injili inatakiwa iende na tunatakiwa kuufikia ukamilifu ambao hatutaweza kumwona BWANA pasipokuwa nao (Waebrania 12:14). Ikiwa tunahitaji kuokolewa sisi sote pamoja na familia zetu, tafadhali tushughulikie ili somo la leo.
Nimalizie kwa kusema hivi, "Utakaso na Ukomavu" havifikiwi na watu kwa kujitenga. "Utakaso na Ukomavu", vinafikiwa na watu katika jamii". Yaani ni kwamba; Tunapokaa katika ushirika na kuzitumia karama tulizopewa vizuri ( wengine wakihubiri, wengine wakifundisha, wengine wakiimba, wengine wakionya) tunatakasana sisi kwa sisi! Lakini pia, tunapopitia changamoto kwa pamoja k**a jamii na kuzitatua pamoja kwa namna mbalimbali kutoka kwa wenzetu- hii hutusaidia kukomaa kiroho. Mwisho, neno Jamii lina maana ya "Mkusanyiko wa watu wanaoishi kwa pamoja katika eneo moja la kijiografia wakiunganishwa na vitu fulani vinavyofanana".
TAFAKARI NJEMA SANA...