05/11/2019
KESHA LA ASUBUHI
Jumanne, Novemba, 05, 2019
*SHUKURANI YA WALIOKOMBOLEWA*
📖"Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi"📖. *Mathayo* 25:40.
✍🏻Kila tendo letu la kufanya urafiki kwa watu wa Mungu, litalipwa kana kwamba alitendewa yeye. Kila mvunaji ataridhika sana, wakati sauti angavu ya Yesu iliyo k**a muziki itakaposikika ikisema, "Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu." "Ingia katika furaha ya Bwana wako."
✍🏻Mkombozi atatukuzwa kwa kuwa atakuwa hakufa bure. Wale waliokuwa watenda kazi pamoja na Mungu wataona, kwa mioyo ishangiliayo kwa furaha, mazao ya taabu ya nafsi zao kwa ajili ya wenye dhambi waliokuwa wanaangamia na kufa, nao wataridhika.
✍🏻Saa walizokuwa wakifadhaika, mazingira ya kutatanisha waliyokuwa wanakutana nayo, huzuni ya moyo kwa kuwa wengine walikataa kuyaona na kuyapokea mambo yapasayo amani, vitasahauliwa. Kujikana nafsi walikofanya kwa ajili ya kusaidia kazi, hakutakumbukwa tena.
✍🏻Watakapowatazama watu waliokuwa wakijitahidi kuwaleta kwa Yesu, na kuona wameokolewa milele---alama za rehema ya Mungu na upendo wa Mkombozi---kutasikika sauti za sifa na shukurani kutoka katika matao ya mbinguni.
✍🏻 Mbele yetu kuna mbingu, na miongoni mwa wakazi wake hakutakuwa na mivutano......
✍🏻Tutaipokea familia takatifu ya waliokombolewa, na kusikia maneno ya Kristo, "Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu." Tutavigusa vinubi vyetu, na mbingu itarindima kwa muziki mtamu. Tutazitupa taji zetu zing'aazo katika miguu yake, na kumpa utukufu yeye aliyeshinda kwa niaba yetu.
✍🏻Inawezekana kuna mambo ambayo hatuyaelewi hapa. Mambo mengine katika Biblia yanaweza kuonekana k**a mafumbo kwetu, kwa sababu yako nje ya uwezo wetu mfinyu wa kuelewa.
✍🏻Lakini Mwokozi atakapokuwa akitupitisha kwenye maji yaliyo hai, atayaweka wazi katika akili zetu yale ambayo mwanzoni hayakueleweka vizuri.
*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE*..🙏