Zaburi 23

Zaburi 23 Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Zaburi 23, Church of God, Arusha.

05/04/2023

KUOKOKA

Kuokoka maana yake ni KUOKOKA!, ina maana ya kunasuliwa katika janga ambalo kwamba bila ya kuwepo msaada au mtu mwingine lingesababisha majeraha au hata kifo kwa mhusika. Hivyo kuokoka katika maana ya kiroho ni kuishi maisha ya kumtumainia Mungu ili kwamba hata baada ya mwili kufa, roho yako ibaki kuwa hai milele. Hatua ya kwanza ni kumjua huyo Mungu mwenyewe aliye hai ni nani maana huwezi kumtumainia Mungu usiyemjua wala kuwa na hakika naye. Mungu mwenyewe ndiye anayekuokoa kutoka katika dhambi ambayo ingepelekea mauti yako, maandiko yanasema; “Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima; mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali.” 1 Petro 1:5

Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

05/04/2023

*NIFANYE NINI ILI NIPATE KUOKOKA?*
(Mdo. 16:30-31; 2:37-42)

Ili upate kuokoka chukua hatua ya imani k**a
ifuatavyo:-
1. Tubu Msimamo wako usiokuwa wa kweli kiimani na umwamini BWANA Yesu Kikwelikweli.

2. Omba Msamaha wa dhambi na utakaso kwa damu ya Yesu (Zab 51:1)

3. Kubali Ubatizo wa Roho Mtakatifu na uombe ili BWANA Yesu akubatize.

4. Dumu katika Neno la Mungu usitende dhambi tena. Amini ya kuwa Mungu amekusamehe dhambi zako
na sasa umeokoka! Usitende dhambi tena.

5. Sema/Kiri kwa kinywa chako kwamba umeokoka;
Kufanya hivi si majivuno wala kujisifu (na wala usiwe na nia hiyo moyoni mwako) Bali ni agizo la Mungu!
Kwani unapokiri unayatimiza Maandiko yafuatayo:-
1. Unamtukuza Mungu kwa wokovu aliouleta. (Fil.2:11)
BWANAYesu naye atakukiri mbinguni mbele ya Mungu na Malaika wake (Luka 12:7-12)

2. Unamtangaza BWANA Yesu – Mwokozi kwa wengine ili nao wajue kuwa yuko. Ni sawa na kuvaa vazi safi jeupe ili usiguse uchafu tena. Waovu hawatakushirikisha maovu yao, kwani watajua ya kuwa wewe sasa ni mtu wa tofauti.

Mpendwa msomaji, wewe nawe, unaweza kuokoka ukifuatisha sala ifuatayo ya kukiri makosa na kuomba msamaha kwa dhati kutoka moyoni na kisha ukaishi maisha ya utaua. Yesu Kristo atakupenda sana na kukusamehe kwa hakika, na kukupa wokovu, bila kujali kwamba umefanya dhambi nyingi kiasi gani; kwa maana Yeye ni hakimu wa tofauti. Sema hivi, “Mungu Baba, hakika mimi ni mkosaji, ni mwenye dhambi. Siwezi kupuuza ukweli huu. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha leo. Yesu Kristo, nakusihi unisamehe dhambi zangu, na kunipa uwezo wa kushinda dhambi. Futa jina langu katika kitabu cha hukumu, liandike katika kitabu cha uzima mbinguni. Asante kwa kunisamehe na kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji tayari umesamehewa dhambi zako, na kuokolewa. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho ya Neno la Mungu; katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

31/03/2023

*FAIDA ZA KUOKOKA*

Zipo faida nyingi sana, zisizohesabika, bali hizi ni baadhi tu kati yake!

a) Kukombolewa, yaani Kulipiwa deni (Kufutiwa mash*taka) ili kuondolewa chini ya kongwa la utumwa wa shetani na dhambi. (Wakolosai 2:12-15)

b) Kuhamishwa kutoka utumwa wa shetani na kuingizwa katika ufalme wa Mungu, ndiyo maana BWANA Yesu alianza mahubiri yake kwa neno hili “Tubuni na kuiamini Injili.

c) Kuzaliwa Upya kiroho, yaani kuzaliwa mara ya pili; ili kufanyika Mwana wa Mungu na kuwa kiumbe kipya.
(Yohana 1:12,13; 2Wakorintho 5:17)

d) Kutumikiwa na Malaika wa Mungu; (Waebrania 1:13,14)

e) Kulindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani. (1Petro 1:3-5; Zaburi 34:7)

f) Kupewa ahadi ya Baba, yaani Roho Mtakatifu na Ujazo (kutawaliwa/kuongozwa) na Roho Mtakatifu.(MatendoyaMitume 2:37-
40 )

g) Kuwa Mtakatifu ungali bado upo duniani na Kumpendeza Mungu, jambo ambalo wengi leo wanasema
haiwezekani; LAKINI, (Zaburi 16:3):
(a) Yasiyowezekana kwa Mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.(Mithali 9:25)

(b) Yote yawezekana kwake yeye aaminiye (Marko 9:23).

(c) Tunashinda na zaidi ya kushinda kwake yeye atupendaye. (Warumi 8:31-39).

(d) Ni neema ya Mungu si kwa uwezo wa Mwanadamu. (Waefeso 2:8-9)

h) Kuwa wanafunzi wa Kweli-Kweli wa BWANA YESU. (Yohana 8:31,32)

i) Kusikilizwa na kujibiwa maombi mbele za Mungu.

j) Kuwa na mamlaka na amri juu ya nguvu za shetani, mapepo, majini, magonjwa, sumu, na nguvu zote za
uharibifu (Marko 16:17-20; Luka 10:17-20)

k) Kubarikiwa maishani- milele.

l) Kuruzukiwa na Mungu kuurithi uzima wa milele.

m) Kuepushwa na janga kuu litakaloupata ulimwengu wote, nalo ni,
(1) Dhiki kuu,
(2) Moto wa milele - Jehanamu.
(3) Hukumu ya milele.(Warumi 8:1)

Mpendwa msomaji, wewe nawe, unaweza kuokoka ukifuatisha sala ifuatayo ya kukiri makosa na kuomba msamaha kwa dhati kutoka moyoni na kisha ukaishi maisha ya utaua. Yesu Kristo atakupenda sana na kukusamehe kwa hakika, na kukupa wokovu, bila kujali kwamba umefanya dhambi nyingi kiasi gani; kwa maana Yeye ni hakimu wa tofauti. Sema hivi, “Mungu Baba, hakika mimi ni mkosaji, ni mwenye dhambi. Siwezi kupuuza ukweli huu. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha leo. Yesu Kristo, nakusihi unisamehe dhambi zangu, na kunipa uwezo wa kushinda dhambi. Futa jina langu katika kitabu cha hukumu, liandike katika kitabu cha uzima mbinguni. Asante kwa kunisamehe na kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji tayari umesamehewa dhambi zako, na kuokolewa. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho ya Neno la Mungu; katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

30/03/2023

*HATUA TANO ZA KUEPUKA ZIWA LA MOTO*

➡️ *Kukubali*
Kubali kwamba umetenda dhambi na una hatia ya dhambi. Katika Warumi 3:23, Biblia inatuambia kwamba “wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”.


➡️ *Tambua*
Tambua kwamba dhambi ina adhabu - kifo - hukumu ya milele (Warumi 6:23). K**a vile matendo mema yana ujira, na matendo mabaya yana mshahara. Mshahara wa dhambi ni mauti.
Uzima wa milele ni zawadi ya bure kutoka kwa Mungu.

➡️ *Kubali*
Kubali kwamba adhabu ya dhambi lazima ilipwe au kuondolewa. Lakini kwa hakika, hakuna ondoleo la dhambi isipokuwa kuna mambo mawili: toba na kumwaga damu.

[Waebrania 9:22 KJV] “Na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu; na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo”.

Ni muhimu kukiri kwamba damu ya Yesu Kristo ndiyo damu pekee inayomwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi za wote.

[Mathayo 26:27-29 KJV] “Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini nawaambia, sitakunywa tena tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

➡️ *Amini*
Hatua ya nne ya kuingia katika ufalme huu ni kuamini kwamba dhambi zako zinaweza kusamehewa kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka kwa ajili yako.

[Warumi 10:8-13 KJV] “Lakini yasemaje? Neno li karibu nawe, katika kinywa chako na moyoni mwako, yaani, lile neno la imani tunalolihubiri; Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki; na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Maana Maandiko Matakatifu yasema: "Kila amwaminiye hatatahayarika." Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani; Kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka”.

➡️ *Endelea Kwa Uthabiti*
Katika Matendo 14:22, tunahimizwa kuendelea kwa uthabiti kwa sababu “lazima tupitie dhiki ili kuingia katika ufalme”.
Katika Matendo 2:42-47, wale walioamini na kuongezwa waliendelea kwa uthabiti. Ni lazima uendelee kwa uthabiti ili kuingia katika ufalme.

Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

30/03/2023

*SABABU ZA KUUGUA*

➡️Dhambi (ZABURI 38:3-4; YEREMIA 30:12-14; YOHANA 5:14);

➡️Ili Mungu ajipatie utukufu kwa kumponya kwa muujiza (YOHANA 11:1-4);

➡️Ili kazi za Mungu zidhihirishwe ndani ya mtu huyo (YOHANA 9:3);

➡️Kutokana na KUONEWA na Ibilisi (MATENDO 10:38);

➡️Kumpa Ibilisi nafasi kwa kushindwa kumpinga na kumkemea (WAEFESO 4:27; YAKOBO 4:7);

➡️Upungufu wa Imani (MATHAYO 17:18-20; MARKO 6:5-6).

Ikiwa hatujatenda dhambi yoyote, hatupaswi kudanganywa na Ibilisi kwamba ugonjwa uliotupata umetupata sababu ya dhambi. Zakaria na Elisabeti walikuwa tasa, lakini walikuwa wenye haki mbele za Mungu bila lawama yoyote (LUKA 1:5-7). Tukimruhusu Shetani atudanganye hivyo, mioyo yetu hutuhukumu bure na kutukosesha ujasiri kwa Mungu, na hivyo maombi yetu huwa hayapati majibu (1 YOHANA 3:21-22).

Je! Unataka kuokoka sasa?
Tunasoma haya katika LUKA 1:77, “Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao”. Hii ina maana kwamba ukiisha kutubu dhambi zako leo utasamehewa kwa hakika, na hivyo kupata wokovu mara moja. Je, kweli utasamehewa? Jibu ni Ndiyo! Yesu mwenyewe anasema katika YOHANA 6:37, “……….Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”. Hivyo kwa dhahiri, leo hii, dakika hii hii, utasamehewa na kupata wokovu. Je, uko tayari kuokoka sasa na kuhesabiwa miongoni mwa wale watakaoingia mbinguni na kuishi na Mungu milele, hata wakiiaga dunia sasa hivi? Ukiwa tayari kuifuatisha sala ifuatayo ya toba, mara tu baada ya sala hii, nitakuombea na kwa ghafla utawezeshwa kushinda dhambi. Je, uko tayari kuifuatisha sala hii sasa? Najua uko tayari. Basi sema maneno haya, “Mungu Baba, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Naomba unisamehe na kuniosha dhambi zangu kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani. Niwezeshe kushinda dhambi kuanzia sasa. Liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima mbinguni. Asante kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu, Amen”. Sasa ninaomba kwa ajili yako, “Mungu Baba msamehe kiumbe wako huyu dhambi zake zote, na mpe uwezo wa kushinda dhambi kuanzia sasa na kumuokoa. Mbariki kwa baraka zote katika Jina la Yesu, Amen”. Tayari umeokoka. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI!!!

30/03/2023

*NJIA AMBAZO ROHO MTAKATIFU ANATUMIA KUSEMA NA MTU.*

👉Ndugu wasomaji Mungu anawaonya watu duniani kupitia mawazo yao lakini wengi hawaelewi. Hawazingatii maonyo ya Mungu na wanaishia kwenye matatizo makubwa.

Katika makala hii, nitakuonyesha jinsi Mungu anavyotumia mawazo yako kukuonya.

1. Kutoingia kwenye uhusiano mpya.
Ikiwa unahisi kutoanzisha uhusiano mpya, basi jua kwamba ni Mungu Baba yetu ambaye anakuonya kupitia mawazo yako.

Ikiwa unatii sauti ya Mungu ya onyo katika mawazo yako, basi hivi karibuni utavuna baraka zake. Unaishia kwenye shida ikiwa unakataa onyo la Mungu kupitia mawazo yako.

2. Vyakula na vinywaji.

Ikiwa chakula au kinywaji chochote kinaletwa kwako, na hujisikii kukinywa au kula, basi ujue kwamba ni Roho Mtakatifu anakuonya.

Ni bora kutoa udhuru, na kukataa chakula au kinywaji hicho.
Ikiwa mawazo yako hayana amani na chakula au kinywaji chochote, ni Mungu anakuonya. Usichukue.

3. Safari.

Iwapo unahisi kutokwenda fulani safari, basi jua kwa hakika kwamba ni Baba yetu wa Mbinguni ambaye anazungumza nawe kupitia mawazo yako.

Ghairi safari hiyo mara moja. Kaa nyumbani au fanya kitu kingine.
Ikiwa unahisi mawazo yoyote hasi kuhusu safari yako, ghairi safari hiyo mara moja na ubaki nyumbani.


4. Kutonunua kitu fulani.
Ikiwa unahisi hutaki kununua kitu, basi jua hakika kwamba ni Mungu ambaye anakuonya kupitia mawazo yako. Usiendelee na ununuzi huo.

5. Wageni.
Ikiwa mawazo yako hayana amani na mgeni, basi uondoke haraka. Yesu Kristo anakuonya kwamba mgeni si mtu mwema. Unaweza kujuta ikiwa hutafuata onyo la Mungu.

6. Mikataba.
Ikiwa una mashaka kuhusu kutia sahihi mkataba wowote, basi ujue ni Baba yetu aliye mbinguni ambaye anakuonya.sitisha na uombe muda zaidi wa kufanya maamuzi.

7. Kufunga nyumba yako.

Ukipata wazo la kufunga mlango wako, basi funga mlango huo mara moja. Ni Mungu anakuambia.

Ikiwa ghafla unapata mawazo ya kufunga mlango wako, kisha uufunge mara moja. Mungu ndiye anayekuambia. Unaweza kujuta ikiwa utashindwa kufunga mlango huo haraka k**a Mungu alivyokuagiza.

8. Kutenda dhambi:
Ukipata wazo la kufanya ngono, kupiga punyeto, kuiba, kupigana, kusema uwongo n.k... Na kitu kinakuambia, usifanye hivyo... Huyo ni Roho Mtakatifu anakuonya.... Lakini mara moja ulimwasi Roho na uifanye... Roho Mtakatifu atakuacha mara moja kwa muda mrefu hadi utakapotubu kabisa makosa yako yote.

Roho Mtakatifu anachukia miili ya wenye dhambi, hawezi kuingia katika mwili wa wenye dhambi...k**a Wazinzi, Wapiga punyeto, mavazi yasiyofaa, mashoga, wasagaji na kulala na wanyama.

👉Ili Roho Mtakatifu wa kweli akuingie... Hupaswi kuishi katika Dhambi. Ukijiona unafanya dhambi mbalimbali kila mara, hiyo ni dalili tosha kwamba huna Roho Mtakatifu ndani yako....Biblia inasema, *Kwa matunda yao tutawatambua*

Je, uko tayari kutubu sasa ili kukaribishaRohoMtakatifu? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

30/03/2023

*KUJARIBU KUINGIA MBINGUNI KWA KUFANYA MEMA*
Mathayo 19:16-21

Hapa tunajifunza juu ya mtu mmoja ambaye alifundishwa kutenda mema tangu utoto wake na akafanya yote yaliyoelekezwa kuyatenda kutokana na jitihada zake. Akawa amezishika amri za Mungu tangu utoto wake (LUKA 18:21), na kuona kwamba hakuna jingine alilopungukiwa ili kuurithi uzima wa milele. Ni kweli kabisa kwamba alizishika amri, hata Yesu alithibitisha hivyo lakini katika kipimo cha Mungu, akaonekana bado AMEPUNGUKIWA NA NENO MOJA (LUKA 18:22). Hakuwa na sifa ya kuingia mbinguni kutokana na mema aliyoyatenda. Mbele za macho ya Mungu, hakuna mwanadamu mwema hata mmoja. Mwema ni Mungu peke yake. Hapa Yesu anamwambia kwamba ikiwa anamwita mwema, basi hiyo inathitibisha kwamba Yesu ni Mungu (LUKA 18:18-19). Matendo yoyote mema ambayo atayafanya mwanadamu kwa jitihada zake binafsi, ni k**a nguo iliyotiwa unajisi (ISAYA 64:6), hayafai lolote katika kumpa sifa ya kuingia mbinguni. Mbele za Mungu, wanadamu WOTE kwa kuzaliwa na kutenda, ni wenye dhambi (ZABURI 51:5; 58:3; AYUBU 25:4; MHUBIRI 7:20; WARUMI 3:10-12, 23). Mwanadamu yeyote hata akijitahidi namna gani kuzishika amri za Mungu kwa nguvu zake tu, bado atakwenda tu Jehanum. Ni kutaabika BURE (AYUBU 9:29-31). Huu ndiyo msingi ulio batili wa taratibu nyingi za kidini za wanadamu – kujaribu kuingia mbinguni kwa kufanya mema fulani.

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

30/03/2023

*UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU*

Mtu aliyeokoka anapokufa moja kwa moja dakika ileile anakwenda mbinguni (LUKA 23:39-43; 16:22; MATHAYO 17:1-3; WAFILIPI 1:21-23; 2 WAKORINTHO 5:6,8). Mtu huyu anapokufa, roho yake huvaa mwili wa roho au wa mbinguni na kwenda mbinguni (1 WAKORINTHO 15:40, 41, 44, 46). Hatimaye katika Ufufuo wa Uzima wote waliokwenda mbinguni, watafufuliwa tena yaani watakuja katika miili ya duniani na kuiungana na waliopo duniani, kubadilishwa tena na kupaa kumlaki Yesu wakati wa kunyakuliwa kwa Kanisa. Huu ndiyo Ufufuo wa Uzima au Ufufuo wa Kwanza au ufufuo ulio bora (1 WATHESALONIKE 4:15-17; 1 WAKORINTHO 15:51-54). Watu wanapokufa bila kuokolewa, hakika ileile wanakwenda motoni au kuzimu penye mateso makali (LUKA 16:22-24). Wanaenda motoni bila kuelezwa kwa nini wamepewa hukumu hiyo. Hawa watafufuliwa tena katika Ufufuo wa Hukumu au Ufufuo wa pili ili kuelezwa kwa nini wanastahili kutupwa katika ziwa la moto milele. Hapa ndipo watakapojitetea bila kusikilizwa (UFUNUO 20:11-15; MATHAYO 7:22-23; LUKA 13:25-28).

Je! Unataka kuikwepa hukumu hii sasa?
Tunasoma haya katika LUKA 1:77, “Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao”. Hii ina maana kwamba ukiisha kutubu dhambi zako leo utasamehewa kwa hakika, na hivyo kupata wokovu mara moja. Je, kweli utasamehewa? Jibu ni Ndiyo! Yesu mwenyewe anasema katika YOHANA 6:37, “……….Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”. Hivyo kwa dhahiri, leo hii, dakika hii hii, utasamehewa na kupata wokovu. Je, uko tayari kuokoka sasa na kuhesabiwa miongoni mwa wale watakaoingia mbinguni na kuishi na Mungu milele, hata wakiiaga dunia sasa hivi? Ukiwa tayari kuifuatisha sala ifuatayo ya toba, mara tu baada ya sala hii, nitakuombea na kwa ghafla utawezeshwa kushinda dhambi. Je, uko tayari kuifuatisha sala hii sasa? Najua uko tayari. Basi sema maneno haya, “Mungu Baba, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Naomba unisamehe na kuniosha dhambi zangu kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani. Niwezeshe kushinda dhambi kuanzia sasa. Liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima mbinguni. Asante kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu, Amen”. Sasa ninaomba kwa ajili yako, “Mungu Baba msamehe kiumbe wako huyu dhambi zake zote, na mpe uwezo wa kushinda dhambi kuanzia sasa na kumuokoa. Mbariki kwa baraka zote katika Jina la Yesu, Amen”. Tayari umeokoka. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI!!!

30/03/2023

*HAKIMU YESU KRISTO*

Maandiko yanaeleza waziwazi kwamba Yesu ndiye Hakimu atakayeuhukumu ulimwengu wote. Yeye ndiye anampa hukumu mtu mara tu baada ya kufa (WAEBRANIA 9:27). Ikiwa amekufa katika dhambi, anatupwa katika moto wa milele, na ikiwa amekufa katika wokovu anakwenda mbinguni. Mataifa yote yatakusanyika mbele zake Yesu, Mwana wa Adamu kwa hukumu. Maandiko yafuatayo yanataja waziwazi juu ya Hakimu Yesu Kristo (YOHANA 5:22; MATHAYO 25:31-32; MATENDO 10:42; WARUMI 2:16; 2 TIMOTHEO 4:1).

Je! Unataka kuokoka sasa ili kuikwepa hukumu hii?
Tunasoma haya katika LUKA 1:77, “Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao”. Hii ina maana kwamba ukiisha kutubu dhambi zako leo utasamehewa kwa hakika, na hivyo kupata wokovu mara moja. Je, kweli utasamehewa? Jibu ni Ndiyo! Yesu mwenyewe anasema katika YOHANA 6:37, “……….Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”. Hivyo kwa dhahiri, leo hii, dakika hii hii, utasamehewa na kupata wokovu. Je, uko tayari kuokoka sasa na kuhesabiwa miongoni mwa wale watakaoingia mbinguni na kuishi na Mungu milele, hata wakiiaga dunia sasa hivi? Ukiwa tayari kuifuatisha sala ifuatayo ya toba, mara tu baada ya sala hii, nitakuombea na kwa ghafla utawezeshwa kushinda dhambi. Je, uko tayari kuifuatisha sala hii sasa? Najua uko tayari. Basi sema maneno haya, “Mungu Baba, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Naomba unisamehe na kuniosha dhambi zangu kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani. Niwezeshe kushinda dhambi kuanzia sasa. Liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima mbinguni. Asante kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu, Amen”. Sasa ninaomba kwa ajili yako, “Mungu Baba msamehe kiumbe wako huyu dhambi zake zote, na mpe uwezo wa kushinda dhambi kuanzia sasa na kumuokoa. Mbariki kwa baraka zote katika Jina la Yesu, Amen”. Tayari umeokoka. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI!!!

30/03/2023

☆"NAMNA YA KUTEMBEA NA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO"☆

Karibu tujifunze neno la BWANA.

🔹Watu wengi sana wanapenda kutembea na Mungu katika maisha yao, na hicho ni kitu kizuri sana, lakini ni watu wachache sana ambao wanaelewa gharama wanayotakiwa kulipa ili wafanikiwe katika jambo hilo.

🔸Mungu anapenda kuona watu wake wanatembea pamoja nae k**a walivyofanya wakina Henoko, Ibrahimu, Daudi n.k, lakini ana kanuni zake ambazo watu wake wanatakiwa kutembea nazo kila wakati.

🔹Kanuni kubwa ni kufanya mapenzi ya yake (yaani mapenzi ya Mungu) katika maisha yako. Yesu alisema kwamba Baba yake alikuwa pamoja nae siku zote na wala hakumuacha kwasababu tu alikuwa anafanya yampendezayo (mapenzi ya Baba yake), Yohana 8:29

🔹Unapotaka kufanya mapenzi ya Mungu na kutembea pamoja nae katika maisha yako, unatakiwa kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo;

1. LAZIMA UKUBALI KUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA KATIKA MAISHA YAKO.

Unatakiwa kumpa nafasi ya kwanza katika kila eneo la maisha yako.

Nafasi ya kwanza kwenye moyo wako,nafasi ya kwanza kwenye uchumi wako, wokovu wako, utumishi wako, ndoa yako, nafasi ya kwanza kwenye muda wako, nafasi ya kwanza kwenye mipango yako n.k.

2. LAZIMA UWE NA UTAYARI WA KUFANYA CHOCHOTE NA KWA MUDA WOWOTE.

Tarajia kwamba wakati mwingine Mungu atakutaka ufanye vitu ambavyo havikuweko kwenye ratiba yako.

Anaweza akakuambia ingia kwenye maombi ya kufunga wakati wewe haukupanga, anaweza akakuamsha usiku kumuombea mtu wakati wewe ulitaka kulala, n.k. Unahitaji utayari wa wa hali ya juu sana vinginevyo utashindwa kutembea nae. (2Timotheo 4:2)

3. LAZIMA UKUBALI KWENDA KINYUME NA MILA NA TAMADUNI AMBAZO ZIKO KINYUME NA NENO LAKE.

Huwezi kutembea na Mungu wakati mila na tamaduni zingine unazozing’angania haziendani na neno lake, mfano ibada za wafu, matambiko n.k.

Vitu ambavyo viko kwenye jamii yako na yeye havipendi lazima ukubali kuviacha. (1Wakorintho 10:23)

4. LAZIMA UWE TAYARI KUTEMBEA KWENYE MAJIRA YAKE.

Hili sio jambo jepesi, na linawafanya watu wengi wapishane na muda wao wa kuinuliwa na Bwana/muda wa kujiliwa na Bwana/Appointed time.

Yanaweza yakawa ni majira ya kuoa au kuolewa, majira ya kuanza utumishi n.k

Shida kubwa inayokuja hapa ni kwamba sio rahisi sana wanadamu wakakuelewa, kwa hiyo unazungukwa na hofu, na kuogopwa kutengwa.

5. LAZIMA UTAFUTE KIWANGO KIKUBWA CHA IMANI.

Kutembea na Mungu kunahitaji Imani zaidi, kwasababu wakati mwingine hutajua anakupeleka wapi.

Angalia mfano huu, halafu utaelewa kiwango cha imani ambacho kilikuwa kinahitajika, Mwanzo 12:1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.

Huo ulikuwa ni mtihani mgumu saa kwa Ibrahimu ingawa alifaulu.

Sijui ukiambiwa neno k**a hilo na Mungu utajiuliza maswali mangapi moyoni mwako! Na utachukua uamuzi gani!

Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6).

Hata kwenye maisha ni vigumu sana kuambatana na mtu k**a humwamini.

6. UNAHITAJI UNYENYEKEVU.

Unyenyekevu ni wa muhimu sana ili uweze kutembea na Mungu katika maisha yako.

Mungu mwenyewe asema kwamba anaketi pamoja na mtu aliyetubu na kunyenyekea (Isaya 57:15).

Yakobo 4:6 … Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.

7. UNAHITAJI UTII.

Jambo la utii wa mtu ni la muhimu sana kwa Mungu kuliko sadaka zake(1Samweli 15:22)

Mungu anaupa utii nafasi kubwa sana kuliko sadaka.

Utii ni mlango mkubwa sana sana wa mtu kufanikishwa na Bwana (Isaya 1:19, Kumbukumbu la Torati 28: 1-13).

Kukosekana kwa utii huleta laana (Kumbukumbu la Torati 28: 15-68).

Kwahiyo ukitaka kutembea pamoja na Mungu, unahitaji roho ya utii wa hali ya juu na kutambua kuwa yeye ni boss na hivyo unatakiwa kumtii badala ya kusimamia misimamo yako. Tii anachokuambia kila wakati, ndio mtaenda pamoja.

8. LAZIMA USHUGHULIKIE ROHO YA MAZOEA KWA MUNGU WAKO.

Hiki ni kitu muhimu sana sana, kwasababu kadri unavyozidi kuwa karibu nae ni rahisi ukaanza kumzoea.

Hata kwenye maisha ya kawaida, kadri unavyozidi kuwa karibu zaidi na mtu ni rahisi ukajikuta heshima yako kwake inapungua, na unaanza kumuona ni wa kawaida sana.Hili jambo lilimgarimu Nabii Musa.

Angalia watu wengi ambao wameokoka, kadri wanavyozidi kukaa kwenye wokovu, wanajikuta wameanza kutembea kwenye wokovu kwa mazoea.

Pia angalia watumishi wengi (waimbaji, Wahubiri n.k, utagundua kuwa kadri wanavyozidi kutumika ndipo wanapoanza kutumika kwa mazoea na kutumia uzoefu wao badala ya kumtegea Roho Mtakatifu.

9. LAZIMA UAMUE KUICHUKIA DUNIA NA MAMBO YAKE MAOVU.

Ukitaka kuambatana na Mungu kwenye maisha yako ni lazima uamue kuyachukia mambo maovu ya dunia hii (Yakobo 4:4).

Mungu anachukia sana sana dhambi, ndio maana pamoja na kwamba Daudi alimpenda sana na alikuwa rafiki yake, lakini alipofanya zinaa na mke wa mtu alimkasirikia sana na hakumuacha bila adhabu.

10. LAZIMA UWE TAYARI KUBEBA LAWAMA KUTOKA KWA WANADAMU NA KUKATALIWA NA KUDHARAULIWA WAKATI MWINGINE.

Ukitaka kumpendeza Mungu na kutembea pamoja nae, ni lazima utambue kuwa muda mwingi wanadamu watakupinga sana, na utakataliwa na watu ambao wakati mwingine haukuwategemea.

Ndio maana watu wengine wakiokoka wanatengwa na ndugu zao, wengine wanaacha kusaidiwa na ndugu zao.

Unaweza ukakataliwa na kusemwa vibaya na wazazi wako, mke/mume wako, rafiki zako, watumishi wenzako, wafanyakazi wenzako n.k.
Yesu mwenyewe alipokuja duniani kufanya mapenzi ya Baba yake, alikataliwa na ndugu zake kabisa (Yohana 1:11).

Kwahiyo maeneo mengine ukikataliwa na kusemwa vibaya, usikasirike sana na kuharibu uhusiano wako na Mungu, kwasababu hata Mwokozi wetu Yesu alifanyiwa hivyo. Mtume Paulo alikataliwa, Daudi alikataliwa, Yusufu alikataliwa n.k

Jambo la muhimu kwako, ni kuendelea kusimama pamoja na Mungu wako na Imani yako. Shetani huwa anatumia watu ili kuharibu uhusiano wako na Mungu wako.

☆ZINGATIA: Ni vigumu sana ukayaweza mambo yote hayo kwa wakati mmoja,hivyo anza taratibu, jambo moja baada ya jingine. Mtegemee zaidi Roho Mtakatifu ili akusaidie kutembea kwenye hizo kanuni. Tamani sana awe rafiki yako na mshauri wako wa karibu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

30/03/2023

*HATARI ZA KUTOKUOKOKA*

Zipo hatari/hasara nyingi sana, zisizohesabika, bali hizi ni baadhi tu kati yake!

a) Kuwa mtumwa wa dhambi na wa shetani.

b) Kushindwa kuacha dhambi, kuwa mwenye dhambi, na kufa na dhambi.

c) Kutokuzaliwa Mara ya pili.

d) Kukosa ulinzi wa nguvu za Mungu.

e) Kuwa mwana wa Ibilisi/Shetani.

f) Kusumbuliwa na mapepo na mashetani.

g) Kuikosa ahadi ya Mungu Baba (Kumkosa Roho Mtakatifu)

h) Kulaaniwa maishani-milele.

i) Kufutwa jina katika kitabu cha uzima wa milele.

j) Kutokusikilizwa na kutokujibiwa maombi mbele za Mungu.

k) Kuukosa Urithi wa Uzima wa milele.

l) Kutupwa katika ziwa liwakalo moto wa kiberiti (Moto wa milele, au Jehanamu).

m) Kuingia gizani kwenye kilio na kusaga meno milele.

Mpendwa msomaji, wewe nawe, unaweza kuokoka ukifuatisha sala ifuatayo ya kukiri makosa na kuomba msamaha kwa dhati kutoka moyoni na kisha ukaishi maisha ya utaua. Yesu Kristo atakupenda sana na kukusamehe kwa hakika, na kukupa wokovu, bila kujali kwamba umefanya dhambi nyingi kiasi gani; kwa maana Yeye ni hakimu wa tofauti. Sema hivi, “Mungu Baba, hakika mimi ni mkosaji, ni mwenye dhambi. Siwezi kupuuza ukweli huu. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha leo. Yesu Kristo, nakusihi unisamehe dhambi zangu, na kunipa uwezo wa kushinda dhambi. Futa jina langu katika kitabu cha hukumu, liandike katika kitabu cha uzima mbinguni. Asante kwa kunisamehe na kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji tayari umesamehewa dhambi zako, na kuokolewa. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho ya Neno la Mungu; katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

30/03/2023

SOMO : MUNGU HUWAPIGA WENYE KIBURI

Jana tulianza kuangalia sehemu ya kwanza ya kiburi na leo basi kwa Neema ya Mungu tumalizie sehemu ya pili na mwisho.

KIBURI CHA UZIMA:

Kiburi cha uzima ni kile kinachozungumziwa katika.. 1 Yohana 2:16

“Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na KIBURI CHA UZIMA, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.”

Kiburi cha Uzima ni kiburi kinachompata mtu kutokana na Vitu alivyonavyo, au anavyotegemea kuwa navyo..

Watu wengi wenye mali wanakuwa na hiki kiburi(japokuwa si wote, bali asilimia kubwa).. Wanaona mtu asiyekuwa na mali k**a wao hawezi kuwaambia chochote,..kiburi hiki cha mali kinamfanya mtu aone hata Mungu hana maana, Neno la Mungu kwake ni k**a habari zilizopitwa na wakati.

Kulifanyia mizaha Neno la Mungu, ni habari ya kawaida kwao…hata wasikie maonyo ya Mungu kiasi gani, kwao ni habari tu upuuzi.. Mioyo yao imeinuka kutokana na Mali au vitu walivyonavyo, wanaona wanaweza kula hata pasipo kumwomba Mungu, wanaweza kuendeleza maisha yao hata pasipo kupiga magoti.. hivyo hawamhitaji Mungu tena..

Kiburi hiki ndio kibaya kuliko vyote, na ndicho kilichozungumziwa sehemu nyingi katika biblia.. naa watu wote wenye hiki kiburi, biblia imeandika hatima yao..

Isaya 2:12 “Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote WENYE KIBURI NA MAJIVUNO, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.”

Mithali 16:5 “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu”.

Mithali 8:13 “Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.”’

Ayubu 40:12 “Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo”.

Zaburi 119:21 “Umewakemea wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako”.

Soma pia Mithali 21:4, Mithali 16:18, Zaburi 31:18, Zaburi 119:51, Mithali 11:2, na Malaki 4:1 biblia imeelezea zaidi juu ya kiburi na madhara yake..

Tujiepushe na kiburi, tunyenyekee chini ya mkono wa Mungu ulio hodari

Ukitubu leo toba ya kweli, ndipo utakapopata rehema za Mungu(MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zaburi 23 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category