Adonai Deliverance & Healing Foundation

Adonai Deliverance & Healing Foundation Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Adonai Deliverance & Healing Foundation, Religious organisation, Arusha.

Huduma ya maombi na maombezi iliyopo Moshono Arusha
HUDUMA ZETU NI KILA SIKU ZA JUMATATU | JUMATANO | IJUMAA | JUMAMOSI SAA 9 Alasiri - Saa 12 Jioni KARIBU SANA

25/12/2023

Salamu za Christmas toka kwa Huduma ya Adonai.

Bwana Yesu asifiwe sana.

Katika kutafakari sikukuu hii muhimu katika safari yetu ya wokovu naomba tuangalie jambo hili:

Luka 1:26-38.............[34]Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?

[35]Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika k**a kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

Mariamu aliambiwa kwa habari za kumzaa Mwana, mtoto mwanamume ambaye jina lake litaitwa Yesu. Lakini Mariamu aliuliza swali ambalo hata mimi na wewe tungeweza tukauliza... LITAKUWAJE NENO HILI? au kwa maneno mengine unaweza kusema ni LITAWEZEKANAJE NENO HILI?

Lakini malaika alimwambia Roho Mtakatifu atakujilia juu yako na nguvu zake aliye juu zitakufunika k**a kivuli. Akiwa na maana kwamba hata k**a hajamjua mume bado lakini Roho Mtakatifu ndo atakayewezesha jambo lile liwezekane.

Mtu wa Mungu inawezekana Kuna vitu unatamani vizaliwe kwako lakini kwa mazingira ya nje unaona haiwezekani kabisa.

Kuna ahadi za Mungu unaona kabisa ni halisi kwako na ni majira lakini mazingira yako ya nje yanakataa. Unabaki kujiuliza litawezekanaje neno hili? Amini kwa Mungu yote yanawezekana.

Nakuombea leo nguvu za Roho Mtakatifu ziwe juu yako na uweza wa aliye juu ukufunike vitu vipya vikazaliwe kwako kwa jina la Yesu na kile Mungu amesema kwako kupitia neno lake kikavae mwili na kuwa thabiti kwa jina la Yesu.

Heri ya sikukuu ya Christmas.
Adonai Deliverance foundation

Address

Arusha
255

Opening Hours

Monday 09:00 - 06:00
Wednesday 09:00 - 06:00
Friday 09:00 - 06:00
Saturday 09:00 - 06:00

Telephone

0755 670 500

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Adonai Deliverance & Healing Foundation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share