11/12/2023
SADAKA ILIYO KUU NI KUWAJALI WAHITAJI
Hata fungu la Kumi kwa Kanisa haizidi sadaka ya kutoa kwa wenye uhitaji walio ndugu.
Nasema si kwa sheria bali kwa Imani ya Kristo Yesu aliye Kuhani Mkuu mwenye kustahili Sadaka za Kikuhani ikwepo Fungu la Kumi.
“Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.” Yakobo 1:27
Ndugu zangu, imetupasa kuufikia kimo cha ukamilifu ambao ni UPENDANO WA KINDUGU katika Kristo Yesu. Ndiyo maana nasema nawe kuhusu utoaji wako katika kumtolea Mungu sadaka.
Sadaka tuzitoazo katika Madhehebu yetu, Je hutusaidia kufikia kimo cha Ukamilifu ambao ni UPENDANO WA KINDUGU?
Mfano, Katika sadaka za fungu la Kumi ambayo ni sheria kutoa kwa kuhani asiye na asili ya kufa au kutoa kwa yeye aliyekusudiwa k**a maandiko yasemavyo. Na kuhani asiye na asili ya Kufa ni MELKIZEDEKI Mfalme wa Salemu ambaye kwa Ufunuo ni YESU KRISTO aliye Hai hata Milele naye ni Kuhani wetu Mbinguni.
“Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine (Yesu Kristo) mithili ya Melkizedeki; 16 asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;17 maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki. Ebr 7:15”
Kwa asili Ibrahimu alistahili kupokea sehemu ya Kumi kutoka kwa Israel kwa maana hapakua na aliye mkuu kuliko yeye, na kwa Sheria kabila la Lawi naye alipokea.
Lakini Je, kwa Sheria ya Roho, yuko wapi Kuhani mwenye kustahili sadaka za FUNGU LA KUMI? Au kwa sheria ya Roho, Kristo Yesu aliye kuhani husema nini kuhusu Kumtolea? Kwa maana imekwisha kunenwa kuwa “Basi, ile amri ya zamani inawekwa kando kwa sababu ni dhaifu na haifai.Kwa maana Sheria haikufanya kitu chochote kiwe kikamilifu, lakini kuletwa kwa tumaini bora kulifanya hivyo, na kupitia tumaini hilo tunamkaribia Mungu”
Kinachofanya Sheria ya zamani kuwa dhaifu ni kuwepo kwa sheria mpya ya Roho kwa Kristo Yesu aliye Kuhani Mkuu sana.
“Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu (Yesu), umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye; 33 na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani k**a nafsi yako, KWAFAA KULIKO SADAKA nzima za kuteketezwa na DHABIHU ZOTE pia.”
Marko 12:32
UTIMILIFU wa Sheria yote upo katika UPENDO. Ndiyo maana imetupasa kupenda Rehema kuliko Sadaka.
Kutoa sadaka za fungu la Kumi na Zaka Madhabahuni kwa mapokea ya Kanisa imepaswa kuwa kwa Sheria ya Roho ambayo ni kwaajili ya UPENDO na wala si kwa Sheria ya zamani iliyo dhaifu. Kwa maana kumtolea Mungu kwa njia ya Upendo kunafanya kumkaribia Mungu zaidi kuliko kutoa kwa Sheria. Hata sasa hakuna Wakristo wengi wanaotoa kwa Sheria bali kwa UPENDO.
Wala tusidhani kuwa UTII wetu upo katika kutoa Sadaka za Mapokeo katika Madhehebu yetu, bali UTII wetu upo katika Amri iliyo Kuu iliyotoka kwa Bwana mwenyewe Akisema “Amri mpya nawapa, Mpendane. K**a vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.” “Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.” Hapa ndipo kipimo cha UTII wala si katika sadaka za Mapokeo.
BASI SASA, Tumtolee Kuhani wetu YESU KRISTO k**a anavyotaka yeye wala si kwa Mapokeo na Sheria iliyo dhaifu. Na kumtolea yeye ni njia ya Amri yake kwamba Mpende jirani yako ambaye ni mwenye uhitaji hasa kwa aliye ndugu yako katika kanisa au Familia.
Achana na kusema, Nimekwisha kutoa fungu la Kumi au zaka hivyo nasubiri baraka za Mungu’. Hatuna sheria hiyo kwa sasa ila Sheria ya kuwajali masikini na wenye njaa na walio dhaifu. Acha kuweka nguvu katika sadaka za bahasha zisizolenga kuwainua walio dhaifu katika Kanisa na Familia.
Fungu la Kumi na Sadaka za Zaka Madhabahuni tutatoa ikiwa ni kwaajili ya kuwajali watumishi k**a sehemu ya kuwapenda kwa huduma zao ili nao wapate vya mwilini. Lakini hatutoi ili kutimiza sheria ya zamani au kutimiza mapokeo.
Katika Agano Jipya Tumeitwa kwa Amri Moja tu ya UPENDANO WA KINDUGU wala hatukiutwa kwa Amri ya Sadaka za Mapokeo katika Madhehebu yetu.
“Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.” Yakobo 1:27