Ps. Emmanuel Cliff

Ps. Emmanuel Cliff Turning People to Become God's Sons. Galatians 4:7

✍ Nyenyekea━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 1 Petro 5:6-7 SRUV[6]  Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakwe...
07/09/2026

✍ Nyenyekea
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 1 Petro 5:6-7 SRUV
[6] Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; [7] huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Kunyenyekea chini ya mkono wa Mungu ulio hodari ina maana kwamba kumpa Mungu mambo yote yanayokusumbua ili kwamba Yeye aweze kukusaidia, ashuhulikie.

Neno linasema "mkono wa Mungu ulio hodari," ina maana kwamba tujitiishe chini ya nguvu za Mungu ambazo ni Kuu kuliko jambo lolote au kitu chochote. Yaani, ni Kuu kuliko magumu uliyonayo.

"mkimtwika yeye fadhaa zenu zote." Fikiria una mahali ambapo ukiwa na tatizo unaweza kwenda na pasipo kutumia nguvu zako ukasaidiwa; Mungu hakudai chochote ili kukusaidia.

Unapompa mambo yanayokusumbua yote, huo ndio unyenyekevu wenyewe, unamuonyesha Mungu kwamba hujitegemei bali unamtegemea Yeye. Kwa kufanya hivyo atashuhulikia mambo yako yote.

Wewe kupambana mwenyewe na mambo ya maisha ambayo yanakushinda ni ishara kwamba una kiburi, na Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi. Mpe Mungu akusaidie na kukuinua kimaisha.

"nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake" Aina ya maisha unayoishi huyapendi, huna uwezo wakubadilisha lakini Mungu anaweza kuyabadilisha.

Badala ya kuhangaika na kukosa usingizi, mpe Mungu akusaidie na kukuinua pasipo wewe kuteseka. Atakuinua, atakupumzisha na utayafurahia maisha siku zote ndani ya Kristo. Hallelujah!

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Bwana Yesu Nakupa Kila Jambo Gumu Kwenye Maisha Yangu Unisaidie. Kazi Yangu Ninayofanya Kila Siku Naiacha Mikononi Mwako, Ukanisaidie Wewe Mungu Wangu. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Yakobo 4:10 BHN
[10] Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni.

Ayubu 22:29 SRUV
[29] Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.

Luka 14:11 BHN
[11] Kwa maana yeyote anayejikweza atashushwa na anayejishusha, atakwezwa.”

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Kwa Kuwa Hamwombi━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Yakobo 4:2 SRUV[2] Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwez...
06/09/2026

✍ Kwa Kuwa Hamwombi
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Yakobo 4:2 SRUV
[2] Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Huna haja ya kuwa na tamaa ya vitu vya watu wengine kiasi cha kuanza kuwa na wivu. Tamaa na wivu havikufanyi wewe kupata alichonacho mtu mwingine; siri ipo kwenye kuomba.

Mathayo 6:8 SRUV
[8] Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

Napenda kukukumbusha kwamba kabla hujaomba wala kusema kitu chochote kwa Mungu Baba yako, tayari anajua kwamba unahitaji kitu fulani. Mungu anatujua kuliko tunavyojijua.

Je! Kuna kitu ambacho mtu mwingine anacho na unakipenda na unadhani ni muhimu na wewe uwe nacho? K**a ndio, basi usiwe na tamaa, mshukuru Mungu aliyempa huyo kwanza.

Baada ya kumshukuru Mungu kwa kumpa huyo, sasa ni wakati wa kumwambia Mungu kwamba imekupendeza na wewe kuwa na kitu hicho pia, na Mungu atakupa kwa sababu huna wivu wala tamaa.

Mungu anatupenda sisi watoto wake, anatujua na anatujali kuliko tunavyoweza kuwaza. Mahitaji yako yote ya leo na kila siku anayajua, hakuna unachoweza kumdanganya. Mwambie atakupa!

Mungu aliyesema "ombeni mtapewa" anasubiri kila mtu aombe kwa sababu na Yeye yupo tayari kutupa tunachoomba. Mungu hachoki ukiomba, endelea kumuongezea maombi atakupa vyote. Hallelujah!

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba Kwa Jina La Yesu Kristo Ninakushukuru Kwa Neema Yako, Unanipa Kila Kitu Ninachoomba Kwa Sababu Unanipenda na Unaujua Moyo Wangu. Asante Baba Yangu, Naamini Nimepokea Mahitaji Yote ya Moyo Wangu. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mathayo 7:7-8 SRUV
[7] Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; [8] kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Mawazo Ya Mungu━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Yeremia 29:11 SRUV[11] Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni ...
06/09/2026

✍ Mawazo Ya Mungu
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Yeremia 29:11 SRUV
[11] Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Tunaye Baba ambaye ni mzuri tofauti na watu wanavyomchukulia; wapo wanaomuona ni mkorofi, mchoyo, hana upendo na anawawazia watu wake mambo mabaya tu. Lakini sio kweli!

Kila kitu alichokifanya kwa mwanadamu ni kwa ajili ya faida ya huyo mtu. Pia, mapenzi yake sio kuona mambo mabaya yanampata mtu, ni kwa sababu watu wameruhusu mabaya kuwapata.

K**a ukiiba kitu na ukak**atwa, kisha ukapigwa na kuumizwa, huwezi kulalamika na kusema mbona mambo mabaya yamekupata; umeyakaribisha kwa kufanya kitendo kiovu.

Mungu anatuwazia mawazo ya amani, je! Unajua maana ya Amani? Maana yake ni shalom, maana ya shalom ni Afya, Amani, Ustawi, Furaha, Mafanikio na Maisha ya Raha.

Swali, ni kweli Mungu anatuwazia mambo mazuri na ya kutupa mafanikio, afya na ustawi, lakini mbona mambo yanazidi kuwa mabaya kwenye maisha? Soma mistari inayofuta utapata majibu.

Yeremia 29:12-13 SRUV
[12] Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. [13] Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Maombi ndio ufunguo wa kufungulia mambo yote mazuri ya Mungu maishani mwako. Chochote unachodhani kwamba unakihitaji muombe atakupatia kwa sababu anapenda kukupa.

Mapenzi mazuri ya Mungu hayatimii maishani mwetu yenyewe, yanatimia kwa mtu kuomba. Mungu alipotaka kunyeesha mvua, Eliya aliomba mpaka mvua ikanyeesha.

Omba mpaka umekipata kile unachohitaji kwa maana Mungu anakuwazia mambo mazuri. Anataka kuona unapata vitu vizuri na kuishi maisha mazuri na nyenye ustawi na mafanikio. Amen

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mungu Wangu Ninakushukuru Kwa Kuwa Unaniwazia Mambo Mazuri, Kiasi Kwamba Upo Tayari Kunipatia Chochote Ninachopenda. Asante Baba Kwa Kuwa Kila Ninachoomba Unanipa. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Kumbukumbu la Torati 4:29 SRUV
[29] Lakini huko, k**a mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.

Mathayo 7:7-8 SRUV
[7] Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; [8] kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Kumpaka Mafuta━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Yakobo 5:14 SRUV[14]  Mtu wa kwenu amekuwa mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa; nao...
05/09/2026

✍ Kumpaka Mafuta
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Yakobo 5:14 SRUV
[14] Mtu wa kwenu amekuwa mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Watu wengi wamekuwa wakipishana katika swala la matumizi ya vitu mbalimbali k**a maji, chumvi, juice na mafuta. Vitu hivi havina tatizo, tatizo linakuja kwa watu kuweka imani katika vitu badala ya Mungu.

Kwenye Agano Jipya matumizi ya mafuta kwenye maombi yapo, Yakobo na Marko wameandika katika vitabu vyao. Sasa ni jinsi gani ambavyo mafuta yalitumika katika uponyaji?

"kumpaka mafuta kwa jina la Bwana." Mafuta hayaponyi, Jina la Yesu ndilo linaloponya; mitume waliwapaka wagonjwa "mafutwa kwa Jina la Bwana" ambalo ndilo linaloponya.

Marko 6:12-13 SRUV
[12] Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. [13] Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaponya.

Kanisa la sasa hivi limesahau Jina la Yesu na limehamishia imani katika mafuta, juice, chumvi, maji nk; wanavitumia k**a mbadala wa Jina la Yesu na imekuwa k**a ibada ya sanamu au uganga.

Je! Kuna umuhimu wa kutumia vitu hivi? Jambo la kwanza kabisa, lazima tuelewe kwamba sisi hatujiongozi wenyewe, Roho Mtakatifu ni kiongozi wetu na anaweza akakwambia uvitumie.

ONYO: Roho Mtakatifu akisema utumie mahali fulani, haina maana kila mahali utumie tena, ni lazima umsikilize tena k**a atakwambia utumie.

Jambo la pili na muhimu kufahamu ni neno hili;

Wafilipi 2:9-10 SRUV
[9] Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia JINA LILE LIPITALO KILA JINA; [10] ili KWA JINA LA YESU KILA GOTI LIPIGWE, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

Marko 16:17-18 SRUV
[17] Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa JINA LANGU watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; [18] watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kuua, hakitawadhuru kamwe; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapona.

Tumepewa Jina la Yesu tulitumie kuponya na kufanya ishara, maajabu na miujiza. Hakuna mahali ambapo Jina la Yesu limetajwa na mtu asipone au tatizo lisiondoke. Ukiwa na jina la Yesu kila kitu kinatii!

Weka imani yako katika Jina na sio katika vitu ambavyo vinaharibika, ikitokea umeambiwa na Roho Mtakatifu tumia kitu fulani, kitumie kwa Jina la Yesu, imani yako ikiwa kwa Yesu sio kwenye hicho kitu.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mungu wangu na Baba Yangu Asante Kwa Uwepo wa Nguvu Zako Za Uponyaji Zinazoambatana na Jina Lipitalo Majina Yote, Jina la Yesu. Ninapotumia Mafuta Katika Uponyaji, Imani Yangu Ipo Katika Jina la Yesu Kristo. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Yakobo 5:15 SRUV
[15] Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.

Warumi 14:23 SRUV
[23] Lakini aliye na mashaka, k**a akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na KILA TENDO LISILOTOKA KATIKA IMANI NI DHAMBI.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Kataa Hofu━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 1 Yohana 4:18 SRUV[18] Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje...
05/09/2026

✍ Kataa Hofu
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 1 Yohana 4:18 SRUV
[18] Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Chanzo cha hofu ni kutokuwa na pendo la Mungu! Najua ni ajabu unaposikia hivyo kwa sababu ulidhani hofu inakuja kwa kutishiwa na watu au vitu. Hofu inakuwepo ambapo hakuna Pendo.

1 Yohana 4:8 SRUV
[8] Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

Pendo ni nani? Ni Mungu! K**a hauna Mungu utaishi kwa hofu lakini k**a una Mungu huwezi kuwa na hofu. Sababu ni hii; Mungu ndiye Muumba wa kila mtu na kila kitu.

K**a Mungu ndiye Muumbaji wa kila kitu na upo pamoja nae, unadhani ni nini hicho ambacho kinaweza kukutisha au kukudhuru? Hata k**a vipo na unaviona, huwezi kuviogopa.

Sisi ni watoto wa Mungu! Mtoto akiwa na mzazi wake hakuna kitu anachoogopa kwa sababu anajua baba au mama yupo. Mkristo haogopi kwa sababu anajua yupo na Mungu Baba yake.

Ulimwenguni kunayo dhiki k**a Bwana Yesu alivyosema, na Bwana Yesu pia anasema hivi;

Mattayo MT. 28:19-20 SWZZB1921
[19] Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; [20] mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.

"tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata mwisho wa dunia." Hii ni ahadi ya Bwana Yesu na uhalisia wa maisha ya kila Mkristo, kwamba, Bwana Yesu yupo pamoja na sisi milele.

Shetani na jeshi lake wanaweza kuja kwako kwa kila namna lakini huna haja ya kuogopa, Bwana na Mfalme wa Mbingu, Dunia na Kuzimu yupo na wewe, hakuna anayeweza kukudhuru.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Sina hofu juu ya jambo lolote, nina Mungu wangu Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka, Mtawala juu ya mambo yote; yupo na mimi na haniachi milele. Ananilinda, ananitunza, haniachi wala hanipungukii.

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Marko 16:20 SRUV
[20] Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]

1 Yohana 4:4 SRUV
[4] Ninyi, watoto wadogo, mnatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Omba Kwa Imani━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Yakobo 1:6-7 SRUV[6]  Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye ...
04/09/2026

✍ Omba Kwa Imani
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Yakobo 1:6-7 SRUV
[6] Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni k**a wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. [7] Maana mtu k**a yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Imani ni kuwa na uhakika kwamba unachoomba au ulichokwisha kuomba unakipata. Neno linapotuambia tuombe kwa imani, linatuambia tuombe tukiwa na uhakika kwamba tutapata tunachoomba.

Shaka ni kinyume cha imani, shaka pia ni kuwa na uhakika; lakini, shaka inakuwa na uhakika wa kukosa na kupata mambo mabaya. Mtu mwenye shaka pia ni mtu anayeomba, ila ana uhakika wa kukosa.

Mtu mwenye mashaka ni yule ambaye anasema nina amini halafu baada ya muda haamini tena. Mtu wa imani ni yule ana amini wakati wote na siku zote na wala harudi nyuma au kukata tamaa.

Kwa nini umeomba lakini huna raha kabisa? Kwa nini bado una wasiwasi? Kwa nini unakosa usingizi? Ni kwa sababu una uhakika kwamba huwezi kupata ulichoomba. Hiyo ndio shaka!

Mtu mwenye imani akishaomba anakuwa na furaha kwa sababu ana uhakika wa kupata alichoomba, hata k**a haoni dalili ya kupata lakini ana uhakika kwamba muda wowote atapata.

Unapo-omba kitu kwa Mungu kuwa na uhakika kwamba utakipata, hiyo inaitwa imani. Mawazo ya kukuonyesha kwamba huwezi kupata yatakuja, wewe tamkaa hivi, "nina uhakika nitapata."

Mawazo ya kukosa yanaletwa na adui, wala usihofu na kusema mbona ninawaza hivi; hayo mawazo unayaangusha tu kwa kutamka kwamba "nina uhakika wa kupata nilichoomba." Na Utapata!

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Nina Uhakika Juu ya Mambo Yote Niliyoyaomba Kwamba Nimeyapokea, Ni Yangu na Yanafanyika. Sina Mashaka Juu ya Jambo Lolote, Ninajua Kila Kitu Kitakua K**a Nilivyoomba.

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Waraka kwa Waebrania 11:1 SRUV
[1] Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni kusadiki mambo yasiyoonekana.

Marko 11:24 SRUV
[24] Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Furaha━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Wagalatia 5:22-23 SRUV[22]  Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu ...
04/09/2026

✍ Furaha
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Wagalatia 5:22-23 SRUV
[22] Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, [23] upole, kiasi; juu ya mambo k**a hayo hakuna sheria.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Kabla hatujazungumza kuhusu Furaha, nataka tuweke sawa jambo moja. Neno linaanza kwa kusema "Lakini Tunda La Roho," halisemi matunda ya Roho. Tunda hapo ni moja tu!

Tunda la Roho ni Upendo pake yake, hayo mengine ni sehemu ya Tunda moja la Upendo. Ndani ya Upendo kuna furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi.

Wafilipi 4:4 SRUV
[4] Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

Ndani ya Tunda la Upendo kuna Furaha! Neno linapotuambia tufurahini, haina maana kwamba kila kitu kikiekwenda vizuri ndipo ufurahi; tunafurahi kwa sababu ya Pendo la Mungu lililo ndani yetu.

Mungu ni Upendo, kwa kuwa tuna Upendo wa Mungu, tunajikuta tuna furaha pasipo kujua tupo katika mazingira gani au tunateswa na hali gani. Furaha ya Mungu haichagui mazingira, ipo tu.

Furaha ni udhihirisho wa uwepo wa Roho wa Mungu maishani mwetu; haiwezekani ukawa umejaa Roho Mtakatifu na ukawa una huzuni moyoni mwako. Unaweza kuwa kwenye jaribu na ukawa na furaha!

Shetani anataka uwe na huzuni, ujionyeshe kwa watu kwamba una huzuni na masikitiko; Mungu anataka ufurahi pasipo kujali hali unayopitia. Unachagua kipi hapo? Kumtii Mungu au Ibilisi?

Furaha ya Mungu inaondoa changamoto zote na kumpa nafasi Roho Mtakatifu atawale maamuzi yako na hatua zako, kisha akufikishe kwenye mafanikio na kukutoa kwenye changamoto uliyonayo.

Wafilipi 3:1
[1]Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Ninafurahi Wakati Wote Katika Bwana, Ninamshangilia Mwokozi Wangu Yesu Kristo Kwa Neema Yake Maishani Mwangu. Nina Shangilia Kwa Sababu Ninajua Yale Mema na Mazuri Anayokwenda Kunitendea. Hallelujah!

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Yohana 15:11 SRUV
[11] Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

Warumi 12:12 SRUV
[12] kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Wawili Wakikubaliana━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Mathayo 18:19-20 NEN[19]  “Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana d...
03/09/2026

✍ Wawili Wakikubaliana
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Mathayo 18:19-20 NEN
[19] “Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watatendewa na Baba yangu aliye mbinguni. [20] Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao.”
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Umekuwa ukifanya maombi mwenyewe na ukimaliza kuomba unaona k**a hujaomba, au unapata wasiwasi k**a umeomba vizuri au hofu inakujaa k**a utapata ulichoomba?

Unaweza ukafanya maombi ya makubaliano na mtu mwingine juu ya jambo lako.

Bwana Yesu ameweka vigezo vya maombi ya namna hiyo, kuwa, lazima wawe watu wawili au ziadi, wawe hapa duniani, halafu wakubaliane. Katika eneo la kukubaliana ndilo watu wanakosea.

Mnapaswa kukubaliana kuhusu mnachokiomba, kwamba, hicho kitu kiwe sawasawa na mnavyotaka nyie wawili au watatu. Wote mkubali kwamba tuombe matokeo tunayataka yawe hivi.

Mfano; hamuwezi kuomba fedha, lazima mkubaliane ni fedha kiasi gani muombe; wote mkishakubali, basi mnaomba au mmoja ataomba kwa ajili ya wote na Mungu ataheshimu hayo maombi.

Mungu ni Mungu wa maagano, mnapokubaliana wawili au zaidi, hilo ni agano na Mungu habadilishi bali atalitenda. Mnapokua mnakubaliana Mungu anakuwepo katikati ya makubaliano yenu.

Mnapoomba, Mungu Anawaona na Kuwasikia Kwa Sababu Yupo, Na Atafanya Mlichokubaliana. Anaheshimu Makubaliano Yenu!

Maombi ya makubaliano yatakusaidia nini? Yatakuondolea hali ya kutokuamini, hofu, mashaka na wasiwasi wa kukosa ulichokiomba. Kwa sababu mlikubaliana, hutaweza kuvunja makubaliano wala kurudi nyuma.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Baba Yangu Mpendwa Nakushukuru Kwa Kuwa Unasimamia Makubaliano na Kuyatimiza. Wewe ni Mungu Ushikaye Maagano! Asante Kwa Maombi Yote Niliyoyaomba Kwa Makubaliano, Nina Amini Unayatenda Sawasawa na Neno la Kristo. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Marko 11:24 SRUV
[24] Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Katika Amani━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Isaya 26:3 NEN[3] Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti k...
03/09/2026

✍ Katika Amani
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Isaya 26:3 NEN
[3] Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Unapitia mateso mengi pengine kuliko Ayubu, lakini, moyo wako unamtumaini nani? Mambo ya maisha yamekuwa magumu unajuta hata kuzaliwa, moyo wako una-mtumaini nani?

K**a tumaini lako lipo kwako mwenyewe mateso hayataisha, k**a unamtumaini mtu fulani usitegemee kupata amani na k**a unatumaini mali zako basi utateseka sana. Mtumaini Mungu Tu!

Adui anapenda sana unapokosa amani, kwa sababu anajua k**a huna amani basi unayo hofu; na hofu ni mlango wa shetani kufanya uharibifu wa kila aina kwenye maisha ya watoto wa Mungu.

Ukiwa huna amani fahamu kwamba ni kwa sababu Mungu sio tegemeo wala tumaini lako.

Ipo dawa ya kudumu katika amani, ni kuweka tumaini lako kwa Mungu kwa njia ya neno lake bila kujali hali inavyokwenda. Hali inaweza kuwa mbaya lakini muamini Mungu kwa alichosema.

Pengine kuna kitu umeomba lakini hakuna dalili ya kupata ulichoomba, hali inazidi kuwa mbaya nk; unaweza kuwa katika amani k**a utaendelea kumtumaini Mungu na kumshukuru kwa alichosema.

Kwa kuwa unamtumaini Mungu kukubadilishia hali fulani, endelea kumtumaini hivyo hivyo na usiyumbe hata k**a shetani anajaribu kukwambia hautapata unachosubiria; endelea kusubiri utapata.

Hakuna mtu aliyewahi kuomba akanyimwa, wewe huwezi kunyimwa pia. Mwamwini Mungu kwamba anaweza kukupa; na k**a una amini hivyo basi kuanzia sasa kuwa na amani, subiri.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mungu Wangu na Bwana Wangu Yesu Kristo, Tumaini Langu na Tegemeo Langu ni Wewe Katika Hali Zote na Mahitaji Yangu Yote. Ninakuangalia Wewe na Kile Ulichosema, Ninajua Unaweza Kunitendea na Utatenda. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
2 Wathesalonike 3:16 SRUV
[16] Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

✍ Usisumbuke, Uwe na Amani━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━🪙 Wafilipi 4:6-7 SRUV[6]  Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila ne...
02/09/2026

✍ Usisumbuke, Uwe na Amani
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
🪙 Wafilipi 4:6-7 SRUV
[6] Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. [7] Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Mkristo ni mtoto wa Mungu, na Mungu ambaye ni Baba hajamzaa mtoto wake ili asumbuke wa kitu chochote cha kimaisha hapa duniani; bali awe na maisha ya Amani itokayo kwa Mungu.

Mungu anataka amani kwa watu wote sio kusumbuka, mtu anaposumbuka kwa ajili ya jambo lolote, Amani ya Mungu inaondoka maishani mwake na hakuna ambacho atafanikiwa.

Kila mtu ana mahitaji yake ya kila siku na Mungu ambaye ni Baba anayajua kabla hata hujamuomba; ametupa njia ya kuyapata mahitaji yetu yote, ni kwa kusali, kuomba pamoja na kushukuru.

Huwezi kupata unachotaka kwa njia ya kujisumbua, kuhangaika na kuwa na wasiwasi. Maisha aliyotuitia Mungu sio ya shida wala mapambano; anataka tutulie katika Amani ili atuhudumie.

K**a Mungu amesema tuombe ni kwa sababu anataka kutupa, na tunapotii na kumuomba tunapata Amani ambayo inatoka kwake. Siku zote amani inakuja kwa kufanya alichoagiza Mungu.

Ukiomba unapata amani ya Mungu kwa sababu mzigo wa mahitaji unaondoka kwako na kwenda kwa Mungu; ghafla huna wasiwasi tena wala husumbuki kwa sababu Mungu amechukua jambo lako.

Ukipata Amani, basi unakuwa na uhakika kwamba jambo lako limefika mikononi mwa Mungu na analishuhulikia ili upate unachohitaji. Katika hitaji lolote, Omba na Kushukuru, Mungu atakupa.

🔑 Sala:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Sina Wasiwasi Wala Sisumbuki Kwa Ajili ya Jambo Lolote Maishani Mwangu, Bali Nina Sali na Kuomba Pamoja na Kushukuru Kwa Ajili ya Mambo Yangu Yote. Nina Amani Tele Itokayo Kwa Mungu Baba Yangu. Amen

🪙 Soma:
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Zaburi 145:18-19 BHN
[18] Mwenyezi-Mungu yuko karibu na wote wanaomwomba, wote wanaomwomba kwa moyo mnyofu. [19] Huwapatia mahitaji yao wote wanaomcha; husikia kilio chao na kuwaokoa.

Wakolosai 4:2 SRUV
[2] Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba mkiwa na shukrani;

✍ ps_emmanuel_cliff
━━━━━━━━━━━━━━━━━━━━
Karibu Tujifunze Neno Kwa Njia Whatsapp na Telegram LIVE Saa Nne Kamili Usiku (4:00),
Karibu Pia Ushiriki Na Maombi Saa Kumi Na Moja Na Nusu Alfajiri (11:30).
Unaweza Kujiunga Kwenye Group Kwa Kubonyeza Link Ya Whatsapp au Telegram.

- Whatsapp:
https://chat.whatsapp.com/KnrRt1D9CtIIiaCI7nlODm

Address

Arusha
23306

Telephone

+255787131824

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ps. Emmanuel Cliff posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share