NCHI YA WALIO HAI.

NCHI YA WALIO HAI. maarifa ya neno la Mungu ndio msingi sahihi wa mafanikio yadumuyo

20/03/2023
06/05/2022

K**a Huna Yesu kristo hujaokoka Umepotea

Hii ni sehemu ya Mambo mazuri yanayoendelea kuachiwa katika Group la Great 2022 K**a bado hujajiunga unapitwa na vitu vi...
23/01/2022

Hii ni sehemu ya Mambo mazuri yanayoendelea kuachiwa katika Group la Great 2022
K**a bado hujajiunga unapitwa na vitu vizuri
Karibu kwa link ipo mwisho

1.KUWA NA MAONO||(MALENGO THABITI)*

*Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.*
Mithali 29:18

Maono ni picha ya akili iliyoingia moyoni inayokupa taswira namna Kesho Yako utakavyoonekana. Maono ndio yanayotoa ujasiri na nguvu kwa mtu juu ya maisha yake ya kesho licha ya maisha mabaya na magumu ya leo. Kitakachobadilisha hali mbaya na ngumu ya sasa sio kuomba sana bali ni kuwa na picha kubwa ya maisha Yako ya baadae yaweje na kuanza kufanyia Kazi kwanzia sasa.

Mtu mwenye maisha bora na mazuri ya kesho ni mtu aliyeyaona anatia nia na juhudi kuyafikia.

Sasa ili tuwe na matokeo mazuri mwaka huu ni lazima tuwe na maono na tuweke mipango kulingana na kile tunapotaka tufikie.

Mtu asiye na maono hana mpigango thabiti na mtu asiye na mipango hajui nini anakitaka kwenye maisha yake hawezi kufanikiwa mtu k**a huyu

K**a huna MAONO hujui nini unakitaka katika maisha Yako|| kwa kifupi umekuja kuzurura duniani. Unatia hasara na kuongeza idadi ya watu tegemezi wasiojielewa

Sasa jua Maono|mipango Yako ya mwaka ndio itakupa nidhamu ya namna ya kutumia rasilimali zako vizuri. (Pasipo maono watu huacha kujizuia)
[1/23, 17:01] Davis Eneza: Sasa...
Ukishakua na picha kubwa kwamba unataka nini kwenye mwaka huu unaweka Malengo la namna Gani ya kuyafikia. Malengo hayo lazima yawe Thabiti. Kuwa na Malengo thabiti ni Smart Plans ambayo unaweza kutazama na kujipima unapofika mwisho wa mwaka

Ninapozungumzia Smart plan ninamaanisha Malengo ambayo ni
👉 *S-Specific*
Lengo linalogusa eneo maalumu na sio mipango ya jumla tu. Mfano lengo la kiuchumi labda unasema hadi mwaka December ninataka nikuze kipato changu kwa mwezi iwe 1.5mil ) hili ni l
👉 *M-Measurable*
Lengo ambalo unaweza kulipima na kujua nimefanikiwa kwa kisasi gani na nimeshidwa kwa kiasi Gani

👉 *A-Attainable*
Lengo ambalo unauwezo wa kulifikia, sio unapanga ilimradi umepanga mipango tu. Jiulize je ninaweza kulifikia hili Lengo,, bibilia inasema usinie makuu kupita uwezo wako. Hilo unalopanga unauwezo. Sio binti unapanga mwaka huu nitakuwa na watoto mapacha alafu hata mchumba anayeeleweka hayupo. *Panga kutimiza na sio utimize tu kupanga*

👉 *R-Realistic*
Weka Malengo ambayo yanaeleweka na sio Malengo ilimradi ni Malengo,, mfano wewe ni mwanafunzi unapanga kuwa na familia,, au kuwa na Kazi Yako waka huu hujamaliza chuo,, that not realistic

👉 *T-Time Frame*
Malengo Yako yote yape mda maalumu wa kuyakamilisha. Kwa hapa tunataka yawe Malengo ya 2022 ila binafsi unaweza ukayagawanya na kuyapa mda labda ndani ya miezi 6 au miezi 9 kulingana na uzito wa mpango wako.
Malengo yasiyo na mda sio Malengo ni matamanio

Watu wengi wanatamani wawe na maisha mazuri,, gari, nyumba nzuri,, Kazi safi ila k**a hujaweka Malengo na mikakati ya namna ya kuifikia ndani ya muda Gani yatabaki kuwa matamanio tu

Nimekufundisha namna ya kuweka Malengo ya mwaka huu nikupe WITO k**a unajua huna Malengo pangilia sasa na uyaandike na k**a utahitaji usimamizi (Mentor) mtu atakaye kushauri na kukusimamia ili kuyafikia unaweza kunitafuta in-box nitakusaidia
I need kuona unafanikiwa kweli kweli 2022
[1/23, 17:26] Davis Eneza: *Nimalizie kwa kukupa utaratibu mzuri wa kupangilia Malengo Yako*

K**a umeshapanga basi yaweke vizuri katika mtiririko huu,, na k**a hukuwa umepanga Malengo Yako
Mda ndio huu..

Mpangilio bora wa Malengo wa Mtu aliyeokoka

1.Malengo ya kiroho
2.Malengo ya kihuduma
3.Malengo ya kiuchumi
4.Malengo ya kifamilia
5.malengo ya kujiendeleza (Personal development)
6.Malengo mengine kwa kadiri unavyoyaweza kupangilia

WITO
Ninaomba nione kila mmoja ambaye unatamani uwe na matokeo yanayoeleweka mwaka huu ukiwa umepangilia Malengo Yako,, ninatoa nafasi ya kukusaidia (Mentorship) kwaambaye yupo tayari

Kwa leo nitaishia hapa.

WhatsApp Group Invite

21/01/2022

Let me see your Comment

Karibu ubarikiwe na wimbo huu mzuri wa Mtumishi wa Mungu Entujael  msangi Subscribe chanel kwaajili ya kupata nyimbo zai...
21/01/2022

Karibu ubarikiwe na wimbo huu mzuri wa Mtumishi wa Mungu Entujael msangi
Subscribe chanel kwaajili ya kupata nyimbo zaidi

Jenga moyoni mwako itakayomwabudu Mungu nyakati zote, Madhabahu itakayomwabudu Mungu kiangazi na Masika, Wakati wa kushonwa na wakati wa kuraruliw...

Karibu ujifunze Kupitia Whatsapp hii.Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.Mithal...
22/09/2021

Karibu ujifunze Kupitia Whatsapp hii.

Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Mithali 4:7

WhatsApp Group Invite

" A Man is fearfully and wonderfully Made | No any other Man can be able to Fix Him 💯% " I will praise thee; for I am fe...
22/09/2021

" A Man is fearfully and wonderfully Made |
No any other Man can be able to Fix Him 💯% "

I will praise thee; for I am fearfully and
wonderfully made: Marvellous are thy
works; And that my soul knoweth right well.
Psalm 139:14 KJV

Zaburi 139:14
[14]Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.
Matendo yako ni ya ajabu,
Na nafsi yangu yajua sana,

Mwanadamu ameumbwa kwa jinsi ya Ajabu na kutisha | Kwahiyo Hakuna mwanadamu mwingine mwenye uwezo wa kuufahamu mwili wake na kuutibu kwa ukamilifu asilimia zote 100

Ndio maana Dawa nyingi utakuta zinatibu Lakini side effect Ni kubwa wakati mwingine zaidi hata ya Tiba | Ni kwasababu mwili wa mwanadamu Ni Sana [ Sio Gari ulisambaze Lote ]

Ninaamini Sayansi itahangaika sana na mwanadamu na itachoka kwasababu mwanadamu sio panya kumfanyia majaribio ukammaliza | aliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu | Kuna kitu Cha Mungu kwa kila mwanadamu awe ameokoka au hajaokoka

Sayansi Itahangaika na Maiti na kuzifanyia utafiti Lakini haitafika katika ukamilifu wa Kumjua mwanadamu | Tuliumbwa katika ukamilifu wa Mungu

Watajitahidi Sana | Lakini Itawachosha
Hakuna kitu wanahangaikia Wanasayansi K**a
Kuweza kummaliza Mtu kiutafiti | haswa ambaye
Yuko hai na anatembea

Wanafanya mambo Mengi kujua Namna ya kumwendesha Mtu
Ikiwezekana kwa kuweka Vifaa ndani yake ili waone K**a wanaweza kum-Control | NDIO MAANA USIWAPE WATU MWILI
WAKO WAUFANYIE MAJARIBIO | HUO MWILI NI HEKALU LA
MUNGU

Mpaka Leo hakuna Tiba ya Kansa
Hakuna Tiba ya Ukimwi
Unafikiri kwanini

Lakini Watu wengi wamepona Asilimia 💯
Kwa Nguvu za Mungu

NDIO MAANA

" Neno la Mungu Pekee ambalo kwa Hilo mwanadamu aliumbwa ndilo lenye uwezo wa kuleta Uponyaji, Tiba , Kinga, Ustawi , na uhai wa mwili 💯% "

Lakini K**a moyoni mwako haumtumaini Mungu kupitia Neno lake na unatumainia wanadamu ambao mioyoni mwao hawajawahi kuwaza mema isipokuwa nyuma ya kila jema wanalokuletea Wana taget zao | Hautaweza Kuishi maisha ya Amani

Unapaswa

Mithali 3:5-8
[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
[6]Katika njia zako zote mkiri yeye,
Naye atayanyosha mapito yako.
[7]Usiwe mwenye hekima machoni pako;
Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.
[8]Itakuwa afya mwilini pako,
Na mafuta mifupani mwako.

SOMA KWA MAKINI | UKIFANYA YOTE KUANZIA MSTARI WA TANO - TUNAPATA MATOKEO YA MISTARI " 8 " Itakuwa Afya Mwilini Pako [ Biblia inasema Kumtegemea Bwana Kwa moyo wako wote - Itakuwa Afya Mwilini Pako | Je hili sio Jambo la kulipokea kwa Kuruka juu kwa Furaha ] haitoshi Biblia inasema " Itakuwa Mafuta mifupani pako la Mungu linaweza kuwa mafuta kwenye mifupa yako na kukuzia usipate ugonjwa wowote wa mifupa | Swali ni Je Unaamini !

Mithali 4:20-22
[20]Mwanangu, sikiliza maneno yangu;
Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
[21]Zisiondoke machoni pako;
Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
[22]Maana ni uhai kwa wale wazipatao,
Na afya ya mwili wao wote.

K**a ukiwekeza kulisikia Neno la Mungu na kukubali kulipokea K**a linavyosema bila kuchanganya na Elimu yako ya Kidunia | Ukaliacha liingie ,ukaliamini kwa moyo wako wote | Ukakubali Kuishi kwa Hilo Neno la Uzima INASEMA NI UHAI KWA WALE WALIPATAO NA AFYA YA MWILI WAO WOTE

Neno la Mungu ndilo linaloweza kuuratibu na kuuleta mwili wa mwanadamu katika ukamilifu wote

God bless you

Pastor Ibrahim Amasi
ABC KAHAMA

LivingWord|2021
make a Living

18/09/2021

Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.

Mithali 16:7

KWA HABARI YA AFYA YA   Kwa namna rahisi kabisa kuelewa na ambayo inaweza kuingia ndani yako na kukupa matokeo   01KINAC...
16/03/2021

KWA HABARI
YA AFYA YA

Kwa namna rahisi kabisa kuelewa na ambayo inaweza kuingia ndani yako na kukupa matokeo

01

KINACHOFANYA
Mtu aitwe baba wa familia, kiongozi wa familia NI MAJUKUMU [ Ili awe Bwana wa Familia, baba wa familia - Lazima awajibike , majukumu ndiyo yanayomfanya kuwa baba ]

K**a wewe hauwezi kukaa kwenye nyumba iliyo na ufa, iliyotoboka kwenye paa, k**a hauwezi kukaa na nyumba chafu iliyo na takataka na harufu mbaya ndani , huwezi kukubali mchwa wajenge kichuguu sebuleni

BASI Bwana Yesu K**a anakaa ndani yako na uhalali wa kukaa ndani yako Ni Kwasababu unao mwili [ Basi huo mwili Ni wa muhimu kwake , na Kwasababu hiyo Ni Bwana Pia katika mwili wako ] He is the Lord over your body Also | Kwahiyo k**a Ni Bwana wa mwili wako , Basi anakazi ya Kufanya , hawezi kuacha uvimbe ukajiibukia tu kiunoni, ana wajibu wa kuutoa

K**a Mwili wako Ni hekalu la Roho Mtakatifu , Basi Hawezi kukaa na eneo lililoharibika , vidonda vya tumbo, pressure , kisukari, ROHO MTAKATIFU ANA KAZI YA KUFANYA

Biblia Inasema
8:11
[11]Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.

Kazi yake kila siku Ni kuhakikisha , figo iko sawasawa, ini linafanya kazi vizuri , moyo unafanya kazi sawasawa [ hata k**a kulikuwa na uharibifu , anahakikisha anafanya marekebisho kila siku [ anahuisha kila kiungo Cha mwili ]

Na maadam Bwana Yesu Ni Bwana Juu ya mwili wako Pia , Basi anahakikisha kila kitu kinanyenyekea na kuanguka mbele yako [ kansa lazima ipige magoti mbele yako k**a Bwana Yesu anakaa ndani yako ] Every knee should bow

SWALI NI JE | unaamini na uko tayari Kweli hii ifanye kazi kwenye maisha yako , unakubali ufahamu huu ukuweke huru mbali na uonevu wa magonjwa - kazi kwako

UFAHAMU 02

K**a Biblia Inasema | 1 6:20[20]maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu

Ulinunuliwa [ Wewe sio Mali yako, hauishi kwa ajili yako, mwili wako sio wako ] mwili wako ulishanunuliwa

Aliyeununua, alilipa gharama ngumu , alipigwa na kuumizwa vibaya hata kufa, hiyo ndiyo gharama aliyolipa kwa ajili ya mwili wako NA BIBLIA INASEMA

1 Petro 2:24
[24]Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kwake mliponywa.

Aliyeununua mwili wako, aliyegharamikia , aligharamikia Damu yake na mwili wake [ ambaye Ni Yesu ] na kutokana na hayo aliununua kwa thamani ya damu yake [ Damu ya mwana wa Mungu ]

K**a ndivyo ilivyo Basi mwili wako ulinunuliwa ili usipate mashambulizi Tena ya kiafya kila wiki, ulinunuliwa ili usiteswe na magonjwa , ulinunuliwa ili umtukuze Mungu katika mwili huo

SASA BAADA YA KUELEWA HIVYO
Kansa inapokuja kwenye mwili wako na kukutishia kukuua , Kisukari kinapokuja kukutishia kukuua [ Kiulize swali, K**a Nilinunuliwa kwa thamani ambayo hailingani na kitu chochote hapa Duniani ili niwe na Afya " Wewe kisukari umeenda lini kwa Mungu ukawa na Dau kubwa kuliko Damu ya mwana wa Mungu na ukapewa Ruhusa Kuja kwenye mwili wangu ]

Utagundua kuwa Haiwezekani na K**a Haitawezekani kansa kuwa na Dau kubwa kiasi cha kununua mwili wako na kuuanza Kufanya uoze [ Basi Kansa haiwezi kukuua kwasababu ulinunuliwa kwa thamani ili umtukuze Mungu katika mwili huo na sio uoze ]

SWALI NI JE | Mambo haya yatakuelea na utayakubali - ili yaanze kukupa matokeo ya Baraka na ya utukufu kwenye eneo la Afya

Ninakuombea Uk**ate ufahamu huu, utumie kusema mbeze za Shetani | Utaishi maisha huru mbali na kila uonevu wa Shetani

Hii ni Kweli | na ukiifahamu
Inakuweka Huru

God bless you

Pastor Ibrahim Amasi
ABC KAHAMA

LivingWord|2021
Make a Living

Address

Arusha

Telephone

+255743622890

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NCHI YA WALIO HAI. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to NCHI YA WALIO HAI.:

Share