Pentecostal Church of Christ Tanzania-PCCT

Pentecostal Church of Christ Tanzania-PCCT YESU NI BWANA

“16 Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema” (2 Timotheo 3:16-17)

Heri ya siku ya kuzaliwa kwako baba yetu , hakuna njia bora ya kueleza baraka za Mungu kwetu, kwa kutupa mtu k**a wewe! ...
01/01/2022

Heri ya siku ya kuzaliwa kwako baba yetu , hakuna njia bora ya kueleza baraka za Mungu kwetu, kwa kutupa mtu k**a wewe! shukrani zetu kwake ni kumwambia Bwana asante kwa kutupa "MTU MWENYE MOYO WAKO". Ubarikiwe sana Askofu wetu. Hongera kwa kuishi maisha yako ukimtumikia Yesu! Haki tumemwona Bwana kupitia wewe .

IMEISHA HIYO !
24/09/2021

IMEISHA HIYO !

Familia na huduma ya PCCT tunakutakia siku ya Furaha na Amani kutoka kwa Bwana Mchungaji Sabas ,unapoa adhimisha siku ya...
07/07/2021

Familia na huduma ya PCCT tunakutakia siku ya Furaha na Amani kutoka kwa Bwana Mchungaji Sabas ,unapoa adhimisha siku yako ya kuzaliwa .Neema na Mkono Wa Bwana vielendee kuwa pamoja nawe katika maisha na huduma katika jina la Yesu.

Kesho ! Kesho kesho .Hapa hapa kwetu kimara stopover ! .Karibuni tuabudu pamoja.
17/04/2021

Kesho ! Kesho kesho .
Hapa hapa kwetu kimara stopover ! .
Karibuni tuabudu pamoja.

Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho: http://dist...
13/02/2021

Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho: http://distribution.rhapsodyofrealities.org/dept/?team=center1

FANYA NGUVU IWEPO KWANZA

Jumamosi, 13

```Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD```

*…Sala ya bidii (ya moyoni, endelevu) ya mwenye haki hufanya nguvu kuu kuwapo [ijizalishayo katika utendaji wake] ```Yakobo 5:16 toleo la “AMPC”```

Wengi hawaelewi umuhimu wa sala ya moyoni, na endelevu. Wanatamka maneno kabla ya kutumia muda wa kutosha katika sala na kujiuliza ni kwa nini ukiri wao hauna matokeo. Unapaswa kujifunza namna ya kusababisha nguvu iwepo kwanza!

Pindi unapokuwa umeshafanya nguvu iwepo, na kisha kufanya ukiri wa imani, kwamba lile badiliko ulilo na shauku nalo litathibitika (litasimama). Soma habari ya Eliya katika 1 Wafalme 17-18. Aliomba ukame uje katika nchi—na mvua haikunyesha—hakukuwa hata na tone kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu.

Wakati ulipofika wa ukame kukoma, Eliya alimwomba Bwana kwa ajili ya mvua. Haikuwa tu maombi mafupi, maneno ya kawaida ya haraka-haraka katika sala; hapana! Yalikuwa ni ya msukumo mkubwa, ya moyoni, endelevu na ya bidii!

Alimtuma mtumishi wake mara sita kuona k**a kulikuwa na ishara kwa alivyokuwa anaendelea katika sala, akitarajia jibu (badiliko). Mtumishi alirudi mara ya saba na kusema, “Ninaona wingu dogo; nalo ni dogo sana k**a mkono wa mtu.” Hilo ndilo lilikuwa kila kitu Eliya alichohitaji; alitambua kuwa ameshinda!

Alimwambia mtumishi wake, *“Upesi, shika njia. Mwambie Ahabu, ‘Tandika kiti cha farasi na uteremke upesi kutoka mlimani kabla mvua haijakuzuia’”* (1 Wafalme 18:44 toleo la “MSG”). Angalia mlolongo, Eliya alifanya nguvu kuu kuwepo kwanza kupitia sala ya bidii ya moyoni, na kisha akatoa neno.

Kwa njia iyo hiyo, baada ya kuchochea dhoruba ya Roho Mtakatifu katika chumba chako cha siri, hapo ndipo unapotamka “rhema” (Neno). Hiyo ndiyo njia ya uhakika ambayo kwa ufanisi unaweza kubadilisha hali ziende sanjari na mpango wa Kiungu wa Mungu, makusudi na mapenzi Yake katika maisha yako, familia, mji, taifa na kote duniani.

*| SALA

Mpendwa Baba, ninaomba kwa ajili ya mataifa ya ulimwenguni leo, kwamba mapenzi Yako na madhumuni Yako yasimamishwe kila mahali. Mioyo ya viongozi na wale walio katika mamlaka watekeleze na kufuata lile lililo sahihi. Na ninatamka kwamba nguvu na ushawishi wa wale waliodhamiria mioyoni mwao kutenda uovu kuondolewa, na shauku zao hazitotimia wala kutekelezeka katika Jina la Yesu! Kanisa linashinda na kutawala kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Jifunze Zaidi:

*||* Yakobo 5:16-18 AMPC; 1 Wafalme 18:41-44 *||*

SOMA MAANDIKO KILA SIKU

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:

Matayo 28 & Walawi 4-5

MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:

Matayo 14:1-10 & Mwanzo 44

Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional

Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye www.rhapsodyofrealities.org

Improving your life each day, one article at a time

Happy birthday you our father in the Lord .Arc Bishop Eliya Ngalawa .Your the blessing to the family of PCCT ,we love yo...
01/01/2021

Happy birthday you our father in the Lord .Arc Bishop Eliya Ngalawa .
Your the blessing to the family of PCCT ,we love you and thank God for the Gift of you. More grace ! More auction on you sir .

Welcome and join me ,today     stopover ,as we are officiating " PCCT-DODOMA BRANCH .
06/12/2020

Welcome and join me ,today stopover ,as we are officiating " PCCT-DODOMA BRANCH .

Address

Kimara Stopover
Arusha
255

Telephone

+255784364479

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pentecostal Church of Christ Tanzania-PCCT posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Pentecostal Church of Christ Tanzania-PCCT:

Share