26/07/2026
IBADA YA JUMAPILI: TAREHE 26/07/2026
MCHUNGAJI: MERCY KOMBA
SOMO: UTAMBULISHO WAKO UPO KATIKA MUNGU
Utambulisho ni hali, sifa ya vitu vinavyomfanya mtu , kitu au Kundi litambulike au lijulikane.
Mwanzo 1:26-27
Huu ndio utambulisho wetu na asili yetu na ndiyo sababu iliyopelekea Yesu kuja kufa Msalabani, sababu huyu ni mtu alipoteza asili yake pale dhambi ilipoingia kwake kupitia Kusikia. Yesu hakuja kwa Kusudi la sisi kuondolewa magonjwa na taabu bali alikuja ili kuturudisha ktk nafasi yetu ya kwanza ambayo tulikuwa tumeumbiwa kwayo ambayo ni mfano na sura ya Mungu. Watu leo wanamtafuta Mungu ili wapate kuponywa badala ya kumpata Mungu.
Zaburi 82:6
Mwanadamu ni akili ya Mungu, Ubunifu wa Mungu anataka akikuona wewe ajione yeye kwako, mahali popote ulipo aone ukiwa k**a Mungu. Kwa kutokuwa kwenye nafasi yetu ya asili ambayo tumeumbiwa.
Fika mahali jua kuwa wewe sio mtu wa kawaida wala wa hovyo tena mshukuru Mungu kwa jinsi ya ajabu k**a Daudi alivyosema.
Zaburi 139:14
Je umeshawahi Kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuumba?
Ikiwa Mungu ametuumba tutembee ktk Utambulisho wake je yeye yupoje ?
Sifa za Mungu
1. MUUMBAJI
Mwanzo 1:1...
Mungu aliumba kila kitu kinachoonekana leo kutoka mahali pasipokuwa na kitu.
-Ili uweze kuona vitu vikioneka ktk maisha yako,familia, kazi n.k anza kuumba kwa kutamka kile unataka kitokee. Unapotamka tamka kwa Imani.
Waebrania 11:3
-Usiruhusu kinywa chako kuongea hasi bali ongea vema. Baada ya kutamka chukua hatua maana hata Mungu baada ya kutamka alikuja kufanya. Hivyo fanya kazi pia.
2.MTAKATIFU
1 Petro 1:15-16
Ikiwa aliyetuumba ni Mtakatifu basi na sisi tuwe watakatifu, dhambi na uovu visionekane ndani yako.
3.UPENDO
1Yohana 4:8
Mungu ana upendo, Yeye ndiye Pendo. Ikiwa huna upendo hujamjua Mungu bado.
-Hakuna Upendo pasipo kutoa, ndiomaana kwa upendo wake kwetu alimtoa mwanae wa pekee. Huwezi kusema unampenda mtu usiekubali kujitoa kwake.
Waefeso 5:1-2
4.HURUMA
Zaburi 103:8
Tuwe na huruma na wengine, hurumia wenye dhambi k**a yeye anavyohurumia maana ni tabia yake.
Luka 6:36
Inaendelea...........