Tanzania Assemblies of God - World Outreach Mission

Tanzania Assemblies of God - World Outreach Mission Till the whole world comes to Jesus

Karibu ushiriki nasi katika SIKU 7 ZA KUFUNGA NA KUOMBA kwanzia tarehe 20 April 2026 mpaka 26 April 2026.DHIMA : MAOMBI ...
19/04/2026

Karibu ushiriki nasi katika SIKU 7 ZA KUFUNGA NA KUOMBA kwanzia tarehe 20 April 2026 mpaka 26 April 2026.

DHIMA : MAOMBI YA MOTO WA UAMSHO.

Hii si tu kuacha kula. Ni kujipanga upya, kujitoa kabisa, na kuwasha tena ule moto wa kiroho. K**a roho yako imekuwa dhaifu, huu ndio muda wako wa kuanza upya.

SOMO LA LEO : UPEPO WA ROHO MTAKATIFUMHUBIRI : Mch. Timothy wambura-Yohana 3:8🔹Roho mtakatifu ni zaidi ya kimbunga kinac...
12/04/2026

SOMO LA LEO : UPEPO WA ROHO MTAKATIFU
MHUBIRI : Mch. Timothy wambura
-Yohana 3:8

🔹Roho mtakatifu ni zaidi ya kimbunga kinachoweza kubeba majengo.
🔹Roho mtakatifu huleta uzima ndani ya kitu kilichokufa.
🔹Roho mtakatifu kutusaidia kuomba kwa namna ya kipekee sana.
🔹Roho mtakatifu huleta toba ya kweli ndani ya moyo wa mwanadamu.

SOMO LA LEO : UWANAFUNZI.MHUBURI : Mr. Christopher Kombe.Yesu alisema, Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. ...
15/03/2026

SOMO LA LEO : UWANAFUNZI.
MHUBURI : Mr. Christopher Kombe.

Yesu alisema, Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. (Mathayo 28:19–20). Hii ni wito wa kila Mkristo, sio tu kwa wachungaji au viongozi wa kanisa, bali kwa kila mmoja wetu aliyeokolewa. Ukristo sio kukaa kanisani tu, bali ni kuishi maisha yanayoangaza ulimwengu kwa matendo, upendo, na ushuhuda wa kweli. Uwanafunzi ni safari ya kumfuata Kristo kwa uaminifu, kujifunza kutoka kwake, na kuwafundisha wengine kufanya vivyo hivyo. Tunapoitwa kuwa wanafunzi, tunaitwa pia kuwa walimu wa mataifa, tukiwavuta kwa nuru ya injili. Leo tunakumbushwa kwamba jukumu letu ni kueneza mwanga wa Kristo, kuonyesha mfano wa maisha ya kiroho, na kushirikisha ulimwengu tumaini lililo ndani yetu. Hii ndiyo agizo kuu ambalo halina kikomo cha muda, bali ni wajibu wa kila siku kwa kila aliyeamini.

08/03/2026

Usitegemee nguvu zako, bali za Mungu.

Isaya 45:22
Niangalieni mimi, mkaokolewe,
Maisha yamejaa changamoto, lakini pale tunapomtegemea Mungu, hakuna kinachoweza kutuzuia.

🔹 Tumtegemee kwa moyo wote, yeye ndiye suluhisho letu lisilo na kipimo.


Leo kanisani tumejifunza kuwa nguvu halisi ipo pale tu tunapomtegemea Mungu.Isaya 45:22 imeandikwa, "Niangalieni mimi, m...
08/03/2026

Leo kanisani tumejifunza kuwa nguvu halisi ipo pale tu tunapomtegemea Mungu.

Isaya 45:22 imeandikwa, "Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi nchi zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine."

Hata pale maisha yanapokuwa magumu, changamoto zikionekana zisizo na mwisho, tumtegemee Mungu. Yeye ndiye mwanga wetu, faraja yetu, na nguvu isiyoisha.


This Sunday we celebrate the grace, strength, and impact of the amazing women in our church family. Their faith, service...
06/03/2026

This Sunday we celebrate the grace, strength, and impact of the amazing women in our church family. Their faith, service, and dedication continue to inspire generations and push the mission forward.

Join us as we honor the women who lead with love, serve with humility, and walk boldly in purpose.

đź“… 08th March 2026
🕖 7:00AM–9:00AM (English Service)
🕙 10:00AM–12:30PM (Swahili Service)
📍 TAG WOM Church, Moshono – Arusha

Let’s celebrate the women that God Almighty is using to change the world.

SOMO LA LEO : TUNATIMIZA AGIZO KUU KWA KISHINDO.Mathayo 28:18–19“Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…”K...
08/02/2026

SOMO LA LEO : TUNATIMIZA AGIZO KUU KWA KISHINDO.

Mathayo 28:18–19
“Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…”

Kupitia ujumbe wa Mchungaji Simon Samwel, leo Kanisa limekumbushwa wito wake mkuu:
si kukaa — ni kwenda,
si kuongea tu — ni kuishi injili.

Kristo amepewa mamlaka yote, na kwa mamlaka hiyo hiyo ametutuma sisi. Agizo Kuu halihitaji watazamaji, linahitaji watendaji.

Ujumbe huu unasimama sambamba kabisa na kauli mbiu ya mwaka 2026 ya kanisa:

“Tunatimiza Agizo Kuu kwa Kishindo.”

SOMO LA LEO : SIKU YA MAMBO MADOGO- Mungu huanza na kidogo ili kutufikisha kwenye kikubwa.- Uaminifu kwenye mwanzo mdogo...
01/02/2026

SOMO LA LEO : SIKU YA MAMBO MADOGO

- Mungu huanza na kidogo ili kutufikisha kwenye kikubwa.
- Uaminifu kwenye mwanzo mdogo ndio daraja kubwa la baraka.
- Mwanzo mdogo sio kushindwa, ni ushahidi kwamba Mungu bado yuko kazini.

🔹Zekaria 4:10

25/01/2026
Haleluya! Mshukuruni BWANA kwa maana fadhili zake ni za milele. Leo ni siku ya shukrani kwa yote ambayo MUNGU wetu aliye...
18/01/2026

Haleluya! Mshukuruni BWANA kwa maana fadhili zake ni za milele. Leo ni siku ya shukrani kwa yote ambayo MUNGU wetu aliye hai ametutendea.

Somo la leo: KUMSHUKURU BWANA.

📌 1 Wathesalonike 5:18
Leo tumekumbushwa kuwa kumshukuru MUNGU siyo kwa sababu kila kitu kiko sawa, bali kwa sababu Yeye bado ni MUNGU, bado ni mwaminifu, na bado anafanya kazi hata tusipoona. Shukrani ni imani inayoongea kimya kimya.

Address

Moshono
Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Assemblies of God - World Outreach Mission posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share