Northern Tanzania Union Conference

Northern Tanzania Union Conference Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Northern Tanzania Union Conference, Religious organisation, Arusha.

12/12/2023
14/07/2023

Pr. Mark Finley anakualika katika Mahubiri makini kupitia Satelite kutokea, New Life SDA Church in Nairobi kuanzia tarehe 2 - 16 September, 2023

09/06/2022

ATAPE Karatu Net Event kuanzia tarehe 25 June hadi 16 July 2022 "Tabia yangu Furaha yangu"

Pr. Ted Wilson,  The General Conference President of the  Seventh Day Adventist Church.
07/06/2022

Pr. Ted Wilson, The General Conference President of the Seventh Day Adventist Church.

Jesus is Coming get Involved Follow the live stream of the 61st General Conference Session held in St. Louis, Missouri, ...
06/06/2022

Jesus is Coming get Involved

Follow the live stream of the 61st General Conference Session held in St. Louis, Missouri, USA
https://www.youtube.com/watch?v=idMELM50hxE

Join the live stream of the 61st General Conference Session held in St. Louis, Missouri, USA.This morning, Mark Finley, Barry Black & Dwight Nelson will be s...

WASIFU WA MAREHEMU MCH.BERNARD SHAMBA KAZINGO MAMBWE   Mchungaji Bernard S.K. Mambwe alizaliwa Wilayani Kibondo Mkoani K...
14/05/2022

WASIFU WA MAREHEMU MCH.BERNARD SHAMBA KAZINGO MAMBWE
Mchungaji Bernard S.K. Mambwe alizaliwa Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, mnamo tarehe 08 Septemba 1957, mtoto wa tatu kwa tumbo la Mama yake Marehemu, Mama Ntibanyendeza Mambwe na Baba marehemu Mzee Mambwe Katoga.
Bernard S.K. Mambwe alihitimu masomo ya Elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Kigoma mnamo mwaka 1980. Na kisha mwaka 1985 alihitimu stashahada ya Uchungaji katika chuo cha Tanzania Adventist Seminary and college (TASC). Baadaye mwaka 1995 alihitimu Shahada ya kwanza ya Theologia katika Chuo Kikuu cha Bugema (Bugema University) kilichoko Kampala Uganda. Mnamo mwaka 2009, Mchungaji Bernard S.K. Mambwe alihitimu masomo yake ya Umahiri (Masters) katika Uongozi katika Chuo cha Adventist University of Africa (AUA) kilichoko huko Nairobi, Kenya.

Maisha Yake Kiimani
Bernard S.K. Mambwe alizaliwa na kulelewa katika familia ya Kikristo. Baada ya mafundisho na maelekezo ya kutosha kutoka kwa Waadventista Wasabato, alimkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake mnamo mwaka 1977 na kubatizwa. Tangu hapo alifanya kazi mbali mbali ndani ya Kanisa mahalia na kuanza kazi ya Uinjili sti wa Vitabu. Alidumu katika imani ya Waadventista Wasabato na hakuwahi kupata marudi yeyote kikanisa akidumu katika Imani hiyo kwa uaminifu hadi kifo chake.

Familia
Bernard S.K. Mambwe alifunga ndoa na Esther K. Buzubona tarehe 07 Septemba 1983 kwenye Kanisa la Waadventista wa Sabato Cherabulo, huduma iliyoendeshwa na Mchungaji Marehemu Philipo Mwambalagania. Mke wake anamwelezea kuwa alikuwa Mume, Baba, Mchungaji mcha Mungu, mcheshi, Kiongozi, mwenye hekima na busara, aliyempenda na kuwapenda watoto wa ke kwa kuwajali sana katika miaka yake yote takribani 39 ya ndoa yake.
Maisha ya Utumishi
Bernard S.K. Mambwe aliajiriwa Tanganyika General Field (TGF) mwaka 1978 k**a Mwinjilisti wa Vitabu wa kufaulu wa cheti cha Tatu. Alifanya uinjilisti huo tangu 1978 hadi Julai 1981. Mwaka 1981 mwezi Agosti aliitwa na Fildi ya East Tanzania (ETF) kuwa Mchungaji Mlei katika Mtaa wa Kilombero/Ifakara.
Mnamo Julai 1985 aliitwa na Field ya East Tanzania kuwa Mchungaji katika Mtaa wa Dodoma akauongoza mpaka mwezi Desemba 1989. Januar i 1990 aliitwa na kuitika kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Vijana na Shule ya Sabato katika Field ya East Tanzania (ETF) kazi aliyoifanya mpaka mwezi wa August 1991. Mwezi ule wa Julai 1995 aliitwa na Field ya East Tanzania kuwa Katibu wa Wachungaji (Ministerial Director), Ukurungezi alioufanya mpaka Desemba 1998. Mnamo Januar i 1999 aliitwa kuwa Katibu mkuu wa conference ya North East Tanzania kazi aliyoifanya mpaka Desemba ya mwaka 1999.
Mwezi wa Januari 2000 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti (ASKOFU) wa North East Tanzania Conference (NETC) kazi aliyoifanya mpaka Desemba2000 . Mwezi ule wa Januari 2001 aliitwa kuwa Mwenyekiti (ASKOFU) wa East Tanzania Field (ETF) kazi aliyoifanya mpaka mwezi wa Desemba 2002. Ni katika Kikao Kikuu cha Union Misheni ya Tanzania cha Desemba 2002 alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Tanzania Union Misheni, na mnamo Januari 2003 alianza kazi hiyo aliyoifanya mpaka mwezi Desemba 2010.
Ni Session ya Tanzania Union Misheni ya mwaka 2010 alipopendekezwa na kupitishwa Mchungaji Bernard S.K. Mambwe kuwa Mwenyekiti wa Western Tanzania Field (WTF) kazi aliyoifanya mpaka mwaka 2014, Western Tanzania Field ikapewa hadhi ya kuwa Conference na jina likabadilika na kuwa Western Tanzania Conference (WTC). Session hiyo ilimchagua kuwa Mweny ekiti (ASKOFU) wa Western Tanzania Conference mpaka Agosti 2015 alipochaguliwa tena kuwa Mwenyekiti (Askofu) wa Western Tanzania Conference (WTC) akafanya kazi hiyo mpaka kustaafu kwake Desemba 2020.

Alikamilisha miaka ya utumishi katika Kanisa la Waadventista Wasabato, miaka 42 ikiwa ni sawa na miezi 504. Katika utumishi wake, watumishi walimfahamu k**a Mcha Mungu, Mchungaji, Baba, Mlezi, Mpole, mnyenyekevu, mstahimilivu, kiongozi, mwanzilishi wa miradi, m wana maendeleo wa kweli, mwadilifu ambaye alikuwa ni kiongozi kielelezo (Role Model) kwa watumishi wengi mpaka sasa.
Ungonjwa Hadi Kifo
Mchungaji Mstaafu Marehemu Bernard S.K. Mambwe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari (Diabetes) ambao umekuwa ukimsumbua tangu miaka ya 2002. Ni ugonjwa huu wa Kisukari ambao inaelekea ulisababisha uoni hafifu.
Ugonjwa huo ulileta udhaifu mwingine wa viungo kadhaa mwilini mwake na kupelekea alfajiri ya Alhamisi ya tarehe 12, Mei 2022 majira ya 10 na dakika 35 alfajiri Mchungaji Bernard S.K. Mambwe kulala usingizi wa mauti. Marehemu Mchungaji Benard Shamba Kazingo Mambwe ameacha Mke, Watoto Wanne wa Kiume: Ntiyanka, Masengo, Yilafasha na Ntakiyigola na wajukuu nane.


# 180 PANA MAHALI PAZURI MNO
Pana mahali pazuri mno, Twapaona kwa mbali. Baba yetu angoja pale, Amepanga makao yetu. Kitambo tu bado, Tutakutana ng’ambo pale .
Kitambo tu bado, Tutakutana ng’ambo pale. Tutaimba pale kwa moyo, Nyimbo tamu za wenye heri. Na rohoni hatutaona, Tena haja ya kupumzika. Kwa Baba yetu mkarimu, Tutatoa shukrani sana. Kwa kipaji cha pendo lake, Na baraka anazotupa.

11/05/2022

Share kwa kadri ya uwezavyo

  #   # Shiriki katika kuipeleka injili mahali ambapo hutafika wewe kwa kupitia sadaka yako ya tar 12 March 2022 ambayo ...
07/03/2022

# # Shiriki katika kuipeleka injili mahali ambapo hutafika wewe kwa kupitia sadaka yako ya tar 12 March 2022 ambayo itasaidia kuongeza Masafa ya Morning star radio.

19/01/2022

wa zamu ukutani jumamosi tunakuhakikishia usalama wako.

Address

Arusha
P.OBOX1121

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Northern Tanzania Union Conference posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Northern Tanzania Union Conference:

Share