Born 2 Win Ministry

Born 2 Win Ministry We are here to inspire you to live your life to the fullest.

18/07/2026

Pt 2 the presha is getting wesaaaaa🙆‍♀️🤣🤣

14/07/2026

When guessing the books of the bible( goes terribly wrong)🤣pt 1

Ee Yesu! 🙌Sisi k**a vijana tunaviweka vyote chini ya miguu yako. Tunakuabudu Wewe peke yako, kwa maana Wewe ndiye chanzo...
27/06/2026

Ee Yesu! 🙌

Sisi k**a vijana tunaviweka vyote chini ya miguu yako. Tunakuabudu Wewe peke yako, kwa maana Wewe ndiye chanzo cha uhai wetu, tumaini letu na sababu ya sisi kuwepo.

Bado tunaendelea kumtukuza na kumshukuru Mungu kwa yale makuu aliyotenda kupitia Semina Kubwa ya Vijana – Inspired for Change. Mioyo imeguswa, maisha yamebadilika, vijana wameokoka, wamekuwa imara na wengi wamemrudia Kristo.

Tunasema, Asante Yesu! Kwa sababu kila kilichofanyika kilikuwa kwa neema yako na kwa utukufu wa Jina lako.

Jumapili hii utamwabudu Mungu wapi? 🙏Karibu Victory Faith Church – Kijenge Mwanama tuje kwa pamoja kumwabudu na kumsifu ...
27/06/2026

Jumapili hii utamwabudu Mungu wapi? 🙏

Karibu Victory Faith Church – Kijenge Mwanama tuje kwa pamoja kumwabudu na kumsifu Mungu, kisha tusikie Neno lake litakalojenga na kuimarisha afya ya roho zetu.

Usikose nafasi ya kuwa katika uwepo wa Mungu, maana kuna Neno maalum ambalo Bwana ameliandaa kwa ajili ya maisha yako. Huenda ndilo jibu, nguvu au mwelekeo ambao umekuwa ukiuhitaji.

Karibu sana Victory Faith Church – Kijenge Mwanama.

Mungu ana neno kwa ajili ya nafsi yako. Tunakusubiri! ❤️🙏

Appreciation Post – Final Gratitude 🙏❤️Mwisho kabisa,Kwa kila mmoja aliyesimama na sisi vijana na kuwa sababu ya sisi ku...
26/06/2026

Appreciation Post – Final Gratitude 🙏❤️

Mwisho kabisa,

Kwa kila mmoja aliyesimama na sisi vijana na kuwa sababu ya sisi kuwafikia wengi—Mungu wa mbingu na nchi awakumbuke sana.

Tunatambua na kuthamini kwa moyo wote kila dhabihu iliyotolewa: muda, chakula, magari, fedha, mawazo na nguvu zenu. Hakika mchango wenu umeacha alama kubwa katika maisha ya vijana.

Pia tunawashukuru wale wote waliowezesha mazingira kuwa sawa—idara ya chakula, malazi, usafiri na uratibu mzima wa INSPIRED for Change. Kila sehemu imefanyika kwa upendo, nidhamu na moyo wa huduma.

Asanteni kwa utayari wenu na kwa kutochoka, kwa kujitoa bila kuchoka ili kuhakikisha vijana tunafikiwa na kubadilishwa.

Mungu wa mbinguni awabariki sana, awainue, awafanikishe na awatendee mema siku zote za maisha yenu.

Tunawashukuru sana, tunawathamini na tunawaombea baraka tele. 🙏✨

Appreciation Post 🙏❤️Kwenu vijana wote mliotoka sehemu mbalimbali za Tanzania na wale mliokuwa mnatufuatilia kutoka maen...
26/06/2026

Appreciation Post 🙏❤️

Kwenu vijana wote mliotoka sehemu mbalimbali za Tanzania na wale mliokuwa mnatufuatilia kutoka maeneo tofauti pamoja na nchi za nje,

Hakika uwepo wenu umekuwa wa thamani kubwa sana. Tumefurahi kuwa nanyi katika safari hii ya Inspired for Change.

Mmetoka maeneo mengi sana—Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Singida, Dodoma, Babati na mikoa mingine mingi pamoja na wale waliotufuatilia kutoka mbali zaidi. Tunawashukuru sana kwa kujitoa kwenu na kuhakikisha mnahudhuria na kushiriki kwa moyo mmoja.

Tunaamini kila mmoja wenu amepata jambo kubwa kupitia semina hii, jambo litakalobadilisha maisha yenu na kuzaa matunda katika safari yenu ya baadaye.

Asanteni sana kwa kuja, kwa kushiriki na kwa kuwa sehemu ya familia hii ya vijana.

Tuonane tena Season ya 11 🙏🔥✨

Appreciation Post 🙏🎧📸Kwenu Idara ya Sound & Media Team,Asanteni sana kwa utayari wenu uliooneshwa tangu kipindi cha maan...
26/06/2026

Appreciation Post 🙏🎧📸

Kwenu Idara ya Sound & Media Team,

Asanteni sana kwa utayari wenu uliooneshwa tangu kipindi cha maandalizi ya program hii hadi kufikia siku ya mwisho.

Tunawashukuru kwa kazi yenu kubwa ya matangazo, picha, video na sauti. Hakika mmekuwa sehemu muhimu sana ya kuhakikisha kila kilichotokea kinaonekana, kinasikika na kinahifadhiwa kwa uzuri na ubora.

Mchango wenu umesaidia sana kufikisha ujumbe kwa wengi zaidi na kuacha kumbukumbu nzuri ya kile Mungu alichofanya katikati ya vijana.

Mungu wa mbinguni awabariki sana, awazidishie neema, ubunifu na nguvu mpya katika kila mnachofanya. Tunawathamini sana 🙏✨

Appreciation Post – Huduma za Uimbaji 🎶🙏Kwenu Covenant Voice, Healing Voice, Victory Band, kwaya zote za wageni pamoja n...
26/06/2026

Appreciation Post – Huduma za Uimbaji 🎶🙏

Kwenu Covenant Voice, Healing Voice, Victory Band, kwaya zote za wageni pamoja na waimbaji binafsi ❤️,

Asanteni sana kwa kukubali kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa vya sauti zenu na muda wenu.

Kile ambacho Mungu ameweka ndani yenu kimekuwa baraka kubwa na njia rahisi ya kuwafikia vijana wengi. Kupitia nyimbo zenu, tumemwabudu Mungu kwa uhuru, tumepokea uponyaji, tumetiwa moyo na tumekaribishwa zaidi katika uwepo wa Mungu.

Hakika mlitusaidia kuelekeza mioyo yetu juu, na kufanya ibada kuwa hai na yenye kugusa maisha.

Tunawashukuru sana kwa moyo wenu wa kujitoa. Tunawaombea Mungu awabariki, awazidishie neema, mafuta mapya na awafanikishe katika kila eneo la huduma zenu na maisha yenu.

Mungu asiwasahau hata kidogo—bali azidi kuwainua na kuwafanya kuwa sauti inayogusa vizazi vingi zaidi.

Asanteni sana, tunauthamini mchango wenu! 🙏🎶✨

Appreciation Post 🙏❤️Kwenu viongozi wote wa vijana,Kubwa kabisa tunasema asante kwa kusimamia maono haya na kuhakikisha ...
25/06/2026

Appreciation Post 🙏❤️

Kwenu viongozi wote wa vijana,

Kubwa kabisa tunasema asante kwa kusimamia maono haya na kuhakikisha yanakuwa kweli kwa vitendo.

Mmekuwa nguzo muhimu sana katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na vijana wanafikiwa kwa wakati na kwa namna bora. Hakika mchango wenu umeleta matokeo makubwa sana.

Mungu wa mbinguni akumbuke nguvu zenu, muda wenu na hata fedha zenu mlizowekeza katika kukamilisha hili. Mmekuwa sababu kubwa ya wepesi wa vijana kufikiwa na kubadilishwa.

Tunawaombea Mungu awabariki sana, awaongezee neema, awainue na kuwapa nguvu mpya kila siku katika huduma na maisha yenu.

Asanteni sana viongozi wetu, tunawathamini na tunawapenda. 🙏✨

Appreciation PostKwako Pastor Hossiana ❤️,Asante sana kwa kuwa karibu na sisi vijana. Tunathamini sana muda wako na moyo...
25/06/2026

Appreciation Post

Kwako Pastor Hossiana ❤️,

Asante sana kwa kuwa karibu na sisi vijana. Tunathamini sana muda wako na moyo wako wa kujitoa kwa ajili yetu.

Asante kwa kuwa msaada wetu hasa pale ilipotokea changamoto ya kiafya. Umeonyesha upendo wa kweli na kujali bila kuchoka, jambo ambalo limegusa mioyo yetu sana.

Asante pia kwa kutufundisha kuhusu masuala ya afya na kutukumbusha umuhimu wa kujitunza sisi wenyewe. Hakika jamii inahitaji watu wengi k**a wewe—wenye moyo wa huduma, huruma na utayari wa kusaidia wengine wakati wa mahitaji.

Tunakuombea Mungu akuinue zaidi, akupe afya njema, nguvu mpya na baraka katika kila unachofanya.

Asante sana kwa yote. Mungu akubariki sana 🙏❤️✨

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Born 2 Win Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category